CCM ina serikali sikivu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM ina serikali sikivu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masakata, Jun 1, 2011.

 1. Masakata

  Masakata JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: Jan 2, 2011
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Kati ya vitu wanavyonikera viongozi wa CCM ni kusema serikali yao ni sikivu.

  Sikivu wapi, toka lini tumewaeleza waache mashangingi na kuendekeza miposho ili pesa iende kwenye mambo ya maendeleo, tumeieleza wezi wa Kagoda, Meremeta na Deep green, wapelekwe mahakamani aah wapi! Nyumba za serikali zirudishwe, kimya; wezi wa rada washtakiwe na tofauti ya mishahara miongoni mwa tz itazamwe, kimya...etc..

  Eti sikivu, hakuna lolote ULAGHAI tu!
   
 2. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Ndiyo, serikali sikivu hii, huoni kule Tarime imewasikiliza wananchi maskini wanaodai haki zao kwa kuwapa pumziko la milele?

  Hujamsikia Kikwete anavyomsikiliza Lowasa kwa makini na kumhakikishia kuwa hakuna lolote baya litamfika kwa maovu yake?

  Hukumsikiza Mkama alivyo msikivu kwa mafisadi magamba kwa kuwaongezea muda wa kupumua chamani?

  Labda yategemea tunatafsiri vipi usikivu. Mimi naona ni sikivu. Tafakari!!


  (Lowasa) alisema Rais JK alimwelezakuwa hakuna maazimio yoyote ya NEC yaliyomtaka kujiuzuru. Akahoji, 'sasa nimwamini nani, ninyi mnaotaka nijiuzuru au rais aliyesema hakuna azimio kama hilo?' MwanaHalisi-Jtano, juni, 1-7-2011
   
 3. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,237
  Trophy Points: 280
  Inamsikiliza nani, tuwaajiri halafu watuambie wasikivu.... huu si ni wendawazimu. Yaani anajigamba kwa mwajiri wako kuwa wewe ni msikivu wakati unatakiwa usikie na kutii mara moja bila maswali.

  Au serikali imelewa madaraka wanajiona sasa wapo juu ya vichwa vya wananachi
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hivi ile tovuti ya wananchi imeenda wapi?
   
 5. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,273
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  hii nchi inapelekwa kishkaji sn wakuu, ifikie wakti tukatae vitu kwa vitendo aise.
   
 6. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ngugu wana JF nimefuatilia sana bunge kwa siku za karibuni na nimegundua kuwa wabunge kutoka chama fulani wamekuja na staili mpya ya kusifia serikali na kusema ni sikivu

  je kwa mtazamo wako serikali ni sikivu?

  je ni kupotoka kwa mbunge kusema serikali ni sikivu alafu haohapo anaanza kuilaumu serikali kwa matatizo ya jimbo lake?

  je Kwa mustakabali wa bunge la namna hii tutafika kweli?


  Nawakilisha.
   
 7. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Serikali ya Tanzania ambayo inaongozwa na CCM ni SIKIVU.
   
 8. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtu akiwa na mapepo anasema chochote. wabunge wa ccm wana mapepo.
   
 9. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mchungaji lwakatare jana kama nimemsikia akiyakemea, anyway, ngoja tusubiri mh. captain komba na mwaka huu atakemea tena hayo mapepo, na ninahisi yameletwa na yule mganga wa korogwe prof. maji marefu, ndo maana mapepo mwaka huu yameongezeka 7 mara sabini.
   
 10. Y

  Yetuwote Senior Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata Mgonjwa alielazwa haspitali akiulizwa habari gani atasema nzuri tu. Hujambo, atajibu Sijambo.
  Hili la usikivu lisikusumbue kwani mwenye macho haambiwi tazama.
   
 11. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33

  Ndugu Ladslaus nadhani hujanielewa nimeuliza kama lina manufaa kwa bunge, kama ni sikivu au la hilo si swali
   
 12. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Msemo huu ni kwa ajili ya kuwapumbaza wananchi masikini wa mali mpaka mawazo.
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ni sikivu ila kusikia si kutenda!
   
