CCM 2015-2020 ilivyovutia na kupendwa zaidi na Watanzania wengi

Feb 26, 2021
50
150
CCM 2015-2020 ilivyovutia na kupendwa zaidi na Watanzania wengi.

1) Rais alishinda Uchaguzi 2020 kwa 84.4% haijawahi kutokea.
2) Wabunge na madiwani wote walishida Uchaguzi 2020 isipokuwa wachache na haijawahi tokea mpaka kuchukua jimbo la Mbowe.
3) Uchaguzi wa serikali za mitaa CCM ilishida na haijawahi tokea.
4) Uchaguzi 2020 uliendeshwa kitaalam na haijawahi kufanyika hivyo.
5) Humphrey Polepole alionesha umahiri mkubwa sana kuandaa mikutano yote ya JPM na haijawahi tokea.
6) Humphrey Polepole aliandaa tamasha kubwa la wasanii wa CCM kutambulisha nyimbo za CCM na haijawahi tokea kabla.
7) CCM iliungwa mkono na wasanii karibia wote na haijawahi tokea.
8) Dr Bashiru Ally alirudisha mali za CCM zilizoporwa na CCM kuwa chama kinachojitegemea kiuchumi na sio ccm omba omba kwa matajiri.
9) CCM ilirudi kwa wananchi na sio ile CCM ya watu wachache maarufu “CCM ina wenyewe” je tunarudi huko?
10) Watu waliogopa CCM na sio CCM kuogopa watu wachache wanaoimiliki.
11) Vijana wengi walipewa uongozi bila upendeleo na kuonyesha umahiri mkubwa.
12) Ilani ya CCM 2015 – 2020 ilitekelezwa kwa mafanikio makubwa haijawahi tokea toka uhuru.
13) CCM ilikuwa ya watu wote hasa wanyonge na sio CCM ya watu fulani na upendeleo.
14) CCM ilipendwa na watanzania wengi sana. Je, Watanzania watabaki na mapenzi hayo kwa CCM?
15) Chaguzi za CCM hazikuwa na rushwa wala makundi na hii kusaidia vijana wengi sana kugombea ubunge na udiwani.

Watanzania wengi kwa sasa wanajua ni CCM ipi wanayoitaka, hawadanganyiki. Baba kipenzi JPM kashawaonyesha CCM bora ya kisasa inavyopaswa kuwa.

Je, CCM ina uhakika na kuamini tuna ushindi huko tuendako?
 

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,262
2,000
Dua za waliozulumiwa zimemweka kati na hakutoka bado wamebakia lakini ALLAH adhabu zake zinakuja kama onyo kwa wengine ili kuwapa nafasi kutubu ,wazenji wanasema anawapuruzia tu akichambuza anakufa mtu kigogo aliyeshiriki kutesa na kuuwa watu kwenye chaguzi,yaani ni dua tu kwa kwenda mbele.
 

Mac Alpho

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
3,440
2,000
2015 CCM ilikuwa imeoza, emagine hata ukivaa t-shirt ya CCM ilikuwa ni lazima uzomewe mabarabarani ila utendaji kazi wa Magufuli uliiheshimisha mitaani.

2025 wakiamucha Samia Agombee, CCM itapoteza bit vingi bungeni.
 

Dumas the terrible

JF-Expert Member
Jan 20, 2021
1,196
2,000
Taka taka Kama hizo ukiongea mbele za wakubwa na wadogo wanaojitambua my brother

Utakula mtama Kama ule wa Mbasha aliopigwa na Adam Mchomvu wakati wapo pale taifa mbaka wakatuharibia uwanja wetu kwa siasa zenu za double standard!
 

AeIoU

Senior Member
Mar 14, 2008
136
225
Sasa baada ya Rais Mama Samia kuwa Mwenyekiti wa Chama na kuteua kamati tendaji mpya ikiongozwa na Ndugu Chongolo ndio CCM imerudisha imani kwa watanzania
 

nwankoe

JF-Expert Member
Oct 17, 2019
473
1,000
2015 CCM ilikuwa imeoza, emagine hata ukivaa t-shirt ya CCM ilikuwa ni lazima uzomewe mabarabarani ila utendaji kazi wa Magufuli uliiheshimisha mitaani.

2025 wakiamucha Samia Agombee, CCM itapoteza bit vingi bungeni.
Haitopoteza bali itapata inavyostahili. Viti vingi tu ccm haikushinda ilisaidiwa na uchafuzi ndani ya uchaguzi. Jafo anafahamu!
 

rich gang

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
1,497
2,000
2015 CCM ilikuwa imeoza, emagine hata ukivaa t-shirt ya CCM ilikuwa ni lazima uzomewe mabarabarani ila utendaji kazi wa Magufuli uliiheshimisha mitaani.

2025 wakiamucha Samia Agombee, CCM itapoteza bit vingi bungeni.
kwaio agombee magufuli jr?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,540
2,000
2015 CCM ilikuwa imeoza, emagine hata ukivaa t-shirt ya CCM ilikuwa ni lazima uzomewe mabarabarani ila utendaji kazi wa Magufuli uliiheshimisha mitaani.

2025 wakiamucha Samia Agombee, CCM itapoteza bit vingi bungeni.

Ccm ya kipindi cha Magu usingeweza kuzomea maana alikuwa na kundi lake la watu wasiojulikana. Hao ndio waliifanya ccm kutoka kuwa chama cha siasa mpaka kikundi cha mungiki.

Hivyo ccm kabla ya Magufuli iliweza kuzomewa maana ilikuwa imeshachoka kisiasa, Magu kuona hivyo ikabidi aanzishe kikundi cha utekaji na mauaji ili kuilinda ccm mfu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom