CCM, DC, RC wafanya unyama na kusababisha maafa Arusha

CCM, DC, RC wafanya unyama na kusababisha maafa Arusha

Kwanini ni uzushi ? Maamuzi ni baraza la madiwani ambao wengi ni chadema na mgambo waliofanya ni wa manispaa kinachofanyika ni uzushi tu kwa rc na dc

Kama DC na RC hawahusiki wamechukua hatua gani baada ya tukio hilo? Tambua kuwa wao ndio walinzi wa amani. Ukiona kimya hawasemi kitu wala wahusika hawachukuliwi hatua yoyote ujue hakuna walinzi wa amani Arusha ila wazusha vurugu.
 
umechelewa sana kuleta ushuzi wako, ulikuwa wapi tangu asubuhi?

Wewe mpuuzi kwelikweli, unaona kuwaisha habari hapa ndiyo issue?? Au ule ujinga wako wa uwongo ulileta hapa ndiyo umeona ni kitu cha maana??
 
Jana usiku nimekutana na Mh Diwani mmoja akisikitikia sana ujinga ulio fanywa na mgambo. Na amenidokeza kwamba leo kina mama wale wataendelea na biashara zao pale Jakara nda hadi utaratibu utakapo pangwa upya.
 
acheni uoga wana arusha haya mambo siku izi yamekuwa kawaida sn kwa ma DC,RC kwa kujifanya wao ni watawala ss fanyeni maamuzi magumu tu ya kuomba mh rais amuondoe hapo kwanza kaz ameshindwa matukio ya ajabu ya mekuwa meng sn arusha na hao viongozi wanakazi kubwa ya kupambana nao ila dhahil wameshindwa wanaenda kuonea wanyonge,rai yangu kwenu tumien wing wenu kumuondoa hapo alipo kisheria inawezekana tupunguze kulalmika cz wameshazoa wajinga wahaina iyo ni wengi nchi hii
 
Manispaa ya Arusha si iko "chini" ya CHADEMA? maamuzi kama haya CHADEMA wamehusika 100% , Mungi acha kuleta unafiki wako hapa!

Mkuu mbinu za chadema kwa historia yake zinafahamika na habibu mchange alishaeleza hakuna haja ya kupoteza muda ni kuwapuuza na wananchi wameshaanza kiwatambua
 
Wakuu,

Kweli sikio la kufa halisikii dawa, huu ni unyama na udikteta wa ajabu kabisa.

Ni kwamba jana usiku migambo wa jiji kwa maelekezo ya DC, RC ambao kimsingi ni makada wa chama cha mapinduzi wamefanya unyama usiofaa kwa jamii baada ya kumfunga mikono na miguu mlinzi anayelinda matunda katika barabara ya serengeti maeneo ya Jacaranda hapa Arusha, na kumpiga na kumtesa vibaya sana, na kumsababishia maumivu na majeraha makali sana.

Baada ya kumfunga mlinzi usiku wa manane na kumpiga, wakaamua kumwaga barabarani matunda yote yaliyokuwa yamehifadhiwa pale. Kama mnavyokumbuka asilimia kubwa ya wateja wa yale matunda ni watalii, wafanyakazi wa jumuiya ya kimataifa kama UN, EAC na wananchi wa kawaida.

Baada ya migambo kufanya unyama huo, leo asubuhi wamama wauza matunda walipofika pale walishtuka sana biashara yao kuharibiwa, kitendo kilichosababisha wamama baadhi yao kuzimia na kupoteza fahamu, na kwa taarifa zisizothibitishwa ni kwamba mama moja amepoteza maisha hospitali ya mount meru.

Kimsingi kazi ya kuweka jiji katika mazingira safi ni jukumu la kila moja katika jiji, lakini lazima tukubaliane kwamba usafi usiozingatia haki, utu na heshima ya binadamu haina maana katika jamii, lazima kuwe na utaratibu unaojenga heshima na utu wa mtu.

Kwakuweka taarifa sawa, kulikuwa na vikao vinavyoendelea leo kwa ajili ya kupunguza idadi ya wafanyabiashara maeneo yale, na kuweza usafi maeneo yale. Kikao cha jana cha baraza la halmashauri kiliazimia kuwa ni kweli wafanyabiashara wa matunda wapunguzwe pale, lakini kwanza patafutwe mahali pa kuwaweka, maana kuwaondoa bila kuwapatia sehemu ya kufanyia biashara yao siyo sahihi. Madiwani wa chadema walipendekeza kwamba baadhi ya wamama wanaofanya biashara Jacaranda wapunguziwe njia ya breweries na wengine ikiwezekana fillips. Madiwani wote wakaazimia kwamba leo watakaa kikao cha kujadili eneo sahihi na rasmi ya kuwapunguza wafanyabiashara hao.

Jambo la kusikitisha ni kwamba hata kabla hawajafikia uamuzi leo, CCM wakishirikiana na DM na RC wakaamua kuwatuma mgambo usiku wa manane na kusababisha unyama huo.

Kwakuwa madiwani wote walikubaliana kukutana leo, kilichoshangaza madiwani wa chadema wakajikuta wamefika kwenye eneo la kikao wenyewe, wa ccm haijulikani kwanini hawakujitokeza, kumbe walishafanya maamuzi yao yasiyo na chembe ya ubinadamu

Tunaomba update kwa haya, ili tubakiwe na kumbukumbu za kweli na sahihi

1 Blue - Je alipelekwa hospitali? Ana PF 3 anaendeleaje
2 Red - Thibitisha au kanusha habari hizi ambazo siyo ya uhakika
 
Back
Top Bottom