CCM ijifunze kuheshimu Kauli za Watu

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Uchakachuaji.

Neno hili litakaa sana vichwani mwetu na kukumbukwa kwa muda mrefu sana na itakuwa vigumu sana kwa CCM kujivua mapokeo mabaya ya neno hili.

Ni uroho wa madaraka, uchu wa kutawala, ulafi kutopenda kujisafisha na kuwasikiliza Watanzania na hata wanachama wake, ndio maana CCM imejibebesha msalaba wa Uchakachuaji ambao si kwa kuiba kura tuu, bali kutumia ubabe kama kule Mwanza waliko dai "Kaza Buti" hata kwa nguvu ushindi ni lazima na hata kuharuibu mfumo mzima wa uchaguzi kwa kujenga mazingira mabovu na ya kizembe kuendesha uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka huu uliendeshwa kwa manufaa ya CCM na si ya Watanzania!

Uhuni wote uliofanyika ikiwa ni pamoja na kukiukwa kwa kanuni na hata sheria, kulifanywa kwa makusudi kutokana na tamaa na uchu wa madaraka na kule kujiona CCM pekee ndio yenye kustahili kuongoza nchi.

Sikatai isingekuwa rahisi kwa upinzani kushinda kwa ukamilifu, lakini uharamia wa CCM ulihakikisha kuwa hata ndani ya CCM yenyewe, sauti za wanachama zinapuuzwa na matakwa ya wachache walioko katika uongozi na mamlaka ya chama yanatimia.

Nikianzia mchakato wa kugombea nafasi za kuwa wagombea wa CCM, si siri kulifanyika uharamia wa hali ya juu ulioongozwa na baadhi ya viongozi wa kuu wa CCM na ni kitu kilichofikia kuleta mgongano na mpasuko ndani ya CCM. KWa wapinzani hili lilikuwa ni jema na ndio maana majimbo mengi yameweza kwenda kwa Upinzani kutokana na msuguano huo.

CCM Lumumba, haikutaka kuwasikiliza Watanzania hata wanachama wake. Ni hii imeonekana wazi jinsi rushwa ilivyotembea ndani ya CCM yenyewe, kutegeana mitego ya kuhujumiana na walipomaliza safu ya ndani ya Chama chao, wakahamia katika Taifa.

Katika ngazi ya Taifa, CCM imetumia Uchakachuaji kwa kutumia dola na mamlaka zingine kuhakikisha kuwa haipotezi dhamana ya kuongoza Tanzania. Badala ya kuiba kura kama kawaida, safari hii mazingira ya upigaji kura na uchaguzi yalirubuniwa (compromised) hata pamoja na kuwa Upinzani ulikuwa na udhaifu.

Kinana ametoa kauli kuwa "kura za Maoni" zimekiponza CCM na kukifanya kipoteze majimbo. Lakini si kweli.

Kwenye majimbo, wanachama wa CCM walichagua watu wanaowataka, badala ya wao kama ngazi ya Taifa kuheshimu kauli na uchaguzi wa wanachama kwenye majimbo, Wakachakachua na kuweka watu wao.

Zaidi ni kule kupandikizwa kwa mvutano wa makundi yanayogombea madaraka ndani ya CCM katika ngazi ya Taifa ambako kulifikia hatua ya kukipasua chama na kujengeana uhasama.

Lakini ni lini CCM na kwa nini CCM imacha kusikiliza sauti ya Watanzania na hata wanachama wake?

Ushindi wa CCM si kwa manufaa ya Watanzania bali kwa manufaa yao wenyewe na taratibu Watanzania na hata wana CCM wenyewe wameanza kung'amua hilo.

Ukweli ni kuwa ni uroho huu ambao umefikia kwa CCM kushindwa kujenga mazingira bora kwa Demokrasia achilia mbali mazingira bora kwa ustawi na maisha ya Mtanzania. Ushindi wao si wa kujivunia au kujitapa kuwa ni mafanikio ya kazi nzuri, bali ni kitu cha aibu kutokana na mchakato mzima ulivyofanyika.

Kidole hakiendi mbali wala kuangalia mbali bali ni kwenye uongozi!

Pamoja na ushindi wao, bado CCM ina uongozi mbovu na kama somo la mwaka huu halijakolea masikioni na kwenye ubongo wao, waendelee kupuuza kauli za Watanzania na kilichotokea mwaka huu ni trela, sinema inakuja 2015.
 
Umesema kweli Rev. Tumepata msamiati mpya, na daima neno 'uchakachuaji' litahusishwa na ccm. Wengi hawatakumbuka kuwa neno hilo lilitokana na mtindo wa dansi wa Urafiki Jazz katika miaka ya 70!
 
Dingswayo,

Ulevi ni kitu kibaya, na hawa jamaa wa CCM wamelewa chakari madaraka mithili ya yule aliyekunywa pombe ya Pingu!
 
Nawaombea wahusika wote wanaoandaa uhuni huu wafe kabla ya 2015 waishe na itakuwa hivyo

hapo kwenye bluu naungana na wewe kabisa......lakini bila kuingia kwa style ya imani zaidi haitafaa.....hata maandiko yanaruhusu ya kwamba mchawi na afe....hata Jericho iliangushwa bana
 
CCM will remain to be overconfident until the day they are out of power. This years election may bring CCM down to earth for a while but I guarantee you after surviving this "tsunami" in a while they may start to feel invisible again, maybe more invisible then they have ever been? It is up to the opposition parties now to continue the pressure and never give CCM the chance to forget these elections. The ball is now on the opposition side of the court. Kazi kwao.
 
Uchakachuaji.

Neno hili litakaa sana vichwani mwetu na kukumbukwa kwa muda mrefu sana na itakuwa vigumu sana kwa CCM kujivua mapokeo mabaya ya neno hili.

Ni uroho wa madaraka, uchu wa kutawala, ulafi kutopenda kujisafisha na kuwasikiliza Watanzania na hata wanachama wake, ndio maana CCM imejibebesha msalaba wa Uchakachuaji ambao si kwa kuiba kura tuu, bali kutumia ubabe kama kule Mwanza waliko dai "Kaza Buti" hata kwa nguvu ushindi ni lazima na hata kuharuibu mfumo mzima wa uchaguzi kwa kujenga mazingira mabovu na ya kizembe kuendesha uchaguzi.

Uchaguzi wa mwaka huu uliendeshwa kwa manufaa ya CCM na si ya Watanzania!

Uhuni wote uliofanyika ikiwa ni pamoja na kukiukwa kwa kanuni na hata sheria, kulifanywa kwa makusudi kutokana na tamaa na uchu wa madaraka na kule kujiona CCM pekee ndio yenye kustahili kuongoza nchi.

Sikatai isingekuwa rahisi kwa upinzani kushinda kwa ukamilifu, lakini uharamia wa CCM ulihakikisha kuwa hata ndani ya CCM yenyewe, sauti za wanachama zinapuuzwa na matakwa ya wachache walioko katika uongozi na mamlaka ya chama yanatimia.

Nikianzia mchakato wa kugombea nafasi za kuwa wagombea wa CCM, si siri kulifanyika uharamia wa hali ya juu ulioongozwa na baadhi ya viongozi wa kuu wa CCM na ni kitu kilichofikia kuleta mgongano na mpasuko ndani ya CCM. KWa wapinzani hili lilikuwa ni jema na ndio maana majimbo mengi yameweza kwenda kwa Upinzani kutokana na msuguano huo.

CCM Lumumba, haikutaka kuwasikiliza Watanzania hata wanachama wake. Ni hii imeonekana wazi jinsi rushwa ilivyotembea ndani ya CCM yenyewe, kutegeana mitego ya kuhujumiana na walipomaliza safu ya ndani ya Chama chao, wakahamia katika Taifa.

Katika ngazi ya Taifa, CCM imetumia Uchakachuaji kwa kutumia dola na mamlaka zingine kuhakikisha kuwa haipotezi dhamana ya kuongoza Tanzania. Badala ya kuiba kura kama kawaida, safari hii mazingira ya upigaji kura na uchaguzi yalirubuniwa (compromised) hata pamoja na kuwa Upinzani ulikuwa na udhaifu.

Kinana ametoa kauli kuwa "kura za Maoni" zimekiponza CCM na kukifanya kipoteze majimbo. Lakini si kweli.

Kwenye majimbo, wanachama wa CCM walichagua watu wanaowataka, badala ya wao kama ngazi ya Taifa kuheshimu kauli na uchaguzi wa wanachama kwenye majimbo, Wakachakachua na kuweka watu wao.

Zaidi ni kule kupandikizwa kwa mvutano wa makundi yanayogombea madaraka ndani ya CCM katika ngazi ya Taifa ambako kulifikia hatua ya kukipasua chama na kujengeana uhasama.

Lakini ni lini CCM na kwa nini CCM imacha kusikiliza sauti ya Watanzania na hata wanachama wake?

Ushindi wa CCM si kwa manufaa ya Watanzania bali kwa manufaa yao wenyewe na taratibu Watanzania na hata wana CCM wenyewe wameanza kung'amua hilo.

Ukweli ni kuwa ni uroho huu ambao umefikia kwa CCM kushindwa kujenga mazingira bora kwa Demokrasia achilia mbali mazingira bora kwa ustawi na maisha ya Mtanzania. Ushindi wao si wa kujivunia au kujitapa kuwa ni mafanikio ya kazi nzuri, bali ni kitu cha aibu kutokana na mchakato mzima ulivyofanyika.

Kidole hakiendi mbali wala kuangalia mbali bali ni kwenye uongozi!

Pamoja na ushindi wao, bado CCM ina uongozi mbovu na kama somo la mwaka huu halijakolea masikioni na kwenye ubongo wao, waendelee kupuuza kauli za Watanzania na kilichotokea mwaka huu ni trela, sinema inakuja 2015.

Kwanza nakupongeza kwa uamuzi wako wa busara, unajua nina maana gani. Pili Ninataka kukupa asante ila naomba uhariri hapo nilipoonyesha nyekundu andika kuchakachua ndio neno linalofaa kutokana na ujumbe uliondika kwa sababu kuchakachua hakuwezi kuwa ushindi. Ukishahariri nami nitaondoa hii posti yangu na kukupa asante
 
Nawaombea wahusika wote wanaoandaa uhuni huu wafe kabla ya 2015 waishe na itakuwa hivyo

hapo kwenye bluu naungana na wewe kabisa......lakini bila kuingia kwa style ya imani zaidi haitafaa.....hata maandiko yanaruhusu ya kwamba mchawi na afe....hata Jericho iliangushwa bana

HAPANA NDUGU, TUSIOMBEANE MAAFA. HATA MITUME HAWAKUTAKA waovu wafe katika vizazi vyao. waliomba waendelee kuishi ili wapate nuru ya wokvu na kubaki kuwa ushuhuda hai ili wapate kuzaa matunda mengi.

ni uchungu wa kitambo tu utaisha, na neno "uchakachuaji" ni msamiati tu wa msimu nao utapita. leo unahusishwa na CCM ni kwa sababu CCM iko madarakani, kwa hiyo hakuna ubaya, muhimu kuzishughulikia changamoto zilizojtokeza kwenye uchaguzi huu tusonge mbele.

Mungu atubariki sote
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Hicho kisingizio cha kuombeana amani ndio kinawapa kiburi..... wao wanacheza rafu watuwakilalamika ooh nchi yetu ya amani. Kama kweli mnapenda amani kwanini msiache uchaguzi uwe wa huru. Sikuwahi kudhani CCM itaniudhi zaidi nilivyokuwa nawachukia lakini mwaka huummeboooa zaidi. Hicho kisingizio cha amani mkifikirie nyie kwanza......
 
HAPANA NDUGU, TUSIOMBEANE MAAFA. HATA MITUME HAWAKUTAKA waovu wafe katika vizazi vyao. waliomba waendelee kuishi ili wapate nuru ya wokvu na kubaki kuwa ushuhuda hai ili wapate kuzaa matunda mengi.

ni uchungu wa kitambo tu utaisha, na neno "uchakachuaji" ni msamiati tu wa msimu nao utapita. leo unahusishwa na CCM ni kwa sababu CCM iko madarakani, kwa hiyo hakuna ubaya, muhimu kuzishughulikia changamoto zilizojtokeza kwenye uchaguzi huu tusonge mbele.

Mungu atubariki sote
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Nasema tena nawaombea wale wote wanaojihusisha na maafa ya nchi hii kwa udanganyifu WAFE kabla ya mwaka 2015. Ni kitu kigumu lakini itanibidi niumie kwa kufunga muda mrefu na kuomba. Na majibu ni obvious. Chaguzi ndogo haziko mbali. Kama hujahusika usiwe na wasi wasi, utapeta hadi 2015 si hivyo subiri ukutane na mkono wa Mungu aliye hai.
 
Mwomba janga ula na ndg zake. naungana na wale waonao ukweli wa mambo. kwanini hamtwambii musoma, mwanza, nyamagana, arusha, moshi mjini, kawe, ubungo nk yale majimbo ambayo mmepata kwamba ndo uchaguzi ulikuwa mbovu bali waloshinda ccm ndo uchakachuaji ulifanya kazi??? jamani kumbuka nyie ni wachanga na mchezo wa siasa bado mnajifunza. CCM haijaiba kura bali wananchi wa sehemu hizo ilipotwaa ushindi hawadanganyiki na helkopta na uwongo wa mchana kweupe. Ebu angalia kiongozi wa nchi mtarajiwa anadanganya watu wazima na akili zao mchana kweupe ohoo mbeya wamekamata gari yenye kura za ccm, oohoo mwanza kikao kilipanga mkakati wa wizi je musoma walikaa hoteli gani, tarime, monduli nk??? acha hizo ndg zangu kubali mmeshindwa uchaguzi longolongo hazifai.
 
There should be no room for complancency among the opposition parties, particularly to the party for democracy and social progress (Chadema) and the Civic United Front (CUF), Which have in these elections proven to be a thorny and a force to reckon with to the ruling CCM,Now i would suggest the opposition camp, after the just ended general elections, to intensify their penetration in the rural areas.Operesheni Sangara, for instance, should be re-launched and make sure inafika kwa majimbo yote 239 ya uchaguzi.NGOs nazo ziendeleze elimu ya uraia (civic education) ili watu wazidi kupata mwamko zaidi umuhimu wa kuweka viongozi wachapa kazi na waadilifu kwa ajili ya nchi yetu.Wale wababaishaji walioshinda mwaka huu kwa corruption au ujanja, basi wajue in the year 2015 watu watakuwa wameamka zaidi and their weak and dysfunctional political leadership will and for sure must come to the end.
 
Taratibu wana-CCM wanaanza kugundua kuwa wanatumika kuwafaidisha mafisadi.

' ... wao wana pesa, sisi tuna Mungu ... ' (Godbless Lema, MB)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom