~>>~ Capri Point ~<<~ The Erica Tossi Story... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

~>>~ Capri Point ~<<~ The Erica Tossi Story...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 8, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  From an "Upcoming novel"


  SURA YA 1X

  MIEZI MITATU ILIPITA tangu siku ile niliyokutana na mwanamke wa mwisho siku moja kabla ya kuamua kumpigia simu Erica na kumbembeleza anipe nafasi nyingine. Sikuamini nimeweza kukaa miezi mitatu bila kukutana na mwanamke kwani tangu uvuliana wangu sikuwahi kupita wiki nzima bila kufanya hivyo hadi nilipoanza kukutana na Erica. Sijui kama ilikuwa ni uponyaji wa aina yake au ni nafuu kwangu lakini Erica alikuwa ameniteka vizuri na alihakikisha habanduki kwangu. Na kweli hakunipa nafasi ya kuwa na mwanamke mwingine. Alizungumza na mimi akiwa kazini; na jioni tulikuwa pamoja na pale ambapo hatukuwa pamoja tulikuwa na mawasiliano ya simu au kutumiana ujumbe mfupi mfupi. Hakuwahi kupiga simu na kunikosa na alikuwa na tabia ya kupiga simu hata usiku wa manane na kwa woga wangu niliitikia hata kama nimechoka kiasi gani. Sikutaka afikirie kabisa kuwa kuna mtu mwingine zaidi yake.

  Hakuwa amenipa mapenzi kabisa zaidi ya kubusiana na kushikana shikana na wakati mwingine kunimaliza hamu zangu kwa njia alizozijua yeye &#8211; ambazo kwa kweli hazikuwa mbaya sana. Lakini alikataa kabisa kuvua nguo kabisa tuwe pamoja katika kumbatio la mapenzi. Aliniruhusu nimfanyie baadhi ya vitu ambavyo nilivjua anapenda lakini mara zote akiwa na nguo zake zote na kamwe si kitandani. Wakati tukilala kitandani alihakikisha sote tuko kwenye nguo zetu. Vyote hivyo vilinifanya nimpende zaidi nimtamani zaidi.

  Mwanzoni tuliporudiana tu alinilazimisha au kunikokota twende tukapime HIV na tulienda na pamoja na hofu zangu zote tulikutwa wote hatuna. Sikuwahi kuwa na mwanamke bila kutumia kinga. Ilipopita miezi mitatu alinikokota tena na miye sikuwa na wasiwasi wowote safari na kweli sote tulikutwa hatuna HIV. Alinifanya nijue ananijali na kunitakia mema japo mwanzoni niliona ni kama anataka kunipima. Nilitarajia tulipotoka Kliniki basi angenipatia vitu lakini haikuwa hivyo.

  "Usiwe na haraka very soon"

  "Ah miye na haraka tena wala sina, namna hii tunaweza kwenda mwaka mzima" na nilimaanisha. Kwani, hakuninyima kabisa na hakunipa kabisa lakini nilikuwa nataka nione vitu vyote vya ukweli niache kusingiziwa.

  "That's why I like you Shedrack" aliniambia na kujiachilia mikononi mwangu kunibusu na kuushikilia mdomo wangu kwa mdomo wake kwa sekunde kadhaa. Nilimvuta karibu yangu na kumminya karibu yangu nikisikia joto la mwili wake na moyo wake ukidunda.

  "Bora uniachie maana" nilisema kwani nilijihisi sehemu zilizokuwa zimelala zikiamka taratibu. Aliniachia. Niliamua kwenda kumuonesha nyumba yangu nyingine iliyoko Mwanza kwa siku mbili ili pia kupata nafasi ya kumtembelea Padre Smith ambaye baada ya kustaafu aliamua kufundisha Chuo Kikuu cha Mt. Augustino, Nyegezi Mwanza. Mzee kama nilivyozoea kumuita alikuwa amezeeka na nilikuwa najitahidi kwenda kuona mara moja kila miezi mitatu kwani ndiye mtu pekee ukiondoa mzee Peter na mkewe aliyekuwa kwangu kama familia.

