Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Uchakachuaji.
Neno hili litakaa sana vichwani mwetu na kukumbukwa kwa muda mrefu sana na itakuwa vigumu sana kwa CCM kujivua mapokeo mabaya ya neno hili.
Ni uroho wa madaraka, uchu wa kutawala, ulafi kutopenda kujisafisha na kuwasikiliza Watanzania na hata wanachama wake, ndio maana CCM imejibebesha msalaba wa Uchakachuaji ambao si kwa kuiba kura tuu, bali kutumia ubabe kama kule Mwanza waliko dai "Kaza Buti" hata kwa nguvu ushindi ni lazima na hata kuharuibu mfumo mzima wa uchaguzi kwa kujenga mazingira mabovu na ya kizembe kuendesha uchaguzi.
Uchaguzi wa mwaka huu uliendeshwa kwa manufaa ya CCM na si ya Watanzania!
Uhuni wote uliofanyika ikiwa ni pamoja na kukiukwa kwa kanuni na hata sheria, kulifanywa kwa makusudi kutokana na tamaa na uchu wa madaraka na kule kujiona CCM pekee ndio yenye kustahili kuongoza nchi.
Sikatai isingekuwa rahisi kwa upinzani kushinda kwa ukamilifu, lakini uharamia wa CCM ulihakikisha kuwa hata ndani ya CCM yenyewe, sauti za wanachama zinapuuzwa na matakwa ya wachache walioko katika uongozi na mamlaka ya chama yanatimia.
Nikianzia mchakato wa kugombea nafasi za kuwa wagombea wa CCM, si siri kulifanyika uharamia wa hali ya juu ulioongozwa na baadhi ya viongozi wa kuu wa CCM na ni kitu kilichofikia kuleta mgongano na mpasuko ndani ya CCM. KWa wapinzani hili lilikuwa ni jema na ndio maana majimbo mengi yameweza kwenda kwa Upinzani kutokana na msuguano huo.
CCM Lumumba, haikutaka kuwasikiliza Watanzania hata wanachama wake. Ni hii imeonekana wazi jinsi rushwa ilivyotembea ndani ya CCM yenyewe, kutegeana mitego ya kuhujumiana na walipomaliza safu ya ndani ya Chama chao, wakahamia katika Taifa.
Katika ngazi ya Taifa, CCM imetumia Uchakachuaji kwa kutumia dola na mamlaka zingine kuhakikisha kuwa haipotezi dhamana ya kuongoza Tanzania. Badala ya kuiba kura kama kawaida, safari hii mazingira ya upigaji kura na uchaguzi yalirubuniwa (compromised) hata pamoja na kuwa Upinzani ulikuwa na udhaifu.
Kinana ametoa kauli kuwa "kura za Maoni" zimekiponza CCM na kukifanya kipoteze majimbo. Lakini si kweli.
Kwenye majimbo, wanachama wa CCM walichagua watu wanaowataka, badala ya wao kama ngazi ya Taifa kuheshimu kauli na uchaguzi wa wanachama kwenye majimbo, Wakachakachua na kuweka watu wao.
Zaidi ni kule kupandikizwa kwa mvutano wa makundi yanayogombea madaraka ndani ya CCM katika ngazi ya Taifa ambako kulifikia hatua ya kukipasua chama na kujengeana uhasama.
Lakini ni lini CCM na kwa nini CCM imacha kusikiliza sauti ya Watanzania na hata wanachama wake?
Ushindi wa CCM si kwa manufaa ya Watanzania bali kwa manufaa yao wenyewe na taratibu Watanzania na hata wana CCM wenyewe wameanza kung'amua hilo.
Ukweli ni kuwa ni uroho huu ambao umefikia kwa CCM kushindwa kujenga mazingira bora kwa Demokrasia achilia mbali mazingira bora kwa ustawi na maisha ya Mtanzania. Ushindi wao si wa kujivunia au kujitapa kuwa ni mafanikio ya kazi nzuri, bali ni kitu cha aibu kutokana na mchakato mzima ulivyofanyika.
Kidole hakiendi mbali wala kuangalia mbali bali ni kwenye uongozi!
Pamoja na ushindi wao, bado CCM ina uongozi mbovu na kama somo la mwaka huu halijakolea masikioni na kwenye ubongo wao, waendelee kupuuza kauli za Watanzania na kilichotokea mwaka huu ni trela, sinema inakuja 2015.