Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
CCM, chama kilichokuwa kinasimamia serikali zote tangu uhuru ndio chama kinachopaswa kuwajibika kwanza kwa mali zake kutaifishwa kabla ya mtu mwingine yoyote yule kuwajibishwa kwa uzembe alioutenda.Tulipaswa kuwa na sheria ya aina ili kutoa adhabu kwa chama kilichoshindwa ku-deliver na badala yake kulea wizi na ufisadi serikalini.
Wote hawa leo hii wanaojidai kuwa wakali walikuwepo ndani ya chama na serikali kwa miaka zaidi ya 20 lakini hawakujitoa ndani ya chama wala kukemea uchafu huu hadharani ili hali madudu haya yalikuwa yanafanyika na zaidi walikuwa mstari wa mbele kutetea serikali yao na kubeza wapinzani ndani na nje ya Bunge.
Nachojiuiliza haya mapenzi ya ghafla na nchii yametoka wapi?Baadhi ya mawaziri hawa wanaojidai kutumbua majibu leo hii siwalikuwepo katika serikali iliyopita mbona na hawakuchukua hatua yoyote?Waliokuwepo ndani ya chama na leo wako serikalini sio ndio hawa walikuwa vinara wa kusifia na kutetea utendaji wa serikali iliyopita?Haya wanayoyaona leo wakati wa Kikwete walikuwa vipofu?
Ukweli ni kwamba CCM ilistahili kutorudi madarakani na zaidi mali zake kutaifishwa na kupigwa mnada na fedha zitakazopatikana zipelekwe hazina kusaidia kutatua matatizo ya nchi hii japo mali zingine walizipata chini ya Mfumo wa Chama Kimoja na hivyo zinaweza kuwa ni mali ya umma.
Tanzania ingekuwa ni nchi ya Ulaya leo hii CCM ingekuwa bench na muda huu tungekuwa tuko kwenye uchunguzi mkubwa wa kashifa mbalimbali kama vile Kagoda,Deep green,EPA, Escrow,Meremeta, Vivuko vibovu,Uuzaji wa nyumba za serikali, n.k.Ila kwasabubu sisi ni Waafrika ndio maana leo hii tunashangilia chama kile kile na watu wale wale kujigeuza kuwa malaika pasipo hata kuhoji mbona wao wenyewe ndani ya chama chao hakuna anaewajibika licha ya uozo wote huu.
Waafrika ndivyo tulivyo!!!