Habari zenu wanaJF,
Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni.
Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sasa hivi? Mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. uliongea na nani? Akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu.
Nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie.
Sasa hii ya juzi imenishangaza, niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpaka hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo.
Usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. Nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? Dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wa kuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavyokuheshimu tukamaliza hapo.
Siku ya pili dada akaniita ana shida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivyo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vipi ukiondoka utajisikia amani? Akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka yake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka yake kumwambia kilichotokea, hivyo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vipi?
Nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivyo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka.
Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani.
Hivyo ubabe huu anaojitika ni wa nini? Niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao, hivi ni pepo au wapuuzi?
Naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo.