CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

Hii ccm ya wala rushwa,ya watu kupigana hadi kuzimia kwenye kura ya maoni? Au una maana ya ccm ipi? Ni hii ya Escrow,EPA,Meremeta,Ujangili,madawa ya kulevya nk au una maanisha ccm ipi mkuu?
 
Mkuu hivi CCM ina wanachama wangapi as today? ....... na
  • inakuwaje na ukongwe wenu bado mnafanya chaguzi kwenye ndoo za Korie???
  • Ni chama kinachofuata maadili na kusimamia- Mmeyasimamia Kweli kwenye Kura za Maoni tumeona!
  • Unataka upinzani ujifunze tabia mbaya ya kuiba kura na rushwa mchana kweupe??
Hii ngoma haiuzi tena Jombaa.... soon mtaomba poa yaan wewe baadala ya kumtangaza Mgombea wako unaleta General Ngonjera zile zile za kila siku?:whoo:
 
UKAWA moto unawaka. CUF shitukieni hii la sivyo mtashindwa kupata hata Serikali ya mseto Zanzibar.

Mnapoteza nguvu nyingi sana kuwatangaza wapinzani kama hamjui ... wema wa mshumaa kuwamulikia wenzako wakati wewe unateketea
 
Hiyo ndio ccm mpya sio rahisi kuzaliwa upya labda kizazi hiki cha Mafisadi KIFE
 
CCM ni chama kikongwe na chenye nguvu kubwa barani Africa. Ni chama pekee chenye mikakati chanya na yenyetija ukilinanisha na vyama vingine vilivyoleta uhuru Tanzania.

Kwa muda mrefu chama hiki kimepitia katika kipindi kigumu sana na ilikuwa ni vigumu kukitakasa katika kipindi hicho. Kuna kitu Yesu alisema msiyang'oe magugu yaacheni yamee na ngano yakikomaa tutayaona. Kweli sasa hivi magugu yameonekana na lazima yatoke.

CCM sasa imeimarika na inakuwa na nguvu mpya katika uringo wa siasa Africa. Kimeonesha demokrasia iliyokomaa na kuwakumbusha watanzania maadli ndani ya chama ni muhimu sana. Yeyote anayekiuka maadili lazima awajibishwe kwa vitendo. Na pia ni fundisho katika vyama vichanga kama "CDM, CUF NCCR nk" vijifunze kutokana na CCM chama kilichosheheni watu waliosoma Political Science.

Baada ya makando kando kuanzakujiengua yenyewe sasa hivi CCM inaendelea kuwa safi na kuimarika zaidi. Vyama vya siasa Africa havina budi kujifunza kutoka CCM. Ni chama kinachofuata maadili na kusimamia. Heshima kwa Mzee Kinana kwa kukijenga chama na hakika tutazidi kuenzi miaka yote. Pia tunamuheshimu Ash Rose Migiro kwa kusimamia na kujenga chama na wengine wote ambao sijawataja.

CCM imejenga demokrasi kwenye nchi yetu, pomoja na kwamba vyama vya upinzani vimeshindwa kujifunza demokrasia miaka 20+ bado vinavyaa nepi. Viongozi wake wanalia lia tu na sasa wamegeuza vyama vya siasa kuwa biashara. Hii ni hali mbaya sana. Nawasihi vyama vya upinzani kuanzia mwaka 2016 muanze kujengwa vyama vyenu ili ifikapo mwaka 2035 muweze kusimamisha mgombea wenu mliyemjenga na muweze kushinda.

Chama kinapofikiria kusimamisha mgombea uraisi kijue kuwa Urais ni taasisi. Sasa iweje mtu mmoja na hamjawahi kukaa na kumjenga kufuata maadili na miiko ya chama chenu aje moja kwa moja paka chumbani? Lazima vyama vya upinzani vistep down mwaka huu kwenye urais na vijikite kwenye ubunge viweze kujijenga, la sivyo vitapoteza dira na kuchukua mda mrefu tena kujijenga.

CCM sasa hivi imetua mzigo mzito iliokuwa imeubeba, ule mtandao sasa umefutika na CCM imara imezaliwa mara ya pili na imetakaswa. CCM mathubuti aliyokuwa anaisema Mwalimu Nyerere ndio hii sasa. CCM Mathubuti sasa itatufanya kuvuka kwa kasi na kuendelea mbele. CCM mathubuti ndio hii italifanya bara la africa kujifunza.

Huu ni utakaso wa CCM ni utakaso wa Tanzania.
25 Oct 2015 CCM itashinda kwa kishindo
Kumbuka "Umoja ni Ushindi"

Kitakuwa kisafi tu majambazi woote watapukutika, majambazi sugu bado wapo ndani ya chama wanajificha bila hata ww mwanachama kujua (amka usingizini) kwa sasa ccm imeishushia hadhi nchi yetu ya tanzania, na kuwa nchi katika tano bora kwa ufisadi, sijui unachosifia nn ni ili na ww upate nafasi ya kuiba na kutufanya ss wtz kuwa mambulula kila wakati. Tumechoka na chama jangili kwa wananchi wake. Viongozi au sijui niseme ni majambazi unaowataja kuwa ni wazuri wamekuwa wakihujumu nchi yetu, wanauza rasilimali kwa bei ya karanga lakini watu wenye upungufu wa akili kama zako ambao wanahitaji kupelekwa milembe hospital wanakaa n kusifu wezi. Ulaaniwe na kama kuna jehanamu upelekwe huko. Ccm ni kama fisi aliyekabidhiwa bucha unategemea nn? Lazima tumuuwe fisi huyu ili bucha ipone.
 
kujadili post kama hii ni kupoteza muda ngoja nipitie post nyingine!
 
uzuri watu upofu umewashka alaf hawajui adui ni nani, na hata ukisema ccm au ukawa ni safi au mbaya watu hawaelewi...Propaganda za kizamani watu wamemeza na kuweka ushabiki mbele..Tumepigwa changa padogo tu Ccm,Cdm,Nld,Tlp nk ni taasisi.Ndo mana waliohujumu uchumi wanafungwa personally, hufungi chama unafunga mhalifu..Jiulize adui ni nani? ndo mana wapo wanaoamin kuwa slaa anahjajika japo cdm ipo kwakuwa sio cdm au ccm bila watu mahiri ndani.Kwahyo ni utoto kung'ang'ana na propaganda ya ccm ni adui huku waliofanya madudu wanahamia upinzani eti wanadai wanataka mabadiliko-ni uongo wanajificha tu -au ndo ile kuendekeza urafiki ,.Mi naamin ccm itabaki na watu waliotayar kuhukumiwa kwa waliyofanya, na naamini wanaobaki wanapenda kujadiliwa na sio kujificha kama wafanyavyo wahamiaji.CCM :REBORN wajanja wanatafta mpenyo mapema
 
[h=2]CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa[/h]
CCM ni chama kikongwe na chenye nguvu kubwa barani Africa. Ni chama pekee chenye mikakati chanya na yenyetija ukilinanisha na vyama vingine vilivyoleta uhuru Tanzania.

Kwa muda mrefu chama hiki kimepitia katika kipindi kigumu sana na ilikuwa ni vigumu kukitakasa katika kipindi hicho. Kuna kitu Yesu alisema msiyang'oe magugu yaacheni yamee na ngano yakikomaa tutayaona. Kweli sasa hivi magugu yameonekana na lazima yatoke.

CCM sasa imeimarika na inakuwa na nguvu mpya katika uringo wa siasa Africa. Kimeonesha demokrasia iliyokomaa na kuwakumbusha watanzania maadli ndani ya chama ni muhimu sana. Yeyote anayekiuka maadili lazima awajibishwe kwa vitendo. Na pia ni fundisho katika vyama vichanga kama "CDM, CUF NCCR nk" vijifunze kutokana na CCM chama kilichosheheni watu waliosoma Political Science.

Baada ya makando kando kuanzakujiengua yenyewe sasa hivi CCM inaendelea kuwa safi na kuimarika zaidi. Vyama vya siasa Africa havina budi kujifunza kutoka CCM. Ni chama kinachofuata maadili na kusimamia. Heshima kwa Mzee Kinana kwa kukijenga chama na hakika tutazidi kuenzi miaka yote. Pia tunamuheshimu Ash Rose Migiro kwa kusimamia na kujenga chama na wengine wote ambao sijawataja.

CCM imejenga demokrasi kwenye nchi yetu, pomoja na kwamba vyama vya upinzani vimeshindwa kujifunza demokrasia miaka 20+ bado vinavyaa nepi. Viongozi wake wanalia lia tu na sasa wamegeuza vyama vya siasa kuwa biashara. Hii ni hali mbaya sana. Nawasihi vyama vya upinzani kuanzia mwaka 2016 muanze kujengwa vyama vyenu ili ifikapo mwaka 2035 muweze kusimamisha mgombea wenu mliyemjenga na muweze kushinda.

Chama kinapofikiria kusimamisha mgombea uraisi kijue kuwa Urais ni taasisi. Sasa iweje mtu mmoja na hamjawahi kukaa na kumjenga kufuata maadili na miiko ya chama chenu aje moja kwa moja paka chumbani? Lazima vyama vya upinzani vistep down mwaka huu kwenye urais na vijikite kwenye ubunge viweze kujijenga, la sivyo vitapoteza dira na kuchukua mda mrefu tena kujijenga.

CCM sasa hivi imetua mzigo mzito iliokuwa imeubeba, ule mtandao sasa umefutika na CCM imara imezaliwa mara ya pili na imetakaswa. CCM mathubuti aliyokuwa anaisema Mwalimu Nyerere ndio hii sasa. CCM Mathubuti sasa itatufanya kuvuka kwa kasi na kuendelea mbele. CCM mathubuti ndio hii italifanya bara la africa kujifunza.

Huu ni utakaso wa CCM ni utakaso wa Tanzania.
25 Oct 2015 CCM itashinda kwa kishindo
Kumbuka "Umoja ni Ushindi"
​
 
Kumbe kuna watu hawajui kutofautisha kati ya kifo na kuzaliwa.
 
Sio kila mabadiliko ni chanya. Mabadiliko mnayotaka chadema na ukawa ni hasi kupindukia!!
Hatutaki kujuta kwanini tumechagua chama mbadala. Endeleeni kusubiri mlangoni!
 
ccm ilikuwa na maudhi sana hasa viongozi niliwahi kuwaona wenyeviti wa ccm mkoa kama singida shinyanga wakichukua vitu kwenye maduka makubwa hawalipi na kama wanalipa nusu nusu.
sasa navyowasikia wamehama ccm moyo wangu nazidi kuipenda sana ccm naona nafasi ya vijana wa leo wasomi wanapata nafasi.
akina lowasa masai feki (sio mtoto wa boma) wamehama vizuri sana.
na kuna kiongozi mmoja wa chama nilimuona kwa macho yangu akimkwida askari barabarani naye nasikia kahamia chadema bora
mungu ibariki ccm mungu ibariki tanzania
 
Kipindi CCM inaanzisha dhana ya kujivua gamba na kuwatosa mafisadi Wenye tuhuma vyama vya upinzani vilikuwa vikikebehi na kudai magamba yameshindwa kuwavuka.

Lakini hili wimbi la watuhumiwa wa ufisadi kuhamia upinzani na kusafishwa au kusamehewa dhambi za ufisadi wao linatia shaka,wimbo wa wapinzan umegeuka toka kwenye kupinga ufisadi mpaka kuondoa mfumo was ki CCM.

Kwa Lowasa kuingia CHADEMA ina maana mafisadi wenzake wote kama akina Karamagi wapo huko kiroho,upinzani umepoteza hoja na kupoteza misingi na uhalisia wake na ndio maana wajuvi kama akina Dr was ukweli Slaa na profesa Lipumba wamejiondoa kwenye nyadhifa zao.
 
Kipindi ccm inaanzisha dhana ya kujivua gamba na kuwatosa mafisadi Wenye tuhuma vyama vya upinzani vilikuwa vikikebehi na kudai magamba yameshindwa kuwavuka,lakini hili wimbi la watuhumiwa wa ufisadi kuhamia upinzani na kusafishwa au kusamehewa dhambi za ufisadi wao linatia shaka,wimbo wa wapinzan umegeuka toka kwenye kupinga ufisadi mpaka kuondoa mfumo was ki ccm,kwa lowasa kuingia chadema INA maana mafisadi wenzake wote kama akina karamagi wapo huko kiroho,upinzani umepoteza hoja na kupoteza misingi na uhalisia wake na ndio maana wajuvi kama akina Dr was ukweli Slaa na profesa lipumba wamejiondoa kwenye nyadhifa zao

Pathetic..!
 
Kumbuka unabii aliowahi kuutoa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa kweli wa kisiasa hapa nchini utatokea baada ya CCM kumeguka vipande vipande.

Huo unabii ndiyo umeanza kutimia kikamilifu mwaka huu, kwa kuwa kinachotokea hivi sasa la wimbi kubwa la makada wakubwa kabisa ndani ya CCM na kujiunga na upinzani ni dhahiri inaonyesha kuwa CCM inameguka vipande vipande.

Hata hivyo siyo kweli kuwa wote wanaotoka CCM ni mafisadi walokubuhu, hebu ipitie listi kama ya akina Lembeli, Esther Bulaya, Ole Madeye na wenyeviti kadhaa wa CCM wa mikoa.

Hata hivyo huyo uliyemtaja Karamagi vyombo vya habari vimemripoti kuwa amejiunga na CUF.

Vile vile ifahamike kuwa kinacholiumiza sana Taifa hili kwa sasa ni mfumo uliolelewa na CCM kwa nyakati hizi wa ufisadi.

Kwa maana hiyo basi hata kwenye vitabu vya dini maandiko yanasema kuwa mtu anayetubu dhambi zake hata kama dhambi zake zilikuwa nyekundu zitatakaswa na kuwa nyeupe kama theluji.

Hlo wimbi la maccm linapoingia Chadema hao watu wanatubu dhambi zao za ufisadi na wanazaliwa upya katika mfumo mpya.

Kwa hiyo lililo la umuhimu kwa Taifa hili kwa sasa ni kuundoa mfumo wa ufisadi wa CCM uliolelewa kwa kipindi kirefu, kupitia sanduku la kura ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
 
Back
Top Bottom