Call ya house girl kwa mume wangu

Call ya house girl kwa mume wangu

Asante mkuu lakini issue pia kwanini alificha ile simu wakati yeye alipigiwa? si angesema tu ni dada wa kazi? sasa hii ya kuficha ndio ambayo imenipa maswali zaidi
Alikuwa ameshakudanganya kwahiyo akikupa simu utaona call ya house girl na ww utalalamika kwanini unanidanganya na utasema kwanini unidanganye lazima kuna kitu,na wanawake mnavyopenda kuforce mambo,imenitokea Mara nyingi sometimes nakuwa sijakusudia kitu ila kwake italeta picha mbaya lazima nidanganye,hiyo ishu ni ndogo mno mi naona we ndo unacomplicate
 
kumbe shida ni kukubali maneno ya nje ya umbea umbea..hata mkibadilisha vipi ni yaleyale

Philosophy za binadamu linapokuja swala la kuchitiana zinatofautiana sana. Kila mtu ana njia yake ya kujaribu kutatua tatizo na inaweza kuwa nzuri au mbaya; hasa hasa unaposhtukizwa.

Ni kumwomba Mungu haya yatupite kwa mbali au yakitukuta basi tujue ni namna gani tunaweza kupambana nayo.
 
Kumuondoa huyo dada siyo suluhisho. Tatizo liko kwa mumeo. Mume kama hajiheshimu tatizo litaendelea hata kama utaleta mwingine labda ukae bila housegirl. Hakuna msichana anayezoeana na mwanaume kama mwanaume mwenyewe hajakaribisha kuzoena naye. Mumeo akiwa serious sidhani kama kuna msichana atakaye msogelea.

Utamchunga mumeo dhidi ya housegirl, Je; na huko barabarani au mtaani au ofisini utaweza kumchunga kote huko? Punguza munkari endeleeni kuaminiana maisha yasonge.

Halafu kaa na mumeo muulize ni kitu gani anachomiss kutoka kwako mpatie. Unaweza kuta ni kitu kidogo tu kinamtwist mumeo ambacho ungeweza kumfanyia mumeo akasahau kabisa hayo maujinga ya housegirl/wadada wa huko mtaani. Wanaume wengi ni wagumu sana kuwaambia wake zao kitu wanachohitaji kufanyiwa ili waridhike.

Nakutakia kila la heri kwa hili uweze kulitatua kwa kutumia busara.
Wako mtiifu katika ujenzi wa Taifa.
Ujumbe unefika
 
Habari zenu wanaJF,

Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni.

Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sasa hivi? Mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. uliongea na nani? Akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu.

Nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie.

Sasa hii ya juzi imenishangaza, niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpaka hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo.

Usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. Nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? Dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wa kuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavyokuheshimu tukamaliza hapo.

Siku ya pili dada akaniita ana shida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivyo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vipi ukiondoka utajisikia amani? Akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka yake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka yake kumwambia kilichotokea, hivyo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vipi?

Nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivyo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka.

Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani.

Hivyo ubabe huu anaojitika ni wa nini? Niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao, hivi ni pepo au wapuuzi?

Naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo.[/QUOTE
This shit is really fucked up what she did.
 
Asante mkuu lakini issue pia kwanini alificha ile simu wakati yeye alipigiwa? si angesema tu ni dada wa kazi? sasa hii ya kuficha ndio ambayo imenipa maswali zaidi
Alikuwa ameshakudanganya kwahiyo akikupa simu utaona call ya house girl na ww utalalamika kwanini unanidanganya na utasema kwanini unidanganye lazima kuna kitu,na wanawake mnavyopenda kuforce mambo,imenitokea Mara nyingi sometimes nakuwa sijakusudia kitu ila kwake italeta picha mbaya lazima nidanganye,hiyo ishu ni ndogo mno mi naona we ndo unacomplicate
uache kutengeneza mahusiano yasiyofaa na wanawake wewe. jiheshimu.

sifanyi utani wa hivyo mimi.
Utataniaje na friends WhatsApp groups na kuitana baby?hizo ni dalili za kuchepuka,unajua umeolewa kwann usikae mbali na mambo yanayohatarisha ndoa?matani ya hivo ni kutokujielewa,unasikia raha gani kuambia baby wakati umeolewa kama sio pepo la ngono
 
"...kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie..."
Your households is not built on trust, if you don't solve it soon or later it will crumble down.
Chukua muda kaa na mumeo na muamue kuishi kwa uaminifu.
 
Mleta mada, hapo kwenye "mume akashuka, then mimi nikaondoka", mmmh. Kwa nini mlifanya hivyo? Nani mmiliki wa usafiri wenu, wewe au mumeo?
Hata kama usafiri ni wa kwake, hakupaswa kufanya hivyo. Mtani Ukikuta popote wanakofunza kuhusu ndoa , basi hawaishi kutaja neno uvumilivu, hicho ndicho alichokikosa dadaetu, Na ndicho kinachomtesa mpaka sasa. Namuusia tu kuwa ajishushe amwombe mumewe msamaha kwanza kwa kosa la kuondoka na kumwachan njiani, kwa kosa la kumuuliza kosa na kumkanya mbele yaHouse Girl. Vingnevyo asitarajie kuwa mumewe atajishusha aombe msamaha. Hiyo haitokei mtani.
 
Sasa unajiumiza nini wakati huna ushahidi... na kwa nini muishi maisha ya kupekuana simu..m daah poleni sana...
 
