Call ya house girl kwa mume wangu

Call ya house girl kwa mume wangu

Mpe chake housegirl aende, kikubwa watakachokifanya ni ku improve level of secrecy na intelligence, usisite kufanya maamuzi. Kama una evidence mwache aende.
 
Nimesoma page ya kwanza tu nikahamasika kuchangia. Sijui wengine wamechangia nini! Cha kufanya fanya uchunguzi wa kina kabla ya kumfukuza huyo dada. Pia, kwa jinsi ulivyowaonya inawezekana Mr. akajirekebisha. Anza kutafuta dada mwingine taratibu bila papara ili utakapojiridhisha umrudishe kwao wakati umeshapata wa kuziba nafasi yake. Kama Mr ameshamuonja huyo dada, bado wataendelea na mahusiano hata kama ataondoka huyo dada. Jitahidi kidhibiti mahusiano yao ili Mr asije akanogewa akamfanya nyumba ndogo huyo binti, vinginevyo utajuta kuolewa!
 
Na wewe kiherehere kimezidi, achana na simu ya mumeo. Inawezekana kakuchoka una kimbelembele. Uangalie simu ya mumeo ili iweje wakati umemsikia akiongea?

wewe ndie una kiherehere ulitaka niangalie simu yako wewe? usikute mwanaume unaandika hayo itakuwa hasara kwa mkeo maana umeandika kimipasho sijui wa jahazi modern wewe
 
Umeshindwa kutuwekea ushahidi wa jambo hilo, bali unalazimisha utoe hukumu kwa hisia zako... Me naona unajitengenezea stress bure tu. Msichana ana siku ya 3 - 5 hawezi jengo mahusiano haraka hivyo, nakataa. Umeunganisha unganisha matukio ukaona inafanana na uwazalo, lakini huo ni wivu tu,... Mume huwa anachukua mda mrefu sana kupigwa housegirl, lazima ajihakikishie Kuwa mdada ana moyo na muelewa wa kuficha mambo haya. Utamaliza mabinti aisee.....
 
Nimesoma page ya kwanza tu nikahamasika kuchangia. Sijui wengine wamechangia nini! Cha kufanya fanya uchunguzi wa kina kabla ya kumfukuza huyo dada. Pia, kwa jinsi ulivyowaonya inawezekana Mr. akajirekebisha. Anza kutafuta dada mwingine taratibu bila papara ili utakapojiridhisha umrudishe kwao wakati umeshapata wa kuziba nafasi yake. Kama Mr ameshamuonja huyo dada, bado wataendelea na mahusiano hata kama ataondoka huyo dada. Jitahidi kidhibiti mahusiano yao ili Mr asije akanogewa akamfanya nyumba ndogo huyo binti, vinginevyo utajuta kuolewa!

Nimekuelewa Mshua asante kwa ushauri wako, ubarikiwe kwa busara na hekima hii iliyokujaa
 
Jaribu kumkanya na mumeo maana ndio yanaanzaga hivo hivo mwisho utaondoka wewe.
Amkanye mume nani kakuambia mwanaume anatishiwa poooo,chamsingi dada mwenye mume abadilike afundwe kwanza namna yakudili na mwanaume,sasa siata mama yake atamuonea wivu kama akija na akiwa karibu na mume wake,acha kutafuta ushauri kwa walioshindwa kwenye ndoa zao,mtangulize MUNGU MKUU ndio jawabu kubwa,umeniuzi sana ningekuwa karibu kadi nyekundu,nakuambia Leo kbsa,usiombe ushauri Wa mapenzi yako na mume wako kwa wanawake Wa rika lako,tafuta ata kwa wanaume warika lako watakupa majibu mema kwani sisi tunajuana tulivyo,watakupoteza hao wanasichana wenzako ambao kwao yamewashinda
 
nashangaa mnaosema eti usiguse simu ili usipate pressure. hivi mnajielewa lakini! au ndo mshakata tamaa kuwa Hamna vya Peke yenu?

poleni. ndo madhara ya kuendekeza michepuko. mshaona kitu cha kawaida..

