CCJ kuomba usajili wa kudumu leo; yakusanya wanachama 20,000!!

chama kilichokuja kwa mbwembwe nyingi hapa nchini kimekuwa kimya kiasi cha kutisha wananchi na kuamini kuwa ilikuwa ni nguvu za soda... tutegemee nini kwa ukimwa huu
 
inawezekana wanajipanga lakini je wingi wa vyama vya siasa vina tija gani katika taifa letu
CCJ inawezekana kikaja kushika hatamu na kuwa kama ccm ya sasa tuu
 
Vyama vya upinzani vimetoa kauli gani kuhusu Wafanyakazi kutukanwa na rais wa Jamuhuri?
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu inaonyesha una imani kubwa na hiki chama tofauti na vyama vingine. Pengine wewe unaweza kutuambia ni kitu gani kimekuvutia zaidi.. Ni bora kuanzia hapo kabla hatujatoa hukumu.
 
CCJ kutinga kwa Msajili leo Send to a friend Friday, 14 May 2010 03:56

Waandishi Wetu
CHAMA Cha Jamii (CCJ) kimesema leo kinapeleka maombi ya usajili wa kudumu kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini John Tendwa na kinajipanga kusimamisha wagombea katika ngazi zote za uongozi kwenye uchaguzi ujao.

Mwenyekiti wa CCJ ,Richard Kiyabo, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa hatua hiyo Inafanyika baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wanachama katika mikoa yote.

Akizungumza na Waandishi wa habari , mwenyekiti wa chama hicho ,Kiyabo alisema kwa sasa mchakato wa kupata wanachama hauna kasoro yoyote na kwamba wanaamini hakuna itakayokwamisha usajili huo.
Alisema hadi sasa chama hicho kimepata wanachama zaidi ya 20,000 ambao walipatikana katika mikoa 10 ya bara na visiwani Zanzibar kama msajili alivyotaka.

Naye msemaji wa chama hicho, Fred Mpendazoe aliyekuwa Mbunge wa Kishapu kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alisema kwa mujibu wa taarifa za chama hicho wapo Watanzania kutoka nchi za nje kama Marekanai Japani na Uingereza waliojiunga na chama hicho.

Aidha, msemaji huyo alijigamba kuwa wanauhakika kuwa chama hicho kitashiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Oktoba mwaka huu, kwa kuwa hawana sababu ya kuzuiwa kufanya hivyo.
Alisema kama Msajili waVyama vya Siasa ana nia njema wananchi na anataka demokrasia ndani ya nchi hii, hana sababu ya kukinyima usajili wa kudumu chama hicho.
"Imebaki miezi miwili na siku tisa kumalizika kwa muda wa usajili wa muda, hivyo tunaamini kama demokrasia ya Tanzania ni ya kweli usajili wa kudumu hautashindikana" alisema Mpendazoe.
Alisema CCJ kitasimamisha wagombea katika nafasi zote kuanzia Urais, ubunge na udiwani, ingawa yeyote atakayokubalika anaweza kugombea nafasi ya Urais.

Alibainisha kuwa asilimia 90 ya Watanzania wenye umri wa kupiga kura hawana uanachama wa chama chochote, hivyo CCJ ana hakika kuwa watapata wanachama zaidi.
Katika hatua nyingine, Mpendazoe alisema atarejesha kadi ya CCM wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha mchakato wa kukisajili chama hicho.

Hata hivyo, pamoja na kuwepo kwa madai kuwa bado anapokea mshahara kama mbunge wa Kishapu, Mpendazoe alikataa kueleza kama madai hayo ni ya kweli.
"Mimi sijui kama bado napokea mshahara kwa sababu hainihusu sasa kama unahitaji kujua hilo naomba kaulizie kwa Katibu wa Bunge," alisema Mpendazoe.
Mpendazoe alizitaka taasisi za serikali ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutopendelea upande wowote katika kutekeleza majukumu yake.

Katika hali inayoonyesha kujiandaa na uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, CCJ kimewaomba wananchi kukichangia chama hicho ili kukisaidia kupata viongozi bora.
Wakati huo huo, chama hicho kimelalamikia hujuma zinazofanywa kwa chama hicho baada ya polisi kuwakamata baadhi ya viongozi wake wa mikoa na kubambikizwa makosa

"Kiongozi wa Mkoa wa Mara na Mwanza walikamatwa na polisi na kubambikiwa makosa, hata kule Arusha ilitaka kutokea tukio kama hilo" alidai Kiyabo ingawa hakuwataja viongozi hao.

