CCJ kuomba usajili wa kudumu leo; yakusanya wanachama 20,000!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCJ kuomba usajili wa kudumu leo; yakusanya wanachama 20,000!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 12, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Chama kipya chenye usajili wa muda cha CCJ ambacho ni mbadala wakiitikadi, mwelekeo, mfumo na uongozi wa CCM kitafanya mkutano na waandishi wa habari Alhamisi Mei 13, 2010 majira ya saa saba mchana kwenye ukumbi wa MAELEZO kutoa utafafanuzi wa mambo mbalimbali kikiwa njiani kuelekea kupata usajili wa kudumu.

  CCJ hadi hivi sasa kimekamilisha uhakiki wake wa ndani wa wanachama wake katika mikoa mbalimbali na mkoa wa Mwanza tu ndio uhakiki wa ndani utakamilika mapema Alhamisi na hivyo kuwa tayari kwa uhakika wa Msajili.

  Sehemu mbalimbali ambako viongozi wa CCJ wamepita wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kutaka kujiunga na kujua undani wake wakiamini kuwa hatimaye kile Chama ambacho Nyerere alikuwa anakiotea kije ili kiwe mbadala (siyo tishio tu) la CCM hatimaye kimewadia.

  Hata hivyo "vi-nzi" vinadokeza kuwa kutokana na utofauti wa CCJ na vyama vingine viliyvyopo kuna uwezekano mkubwa wa wakuu kuhakikisha kinacheleweshewa usajilii wa kudumu ili kisiweze kushiriki uchaguzi mkuu. Hata hivyo, support ambayo imepatikana hadi hivi inahakikisha kuwa msajili hatakuwa na kisirani cha kukinyima usajili na jambo hili litafanyika mapema zaidi ili kuwatendea haki wanachama maelfu ambao wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu chama kama hiki.

  Tutawaletea taarifa mbalimbali kesho kwa kadiri nitakavyozipata.

  CCJ - Tumaini Jipya la Watanzania, kuelekea mabadiliko ya kweli!'

  Kwa maelezo zaidi:

  Constantine Akitanda
  CCJ, Katibu Mwenezi Taifa
  Tel:
  Dar es Salaam
  +255 717 116 386

  KUTOKA KWA MICHUZI

  CCJ yakabidhi majina ya wanachama wake leo
  [​IMG] Mwenyekiti wa CCJ Mh. Richard Kiyabo akionesha risiti ya stakabadhi ya malipo ya kuwakilisha majina ya wanachama leo ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa jijini Dar
  [​IMG]
  Viongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ) wakimkabidhi majina ya wanachama wa bara na visiwani Mkuu wa Masijala katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Bi. Mwajuma Amir. Kutoka kulia ni Naibu Katibu wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Mh. Ali Hatibu Ali, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mh. Renatus Muabhi, Mwenyekiti wa Chama hicho, Mh. Richard Kiyabo na Katibu Mwenezi Taifa, MNh. Costantine Akitanda. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za msajili wa vyama vya siasaMtaa wa Shaaban Robert jijini Dar.
  [​IMG] Viongozi wa kitaifa wa CCJ wakiondoka ofisi za Msajili wa Vyama baada ya kukabidhi majina ya wanachama wao wa bara na visiwani

   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  May 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, asante kwa taarifa hii. Nami nitajitahidi kuhudhuria ili kuifahamu hii CCJ kwa karibu maana hapo mwanzo niliwahi kucoment kuwa CCJ ni Hoax, Boya, Famba na Zuga ambayo ni System created kupunguza kasi ya Chadema na CUF. Press conference nitazamia na nitajiridhisha kuondoa mashaka yangu.
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  May 13, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Haya wakati umeshataradadi tupeni yaliyojili.
   
 4. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #4
  May 13, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  .