  TULITOKA KUMUONA MZEE Nyegezi majira ya saa kumi na moja na kuelekea kwenye nyumba yangu maeneo ya Capri Point. Nyumba yangu iko upande wa kushoto baada ya kupita Tilapia Hotel kama unaelekea Mwanza Yatch Club. Haikuwa karibu kabisa na ziwa Victoria lakini kutoka nyumba ilipo siyo mbali sana na unaweza kuona Ziwa Victoria vizuri kabisa. Nilinunua kiwanja eneo hilo kabla watu wengi hawajahamia na nilifanikiwa kununua baadhi ya eneo la nyumba ya mzee moja ambaye kwa kweli alikuwa ameanza kuchoshwa na ujio wa watu wengi eneo lile na hivyo kunipa nafasi ya kujenga nyumba kubwa ya kisasa. Kwa kawaida, nyumba yangu nilikuwa napangisha wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Wakimbizi.

  Kabla ya kwenda na Erica nyumba ilikuwa imemaliza kufanyiwa matengenezo makubwa kufutia kuondoka kwa Mkurugenzi wa UNHCR pale Mwanza ambaye alikuwa anaishi pale na nilikuwa nafikiria kupangisha kwa mtaalamu mwingine kutoka nje. Ilikuwa pia ni nafasi yangu kuangalia maendeleo ya matengenezo hayo na kuwalipa baadhi ya mafundi na makandarasi. Tulifika Mwanza asubuhi ya Jumamosi kwa ndege na baada ya kufika nyumbani na kutua mizigo tulipokezana kuoga na baadaye ndio tulienda kumuona Fr. Smith kwenye nyumba yake pale Chuo Kikuu cha Nyegezi. Tulikula chakula cha mchana huko na kukaa naye kupiga soga hadi jioni. Fr. Smith alimpenda Erica na Erica alimpenda Fr. Smith mara moja; niliweza kuona furaha kutoka kwa mzee. Nakumbuka wakati tunaondoka aliniambia "don't lose this one son" nilijibaraguza kwa kucheka.

  Tulipofika nyumbani Erica aliingia jikoni na jiko lilimkoma. Nilijua kuwa Erica anajua kupika kwani alikuwa anafanya hivyo akija siku za Jumapili nyumbani kwangu kule Dar lakini siku ile ya Jumamosi nilikuwa na uhakika kuwa ni kweli alikuwa anajua kupika. Nilitaka kumsaidia lakini alinifukuza jikoni kwa busu la moto moto. Niliamua kwenda na kuangalia vyumba mbalimbali pale ndani na kujaribu kupata picha ya vitu ambavyo ningependa kuvifanyia mabadiliko. Kwa ujumla nyumba ilikuwa imesafishwa na kupakwa rangi na kuwa kama mpya. Taa za ndani zote na za nje zilikuwa ni mpya pamoja na bustani mpya ya maua iliyokuwa iko mbele ya bwawa dogo la kuogelea Pembeni ya bustani kulikuwa na miamba miwili mkubwa iliyoibuka toka ardhini na kufanya bustani ionekane ya asili kabisa.

  Mara baada ya chakula cha jioni tulikaa na kuzungumza kwa muda lakini binafsi nilikuwa nimechoka na ilikuwa ni nafasi ya kwenda kupumzika. Nilimuaga Erica kuwa naenda kupumzika kwani nilikuwa hoi bin taabani. Kesho yake tulikuwa tumepanga kwenda mjini kumuonesha jiji la Mwanza. Erica alikuwa hajawahi kufika Mwanza na ujanja wake wote na hiyo ilikuwa ni nafasi ya pekee kumuonesha mahali ambapo binafsi nilipaona kama nyumbani ukiondoa Tanga. Erica alibaki kuendelea kusafisha jikoni na akaniambia kuna kazi moja ya ofisini ambayo alitaka kuimalizia. Kama kawaida nilipoingia chumbani nilibadilisha na kuingia katika pajama zangu na haikunichukua dakika usingizi ukanichukua jumla jumla.

  Sikumbuki Erica aliingia chumbani muda gani kwani hata taa hakuwasha. Mwangaza wa mbalamwezi ulimulika chumbani kama unavyomulika kwenye nyumba yangu ya Dar. Napenda vioo sana na kuacha mwanga wa asili kumulika ndani. Kilichonishtua usingizini ilikuwa ni harufu ya manukato yale yale ambayo harufu yake haikunitoka. Ninayakumbuka kwani Erica alijipulizia ile mara ya kwanza nilipoenda kumchukua na nilisahau hata kumuuliza yalikuwa ni manukato gani. Nilishtuka usingizini baada ya kuhisi chumba kizima kimejawa na manukatayo yale na nilijisia furaha ya aina fulani. Nilifikisha macho kuweza kuangalia vizuri.

  "Erica!" niliita kuhakikisha kuwa ni yeye yumo mle ndani kwani niliweza kuona mtu kasimama mbele kabisa ya kitanda akiw anatokea mlangoni. Nilikuwa na uhakika ni mwanamke kwani umbile lake pamoja na giza lilikuwa wazi kuwa mwanamke.

  "Shhhhhh" aliniambia huku akitembea kwa taratibu kuja kitandani. Nusura nikimbia kwani macho yangu hayakunidaganya. Erica alikuwa kama alivyokuja duniani. Nilifikicha macho yangu tena kuhakikisha kuwa haikuwa ndoto moja tamu lakini nilipokaa sawasawa Erica alikuwa amesimama pembeni yangu upande wa kulia wa kitanda jinsi alivyo, kila nchi ya mwili wake ikiwa shahidi yangu. Nilijikuta nameza fundo kubwa la mate kwa nguvu na kupaliwa kwa ghafla. Nilikohoa.

  "What are you doing?" nilimuuliza kwa kushtuka huku nahema kwa nguvu.

  "What do you think I'm doing" Alisema kwa sauti ya upole. Nilivuta swichi ya taa ndogo ya umeme pembeni ya kitanda ambayo iliwaka na kuleta mwanga kama wa mshumaa. Mwanga ule ulifanya mwili wake mtupu ung'are kwa rangi ya dhahabu kama kuku wa kuokwa. Nilinyanyua mkono wangu wa kulia na kuutuliza upande wa kushoto wa paja lake. Niliupapasa mkono wangu kwenda juu kiunoni taratibu kama kuhakikisha kuwa ni yeye. Aliguna kidogo. Nyuma yake kulikuwa na meza ya kujipambia ambayo ilikuwa na kioo kikubwa.


  Kioo kile kilinipa nafasi ya kumuona Erica kwa nyuma na kulifurahia umbo lake la kike. Alikuwa amevaa shanga za dhahabu zilizotengeneza mistari miwili kiunoni. Macho yetu yalikutana na kabla sijasema lolote alinibusu midomoni. Usingizi wote ukanipeperuka kama mvuke. Niliamua kuamka kabisa na kuketi kwenye ukingo wa kitanda; nilifungua miguu yangu na Erica akasimama yangu mikono yangu nimeizungusha kwenye kiuno chake. Moyo ulikuwa unanienda mbio kuliko daladala lililokosea njia. Macho yake yalikuwa yanamulika mulika kama nyota za alfajiri huku nisikiliza sauti ya kuhema kwake. Alikuwa amepandwa na ashki ambazo nilitakiwa nizitulize. Sikutaka kukurupuka kwani nilitambua hii ilikuwa ni uchaguzi wake, kwa muda wake na namna yake. Nilikuwa kama mbuzi akipelekwa machinjioni. Nilikuwa nafuata tu.

  Nilibusu tumbo lake.