Habari hi imeandaliwa na Hussein Kauli, Mahija Mpera na Mussa Mkama




Source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/5-habari-za-siasa/1590-ccj-kutinga-kwa-msajili-leo
 
Jamaa sijasikia haswa nini watafanya zaidi ya CHADEMA; TLP; CUF nk...............ni PANDIKIZI la CCM hilo jamani!!!

Ni kweli mkuu, kama mnataka kujenga nyumba moja kwa nini mpiganie fito? Je CCJ inakuja na lipi jipya ambalo CHADEMA, NCCR Mageuzi, CUF, TLP na vinginevyo halimo kwenye nia au dhamira ya kumkomboa mtanzania? Kadri vyama vinavyozidi kuongezeka ndiyo CCM inavyozidi kufurahi kwani bila kufikiria kuunganisha nguvu itakuwa ndoto kukiangusha Chama kongwe kama CCM.

YES, kama nikipata key issues ambazo CCJ inakuja ku-address kwetu ambazo CHADEMA na vingine vyote vimeshindwa ningefurahi zaidi, otherwise i'm not interested na hata taifa halifaidiki sana na ujio wa chama hiki, kusajiri vyama utitiri ni kuwachanganya watanzania.

Matokeo yake watanzania wanasema bora tuchague CCM zimwi likujualo.., na pia wahenga wanasema mkataa wengi ni mchawi - CCJ imewakataa wote hivyo lazima tuwe na wasiwasi nacho.
 
Tumtadhalishe Tendwa ,sasa hivi kuna vuguvugu kubwa sana la kisiasa. kama atalichukulia jambo hili kimsahamsaha baadaye atajilaumu. Mfano matukio yanayoonekana sasa, kubemba mapanga kudai haki zao - MSAKI bonde la mpunga, Mbezi JUU, Pugu KAJIUNGENI ,huko NGARA kwa kutaja maeneo machache tu inaonyesha watu wamechoka .Sasa tusubiri , haoni mkuu sasa anajisogeza kwa wakuu wa dini ,Mambo mazito kweli.
 
Mzee Mwanakijiji,
Mkuu inaonyesha una imani kubwa na hiki chama tofauti na vyama vingine. Pengine wewe unaweza kutuambia ni kitu gani kimekuvutia zaidi.. Ni bora kuanzia hapo kabla hatujatoa hukumu.

will do the needful.. next week..
 
Na mimi pia matumaini yapo kama hawatakuwa "Real Madrid" kwenye siasa zetu hapa. Waachane kabisa na "Ma- Galacticos"
 
Nimekuwa nikisema kuwa mabadiliko siyo tunayoyangojea au tunayoyaombea ni yale tunayoyaleta.. usalama pekee ni kwa msajili kutafuta sababu ya kunyima usajili wa kudumu!!! Nimekuwa nikimonitor wiki hizi chache wakati uhakiki wa ndani ulikuwa ukifanyika and I'm totally amazed... kwa wanaotaka vyama vya kisomi na wasomi vipo tayari. Kwa anayetaka mabadiliko CCJ is the answer!
 
kwani sheria inasemaje kuhusu ni muda gani vyama viandikishwe au visajiliwe? kwa nini uchaguzi ukikaribia ndio watu wanaanza kuandikisha na kusajili vyama halafu baada ya uchaguzi havisikiki tena. Vyama vilivyo serious vinasikika sikika mda wote hata kama havina wawakilishi bungeni hivi vinavyoibuika kwa moto na changamoto wakati wa uchaguzi huwa navitilia mashaka sana. only time will tell
 
Mimi hapa sioni hoja, kwamba CCJ ni mkombozi wa watu siju! kwamba Ndo suluhisho sijui Ila mambo yote yatakuwa wazi tu. Mimi namuomba Msajili wa Vyama akipe nafasi CCJ kionyeshe sera watu wachambu vinginevyo basi tutaamini kuwa na Msajili nae ni kibaraka wa CCM. Sisi tunataka ushindani wa Kweli. Kama CCM inajiamini kuwa ilishinda kwa kishindo mbona Basi inakiwekea mizenge chama cha CCJ? Ila hata kama CCJ kitapata usajili wa kudumu. Tuchambue sera zake na pia tuangalie ni kina nani watazama huko! Yasije kuwa Magarasa. Mimi sina chama Ila kwa Sera ya vyama Bado naona CHADEMA kinatoa sera Nzuri.
Maoni yangu kwa CCJ. '' Mkinyimw asajili wa kudumu, kwa wale wanaoona wana nia ya dhati kupigania taifa wajiunge CHADEMA.
 
mimi bado sijajiunga na chama chochote cha siasa...kwa anayefahamu wapi ntazipata sera za CCJ naomba anifahamishe ili nizisome, ila inaonyeshe uchaguzi mwaka huu unavutia, I'm interested in anything that can shake CCM!
 
