CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

CCM imeanza kuzaliwa upya na kutakaswa

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,965
CCM ni chama kikongwe na chenye nguvu kubwa barani Africa. Ni chama pekee chenye mikakati chanya na yenyetija ukilinanisha na vyama vingine vilivyoleta uhuru Tanzania.

Kwa muda mrefu chama hiki kimepitia katika kipindi kigumu sana na ilikuwa ni vigumu kukitakasa katika kipindi hicho. Kuna kitu Yesu alisema msiyang'oe magugu yaacheni yamee na ngano yakikomaa tutayaona. Kweli sasa hivi magugu yameonekana na lazima yatoke.

CCM sasa imeimarika na inakuwa na nguvu mpya katika uringo wa siasa Africa. Kimeonesha demokrasia iliyokomaa na kuwakumbusha watanzania maadli ndani ya chama ni muhimu sana. Yeyote anayekiuka maadili lazima awajibishwe kwa vitendo. Na pia ni fundisho katika vyama vichanga kama "CDM, CUF NCCR nk" vijifunze kutokana na CCM chama kilichosheheni watu waliosoma Political Science.

Baada ya makando kando kuanzakujiengua yenyewe sasa hivi CCM inaendelea kuwa safi na kuimarika zaidi. Vyama vya siasa Africa havina budi kujifunza kutoka CCM. Ni chama kinachofuata maadili na kusimamia. Heshima kwa Mzee Kinana kwa kukijenga chama na hakika tutazidi kuenzi miaka yote. Pia tunamuheshimu Ash Rose Migiro kwa kusimamia na kujenga chama na wengine wote ambao sijawataja.

CCM imejenga demokrasi kwenye nchi yetu, pomoja na kwamba vyama vya upinzani vimeshindwa kujifunza demokrasia miaka 20+ bado vinavyaa nepi. Viongozi wake wanalia lia tu na sasa wamegeuza vyama vya siasa kuwa biashara. Hii ni hali mbaya sana. Nawasihi vyama vya upinzani kuanzia mwaka 2016 muanze kujengwa vyama vyenu ili ifikapo mwaka 2035 muweze kusimamisha mgombea wenu mliyemjenga na muweze kushinda.

Chama kinapofikiria kusimamisha mgombea uraisi kijue kuwa Urais ni taasisi. Sasa iweje mtu mmoja na hamjawahi kukaa na kumjenga kufuata maadili na miiko ya chama chenu aje moja kwa moja paka chumbani? Lazima vyama vya upinzani vistep down mwaka huu kwenye urais na vijikite kwenye ubunge viweze kujijenga, la sivyo vitapoteza dira na kuchukua mda mrefu tena kujijenga.

CCM sasa hivi imetua mzigo mzito iliokuwa imeubeba, ule mtandao sasa umefutika na CCM imara imezaliwa mara ya pili na imetakaswa. CCM mathubuti aliyokuwa anaisema Mwalimu Nyerere ndio hii sasa. CCM Mathubuti sasa itatufanya kuvuka kwa kasi na kuendelea mbele. CCM mathubuti ndio hii italifanya bara la africa kujifunza.

Huu ni utakaso wa CCM ni utakaso wa Tanzania.
25 Oct 2015 CCM itashinda kwa kishindo
Kumbuka "Umoja ni Ushindi"
 
Annael wewe si ndio muumini mkubwa wa falsafa ya hakuna Mungu??

Wewe si ndio wajifanya hakuna Yesu...Mungu wala kiyama wala utakaso??

Kitu gani umeandika hapo?? unakumbuka kwenye nyuzi zako nimewahi kukwambia wewe ni mpuuzi tu kama wengine??

Ha ha yaani CCM ndo imefikia kuwatumia watu kama nyinyi wenye mafundisho ya kishetani kuwatetea?? ndio maana CCM inafanyia ukatili wakutisha raia zake coz inaongozwa na kutetewa na watu wenye mrengo wa shetani kama wewe....

Kama ni huo utakaso waambie CCM wafukuze watu hawa wafuatao....

1. Jakaya Mrisho Kikwete (ESCROW...RICHMOND)

2.Benjamin William Mkapa (EPA...NBC....TANGOLD...MEREMETA)

3.Abdulrahman Kinana (ujangili wa pembe za ndovu)

4.Benard Membe (mabilioni ya gaddafi)

5. Anna Tibaijuka (ESCROW)

6.Mhongo (ESCROW)

Wapo wengi sana ambao nyie vidampa mmezibwa macho kuwaona fukuzeni hao tuone utakaso ukikamilika Kima wewe....
 
Last edited by a moderator:
Tatizo la BAVICHA hawasomi alama za nyakati. Mnamengi sana ya kujifunza toka CCM ili angalau muweze kusonga mbele. Mwaka 2010 tulifanya makosa makubwa sana, na hatuwezi kuyarudia. Mwaka huu utaona fimbo tutakazo wachapa.

CCM imeimarika mara dufu. Inabidi mtulie tu muweze kujipanga upya. La sivyo CDM itapotea kabisa na kujikuta ACT inakuja juu.
 
Kwa jinsi mlivyotuelekeza namna ya kutoa rushwa,kupigana ndiyo mnataka tuige?Pole wale wote waliotoa HONGO ndiyo hao wanapetea,waliopiga wengine nao wanapeta duh chezea CCM kweli kwenye RUSHWA halina mpinzani
 
Nina wahakikishieni vyama vya upinzani hususana vinavyounda UKAWA kama mtang'ang'ania mwaka huu. Nina uhakika mwaka 2016 mtaanza "0" na kujakuyafikia aghalau mafanikio mliyoyapata mika 20+ itawachukua miongo mingi au mnaweza mkapotea kabisa na kuwakatisha wananchi juua ya vyama vya upinzani.
 
