mkulimamiwa
JF-Expert Member
- Mar 4, 2025
- 2,254
- 4,466
Mbwa aliye huru ni rafiki wa kila mtu, labda umchokoze
Mbwa aliyefungwa na kutiwa minyororo bandani, hana rafiki, hata anayempa chakula, siku atakapojua haki zake, atamtia majeraha, atamchapa meno mpaka boss wake
Ndicho sisiem walichowafanya Watanzania, waliwafungia bandani miaka mingi huku wakiwatishia eti mkiwapa wapinzani kutakuwa na vita, 🤣🤣, ila ccm nyie...!!
Watanzania kujua haki zao imekuwa ni kosa, wao wanachokifanya, ni kuwateka, kuwauwa na kuwapeleka magereza bila hata sababu
Haki ya kuchagua ipo, haki ya kuwa na tume huru, hii haipo, na hii ndiyo vita kali iliyopo na ndilo dai kubwa kwa vyama vyote hata ccm wenyewe
Haiwezekani, tume iundwe na Rais ambaye pia anaingia kwenye kinyang'anyilo cha kupigiwa kura! Huu ni wizi wa wazi wazi
Hiki ndicho kilio cha Watanzania
Sasa Mbwa kajua haki zake, ni mkali hataki kusogelewa hata na boss wake, maana kesha kata mnyororo na kupenda vya kujitafutia!
Kwa hali hii, CCM mnadhani mtalazimisha hivi mpaka lini?