iNine9
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 5,008
- 9,408
Kuna siku niliplay hizi ngoma studio kwa Radio station moja nlkua nafanya kazi, baada ya show kuisha niliitwa na mkuu wa Idara yetu nikaulizwa unatumia majani? Nikawaambia hapana sijawahi hata na ukoo wetu mtu akitumia anawehuka (serious iko ivo kwetu mtu akivuta anadata jumla) nikawaambia ila nazipenda tu hizi ngoma sabu lugha iliyotumika humo ni ngumu kumeza. Nikasikia naambiwa tu kwenye notice ya pale juu tuliyopandika yenye nyimbo zaidi ya 10 zilizozuiwa kuchezwa redioni na TCRA na hizo 2 tunaziongeza DJs tukazuiwa kupiga hizo ngoma bana kwa hiyo station, daah basi bana ikanibidi nitekeleze tu make ngoma ya mmasai ilingiliwa na mmang'ati.