Tofauti kubwa sana iliyopo kati ya CCM na vyama vingine ni kuwa CCM haiwezi kununuliwa na mtu.

Kuna vyama vimenunuliwa na vimeuza nafasi za kugombea urais, jambo ambalo CCM ililikataa ikamkata mtu anayetaka kununua ikulu.

Ikulu sio biashara...
 
Mambo tunayoyashuhudia kwenye kura za maoni hayaonyeshi hilo.
 
Tatizo la BAVICHA hawasomi alama za nyakati. Mnamengi sana ya kujifunza toka CCM ili angalau muweze kusonga mbele. Mwaka 2010 tulifanya makosa makubwa sana, na hatuwezi kuyarudia. Mwaka huu utaona fimbo tutakazo wachapa.

CCM imeimarika mara dufu. Inabidi mtulie tu muweze kujipanga upya. La sivyo CDM itapotea kabisa na kujikuta ACT inakuja juu.

1. Huu uongo na maneno matamu ndio kifo chenyewe, hali hii kweli unaweza sema kuna kuimarika??!!
2. Muda sio rafiki tena, wananchi wameamka saaana wanajua na wanahoji sana mambo madogo na makubwa. . . . .mishipa yao ya fahamu inapokea maumivu kwa ufasaha kuliko kipindi kingine chochote, akili zinafanya kazi vizuri na bila uoga. . . .
3. Kuzaliwa upya sio mbaya lakini itawaambia nini watu waliokaomaa kwa maumivu na hasira??!!

Wako wapi warithi makini wasio na uchu??!! Wako wapi wanaoweka nchi kwanza maslahi yao baadae??!!

Tanzania mama yangu. . . . .
 
Anael mambo vipi naona umeibuka na hoja dhaifu juu ya magamba na kwa kusikitika huamini kwamba ccm itakufa mwaka huu oktoba unajidai eti kuwapa moyo upinzani na kuwashauri kujijenga upya unadhani hawajakomaa kisiasa upinzani. Kiufupi wananchi tumechoka ccm must step down na hata mkitumia bao la mkono mwaka huu hampati kitu
 
Muda huu naona mnawaza namna ya kuiba kura tu, hamna mbinu nyingine ya ziada.
 
Kila kitu ni bora na safi kwa mtu mwenyewe, tungepata kigezo huru ingekuwa heri
 
Annael wewe si ndio muumini mkubwa wa falsafa ya hakuna Mungu??

Wewe si ndio wajifanya hakuna Yesu...Mungu wala kiyama wala utakaso??

Kitu gani umeandika hapo?? unakumbuka kwenye nyuzi zako nimewahi kukwambia wewe ni mpuuzi tu kama wengine??

Ha ha yaani CCM ndo imefikia kuwatumia watu kama nyinyi wenye mafundisho ya kishetani kuwatetea?? ndio maana CCM inafanyia ukatili wakutisha raia zake coz inaongozwa na kutetewa na watu wenye mrengo wa shetani kama wewe....

Kama ni huo utakaso waambie CCM wafukuze watu hawa wafuatao....

1. Jakaya Mrisho Kikwete (ESCROW...RICHMOND)

2.Benjamin William Mkapa (EPA...NBC....TANGOLD...MEREMETA)

3.Abdulrahman Kinana (ujangili wa pembe za ndovu)

4.Benard Membe (mabilioni ya gaddafi)

5. Anna Tibaijuka (ESCROW)

6.Mhongo (ESCROW)

Wapo wengi sana ambao nyie vidampa mmezibwa macho kuwaona fukuzeni hao tuone utakaso ukikamilika Kima wewe....

Mkuu hapo umemsahau nyoka mwenye makengeza(Chenge) alipiga zote izo, ila kura za maoni bado yupo anadunda sjui hyo ccm ya mafisadi imebadilikia wapi. ccm ni pango la wezi,mafisadi,wachawi,wanafk,wapiga deal,maharamia,na wauza madawa ya kulevya.
 
Annael wewe si ndio muumini mkubwa wa falsafa ya hakuna Mungu??

Wewe si ndio wajifanya hakuna Yesu...Mungu wala kiyama wala utakaso??

Kitu gani umeandika hapo?? unakumbuka kwenye nyuzi zako nimewahi kukwambia wewe ni mpuuzi tu kama wengine??

Ha ha yaani CCM ndo imefikia kuwatumia watu kama nyinyi wenye mafundisho ya kishetani kuwatetea?? ndio maana CCM inafanyia ukatili wakutisha raia zake coz inaongozwa na kutetewa na watu wenye mrengo wa shetani kama wewe....

Kama ni huo utakaso waambie CCM wafukuze watu hawa wafuatao....

1. Jakaya Mrisho Kikwete (ESCROW...RICHMOND)

2.Benjamin William Mkapa (EPA...NBC....TANGOLD...MEREMETA)

3.Abdulrahman Kinana (ujangili wa pembe za ndovu)

4.Benard Membe (mabilioni ya gaddafi)

5. Anna Tibaijuka (ESCROW)

6.Mhongo (ESCROW)

Wapo wengi sana ambao nyie vidampa mmezibwa macho kuwaona fukuzeni hao tuone utakaso ukikamilika Kima wewe....

Hahaaaa
Mwanbie huyo

Team escrow wote wameshinda!. Sijui anataka kutuambia nn
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom