Sasa hapo amechangia nini?
Ikiwa ameona haijaenda shule basi na alete yake kama hawezi kaa kimya kuliko kusema haijaenda shule.
Naomba nieleweke kwa yafuatayo:
1.CHADEMA KUTOMTAMBUA RAIS KIKWETE
Kwa hili naona halijaeleweka sawia,kwanza hoja ya msingi ya CHADEMA siyo kutomtambua rais
Bali ni kutokubali matokeo yaliyomuweka rais huyo madarakani.Ikumbukwe kuwa hoja hii ililetwa siku ya tatu ya kutangaza matokeo ambapo mgombea urais Kupitia CHADEMA mh.Slaa aliitaka tume kusitisha utangazaji wa matokeo hayo,kama kweli NEC ingekuwa tume ya haki kwa vyama vyote ingekubali kupitia kwa makini hoja ya mh.Slaa Kabla ya kumtangaza mshindi wa urais.Hapo ndipo ugomvi wa kikatiba unapoibuka.Kwa katiba ya sasa Mshindi wa urais hawezi kutenguliwa baada ya kuapishwa.Swali ni je kwanini hoja ya Slaa ilipuuzwa ilhali vielelezo muhimu alikuwa navyo kabla?
2.KUTOKA NJE YA BUNGE
Hili vyombo vingi vya habari vimeandika kuwa CHADEMA imemsusa rais kwa tafsiri ya kuwa haimtambui.Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA ambaye ndiye kiongozi mkuu wa upinzani mh.Freeman Mbowe amelitolea maelezo kuwa ni shinikizo la kuvunja tume ya sasa ya uchaguzi na kuundwa kwa tume mpya ambayo itakuwa inajiendesha kwa uhuru na kwa haki kwa chaguzi zijazo na katiba mpya,tume ya sasa chini ya Lewis Makame iliundwa kwa parliamentary act ya mwaka 1971 ambayo inafuata mfumo wa chama kimoja cha siasa ndo maana tumeyaona yaliyotokea kwenye uchaguzi wa oct 31
Najaribu ku think critically kwanini vyombo vya habari vime report kwajinsi hiyo hata baada ya maelezo kutolewa na CHADEMA mara kadhaa? My interpretation is kama CCM ina influence na vyombo vingi vya habari; Je then sikwamba ni rahisi kwa CCM kudeal na CHADEMA kuukataa uraisi uliopo kuliko agenda ya Tume huru na Katiba mpya? Why kwasababu agenda ya pili public inakuwa united na ile ya kwanza division ni obviousy kwani ni rahisi kwa agenda ya kwanza CCM kuja na spining ya violence na kuleta division au hata kuwa na sababu tosha yakutumia nguvu kuzima hii hoja! Ama kweli siasa ya hitaji uwe smart kweli kweli ama sivyo inakula kwako!
CHADEMA men you have to be smart and play intelligently in this; kwepeni kabisa hiyo mitego yakupelekwa kwenye hilo la kwanza na mconcetrate na agenda ya tume huru na katiba mpya ili mpate public support ambayo nihitaji la wazalendo wote.
hii itakuwa si mada ya kuhoji kutangazwa "kwake" itakuwa ni kesi ya kuwalazimisha chadema wamtambue Rais na kutambua matokeo ya uchaguzi. Katiba haikatazi kesi ya kulazimisha watu kumtambua Rais.. Katiba inakataza kuhoji kuchaguliwa kwa yule aliyetangazwa kuwa Rais. Kwa hiyo CCM ina uwezo na haki ya kufungua kesi.. naomba tuwasihi walete kesi hiyo..
kesi hiyo itafunguliwa chini ya sheria gani. Naona unataka kumchokoza katibu mkuu wa ccm
si ndo hapo. watu wanaropoka ropoka tu kuhusu katiba. naona ndo limekuwa neno mvuto kwa watu!!
Haropoki, anajua sana anachoandika maana yake ili rais atambuliwe na upinzani lazima kuwe na kesi mahakamani na wadaawa katika kesi watakuwa chadema. Ili ccm washinde itabidi watoe ushahidi ( amabao hawana ) kama rais alishinda kweli na ili kesi utupiliwe mbali lazima CHADEMA watatoa ushahidi ( amabao wanao ) kuwa rais hakupata kura ambazo nec wanasema.
Katika kufanya hivyo CHADEMA watapata jukwaa la uhakuka la kuchambua udhalimu wote uliofanyika kufuatia uchaguzi ( wenzetu wanaita washing the linen in public).
Ndio maana naona kama Mwanakijiji anamchokoza katibu mkuu wa ccm
hii itakuwa si mada ya kuhoji kutangazwa "kwake" itakuwa ni kesi ya kuwalazimisha chadema wamtambue Rais na kutambua matokeo ya uchaguzi. Katiba haikatazi kesi ya kulazimisha watu kumtambua Rais.. Katiba inakataza kuhoji kuchaguliwa kwa yule aliyetangazwa kuwa Rais. Kwa hiyo CCM ina uwezo na haki ya kufungua kesi.. naomba tuwasihi walete kesi hiyo..
Nilikuwa nafikiria namna nyingine ya kutatua mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA kuhusu suala la matokeo ya Urais. Nimefikiria kuna kesi mbili ambazo nikiwasikiliza CCM na wale wenye kulaani kitendo cha "kutoka nje" kilichofanywa na CHADEMA wanaweza kuja nazo.
1. Kesi ya Kikatiba ya kuwalazimisha CHADEMA kumtambua Rais Kikwete kwa vile waliamua kutoka wakati Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali ya JMT alipokuwa anazungumza. Kwa vile kitendo kile kimeelezewa na Kapt. Chiligati kuwa kilikuwa kinavunja Katiba basi mantiki inataka wale wanaotetea Katiba wachukue hatua za kuitetea Katiba hiyo kwa kufungua kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA.
2. Kesi ya pili nayo ni ya Kikatiba vile vile nayo iwe ni ya kulazimisha CHADEMA WATAMBUE matokeo ya Uchaguzi wa Rais kwani kutokutambua matokeo ya kura za Urais yanatuleta kwenye tatizo la kwanza hapo juu. Kwa vile CCM na wengine wanaamini kuwa kura zilizopigwa na kutangazwa zilikuwa ni halali na hakuna mashaka yoyote basi jawabu pekee ni kuwalazimisha CHADEMA KUKUBALI matokeo hayo. Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani! Hivyo, CCM na wanasheria wake wafikirie namna ya kuthibitisha au kuutetea ushindi mahakamani. Hapa napendekeza wao CCM waitishe kura zote za Urais kutoka majimbo yote ili kuonesha kiasi cha kura alizoshinda. Watakapofanya hivyo watafunga kelele zote za Chadema na kuwaridhisha Watanzania kuwa hakuna kura zilizochakachuliwa. Hapa itakuwa ni goli kama la Maradona au lile goli la elfu moja la Pele.
Kwa ufupi naamini CCM wanaweza kutoa mfano wa utawala wa sheria kwa kwenda mahakamani kufungua kesi hizo za Kikatiba.
ok.. ushirikiano kati ya CCM na CHadema.
hakuna "mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA"
get your subject right
hii itakuwa si mada ya kuhoji kutangazwa "kwake" itakuwa ni kesi ya kuwalazimisha chadema wamtambue Rais na kutambua matokeo ya uchaguzi. Katiba haikatazi kesi ya kulazimisha watu kumtambua Rais.. Katiba inakataza kuhoji kuchaguliwa kwa yule aliyetangazwa kuwa Rais. Kwa hiyo CCM ina uwezo na haki ya kufungua kesi.. naomba tuwasihi walete kesi hiyo..
Katiba ina kataza kuhoji matokeo ya Uraisi ambayo yametangazwa na NEC Lakini sina uhakika kama kifungu hicho kina ruhusu kuhoji namna NEC ilivyofikia kuyatangaza hayo matokeo kama anavyosema ndugu yangu Rutashubanyuma hapo juu. Kama hivyo ndivyo nahisi ni kama kitendawili cha Yai na Kuku kipi kilianza, maana kama unazuiwa kuhoji matokeo ya Urais vipi uruhusiwe kuhoji mchakato ulopelekea kuyapata hayo matokeo yalompatia Mr JK Urais??? Mi nafikiri njia muafaka ni CDM ambao wao wanaamini kuwa walishinda kwa mujibu wa returns zao walizopata kwa mawakala wao kama kweli ni AUTHENTIC basi kama walivyofanya kwenye Operation Sangara, basi waufikishe ukweli huu kwa wananchi na kuwaonyesha ushahidi kamili wa nani alifanya nini na kwa wakati gani. Wananchi wa leo si wa jana au juzi, wana uwezo mkubwa wa kuelewa mambo naamini kwa kuanzia na uchaguzi ujao wa serikali za mitaa in 2 yrs time watatoa hukumu inayostahili kwa wote waliodhulumu kura za wananchi na itakapofika 2015 itakuwa ni climax ya hukumu hiyo