TANZIA Captain John Komba afariki Dunia

Mwaka wa kuzaliwa utakuwa umekosewa haiwezi kuwa 1945 labda 1954. Apumzike kwa amani
 
sasa nyimbo tutatoa wapi?

Ndugu yangu kumbuka kuwa MUNGU,ndiye mtoaji wa vipaji tulivyonavyo,kwa hiyo naamini MUNGU ni mwema atatupa tena mtu km yeye,badala ya kuulizana kuwa nyimbo tutatoa wapi.ni vema kutumia muda huu kuwafariji wafiwa na kufanya maombi kumwombea mwenzetu ili basi Mwenyezi MUNGU,ampokee ktk Ufalme wake huko Mbinguni.
 
Mwingine aliyesema kuna Wazee wamekaeibia kufa ni Makonda na Ridhiwani ..na magazeti yaliwakariri haikua Tabia nzuri ,na ingewapasa waombe radhi
 
Wanabodi yoyote mwenye kufahamu historia ya aliekuwa mbunge wa Mbinga magharibi na kiongozi wa tot band marehemu capt komba naomba msaada

Nayotaka kujua toka kwa historia hiyo alijiunga na jeshi mwaka gani kalitumikia jeshi kwa mda gani na yapi aliyafanya ndani ya jeshi

Pia ni msukumo gani ulimfanya aachane na kazi ya jeshi akiwa na cheo cha ukapteni na kuamua kuingia ndani ya siasa.

Na mengineyo pia kama yatakuwepo kama kuzaliwa kwake na elimu yake

Natanguliza shukrani zangu.
 
Hamtakiwi kumsemea mabaya MTU alikufa alienda kaenda ndo mwisho Wa maisha yake hapa dunian tumuombee huko aliko coz hakuna aliyeenda akarudi akasema kukoje hatutamuona tena mh komba
 
kuzaliwa1954, shule ya msingi Lituhi 63-70, sekondari songea boys 71-74, ualimu Kleruu 1976, 1978 diploma ya cadet Monduli-jwtz, 1988-1990 diploma ya siasa ujerumani, 1992 alistaafu jeshini, 2006-2008 shahada ya siasa Washington. So kafanya ualimu for one yr, then jeshini, director TOT, mpaka anakufa alikuwa mkuu wa utamaduni CCM. Kwa kifupi kiongozi
 
Hamtakiwi kumsemea mabaya MTU alikufa alienda kaenda ndo mwisho Wa maisha yake hapa dunian tumuombee huko aliko coz hakuna aliyeenda akarudi akasema kukoje hatutamuona tena mh komba

Kufa kufa tu mkuu, hata tungelemba vp tutakufa tuu na hatuwezi rudi
 
john komba historia kwa kweli is nothing but miracles, binafsi nilisoma shule ya msingi Lugalo ambapo ndipo mkewe alikuwa akifundisha miaka hiyo ya 1980's kwahiyo nilikuwa karibu kidogo na familia kwa upande wa mkewe. komba ki professional ni mwl. wa shule ya msingi lakini mungu alimpa kipaji cha kuimba toka zamani alipokuwa kwy shule ya ualimu ndipo alipokutana na mkewe huyu wa kwanza aikuwahi kujua kama komba alikuwa na mke mwingine. siku moja kulikuwa na mashindano ya kwaya ndipo Rashid kawawa ndiye aliyemuona kwa kileo kawawa angeitwa mzee wa tanzania idol kwa maana aliweza kukiona kipawa chake na kuamua kumpeleka jeshini ili akaimbie jeshini ndio hicho kilichokuwa kikosi cha kwaya ya jeshi yeye ndiye alikuwa founder ambapo TOT ukaja kuwa muendelezo wake mara baada ya mfumo wa vyama vingi ulipoanza the rest is history.
 
Kama Watanzania Taifa la watu wenye UTU(humanity) tumefikia mahali hapa kufurahia kifo cha mtu na kushangilia basi ninasikitika sana KWELI ninasikitika sana, Marehemu Captain John Komba ni mwanadamu kama sisi na kama wanadamu wengine ana mazuri yake na mabaya yake ana mema na mapungufu siyo VEMA hata kidogo kumtukana Marehemu na kufurahia kifo chake! Hebu jiulize mwenyewe kama Captain Komba angekuwa mzazi wako au ndugu yako watu wakawa wanafurahia kifo chake ungejisikiaje? Kuingia msituni kupinga serikali tatu ni mtazamo wake maana anaona mapungufu ya serikali tatu na madhara yake na ninyi mnaopinga serikali mbili mna mitazamo yenu na mnaona mapungufu ya serikali mbili na madhara yake(hiyo ni mitazamo) na inatakiwa kupingana kwa hoja na tofauti zenu za mitazamo iwe ndiyo umoja wenu kama taifa la watu wenye utu na hoja siyo kutukana na kujengeana uadui, hakuna anayejua salio halisi la maisha yake! Komba amefariki but who's next? Labda mimi au wewe! Hivyo tuepuke kutoa majibu emotional maana si VEMA kwa kiongozi kuongozwa na hisia, wengi mmeonyesha hisia za chuki huku mkijinadi kama mbadala wa utawala uliopo I can tell you that the situation will worsen than now because you guys don't think like actual leaders! Act and live like a righteous leader even though you're not in the system, Nimesikitishwa sana na kifo cha ndugu yetu Captain John Komba alikuwa mwimbaji mzuri na mhamasishaji mzuri sana wa yale anayoyaamini, Mungu amrehemu na kumpumzisha, AMEN
na hayo marungu ya polisi mnayowaambia watupasue vichwa vyetu kila siku jee? na je kina mwangosi wao si watu? na hao albino mnaowakatakata kila siku kwa shughuli za matambiko ya kufukuzia madaraka na mali mnafikiri wao ni magogo? kumbe na nanyi mnajua sisi sote ni binadamueeeee???!!! maana mnavotutenda ni kama mwayatenda manguruwe vile
 