  Pasco mimi nakwambia kuwa amini usiamini hawa wanachama wa CCM kokote waendako hawatabadirika. Wanatoka katika chama chenye sera za kijamaa ambazo hawazifuati na kwenda kuazisha chama cha kijamaa kingine ili wazifuate je huko wakikutana na watu aliokengeuka kama wakina kingunge wataendeleza sera hizo kweli? Eti wanafuata sera za Nyerere, wanasahau kuwa nyerere ndiye alikuwa raisi wa nchi hii kwa miaka takribani 25 na pia ni muumini mkubwa wa mkapa wanaemkimbia. Mimi wangeniambia kuwa wanafuata sera za yule raisi wa botswana au basi hata kagame ningeelewa maana wana kitu cha kuonesha ( Lugha na utaifa havileti chakula mezani kwa mtanzania)

  Anyway nawatakia kila laheri na jitihada zenu, at least mkiiua CCM au kuigawa vipande viwili vya Mafisadi na kingine cha waliokosa nafasi ya kuwa mafisadi mtatupa nafasi ya kuwamaliza kiraisi
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Sorry Mzee Mwanakijiji, kwa hapa kwetu leo Alhamisi ni tarehe 13 May, 2010, pia najua kuna Alhamisi hii hii ni tarehe 12 kabla ya international date line. Japo hukusema ukumbi ni wapi, naasume ni pale pale Maelezo kama ni kungine tujulishe.
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Yeah.. ni Alhamisi ya leo.. saa saba na ni hapo Maelezo.. ! sorry.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  May 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Shalom, nawafuatilia kwa karibu sana hawa CCJ, politics is really dirty game, CCM itahakikisha vyama vidogo vinasimamisha wagombea kila kwenye Chadema/CUF bara ili kuhakikisha wapinzani wanagawana kura kwa faida ya CCM, kama hali ilivyo Kilimanjaro.

  Hata Mtikila alivyokwenda Tarime, Busanda na Biharamulo, he must have been funded ili kupunguza kura za Chadema. Ndivyo ninavyoiona CCJ, na itapata usajili wa kudumu na slogan yake itakuwa CCJ ndio chama mbadala kwa CCM, Chadema ni chama cha ukabila (Wachagga) na CUF ni chama cha udini (Waislamu), tena watapewa fungu nene la kampeni, watu watawaamini, watawapigia kura, hivyo kugawanya kura za wapinzani hivyo CCM kuibuka kidedea.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  May 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,532
  Trophy Points: 280
  Thanks, I'll be there.
  Networking ni kitu muhimu sana for getting connections, nimeukubali mtandao wako, yaani sisi tulio karibu tuka gizani, news tip zinatoka mbali kina siye ndio tunazikutia JF!. Thanks.
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  May 13, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mimi bado ni tomaso kwahiyo bado naamini ni pandikizi
   
 10. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa kwa taarifa yako Kagame na marais wengine wenye msimamo kama wake wanafuata sera za Nyerere. Mkapa ni kupenda kwake sifa binafsi ndiko kulikomfanya akengeuke.
   
 11. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #11
  May 13, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pasco, ni kweli kura zinaweza kugawanywa kwa kuwa vyama vya upinzani vimeweka ubinafsi mbele kuliko utaifa. CCJ is a totally different political party. Hawa wameona jinsi ambavyo nchi imekwenda kombo kwa CCM kutofuata misingi ya chama hicho kama ilivyokuwa chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere. Sisemi kwamba lazima washinde leo ama kesho lakini naamini kwamba watafanya jitihada ya kujaribu kurejesha nchi katika msitari kwa kuchukua ile misingi mizuri tuliyojengewa na waasisi wa Taifa hili kwa manufaa ya Watanzania wote.
   
 12. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #12
  May 13, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi siongelei vitu vya kwenye makaratasi bali naongele outputs mzee amaazo kwa nyerere naona zilikuwa haba
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  May 13, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hata kama watainyima CCJ usjili...bado kuna nafasi ya CCJ kuonyesha dhamira yao ya dhati kwa kuunga mkono vyama viwili vya juu au upinzani kwa ujumla na kuhamasisha wafuasi wao kupigia kura upinzani.Hilo tunaweza
   
 14. F

  Felister JF-Expert Member

  #14
  May 13, 2010
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]Nalikuwa katika kutafakari nchi yangu jinsi ya kufanya ili niweze kutoa angalau mchango katika kuisaidia nami nikajiwa na neno hili, "Kama watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza na kuomba nitasikia kutoka juu na kuiponya nchi yao". [/FONT]
  [FONT=&quot]Basi nikiwa katika maombi naliota: [/FONT]
  [FONT=&quot]Nalikua nikipita jirani na nyumba moja ya kiongozi mkuu nikasikia watu waliokua wakitoa angalizo lakini sauti zao hazikusikika hivyo walikua wakiendelea kulalamika jamani eeh, Sikilizeni! lakini wale waliokuwa wakisemeshwa hawakuwa wakitega sikio na hivyo kuonekana kupuuza ...Hao walikua wakiwaambia waandaaji wa safari ya mkuu wa nchi kuwa ndege wanayompandisha huyo kiongozi ni mbovu na yumkini itaanguka kama hawataitengeneza kabla ya kupaa. Nami nikajikuta nikiwauliza, mbona mko mnapiga kelele na hakuna anaewasikiliza? Kwani mbona naona hiyo ndege iko sawa tu? Mara nikaona ndege inapaa nami nikasisitiza, unaona! lakini kwa mshangao mkubwa baada ya dakika chache kishindo kikubwa kikasikika na mara nikaona moto mkubwa kule angani........[/FONT]
  [FONT=&quot]Nikiwa katika kutafakari hayo naliingia katika chumba cha ndani ili kupata ufahamu wa haya nami nikapata majibu haya;[/FONT]
  [FONT=&quot] "So shall the knowledge of wisdom be unto thy soul: When though hast found it then there shall be a reward and thy expectation shall not be cut off" Prov 24:14. [/FONT]
  [FONT=&quot]Nami nikatafuta hilo neno la hekima na tazama nikaota ndoto nyingine tena.[/FONT]
  [FONT=&quot]...Kulitokea vurugu na kutokuelewana na tazama kulikua na makundi yanayopingana na tazama nalikua nimejificha karibu na kundi moja na mara akaja askari mmoja akanichukua katikati ya wengine na kunipeleka nje natazama kulikua na ufunguo mkubwa juu mbele yangu; nikiwa katika kushangaa mara nikasikia sauti kubwa angani ule ufunguo uka katika katika vipande. Tazama nikaingiwa na hofu kubwa kwani kishindo kile kilikua kama tetemeko kubwa la ardhi iliyoigeuza geuza udongo wa nchi. Baada ya muda kidogo kwa mshangao naliona udongo ukibadilika na kuotesha mazao aina kwa aina na mara ikatokea nchi nzuri yenye kupendeza yenye watu wenye afya nzuri, na sura zenye furaha waishio kwenye makazi yaliyopambwa kwa rangi nzuri zenye kuvutia....nami nikauliza ni wapi hapa? Kabla ya kujibiwa nalijikuta kitandani nimelala..... [/FONT]
  [FONT=&quot]Nionapo haya mambo yanayofanana fanana na njozi hizi.....Napata hisia kuwa utimilifu wa unabii huu ukaribu kuifikia nchi yangu bado nipo katika kuuliza ni kwa majira gani haya yatakua? Sijui siku wala saa lakini rohoni mwangu kunasauti isemayoa kuwa saa ikaribu ya haya kutokea....Mwenye sikio na asikie neno Roho awaambia watanzania...[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]As a child of God I declare and decree nchi nzuri niliyoiona katika ndoto ni Tanzania and so I usher the beginning of this country by this declaration. The word of God says whatsoever I open on earth it will be opened in heaven and so is to what I bind! KUANZIA SASA MAFISADI WOTE WATAANGUKA KATIKA MIPANGO YAO NA WAZALENDO WANCHI HII WATAICHUKUA NCHI NA KUIONGOZA KUIPELEKA KATIKA HAYA MAONO/VISION.[/FONT]
  [FONT=&quot]For God is not a man to lie not son of man to repent! Again, surely there is no enchantment against me neither is there divination against my nation Tanzania according to this time it will be said of me what hath God wrought![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]As I decree so shall it be IN JESUS name![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]The only way of this not to happen is iff there would be any way to take Jesus back to the grave! [/FONT]
   
 15. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #15
  May 13, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ....Pasco, u disappoint in these! Aint true that CUF na CHADEMA ni hao tu. Unataumia LABELS recycled from the like of Mtikila. Surely, you can see beyond. Kwani origin yako kabila gani? Who can see that in you hata ukipita mitaa ya Bongo? Ukabila na matambiko ya kwenu is what makes you refer utokako in that sense. otherwise upuuzi mtupu and so is UDINI. Mwalimu aliweka vizuri sana hii
   
 16. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #16
  May 13, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo wapinzani inabidi wazaliwe maana akina Zitto (ambao hawajawahi kuwa wanaCCM) ni wachache. Nadhani dhana hii si ya kweli. Akina Marando, Dr. Slaa, Malim Seif nk walikuwa wanaCCM hapo awali.
   
 17. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #17
  May 13, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  which is true
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  May 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hizi habari za CCJ kusema kweli zinanipa wasiwasi zaidi ya Kufurahia. Ni kutokana na fikra duni (Ujinga) za Wadanganyika wengi kiimani kwamba CCJ ndiye mkombozi wa kweli kwa sababu tu wametumia jina la mwalimu Nyerere kamavile kuanzishwa kwa dhehebu la Kikristu kupinga uongozi wa Papa kufuatana na mafundisho ya Biblia. Tatizo sio la kiimani ila, mara nyingi hutokana na mifarakano ya kiuongozi baina ya viongozi ktk ngazi zao.

  Kuna msemo mmoja alisema mwalimu Nyerere kwamba "Huwezi kupima mafanikio ya Ukristu kwa kuhesabu watu wanaokwenda kanisani".. Hii ina ukweli mkubwa sana lakini pia kuna hitlafu kimtazamo.. Ni kweli waumini wa dini ya kikristu wanokwenda kanisa ni chini ya asilimia 10 ya waumini wote, ila kuna hesabu kubwa ya Wakristu wanaoamini na kufanya ibada za Kikristu ktk maisha yao ya kila siku..Hivyo, Kipimo thabiti cha mafanikio ya Ukristu ni kutazama ongezeko la waumini ktk matendo yao na sii hesabu ya wanao hudhuria kanisani. Ndivyo mwalimu alitaka wazungu wautazame Ujamaa ktk maisha ya Watanzania as if Ujamaa was a divine doctrine...yaani tunakula, kunywa na kulala ndani ya Ujamaa..Ujamaa ni asili ya maisha ya Mtanzania.

  Ni katika mtazamo huo huo wa mwalimu najiuliza maswali mengi magumu.. Ikiwa Ujamaa ni imani iliyoshindikana, umekwisha (umeshindwa) na wengi wetu hatufuati wala hatuamini tena imani hii kutokana na maisha magumu tuliyopitia enzi za Ujamaa. Pamoja na ukweli kwamba hata ukitazama maisha ya waumini wa dini utagundua kwamba maisha yao huzidi kuwa duni kila wanapojaribu kufuata mila, tamaduni na mafundisho ya dini kwa sababu dunia imezungukwa na haramu..Kwa kila muumini wa kweli atakachogusa leo hii kuna Uharamu ndani yake..Hivvyo ktk society zetu tuna preach sana imani za dini, tuna uadilifu wa hali ya juu na tunalia sana makanisani na misikitini lakini ukweli wa maisha yetu unapingana na imani za dini. Hii ndio reality na lazima tukubali kwamba shetani ametawala matendo yetu kuliko imani zetu za kiroho..

  Moja ya makosa makubwa ya Nyerere ilikuwa kuhesabu waumini wa Ujamaa kiimani na kudai mafanikio pasipo kuelewa kwamba hakuna waumini walioukubali Ujamaa kivitendo..Tamaa ya kibinadamu (shetani) ilishinda imani ya kiroho (Ujamaa) hivyo mafundisho ya Ujamaa yamebakia ktk vitabu kama Biblia na Kuran, lakini matendo ya waumini wote wa dini hizi ni pinzani na mafundisho ya vitabu hivi..Hivyo kuhesabu namba ya waumini kuwa Waislaam ni billioni moja na Wakristu ni Billioni mbili haina maana dunia hii tupo ktk wakati mzuri kuwa na waumini wengi..ukweli utasimama kwamba dunia imeharibika zaidi kutokana na matendo yetu na sio imani zetu. hivyo, utaona kila siku madhehebu yakijitokeza kupinga madhehebu mengine sii kwa sababu ya mafundisho yenyewe ila ni mvutano baina ya viongozi wa hizi imani kulingana namatendo yao wenyewe.

  Lengo langu kubwa ktk kutoa mfano huu ni kujaribu kuchuja hii imani potofu ya Unyerere au Ujamaa. Kwamba kuna watu wanaamini kwamba nchi imeacha misingi ya Kijamaa na kuubeba Ubepari ktk mfumo hasi wa Ufisadi. Chanzo cha kuzinduliwa CCJ hakutokani na upinzani ktk katiba ya chama CCM ila ni upinzani baina ya viongozi wenyewe ktk matendo yao. CCJ ni sawa na Nabii mpya ktk dhehebu la Kikristu anayetaka kuahidi watu uzima wa milele akitumia kitabu kile kile cha CCM..Hakuna Jipya.

  Mimi naamini kwamba hatuwezi kuokoka kwa kufungua madhehebu mengi ya dini ila tunaweza tu kuokoka ikiwa mafundisho halisi ya ibada hizi za Ujamaa au Ubepari zitazingatiwa na haswa kufuata miiko na maadili ya imani hizi. Tofauti baina ya CCM na CCJ iwe ni ktk Uharamu, kuharamisha yale yote yanayoidhoofisha jamii nzima na sio kugombea Uongozi kwa sababu Kikwete ameshindwa kuongoza. Hakuna dhehebu lolote la Kikristu limetokana na sababu ya Papa ameshindwa kuongoza, ama wao kutengwa na kanisa Katoliki hivyo kuanzisha Upinzani wa kanisa hilo.. Hii ndio hofu yangu kubwa kwa CCJ na vyama vingine kibao vyenye kutazama nafasi tupu ya Uongozi ktk majimbo au Urais ktk kuwania ruzuku, ambayo ni kodi ya wananchi...
   
 19. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #19
  May 13, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Na Mwandishi wetu. ( Kwa MO BLOG)
  Uongozi wa chama cha Jamii Tanzania (CCJ) wamekutana na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa habari MAELEZO leo ili kutangaza rasmi maombi ya usajili wa kudumu baada ya kukamilisha baadhi ya masharti waliyopewa ili wapate usajili huo.
  Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa (CCJ) Bw.Richard Kiabo amesema mchakato wa kukiandisha chama cha Jamii ili kupata usajili wa kudumu kama chama cha kudumu hapa nchini Tanzania umekamilika na hivyo amesema maswali ya kuwa (CCJ) kimekufa kutokana na ukimya wa muda mrefu Bw.Kiabo ametumia methali isemayo "Kimya Kingi huja na Kishindo" kwa hiyo chama cha CCJ kilikuwa kikikamilisha baadhi ya masharti ili kiweze kupata usajili huo.
  Aidha mwenyekiti wa CCJ Bw.Kiabo amesema wameshituliwa sana na matukio yanayotokea hivi sasa kwa wanachama Viongozi wa Chama hicho katika mkoa wa Mara na Mwanza kwa kukamatwa na kusingiziwa hujuma zisizo na ukweli ndani yake.
  Kwa upande wake msemaji mkuu wa chama hicho aliyekuwa Mbunge wa Kishapu Bw.Fred Mpendazoe amesema,aliamua kutoka kwenye chama tawala na kwenda Chama cha Jamii (CCJ) kutokana na sera zake na pia hakuangalia wingi wa malipo ambayo angepewa bali aliangalia chama chenye sera ya kuisaidia jamii.
  Bw.Mpendazoe amesema CCJ nitumaini la wafanyakazi na wananchi wanaoishi katika mazingira magumu hivyo tumejipanga kutoa mgombea kuanzia ngazi ya chini hadi ngazi ya rais na kinaamini kitafanikiwa tena kwa kishindo kwani watu wankubali sera zake
   
 20. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #20
  May 13, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Jamaa sijasikia haswa nini watafanya zaidi ya CHADEMA; TLP; CUF nk...............ni PANDIKIZI la CCM hilo jamani!!!
   
Loading...