Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
Nilikuwa nafikiria namna nyingine ya kutatua mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA kuhusu suala la matokeo ya Urais. Nimefikiria kuna kesi mbili ambazo nikiwasikiliza CCM na wale wenye kulaani kitendo cha "kutoka nje" kilichofanywa na CHADEMA wanaweza kuja nazo.
1. Kesi ya Kikatiba ya kuwalazimisha CHADEMA kumtambua Rais Kikwete kwa vile waliamua kutoka wakati Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali ya JMT alipokuwa anazungumza. Kwa vile kitendo kile kimeelezewa na Kapt. Chiligati kuwa kilikuwa kinavunja Katiba basi mantiki inataka wale wanaotetea Katiba wachukue hatua za kuitetea Katiba hiyo kwa kufungua kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA.
2. Kesi ya pili nayo ni ya Kikatiba vile vile nayo iwe ni ya kulazimisha CHADEMA WATAMBUE matokeo ya Uchaguzi wa Rais kwani kutokutambua matokeo ya kura za Urais yanatuleta kwenye tatizo la kwanza hapo juu. Kwa vile CCM na wengine wanaamini kuwa kura zilizopigwa na kutangazwa zilikuwa ni halali na hakuna mashaka yoyote basi jawabu pekee ni kuwalazimisha CHADEMA KUKUBALI matokeo hayo. Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani! Hivyo, CCM na wanasheria wake wafikirie namna ya kuthibitisha au kuutetea ushindi mahakamani. Hapa napendekeza wao CCM waitishe kura zote za Urais kutoka majimbo yote ili kuonesha kiasi cha kura alizoshinda. Watakapofanya hivyo watafunga kelele zote za Chadema na kuwaridhisha Watanzania kuwa hakuna kura zilizochakachuliwa. Hapa itakuwa ni goli kama la Maradona au lile goli la elfu moja la Pele.
Kwa ufupi naamini CCM wanaweza kutoa mfano wa utawala wa sheria kwa kwenda mahakamani kufungua kesi hizo za Kikatiba.