Kwa mujibu wa maelezo yake wakati akijitetea kwako ni kwamba siku huyo Dada alipokuja kwako kwa Mara ya kwanza mumeo ndiye aliyempokea(nahisi ni stand) hivyo aliweza kuwasiliana naye kwa simu kujua alipo na atafika muda gani ili apokelewe, kwahiyo hapo unaona kwamba mumeo alifahamiana na house girl wakati huo, je kuna ubaya kwa house girl huyo kuomba vocha kwa mumeo ikiwa aliona ana shida ya haraka anayoona ni muhimu sana kwake? Pamoja na hayo ulipaswa kufanya uchunguzi kwanza ama kumuonya house girl huyo akiwa mwenyewe ili asijue wewe na Mme wako hampatani vizuri.

Matokeo ya wewe kumketisha pamoja na mmeo na kumpiga mkwara kumemfanya ajue kwamba wewe na mmeo mna mgogoro wa ndani na kwamba hata siku ukiwa haupo mmeo akalala nawe hutajua kwa sababu anajua mmeo naye anakuficha hivyo ulikosea na kupatia kwa hatua hiyo ya kumuonya mbele ya mmeo.
 
Dada tulia fuatilia taratibu kama kuna jambo utawakamata tu halafu kaa mumeo muambie umekosea kumtuhumu yeye atafurahi halafu atajiona kashinda halafu atarudia utawakamata tu
 
Hata kama usafiri ni wa kwake, hakupaswa kufanya hivyo. Mtani Ukikuta popote wanakofunza kuhusu ndoa , basi hawaishi kutaja neno uvumilivu, hicho ndicho alichokikosa dadaetu, Na ndicho kinachomtesa mpaka sasa. Namuusia tu kuwa ajishushe amwombe mumewe msamaha kwanza kwa kosa la kuondoka na kumwachan njiani, kwa kosa la kumuuliza kosa na kumkanya mbele yaHouse Girl. Vingnevyo asitarajie kuwa mumewe atajishusha aombe msamaha. Hiyo haitokei mtani.
..asante mtani, umeeleza vema sana. Nilimuuliza makusudi nione atajibu vipi, bahati mbaya Mkebora kaingia mitini. Siamini mke aniache njiani, aende zake home, then atuite mimi na msaidizi wa nyumbani, atuketishe, atudadisi na kutuonya...damn, anionye mbele ya msaidizi wa nyumba yetu. Mungu na atusaidie na kuzisimamia ndoa asee.
 
chanzo ni wewe kutomtumia vocha huyo dada wa kazi. nahisi ungetuma vocha huo mgogoro ungekuwa haupo maana hangempigia mumeo kuomba vocha. Uzuri ni kwamba wewe mwenyewe unasema ulisikia sauti ya huyo dada akiomba vocha kwa mumeo ili apige simu nyumbani kwao. Sion tatizo kwa mumeo zaidi ya wewe kujaribu kulikuza jambo dogo kuwa kubwa.

Pia unaonekana kuhamisha tabia za shemej zako (wadogo zake mumeo) na kuzihamishia kwa mumeo huku ukikiri kwamba mumeo hajawahi kuwa na tabia kama hizo. acha kubomoa ndoa yako kwa mikono yako.
 
Habari zenu wanaJF,

Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni.

Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sasa hivi? Mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. uliongea na nani? Akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu.

Nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie.

Sasa hii ya juzi imenishangaza, niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpaka hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo.

Usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. Nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? Dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wa kuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavyokuheshimu tukamaliza hapo.

Siku ya pili dada akaniita ana shida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivyo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vipi ukiondoka utajisikia amani? Akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka yake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka yake kumwambia kilichotokea, hivyo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vipi?

Nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivyo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka.

Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani.

Hivyo ubabe huu anaojitika ni wa nini? Niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao, hivi ni pepo au wapuuzi?

Naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo.
Nenda Ka print call history. Fanya hivi for your own peace of mind! Otherwise itakupa shida na kuharibu mahusiano na mumeo. Utakuwa unahisi unaibiwa muda wote.
 
Alikuwa ameshakudanganya kwahiyo akikupa simu utaona call ya house girl na ww utalalamika kwanini unanidanganya na utasema kwanini unidanganye lazima kuna kitu,na wanawake mnavyopenda kuforce mambo,imenitokea Mara nyingi sometimes nakuwa sijakusudia kitu ila kwake italeta picha mbaya lazima nidanganye,hiyo ishu ni ndogo mno mi naona we ndo unacomplicate
Kabisa mkuu mimi sijaona kesi kubwa hapa, mumewe aliamua kuepusha shari vizuri tu sasa kisa cha kumnunia mpaka leo ni kipi ukute hata unyumba hampi, sasa si ndo atamtafuna dada vizuri, kumwomba vocha mbona kawaida tu maana huenda alikuwa na jambp la dharura home akaamua ajaribu na kwa mzee, sasa mama wa nyumba umekuja juu kiasi hicho kweli??
 
Huna haja ya kumfukuza huyo dada kwa sasa ila ajiri houseboy...........


Utaona tu panic...
 
Kwa maelezo yako sijaona udhibitisho usio na shaka kwamba ulichohisi kimetokea ndicho. Inaonekana unaamini hata kwa hisia tu. Nilidhani ulipohisi ungetulia kwanza uweke mtego na bila shaka ungewafuma tu maana hiyo kitu haijifichi muda mrefu. Kwa vile umewahi watatafuta mbinu nyingine kama kweli walishaanza uhusiano.
Mpaka anawafuma si mambo yanakuwa tayari heri alivyowahi akakurupua mipango kabla haijatekelezwa.
 
Back
Top Bottom