 14. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  "Walikwapua fedha kwa ajili ya kununua dege la kifahari kwa pesa ya rusha roho,meremeta akachota,pesa zikabaki,kagoda kachota,zikabaki,geedgreen kachota hazikwisha,Tangold wakalamba vijisent nazo zikabaki,mawazili wanakaa kwenye hoteli za kifahari lakini fedha bado zipo,mzee wa kaya anakesha hewani na msafara wa watu zaidi ya 100,lakini bado zipo hadi igunga wametumia bil 3 lakini bado zipo,miaka 50 sherehe zimeanza tangu jan mpaka dec watatumia mabilion lakini fedha bado zipo,haya dorwans nao wanataka chao,kumbuka wanaolipa fedha dowans ndo hao hao wanaochukua:::::kilio cha walimu vp,pamoja na wazee wa east africa??? vp wao washachota?
   
 15. j

  jigoku JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kweli serikali ya CCM ni SIKIVU,Imesikia na kulishghulikia kwa vitendo na kwa dhati sakata la IPTL,RICHMOND na mwanae DOWANS na mjuu SYMBION kapatikana si kwa najisi, kweli imesikia na kushughulikia sakata la KIWIRA na kwa manufaa ya umma aliejiuzia ameshashughulikiwa ipasavyo na sasa anajutia makosa aliyoyafanya.

  Kweli imesikia na kuishughulikia kashfa ya UDA na kina Masaburi orignal wamewajibishwa,CCM jamani atakaebisha hatauona ufalme wa mbingu kama atasema serikali yake ni legelege wakati shule za Tanzania hakuna anaekaa chini kwa kukosa dawati,tena kwa shule zilizoko DAR wenyewe wanakalia viti vya miduu mitatu na nivyakuzunguka.

  Kina mama huko mahospitalini wanapewa huduma bora na dawa za kumwaga maana hazina watumiaji,walimu nao wanapata mishara mikubwa tena kwa wakati,wakulima usiseme maana tangu singo ya kilimo kwanza kila mkulima ana power tila kama hana basi ni mtendaji wa kiji aua kata hivyo mashamba yake ni mshahara tu na takrima ambayo serikali sikivu iliihalalisha.

  Jamani sitaki kubishana juu ya USIKIVU wa serikali ya CCM,nani hajui kama wakurugenzi na wahasibu huko kwenye halmashauri waliojaribu kwiba fedha za umma hawaja shitakiwa na wengine waliofanya hivyo miaka kama 5 hivi wanaozea jela?nami anabisha kwamba kila kukicha CGA hagundui matumizi mabaya ya fedha kwenye halmashauri na sasa hata idara zingine za serikali na adhabu KALIII! ya kuwahamisha idara au kumhamisha halmashauri? wapendwa huo sio usikivu wa serikali.

  Huko kwa Maige watu walijifanya wajanja kwiba wanyama wetu lakini serikali sikivu yenye dola na yenye mkono mrefu ulionyooka mpaka nje ya mipaka na yenye Intelligencia iliyobobea tayari imeshabaini walipelekwa wapi na nani alihusika na tayari muda si mrefu umma utajulishwa na tutaruhusiwa kufanya maandamano ya kuwapokea Twiga wetu.

  Serikali hii jamani ni sikivu anaebisha basi ana Malaria Sugu,kwani hata mauaji ya nyamongo kumbe wale walikuwa majambazi sugu na walikuwa wanajaribu kupambana na askari wao majambazi wakashindwa na ndio maana kuna vichaa wasio kuwa na akili walijaribu kutetea wezi wa dhahabu ya mzungu wakaswekwa ndani kwa manufaa ya umma na maiti za wezi wa dhahabu ya mzungu zikatupwa barabarani maana walifanya kosa kubwa la kumwibia mwekezaji.

  Hata wale wana nchi waliodhurika na maji yenye sumu pamoja na mbwa kumbe ilikuwa ni wao tu walikuwa hawapendi kuoga ndo maana wakatoka mabaka lakini serikali sikivu imeaamua kuwalipa japo yenyewe si chanzo na ikaamua kuwapelekea maji safi na kutibu ngozi zao na za mbwa na ng'ombe wao,jamani nani bado anabisha serikali hii si sikivu?

  Reli wanasema imekufa,ndege nazo za ATCL eti zimepungua wakati wa siku za nyuma Reli ilikuwa inabeba mizigo na abiria ndege nazo zilikuwa kumi na ngapi sijui wanajua hao wambea,lakini serikali sikivu ililisikia hilo ikamleta mhindi kwnye reli na sasa italeta reli ya umeme na dege zitashinda BA hata Fly Emirates hawatafua dafu.

  Nani anasema serikali sikivu inabanbikizia watu kesi,wengine wanaomba wenyewe kwenda jela maana wanakuwa hawana hela ya unga na dagaa,sasa wakipelekwa huko kwa kusikiliza kilio chao utabisha sio sikivu?

  Kwnza hakuna miradi hewa wala hakuna manunuzi hewa,hata ndege ya raisi ile tuliweka oder kiwandani ni Factory manufactured na hata Rada serikali ni sikivundio maana ilisahau kuchukua chenji na sasa iliwayuma watu kuifuata.Hao wazee wa iliyokuwa jumuia ya africa mashariki nao si imewasikiliza?

  Zanzibar CUF nao wamelilia kuonja asali wkiwa serikalini si imewasikiliza? jamani ni mengi sana nanyi mtaongezea
  Kwa hiyo hawa Chadema wanapotaka kuwashughulikia mafisadi,inapotaka haki na demokrasia ya kweli,wanapolalamikia rasilimali za taifa zitumike kwa manufaa ya umma, na wanapolalamika polisi kucheza game ya siasa na pale wanapoona Mahakama inakuwa-remoted na CCM si wana wabunge waambieni waende mjengoni kisha wakifika huko washindane kwa kura ya NDIO au HAPANA,kwa serikali ya CCM ni sikivu haitadhulumu mshindi wa kura nyingi zitakazoamriwa kwa SAUTI kubwa ya NDIO au HAPANA.

  KATIBA nayo kuna viana harakati na hao CDMSerikali sikivu ilikubali juu kuandika katiba na sasa imeshaandika mswada na wao wote waliweka mapendekezo yao sasa tusubiri mjengoni,maana serikali sikivu inategemea maamuzi ya wengi,hivy mjengoni ni wawakilishi wa watanzania tusubiri kura ya NDIO au HAPANA.

  TUIOMBEE SERIKALI SIKIVU IDUMU MPAKA WANANCHI WATAKAPOCHOKA RAHA NA STAREHE NA MAISHA BORA INAYOYAGAWA KWA
  WATANZANIA.

  Nawasilisha wakuu
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Nov 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Huu msamiati wa "USIKIVU" sijui mAGAMBA waliupata wapi, wanatusumbua nao kweli, au ni namna fulani ya kejeli?? Mtu akikutia msafi wakati umchafu nadhani ni kama kejeli fulani haya
   
 17. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #17
  Nov 8, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,419
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  mhhh tunajivunia AMANI na UVUMILIVU!
   
 18. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #18
  Nov 8, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Naam! Sawa na jiwe linavyoelea kwenye maji
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,187
  Likes Received: 563
  Trophy Points: 280
  Duh umejitahidi kweli kuandika insha
  Nafikiri mwalimu wako angekupa mia ya mia
  ila nimetoka kapa sijaelewa unazungumzia nini au unazungumzia Tanzania ipi au hii niijuayo au nyingine
  Au kuna nchi ya peponi inaitwa Tanzania na ina haya mambo ambayo sisi wengine hatuyaoni
  Ngoja nilog off maana naweza pata makengeza ya macho bure
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja anatafuta umaarufu kupitia USIKIVU sometimes huwa wanasema UKOMAVU WA KISIASA
   
Loading...