  "aaah!" aliitikia na mikono yake ikishika kichwa changu. Vidole vyake vilikuwa na ubaridi ambao ulinifanya nami nizidi kupandwa na mzuko. Nilitumia ulimi wangu kulamba mwili kuanzi kitovu kuelekea kifuani. Erica alirudisha kichwa chake nyuma na nywele zake ndefu zikadondoka mgongoni mwake.

  Niliweza kuangalia matiti yake kama vilima vya Kibo na Mawenzi ambavyo juu yake vinara viwili vya Mwenge wa Uhuru vikinikaribisha. Taratibu nilivielekea vinara hivyo kama shujaa aliye tayari kuliteka taji la Ufalme uliotukuka. Kama mchezaji Messi uwanjani nilianza kuonesha umahiri wangu; vidole vyangu vilimvuta saidi. Midomo yangu ilipokamata kilele cha kulia katika vile vilima viwili Erica alipiga ukelele.

  "Ooh Shedrack!"

  "Oh Baby!!" Midomo yetu ilikutana na kusalimiana huku ndimi zetu zikikumbatiana na kugaragazana kama mabingwa wa mieleka. Tulikuwa katika hali hiyo kwa dakika chache. Nilivua shati langu la pajama. Erica alinisaidia kuvua suruali. Nilimpokea mikononi mwangu nikiwa bado nimeketi kwenye ukingo wa kitanda. Alinisukumiza chini kwenye kitanda na bila ajizi nilitii. Sikuwa na ujanja. Erica naye hakunionea huruma, hakunionea haya, na hakunibakisha. Nilikuwa kama swala aliyepotea njia mikononi mwa Simba jike mwenye njaa. Alinirarua. Hatukwenda mjini kabisa kama tulivyopanga na tulibakia pamoja.


  Mgeni pekee aliyekuja siku ile alikuwa ni Msimamizi wa mafundi ambaye alikuja kuchukua malipo yao na maelekezo mengine. Nilikaa naye kwa dakika kama thelathini tu na kumruhusu aondoke &#8211; yeye mwenyewe alifanya haraka ya kutaka kuondoka kwani harufu ya mapenzi ilikuwa katika anga zima la Capri Point. Tulikuwa ni mimi na Erica; Ericca na mimi. Kiu yote ya miezi karibu mitano tangu tufahamiane tulijitahidi kuiondoa. Na tulivyojitahidi ndivyo tulivyozidi kuichochea. Jioni tuliondoka kwenda kwa Fr. Smith kumuaga kwani kesho yake tulikuwa tunarudi Dar. Usiku uliofuatia ilikuwa ni zaidi ya jana yake, nilifurahia jinsi nilivyosubiri na nilifurahia jinsi ambavyo Erica kweli alikuwa si mchoyo wa mapenzi.


  Moyo wangu kwa mbali niliona ukifungua uponye wa kitu ambacho nilikikana kuwa kinawezekana; nilitambua kuwa nampenda Erica na nisingeweza kuishi bila yeye. "Erica, I love you" nilijikuta nasema saa kumi za usiku tukienda kulala. "Shedrack I love you too" Alijibu na kunisindikiza usingizini na busu huku akilaza kichwa chake kifuani kwangu. Usingizi uliponichukua nilijikuta narudi siku ile nilipopata busu langu la kwanza kwa yule binti niliyempenda. Miaka ile mingi iliyopita kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima, Chumbageni Tanga.


  Nakumbuka siku ile isiyo jina niliimba wimbo ule ulioimbwa na mojawapo ya kwaya maarufu za Kikatoliki nchini. Mbingu ni zako Ee Bwana, na nchi ni yako Ndiye uliyeumba binadamu na kila kitu kilichomo. Taratibu nilipeperuka katika usingizi mtamu na mnono; nikijihisi kama natembea kwenye mawingu, kwenye mbingu ya saba. Sikumjua Erica. Sikujua nini kilikuwa kinaningojea.


  (The story continue..)


  Kama unapenda kuweza kukishika kitabu hiki chenye simulizi la kukufanya ulie, ucheke na upatwe na hisia ya joto la ghafla let me know. Tukipata japo watu 100 of die hard fans tutakichapisha TZ mapema zaidi. Hit me with a PM just title "Count me in" kwenye subject na kwenye body andika mji uliopo. Shukrani.
   

  Attached Files:

 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Thank you peopleeeeees!!
   
 3. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Simulizi imetulia binafsi nimeipenda na inamafunzo pia sa sijui kama ni true story inayokuhusu binafsi au ni hadithi tu.
   
 4. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Hii story ni nzuri,ila haifai kusoma ukiwa na upweke,inaleta machungu,watu wazima watanielewa hapo.
   
 5. Y

  YE JF-Expert Member

  #5
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kaka umeanza ugomvi tena.......kiu hii!
   
 6. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #6
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  kudos kiongozi!

  Aah kama napaona capri point, ng'ambo ya pili kisiwa cha Sanane.
  Story tamu sana
   
 7. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #7
  Dec 9, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapo sasa! MMKJJ unatutega ehhh?
  Huo mgongo wa bwana kaka hapo mbona utatupa akina dada tabu!
  Wengine tuko mbali na nyumbani.I feel home sick!
  Mashostito mnasemaje?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Mmh TM mbona hiyo kali! tangu lini wanawake wanaweza kuvutiwa na mgongo wazi au kifua wazi cha mwanamme? Tunaambiwa kuwa wanawake wanasisimuliwa kwa kuguswa siyo kwa kuona sasa hii ya wewe kushtushwa na mgongo umenifanya nichekeee. Kweli hii maana itabidi wengine tuanze kuachilia achilia vifua kidogo! (na mgongo?)
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hee ugomvi tena.. nilidhani ni burudani
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  yeah

  ina maana ni vizuri kuita mashosti msome pamoja?
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Wenzio tuko karne ya 22 teyari,lol!
  Umechokoza kiu.
  High time tuwa-support waandishi wazalendo. Tuanze kununuliana zawadi za vitabu pia. My pm follows, ngoja nikamsake na Lizzy sijui kakufilia wapi!
  NB: unge-alert pia tuseme number of copies tunazotaka...
   
 12. B

  Bhavick JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 314
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Aah,tamu sana,imeniacha hoi na upweke nilionao,nimejickia fresh!
   
 13. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #13
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Touching love story, MMwanakijiji ungeibandika na (c) ili akina Shigongo wasiipore na kuichakachu! Otherwise count me in.
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  dah MM ngoja nicheki kwanza miaka 50 ya uhuru inasemaje nitarudi kusoma hapa najua hii kitu itakuwa si mchezo
   
 15. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #15
  Dec 9, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,865
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Nami nahitaji nakala kadhaa za vitabu hiki kwa ajili yangu na wadau wangu wa karibu, nitakutumia PM
   
 16. amkawewe

  amkawewe JF-Expert Member

  #16
  Dec 9, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 2,029
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  yes MM.
   
 17. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #17
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Your talent is Great Mkuu.... Bravo.
   
 18. kwempa

  kwempa Member

  #18
  Dec 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Help me, I have read this story. In fact, it is too emotional. I need to join the die hard..
  How do I join?
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Dec 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Jamani, ninaposema unitumie PM manake ni kuwa ni rahisi kutrack kujua nani anaweza kwani threads huwa zinapotea n.k Ukiniandikia PM manake naziwekakwenye folder ili kikiwa tayari watu wa kwanza kupewa ofa (yaweza kuwa hata na discount) ni hao 100 wa kwanza ambao ndio nasema ni "die hard" fans. Thanks
   
 20. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu umedanganya kidogo sehemu ambapo nyumba yako ilpo japo ni story. upande wa kushoto ukitoka tilapia hotel inafuata yatch club, hapo katikati hakuna nyumba ya makazi. mbele ya yatch club kuna mlima wa mawe na makaburi
   
Loading...