cariha
JF-Expert Member
- Apr 9, 2015
- 22,077
- 46,326
Intelligence yetu huwa inafatilia mno siasa aisee, wajikite kwenye uchumi, wenzetu wanaanzisha NGOS kwa malengo flani flani huku kwetu kufatilia wakosoaji tu.Ufafanuzi ni kwamba nchini Marekani na nchi nyingine zilizoendelea ndiyo wanaofata vizuri kanuni za kuajiri watu wa kitengo,yani ni wale tu wenye IQ kubwa na si vinginevyo.Na ndiyo maana hata ukiwa bar nchini Marekani huwezi kusikia mtu akijisifia kuwa yeye yupo kitengo.Ushahidi ni huu ufuatao;Marekani hao watu wa kitengo wapo wengine wanaoshughulikia ujasusi wa kiuchumi,yani wanaenda nchi nyingine kwa lengo la kuchunguza namna ya kufanya ili nchi yao ipate uchumi mkubwa kwakupitia nchi nyingine.Wakati viinchi maskini vimejikita ktk ujasusi wa kidola tu,huku uchumi ukiachwa pembeni,na ndiyo maana mikataba ya kijinga inasainiwa.Ikumbukwe watu wote wenye IQ kubwa hufikiri kwa kutumia ubongo na siyo tumbo.