Nimekuwa nikisema kuwa mabadiliko siyo tunayoyangojea au tunayoyaombea ni yale tunayoyaleta.. usalama pekee ni kwa msajili kutafuta sababu ya kunyima usajili wa kudumu!!! Nimekuwa nikimonitor wiki hizi chache wakati uhakiki wa ndani ulikuwa ukifanyika and I'm totally amazed... kwa wanaotaka vyama vya kisomi na wasomi vipo tayari. Kwa anayetaka mabadiliko CCJ is the answer!

MMKJ,

Mpaka sasa na kesho yote yameandikwa. Vitabu vingi wanafunzi wa kuvisoma ni wale wale.

Tatizo sio sera na maneno, ila ni watendaji ambao ni wananchi. GO TO THEM, IF THEY CHANGE, WE CAN MAKE CHANGES. CCJ will bring new good words as always BUT tanzanians will have the last say........Ndio domokasia, ndo mtaji wa CCM.

Goodlucky brother
 
[QUOTE=
Shalom;912098]Mimi siongelei vitu vya kwenye makaratasi bali naongele outputs mzee amaazo kwa nyerere naona zilikuwa haba
[/QUOTE]


Shalom dear, bila shaka umezaliwa juzi tu na hujui vyema historia na yale ambayo Mwalimu Nyerere alifanya kwa Taifa letu. Naomba nikumegee kiduchu. Pengine nifanye hivyo kwa kutoa mfano mmoja tu kuelezea sifa alizowahi kupewa Mwalimu kwa kufanya mambo muhimu kwa manufaa ya wananchi wa taifa alilokuwa akiliongoza.

Rais wa Benki ya Dunia alikuwa mmoja wa viongozi wa Kimataifa waliokuja kwenye mazishi ya Mwalimu Oktoba mwaka 1999. Huyu bwana katika salam zake za rambirambi alizozitoa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alisema hivi:

"Wakati wachumi wa dunia walipobishana juu ya umuhimu wa kupima ufanisi wa mitaji, Mwalimu Nyerere alisema kilicho muhimu zaidi ni watu kuweza kusoma na kuandika, kupata maji safi na huduma bora za afya…." (Tafsiri hii ya maneno ya Rais wa Benk ya Dunia ilitolewa kwenye magazeti wakati ule wa msiba wa Mwalimu).

Si huyo tu, viongozi wote wa kimataifa, wa nchi za Afrika na nchi jirani waliopata fursa ya kutoa salam zao za rambiramba walisema maneno yaliyodhihirisha jitihada na kazi kubwa aliyoifanya Mwalimu kwa maendeleo ya watu wa taifa lake, kusaidia na kuharakisha ukombozi wa bara la Afrika na kutafuta haki na fursa sawa miongoni mwa mataifa yanayoendelea duniani. Hayo yaliyosemwa hayakuwa katika makaratasi bali katika vitendo vya Mwalimu.

Tukichukulia mfano wa maneno aliyoyasema Rais wa Benki ya Dunia juu ya yale ambayo Mwalimu aliyaona ndiyo ya muhimu zaidi kwa wananchi; tukianza na elimu: Wakoloni (Wajerumani na Waingereza) walitutawala kwa takriban miaka sabini. Hawakujali kabisa juu ya elimu ya wananchi waliokuwa wakiwatawala. Matokeo yake mwaka 1961 wakati nchi inapata uhuru na Mwalimu anashika uongozi kulikuwa na Madaktari 12 tu Waafrika nchini, Engineers wawili, kulikuwa hakuna chuo kikuu hata kimoja nchini. Waingereza walipotakiwa kusema watajenga lini Chuo Kikuu nchini walisema labda 1967 wakitoa visingizio kwamba ilikuwa ghali mno kujenga chuo, kusomesha wanafunzi na kwamba kulikuwa hakuna idadi ya wanafunzi wa kutosha kulazimu kuwepo kwa Chuo Kikuu .

1961 Mwalimu alianzisha Chuo Kikuu nchini kikianza na wanafunzi 17, wakati anaondoka madarakani kulikuwa na idadi ya wanafunzi 3,400 katika vyuo vikuu viwili – UDSM na Chuo Kikuu cha madaktari Muhimbili. Wakati huo huo akiongozwa na dira ya Siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea, Mwalimu alijenga vyuo vingine – Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Chuo cha madaktari Muhimbili, Chuo cha Ufundi (DIT) na vingine mikoani. Kwenye shule za Sekondari wanafunzi Waafrika walikuwa wachache mno kwa sababu ya kubaguliwa; kulikuwa na shule za Wahindi, Wazungu na za Waafrika. Utaratibu huo wa kuwepo shule kwa misingi ya rangi ya mtu ukafutwa mara moja ili idadi ya Waafrika kwenye shule za Sekondari iongezeke. Zilikuwepo pia shule za kidini hasa za kikristo ambazo zilikuwa zikisomesha wakristo peke yao. Mwalimu akafuta mpango huo nao na shule zote zikawa zinachukua wanafunzi wa dini zote.

1961 wanafunzi wa shule za msingi walikuwa 480,000. 1985 wakati Mwalimu anaachia uongozi kulikuwa na wanafunzi 3,660,000 kwenye shule za msingi nchini wakisomeshwa bure bila kulipa hata senti tano. Shule za Sekondari za Serikali 1961 zilikuwa na wanafunzi 11,832 (wazungu, wahindi na Waafrika) ambao walikuwa wakilipa ada kwa maana hiyo walikuwa ni watoto wa watu wenye uwezo kifedha – waajiriwa Serikalini na kwenye sekta binafsi na wafanyabiashara. Mwaka 1985 kulikuwa na wanafunzi 40,617waliokuwa wakisomeshwa na Serikali. High School – form V & VI 1961 kulikuwepo wanafunzi 236 mwaka 1985 walifikia 2,125.

Mbali ya hatua za makusudi kuchukuliwa kujenga vyuo na shule za Sekondari ili kuwapa fursa wananchi wengi kupata elimu kulikuwa na training institutions za kila aina chini ya Wizara ya Elimu ilikuwa na zake na wizara zingine nazo zilianzisha kulingana na mahitaji ya Wizara husika kwa mfano kwenye Wizara ya Kilimo kulikuwa na vyuo vya kilimo ili kusaidia kukuza kilimo bora nchini; na kadhalika. Mashirika la Umma nayo halikadhalika yalikuwa na vitengo vyao vya mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi. Majeshi nayo yalianzisha Shule za Sekondari ili kutoa fursa kwa askari kujiendeleza kielimu – kwa gharama za Serikali; ilianzishwa Institute of Finance Management (IFM), Police Colleges, Elimu ya Watu Wazima; you just name them .... Nchi nzima ilikuwa inanuka elimu kwa wote!

Kwa taarifa yako Shalom na wengine wasiojua mambo aliyofanya Mwalimu, elimu ilikuwa ni bure kwa kila mtu na hayo yote yalifanywa na Serikali kupitia mipango ya makusudi ya Maendeleo kwa ajili ya wananchi wote. Serikali ilikuwa na "Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano' na kila baada ya miaka hiyo tathmini ilikuwa ikifanywa kuangalia mafanikio na mapungufu.

Si elimu tu hata upande wa Afya Serikali iliyokuwa ikifuata itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ilifanya makubwa katika kukuza na kuwapatia wananchi huduma za jamii bure bila malipo yoyote. 1961 kulikuwa na jumla ya hospitali za mikoa na wilaya 98 nchi nzima 1985 zikawa 149, vituo vya afya 22 – mwaka 1985, 239. Zahanati 975 mwaka 1961 – 1985 zilikuwa 2,644. 1961 asilimia 11 ya idadi ya wananchi milioni 10 wakati huo walikuwa wanapata maji safi. 1985 asilimia 50 waliweza kupata maji safi majumbani mwao ama umbali wa meta 400 kutoka majumbani kwao. Wafanyakazi wa sekta ya Afya waliongezeka kutoka madaktari 12 wakati tunapata Uhuru – daktari mmoja kwa watu 830,000. 1985 walikuwepo madaktari 782 waliofuzu kiwango cha kimataifa. 1985 AMOs walifikia 436 ukilinganisha na 32 waliokuwepo mwaka 1961. Mbali ya hao walikuwepo jumla ya Medical Assistants na Rural Medical Aids 6,328 mwaka 1985. Infant mortality rate wakati tunapata Uhuru ilikuwa ni watoto 225 wanaokufa kwa kila 1,000 wanaozaliwa hai 1985 ilikuwa ni watoto 137. Life expetancy ilikuwa miaka 35 wakati wa kupata Uhuru, ikafikia miaka 51 mwaka 1985. Leo bila shaka imeshuka kutokana na Sera za kibebari tulizozikumbatia!

