CCM Chama Pendwa: Habari Zake Zatangazwa na BBC!

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
WanaJF,

Mapenzi kwa CCM sasa yamevuka mipaka ya Tanzania na kusambaa mpaka kwenye mataifa yaliyoendelea! Hili linaweza kuthibitishwa na kuonyeshwa kwa habari zake kwenye vyombo vya habari vya kimataifa!

Shirika la utangazaji la kimataifa (BBC) limetangaza habari za CCM kuhusu kikao cha kamati kuu kuahirishwa pia na taarifa ya kamati ya maadili na usalama wa chama iliyotolewa siku ya jana!

Watanzania hili linapaswa kuwa somo kwetu kwa maana ukitizama habari za BBC pindi wanapotangaza juu ya chaguzi za nchi za Afrika, siku zote uwa wanachukua vyama vyenye nguvu, maarufu na vinavyokubalika.

Hata siku moja shirika la utangazaji la BBC haliwezi kutenga hata sekunde yake moja kutangaza habari za vijivyama uchwara na vijisakosi vinavyojiita vyama pinzani!

Aidha, BBC imeahidi watizamaji wake kote ulimwenguni (walengwa wakiwa Watanzania waishio ughaibuni) kuwa watawahabarisha habari juu ya kinachoendelea CCM kadri watakavyopata taarifa.

Je, CHADEMA, CUF na NCCR, habari zenu nje ya gazeti la Mbowe la TanzaniaDaima uwa zinatangazwa wapi kwingine? Iweje chama kinacho lazimisha kuaminisha watu kuwa kinakubalika, hakijulikani hata pale Mtukula? CHADEMA na UKAWA yenu bado mpo kina kifupi, tulipo CCM msipasogelee, mtazama!

All the way to BBC....CCM itadumu milele.
 
Hata mimi nilisikia BBC wakitangaza habari za Ikulu inayokaliwa na kiongozi wa CCM kuwasafisha walioiba hela za ESCROW ACCOUNT. Halafu pia BBC walitangaza habari za spika wa bunge kutoka CCM akimzuia mbunge mmoja kuuliza swali kuhusu uhalali wa kampuni iliyoibia watanzania kuendelea kulipwa na serikali ya CCM sh. BILIONI TANO kila mwezi. Tena pia BBC ikatangaza kuhusu mbunge huyo kuzuiwa na spika wa bunge kutoka CCM kuuliza majina ya watuhumiwa waliopitisha fedha zao kwenye ile benki nyingine ambayo imekatazwa kutajwa.

Kwa ufupi ndugu yangu, jina la CCM linavuma sana kimataifa
 
Kwa sasa CCM inavuma sana.
Lkn jiulize inavuma kwa sifa ipiii?
Loliondo gate,
EPA, Richmonduli . . ., tembo wetu, Escrow ya Jay K vyote vilitangazwa sana dunia nzima not only BBC ila duniani kote na sasa CCM inajigamba na serikali yake inavyotangazwa.
Kwa kweli hamy Dada mko vizury
 
Mtoa mada anapotosha wana jukwaa na watanzania kiujumla.BBC ni shirika la utangazaji la uingereza hutangaza habari zote zinazotokea ulimwenguni bila upendeleo. tofauti na shirika letu la TBC ambalo muda wote hutangaza habari za upande mmoja tu wa ccm. bbc hata mchakato wa ukawa ukianza lazima watangaze.
 
Ni muhimu kufuatiliwa maana kina hali ngumu na kiko katika hatari ya kuporomoka kwa umaarufu wake na kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa 2015 octoba

Au Kupata wabunge wachache kuliko miaka yote tangu kianzishwe!
 
Tuna watu wana akili ndogo kuliko hata za simbilisi....
 
Tuna watu wana akili ndogo kuliko hata za simbilisi....

Atakuja tena kujisifu kuwa biashara yao waliyobuni ya viungo vya albino ni maarufu duniani kwani inatangazwa sana Aljazera, BBC na CNN.
Hivi kweli Elli huko CCM kuna mtu mwenye utimamu amebaki? Hebu ona sifa kama alizoleta huyu jamaa na wapo watakao komaa kumpongeza
 
Last edited by a moderator:
Meno ya tembo yalioenda China yalitangazwa na nani BBC yalikuwa yanaelezea uzaifu wa chama gani kilichoshindwa kulinda tembo
 
Jamani asemehewe tu,kasumba aliyonayo ni ile ya wao wanajuwa kila kitu hata kama mtu hana elimu ya udaktari atataka kufanya hiyo kazi.Kwa taarifa yake hawa BBC watawanyambuwa ile mbaya
 
lazima wafuatilie kinacho endelea ccm,usichezee anguko LA chama kongwe.
ccm imechoka kiasi kwamba hadi BBC wanatamani iondoke madarakani Kama KANU.
Ccm umekuwa genge LA wahuni,wezi wapiga dili na wasiokuwa hata na chembe LA huruma kwa kizazi kijacho.
poor ccm RIP
 
Back
Top Bottom