CCM, DC, RC wafanya unyama na kusababisha maafa Arusha

Mungi

JF Gold Member
Joined
Sep 23, 2010
Posts
16,975
Reaction score
9,580
Wakuu,

Kweli sikio la kufa halisikii dawa, huu ni unyama na udikteta wa ajabu kabisa.

Ni kwamba jana usiku migambo wa jiji kwa maelekezo ya DC, RC ambao kimsingi ni makada wa chama cha mapinduzi wamefanya unyama usiofaa kwa jamii baada ya kumfunga mikono na miguu mlinzi anayelinda matunda katika barabara ya serengeti maeneo ya Jacaranda hapa Arusha, na kumpiga na kumtesa vibaya sana, na kumsababishia maumivu na majeraha makali sana.

Baada ya kumfunga mlinzi usiku wa manane na kumpiga, wakaamua kumwaga barabarani matunda yote yaliyokuwa yamehifadhiwa pale. Kama mnavyokumbuka asilimia kubwa ya wateja wa yale matunda ni watalii, wafanyakazi wa jumuiya ya kimataifa kama UN, EAC na wananchi wa kawaida.

Baada ya migambo kufanya unyama huo, leo asubuhi wamama wauza matunda walipofika pale walishtuka sana biashara yao kuharibiwa, kitendo kilichosababisha wamama baadhi yao kuzimia na kupoteza fahamu, na kwa taarifa zisizothibitishwa ni kwamba mama moja amepoteza maisha hospitali ya mount meru.

Kimsingi kazi ya kuweka jiji katika mazingira safi ni jukumu la kila moja katika jiji, lakini lazima tukubaliane kwamba usafi usiozingatia haki, utu na heshima ya binadamu haina maana katika jamii, lazima kuwe na utaratibu unaojenga heshima na utu wa mtu.

Kwakuweka taarifa sawa, kulikuwa na vikao vinavyoendelea leo kwa ajili ya kupunguza idadi ya wafanyabiashara maeneo yale, na kuweza usafi maeneo yale. Kikao cha jana cha baraza la halmashauri kiliazimia kuwa ni kweli wafanyabiashara wa matunda wapunguzwe pale, lakini kwanza patafutwe mahali pa kuwaweka, maana kuwaondoa bila kuwapatia sehemu ya kufanyia biashara yao siyo sahihi. Madiwani wa chadema walipendekeza kwamba baadhi ya wamama wanaofanya biashara Jacaranda wapunguziwe njia ya breweries na wengine ikiwezekana fillips. Madiwani wote wakaazimia kwamba leo watakaa kikao cha kujadili eneo sahihi na rasmi ya kuwapunguza wafanyabiashara hao.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hata kabla hawajafikia uamuzi leo, CCM wakishirikiana na DM na RC wakaamua kuwatuma mgambo usiku wa manane na kusababisha unyama huo.

Kwakuwa madiwani wote walikubaliana kukutana leo, kilichoshangaza madiwani wa chadema wakajikuta wamefika kwenye eneo la kikao wenyewe, wa ccm haijulikani kwanini hawakujitokeza, kumbe walishafanya maamuzi yao yasiyo na chembe ya ubinadamu
 
Huu ni uzushi mtakatifu

Sio uzushi mkuu kwa maana ya tukio..mimi kama mwananchi wa kawaida nimeona hili tukio, linasikitisha. sijui mambo ya vikao vya madiwani lakini wameondolewa pale kijiweni kwao, na bara bara ilifungwa kwa muda maana ilikuwa patashika.

cc Mungi
 
Last edited by a moderator:
Ifike mahali JK asikilize ushauri wa watu asiowapenda pia. Washauri anaowapenda wamekuwa wakimshauri vibaya rais wetu.
'Mheshimiwa rais, naomba usikilize ushauri wangu hata kama mimi sio kati ya watu unaowapenda watu wanaogopa kukuambia ukweli, nakushauri raisi mtazame tena Mulongo Magesa kama kweli anastahili kuendelea kuwa mkuu wa mkoa wa arusha.
 
Hawa wakubwa wanachofanya ni unyama wakitaka kuonesha waziwazi kwa nini Arusha wapende cdm/Mh Lema na si ccm. Mbinu hii imetumika maeneo yote yenye upinzani baada ya mbinu zao za kifisadi kushindikana kutawala maeneo hayo.

Kimsingi mbinu za ccm kutawala nchi hii zimekuwa za ulegevu wa sheria. Ndo maana utakuta wavuta bangi, walevi majira ya asubuhi, watu wasio raia....matajiri wasiolipa kodi....wote hawa huwachiwa huru na kupeperusha bendera za ccm ilimradi wanaipigia kura. Ikitokea upinzani dhidi yao....watawala hawa ujifanya kuzikumbuka sheria na kuzitumia kama mateso kwa watu ambao hawakuzoea aina hiyo ya utawala.

Naamini sivyo ilivyo Arusha lakini tulitambue hilo.
 
Mungi hata mimi nimeliona hilo tukio asubuhi nikitoka Njiro nimekuta vitu vimemwagwa dah! utafikiri gari limepata ajali.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu,

Kweli sikio la kufa halisikii dawa, huu ni unyama na udikteta wa ajabu kabisa.

Ni kwamba jana usiku migambo wa jiji kwa maelekezo ya DC, RC ambao kimsingi ni makada wa chama cha mapinduzi wamefanya unyama usiofaa kwa jamii baada ya kumfunga mikono na miguu mlinzi anayelinda matunda katika barabara ya serengeti maeneo ya Jacaranda hapa Arusha, na kumpiga na kumtesa vibaya sana, na kumsababishia maumivu na majeraha makali sana.

Baada ya kumfunga mlinzi usiku wa manane na kumpiga, wakaamua kumwaga barabarani matunda yote yaliyokuwa yamehifadhiwa pale. Kama mnavyokumbuka asilimia kubwa ya wateja wa yale matunda ni watalii, wafanyakazi wa jumuiya ya kimataifa kama UN, EAC na wananchi wa kawaida.

Baada ya migambo kufanya unyama huo, leo asubuhi wamama wauza matunda walipofika pale walishtuka sana biashara yao kuharibiwa, kitendo kilichosababisha wamama baadhi yao kuzimia na kupoteza fahamu, na kwa taarifa zisizothibitishwa ni kwamba mama moja amepoteza maisha hospitali ya mount meru.

Kimsingi kazi ya kuweka jiji katika mazingira safi ni jukumu la kila moja katika jiji, lakini lazima tukubaliane kwamba usafi usiozingatia haki, utu na heshima ya binadamu haina maana katika jamii, lazima kuwe na utaratibu unaojenga heshima na utu wa mtu.

Kwakuweka taarifa sawa, kulikuwa na vikao vinavyoendelea leo kwa ajili ya kupunguza idadi ya wafanyabiashara maeneo yale, na kuweza usafi maeneo yale. Kikao cha jana cha baraza la halmashauri kiliazimia kuwa ni kweli wafanyabiashara wa matunda wapunguzwe pale, lakini kwanza patafutwe mahali pa kuwaweka, maana kuwaondoa bila kuwapatia sehemu ya kufanyia biashara yao siyo sahihi. Madiwani wa chadema walipendekeza kwamba baadhi ya wamama wanaofanya biashara Jacaranda wapunguziwe njia ya breweries na wengine ikiwezekana fillips. Madiwani wote wakaazimia kwamba leo watakaa kikao cha kujadili eneo sahihi na rasmi ya kuwapunguza wafanyabiashara hao.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hata kabla hawajafikia uamuzi leo, CCM wakishirikiana na DM na RC wakaamua kuwatuma mgambo usiku wa manane na kusababisha unyama huo.

Kwakuwa madiwani wote walikubaliana kukutana leo, kilichoshangaza madiwani wa chadema wakajikuta wamefika kwenye eneo la kikao wenyewe, wa ccm haijulikani kwanini hawakujitokeza, kumbe walishafanya maamuzi yao yasiyo na chembe ya ubinadamu

umechelewa sana kuleta ushuzi wako, ulikuwa wapi tangu asubuhi?
 
Dizain we utakuwa Khadija Kopa au Isha Mashauzi nyuma ya ID yako...... Mana sredi yako imejaa Mipasho kama si Umbea
 
Kama kuna njia sahihi ya yeye kuleta habari natumai ingekuwa vyema ungemuelekeza na sio kumtukana mtu.. Kuna njia nyingi za kueleweshana...
 
Arusha ni yenu na Mulongo kaletwa na ccm. Fanyeni utaratibu wa kinyama alipe roho za wanyonge wa Arusha wanaozidi kuteketea. Mtashindwaje kwa mtu mmoja tu kama mulongo. Kama hawezi ishi Arusha arudi kwao Mara. Fanyeni kweli huyo yupo kuwaharibia mji.
 
Dizain we utakuwa Khadija Kopa au Isha Mashauzi nyuma ya ID yako...... Mana sredi yako imejaa Mipasho kama si Umbea

Ndio maana hii nchi inazidi kurudi nyuma.. The same news zinatolewa kuhusiana na kuuliwa kwa Albino, kuumizwa kwa raia sehemu mbali mbali, but instead ya watu kutoa ushauri sahihi kwa serikali wanapuuzia mpaka ndugu zao waguswe.. I cannot imagine wewe ukiwa kiongozi wa nchi au mshauri wa kiongozi wa nchi ni namna gani utakuwa unachagua news za kuzifanyia kazi....

Tubadilike... Kama kuna shida kwenye thread yake, mpeni ushauri stahiki na sio kumrushia maneno....
 
Nabado wamwambie Lema awape masoko kwani aliwaahidi
 
Nchi hii bwana! viongozi wanaangalia uchafu unaosababishwa na nyanya ambazo zinaweza kuoza. hao hao viongozi wanashindwa kuona uchafu biashara ya madawa ya kulevya, uchafu wa viwanda na machimbo. Hii nchi haistahili kuwa katika sayari hii
 
Back
Top Bottom