Kweli serikali ya CCM ni SIKIVU,Imesikia na kulishghulikia kwa vitendo na kwa dhati sakata la IPTL,RICHMOND na mwanae DOWANS na mjuu SYMBION kapatikana si kwa najisi, kweli imesikia na kushughulikia sakata la KIWIRA na kwa manufaa ya umma aliejiuzia ameshashughulikiwa ipasavyo na sasa anajutia makosa aliyoyafanya.
Kweli imesikia na kuishughulikia kashfa ya UDA na kina Masaburi orignal wamewajibishwa,CCM jamani atakaebisha hatauona ufalme wa mbingu kama atasema serikali yake ni legelege wakati shule za Tanzania hakuna anaekaa chini kwa kukosa dawati,tena kwa shule zilizoko DAR wenyewe wanakalia viti vya miduu mitatu na nivyakuzunguka.
Kina mama huko mahospitalini wanapewa huduma bora na dawa za kumwaga maana hazina watumiaji,walimu nao wanapata mishara mikubwa tena kwa wakati,wakulima usiseme maana tangu singo ya kilimo kwanza kila mkulima ana power tila kama hana basi ni mtendaji wa kiji aua kata hivyo mashamba yake ni mshahara tu na takrima ambayo serikali sikivu iliihalalisha.
Jamani sitaki kubishana juu ya USIKIVU wa serikali ya CCM,nani hajui kama wakurugenzi na wahasibu huko kwenye halmashauri waliojaribu kwiba fedha za umma hawaja shitakiwa na wengine waliofanya hivyo miaka kama 5 hivi wanaozea jela?nami anabisha kwamba kila kukicha CGA hagundui matumizi mabaya ya fedha kwenye halmashauri na sasa hata idara zingine za serikali na adhabu KALIII! ya kuwahamisha idara au kumhamisha halmashauri? wapendwa huo sio usikivu wa serikali.
Huko kwa Maige watu walijifanya wajanja kwiba wanyama wetu lakini serikali sikivu yenye dola na yenye mkono mrefu ulionyooka mpaka nje ya mipaka na yenye Intelligencia iliyobobea tayari imeshabaini walipelekwa wapi na nani alihusika na tayari muda si mrefu umma utajulishwa na tutaruhusiwa kufanya maandamano ya kuwapokea Twiga wetu.
Serikali hii jamani ni sikivu anaebisha basi ana Malaria Sugu,kwani hata mauaji ya nyamongo kumbe wale walikuwa majambazi sugu na walikuwa wanajaribu kupambana na askari wao majambazi wakashindwa na ndio maana kuna vichaa wasio kuwa na akili walijaribu kutetea wezi wa dhahabu ya mzungu wakaswekwa ndani kwa manufaa ya umma na maiti za wezi wa dhahabu ya mzungu zikatupwa barabarani maana walifanya kosa kubwa la kumwibia mwekezaji.
Hata wale wana nchi waliodhurika na maji yenye sumu pamoja na mbwa kumbe ilikuwa ni wao tu walikuwa hawapendi kuoga ndo maana wakatoka mabaka lakini serikali sikivu imeaamua kuwalipa japo yenyewe si chanzo na ikaamua kuwapelekea maji safi na kutibu ngozi zao na za mbwa na ng'ombe wao,jamani nani bado anabisha serikali hii si sikivu?
Reli wanasema imekufa,ndege nazo za ATCL eti zimepungua wakati wa siku za nyuma Reli ilikuwa inabeba mizigo na abiria ndege nazo zilikuwa kumi na ngapi sijui wanajua hao wambea,lakini serikali sikivu ililisikia hilo ikamleta mhindi kwnye reli na sasa italeta reli ya umeme na dege zitashinda BA hata Fly Emirates hawatafua dafu.
Nani anasema serikali sikivu inabanbikizia watu kesi,wengine wanaomba wenyewe kwenda jela maana wanakuwa hawana hela ya unga na dagaa,sasa wakipelekwa huko kwa kusikiliza kilio chao utabisha sio sikivu?
Kwnza hakuna miradi hewa wala hakuna manunuzi hewa,hata ndege ya raisi ile tuliweka oder kiwandani ni Factory manufactured na hata Rada serikali ni sikivundio maana ilisahau kuchukua chenji na sasa iliwayuma watu kuifuata.Hao wazee wa iliyokuwa jumuia ya africa mashariki nao si imewasikiliza?
Zanzibar CUF nao wamelilia kuonja asali wkiwa serikalini si imewasikiliza? jamani ni mengi sana nanyi mtaongezea
Kwa hiyo hawa Chadema wanapotaka kuwashughulikia mafisadi,inapotaka haki na demokrasia ya kweli,wanapolalamikia rasilimali za taifa zitumike kwa manufaa ya umma, na wanapolalamika polisi kucheza game ya siasa na pale wanapoona Mahakama inakuwa-remoted na CCM si wana wabunge waambieni waende mjengoni kisha wakifika huko washindane kwa kura ya NDIO au HAPANA,kwa serikali ya CCM ni sikivu haitadhulumu mshindi wa kura nyingi zitakazoamriwa kwa SAUTI kubwa ya NDIO au HAPANA.
KATIBA nayo kuna viana harakati na hao CDMSerikali sikivu ilikubali juu kuandika katiba na sasa imeshaandika mswada na wao wote waliweka mapendekezo yao sasa tusubiri mjengoni,maana serikali sikivu inategemea maamuzi ya wengi,hivy mjengoni ni wawakilishi wa watanzania tusubiri kura ya NDIO au HAPANA.
TUIOMBEE SERIKALI SIKIVU IDUMU MPAKA WANANCHI WATAKAPOCHOKA RAHA NA STAREHE NA MAISHA BORA INAYOYAGAWA KWA
WATANZANIA.
Nawasilisha wakuu