WanaJF,
Mapenzi kwa CCM sasa yamevuka mipaka ya Tanzania na kusambaa mpaka kwenye mataifa yaliyoendelea! Hili linaweza kuthibitishwa na kuonyeshwa kwa habari zake kwenye vyombo vya habari vya kimataifa!
Shirika la utangazaji la kimataifa (BBC) limetangaza habari za CCM kuhusu kikao cha kamati kuu kuahirishwa pia na taarifa ya kamati ya maadili na usalama wa chama iliyotolewa siku ya jana!
Watanzania hili linapaswa kuwa somo kwetu kwa maana ukitizama habari za BBC pindi wanapotangaza juu ya chaguzi za nchi za Afrika, siku zote uwa wanachukua vyama vyenye nguvu, maarufu na vinavyokubalika.
Hata siku moja shirika la utangazaji la BBC haliwezi kutenga hata sekunde yake moja kutangaza habari za vijivyama uchwara na vijisakosi vinavyojiita vyama pinzani!
Aidha, BBC imeahidi watizamaji wake kote ulimwenguni (walengwa wakiwa Watanzania waishio ughaibuni) kuwa watawahabarisha habari juu ya kinachoendelea CCM kadri watakavyopata taarifa.
Je, CHADEMA, CUF na NCCR, habari zenu nje ya gazeti la Mbowe la TanzaniaDaima uwa zinatangazwa wapi kwingine? Iweje chama kinacho lazimisha kuaminisha watu kuwa kinakubalika, hakijulikani hata pale Mtukula? CHADEMA na UKAWA yenu bado mpo kina kifupi, tulipo CCM msipasogelee, mtazama!
All the way to BBC....CCM itadumu milele.