sasa ngoja uone wanafiki waliokua wanaponda ila sasa hivi wanajifanya wanakumbuka mazuri tu... Binadamu bna, psychology kweli ina mambo, mtu akifa no matter what utamuonea huruma tu
 
Kama Watanzania Taifa la watu wenye UTU(humanity) tumefikia mahali hapa kufurahia kifo cha mtu na kushangilia basi ninasikitika sana KWELI ninasikitika sana, Marehemu Captain John Komba ni mwanadamu kama sisi na kama wanadamu wengine ana mazuri yake na mabaya yake ana mema na mapungufu siyo VEMA hata kidogo kumtukana Marehemu na kufurahia kifo chake! Hebu jiulize mwenyewe kama Captain Komba angekuwa mzazi wako au ndugu yako watu wakawa wanafurahia kifo chake ungejisikiaje? Kuingia msituni kupinga serikali tatu ni mtazamo wake maana anaona mapungufu ya serikali tatu na madhara yake na ninyi mnaopinga serikali mbili mna mitazamo yenu na mnaona mapungufu ya serikali mbili na madhara yake(hiyo ni mitazamo) na inatakiwa kupingana kwa hoja na tofauti zenu za mitazamo iwe ndiyo umoja wenu kama taifa la watu wenye utu na hoja siyo kutukana na kujengeana uadui, hakuna anayejua salio halisi la maisha yake! Komba amefariki but who's next? Labda mimi au wewe! Hivyo tuepuke kutoa majibu emotional maana si VEMA kwa kiongozi kuongozwa na hisia, wengi mmeonyesha hisia za chuki huku mkijinadi kama mbadala wa utawala uliopo I can tell you that the situation will worsen than now because you guys don't think like actual leaders! Act and live like a righteous leader even though you're not in the system, Nimesikitishwa sana na kifo cha ndugu yetu Captain John Komba alikuwa mwimbaji mzuri na mhamasishaji mzuri sana wa yale anayoyaamini, Mungu amrehemu na kumpumzisha, AMEN
Naungana nawe kwa asilimia 100%.Chuki hata mtu anapofarikibado watu wana chuki nawe Tanzania tumefika pabaya. Capteni Komba hakuwa nazuri hata moja? Yeye ni Binadamu anaweza kusema kitu kiubinadamu tu.
Na kama wapenzi waupinzani mawazo yao ni haya na hulka zao ni hizi nina masikitiko makubwa kwani ni miezi tu imebaki na nachelea kusema hatuna mbadala, hatuna matumaini. Kwa sababuendapo mbadala tunaowategemea na wapenziwao wana hulka kama zinavyoji-display hapa naaam kwa hakika watanzania hatunambadala. Hiki ndio kitu kikubwa nilichojifunza kutokana na comments za kifo chaKapteni Komba, RIP.
 
Kipindi ambapo Mheshimiwa Warioba ni waziri mkuu marehemu John Komba alikuwa anaimba kwaya kwenye bendi ya jeshi(JWTZ) miaka ya 1988 na 1990
R.I.P John Komba(rtd) Captain.
 
Wanabodi yoyote mwenye kufahamu historia ya aliekuwa mbunge wa Mbinga magharibi na kiongozi wa tot band marehemu capt komba naomba msaada

Nayotaka kujua toka kwa historia hiyo alijiunga na jeshi mwaka gani kalitumikia jeshi kwa mda gani na yapi aliyafanya ndani ya jeshi

Pia ni msukumo gani ulimfanya aachane na kazi ya jeshi akiwa na cheo cha ukapteni na kuamua kuingia ndani ya siasa.

Na mengineyo pia kama yatakuwepo kama kuzaliwa kwake na elimu yake

Natanguliza shukrani zangu.

Nakupa mengine.
1.Alikuwa mpenzi wa LULU
2.Mbunge aliyelewa madaraka kwenye bunge la katiba
3.Kafa kwakutunga nyimbo za katiba nyingine wengine watakupa
 
Back
Top Bottom