Haya niliyoyaorodhesha hapa si mambo ya kwenye makaratasi bali ni vitu real vilivyotokea na kutendwa na Mwalimu kama kiongozi wa nchi kwa manufaa ya Taifa. Maamuzi ya makusudi yalichukuliwa ili ‘keki' ya taifa igawanywe vizuri, wananchi wafaidi matunda ya Uhuru na kuwepo uwiano wa mapato kati ya viongozi na wananchi.

Wapo watu humu ukianza kusifu juhudi za Mwalimu wanakuja na hadithi za kupanga foleni ya sukari, sabuni, colgate etc etc. Vitu ambavyo hata leo hii kwa mwananchi maskini ni luxury kwao ambayo hawaipati na hata kama bidhaa hizo zipo bwelele madukani mwananchi hana uwezo kifedha wa kuzinunua tofauti na wakati wa Mwalimu ambapo wananchi walikuwa na fedha mifukoni mwao wakihaha kuzitafuta bidhaa hizo.

Wengine wanadai Mwalimu aliifilisi nchi kwa siasa zake za Ujamaa zilizopelekea atumie fedha nyingi kuwapa wananchi huduma za bure. Kama nchi ilifilisika kwa ajili hiyo basi ilifilisika kwa nia njema na kwa manufaa ya wengi na si kama ilivyo sasa ambapo nchi inafilisika kutokana na ufisadi na ulafi wa viongozi wachache na wananchi wasio waadilifu. Hakuna kiongozi ama mtu yeyote wa ndani ama nje ya nchi anayeweza kudai kwamba Mwalimu alitumia madaraka yake kwa manufaa yake ama ya familia yake na rafiki zake. Ndio maana hata alipofariki wananchi walimlilia sana, viongozi wa Afrika na Dunia wakiwemo viongozi wa Marekani (Reagan akiwemo) walisifu uongozi wake uliokuwa unajali sana watu aliokuwa akiwaongoza kuliko kitu kingine chochote.

Itoshe kusema Mwalimu alijali Maendeleo yanayolenga Watu. Tujiulize, je viongozi wetu wa jana, leo na kesho wanajali maendeleo yanayolenga watu (wananchi waliowapa dhamana ya kuwaongoza) ama wanajijali zaidi wao, familia zao na marafiki zao?

Hivi kiongozi akishahakikisha anawapa wananchi wake elimu (bure), tiba (bure) na pembejeo (bure) kwa wakulima, ili wavitumie kujikwamua katika umaskini, kipi kingine cha muhimu zaidi anachohitaji binadamu?

Shalom, hapo sijaweka idadi ya viwanda vilivyojengwa enzi za utawala wa Mwalimu vilivyokidhi kila hitaji na baadaye vikabinafsishwa na hatimaye kufa badala ya Serikali kuamua kuchukua hatua za makusudi za kuvifufua kwa manufaa ya Taifa. Kama Mwalimu aliweza kuvijenga kwa nini wao washindwe kuvifufua? Ukitaka nikuorodheshee mema ya Mwalimu tutakesha mtandaoni! Nimalizie kwa kusema kwamba Mwalimu kama binadamu naye alifanya makosa ya hapa na pale katika uongozi wake lakini si kweli kwamba "outputs' zilikuwa haba kama ulivyodai.
 
Katibu mkuu wa CCJ anasema wanasubiri kudra za Tendwa katika kuipa Usajili wa kudumu, ila wao wametimiza kila lilipaswa, wanadhani Tendwa anahekima za kutosha, leo wamepokelewa na pale Masijala ya Msajili.
nawaombea kila la heri waweze kupata usajili wa kudumu.
 
Back
Top Bottom