Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,728
- 2,259
Unakumbuka CCM ilidai kuwa CHADEMA ni chama cha msimu, na kwa kupuuza hoja za CHADEMA ya Ufisadi na orodha ya watuhumiwa wa Ufisadi, wakati wa kampeni Kikwete akazunguka nchi nzima akikumbatiana na MAFISADI PAPA? Leo "mende kadondosha kabati" yule yule aliyekuwa akiwakumbatia Mafisadi Papa na kuwanyanyua mikono juu anadai MAFISAI HAO wanachafua taswira ya CCM.
CHADEMA ni chama kinachojisimamia na kubuni hoja zake ambazo ni endelevu kama ile ya Ufisadi, watuhumiwa wa Uifisadi ambazo zimekuwa zikiipeleka puta CCM since 2007. CHADEMA ilibuni na kusimamia hoja ya Katiba Mpya; kwa kuwa CCM is a reactive party ikarukia hoja hiyo japokuwa haipo katika Ilani yake ya Uchaguzi ya 2010. Based on those facts between CCM nad CHADEMA which is reactive party kila kinachobuni hoja zake au kile kinachoacha Ilani yake na kurukia hoja za chama kingine?
I think you have a good argument here Jatropha, but hii dhana ya kujivua gamba haikuanza sasa na mafisadi katika CCM.
Sijui kama unakumbuka enzi za KUNG'ATUKA katika uongozi wa chama miongo kadhaa iliyopita.
CCM inahistoria ya kujisahihisha bila kutibua wananchi na hili la sasa tulilitegemea baada ya makelele mengi.
Ni kweli kwamba sauti nzito na publicly katika siasa za karibuni zilianzia CDM na vyama vingine.
What I can tell you is, hivi karibuni CCM ni kama chombo kilichovamiwa na pirates, na wakaiteka nyara chombo hicho cha watu wengi ambao ni masikini.
Si kwamba wana CCM hawakuona matatizo haya, waliyaona mapema sana lakini ilikuwa nani amfunge paka kengele.
Mimi mwenyewe niltoa hoja ya kuwa chama tawala inaanzankukosa muelekeo na dira-and I was shouted down.
Tuache fikira ambazo mimi naona si za kizalendo, kufikiria it is either CCM or CHADEMA. Vyama vya upinzani vimefanya kazi nzuri tu ya kukiamsha chama na kukikumbusha muelekeo wake-na wamesikia.
Ufisadi haukuwagusa wana CDM tu katika jamii, bali kila mtanzania.
Na kwa hakika nitakuwa mnafiki nisipowapongeza wanaharakati,CDM na wengine wengikwa kampeni ya kuwaamsha CCM toka usingizi mzito wa kutekwa na mafisadi.
Yes sasa CCM wameamka , CDM itaingia usingizini, thats my view.
CDM hawana siasa inyoeleweka vile vile maana hata kama wataingia serikalini mpagilio wa wa kutatua mtatizo ya wananchi hawajaueleza bayana.
Na je CDM ni chama cha kibepari au kisoshalisti?na je juu ya umilikaji wa mali na ardhi wana maono gani?
Masuala ya kodi kwa biashara na wafanyakazi kwa maono ya CDM yakoje?
Hay ni mambo ya muhimu kwa watu kujua na si kukishabikia chama ambacho malengo yake hayajulikani baada ya kukamata dola.