toka mwanzo mmekubaliana ni one man one woman. kama mmoja hawezi aseme toka mwanzo. sio kuja kumuumiza mwenzako baadae.

au kama vipi mkubaliane muwe in an open relationship. atakayejisika kutoka atoke. ndo hapo uone wanaume wa kibongo wanavyotokwa povu. wanataka wachepuke wao tu. ovyo!

semeni usichunguze chunguze simu for privacy purposes. hata kama you're a couple haimaanishi kusiwe na personal privacy.
lakini hata ukiamua unataka kuona kwani kuna tatizo!!!
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
Kumbe huyo muharibifu,ikiwa hivyo hafai
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
Kama uko serious unataka house girl mbona wapo kibao tu sema kuwatoa mashambani huko huwa wanataka pesa za kuacha makwao tu, zaidi ya hapo ni uhakika wa mshahara.... ila pole sana ushauri wangu ni kuacha kumfikiria mr namna hiyo... Hilo lilishawahi kutokea kwa upande wangu ila lilikuwa tofauti kidogo, Ni kwamba mke wangu ni mkali namfahamu vizuri tu sasa hapa tulikuwa na house girl alikuwa mchapa kazi tu kuna siku huyu House girl alikuwa anaumwa mke wangu alipoambiwa akaona kama anakwepa kazi maana asubuhi yake alikwenda mafundisho ya kipaimara vizuri tu hivyo wife akamkatalia kumpeleka hospital, Tukiwa na wife yule binti akanipigia simu nikamuuliza ni nini? akaniambia mwanzo mwisho kuwa ni mgonjwa basi nikamwambia mie nakuja home nitaongea na mke wangu ili tukupeleke hospital.. Nilipomwambia wife hakutaka kuelewa mie nikaona bora nimchukue binti akapime kweli alipopima alikuwa na malaria 3... Nilipo rudi hom hayakuwa maelewano mazuri ila baada ya muda akaelewa na huyo House girl hayupo hapa home.. Hivyo nakuomba umeelewe Mr alishindwa kukueleza akihofia mambo kama hayo.. Ila na yeye alifanya makosa kukukatalia kwamba hajaongea naye.
 
hivo ndio inatakiwa ili kuweka umbali kati ya dada wa kazi na baba mwenye nyumba, maana kesi za hizi zimeshakuwa nyingi sana

Mimi nimeshakaa na house helpers kama 8 sasa kwa miaka 12 ya ndoa na mke wangu. Principle yangu ni kuwa sina ukaribu na hawa kina dada.. mawasiliano yangu yote ni kupitia mama.
Hiyo imenisaidia sana kuondoa utata, kuna mabinti wengine ukijidai ukaribu tu umekwisha. Wengine kabisa huwa wanakuja kwa lengo la kupindua nchi..
 
nashangaa mnaosema eti usiguse simu ili usipate pressure. hivi mnajielewa lakini! au ndo mshakata tamaa kuwa Hamna vya Peke yenu?

poleni. ndo madhara ya kuendekeza michepuko. mshaona kitu cha kawaida..

toka mwanzo mmekubaliana ni one man one woman. kama mmoja hawezi aseme toka mwanzo. sio kuja kumuumiza mwenzako baadae.

au kama vipi mkubaliane muwe in an open relationship. atakayejisika kutoka atoke. ndo hapo uone wanaume wa kibongo wanavyotokwa povu. wanataka wachepuke wao tu. ovyo!

semeni usichunguze chunguze simu for privacy purposes. hata kama you're a couple haimaanishi kusiwe na personal privacy.
lakini hata ukiamua unataka kuona kwani kuna tatizo!!!
Ngoja nikuhulize wewe umesoma na watu mbali mbali na uko na marafiki wakiume wakawaida wangapi unataniana nao baby mambo,,, so akishika simu yako kwenye magroup ya whatsup akakuta mnataniana baby mambo akulime red card wacheni kimshauri vibaya mwezenu,nyinyi ndoa zenu zimewashinda kbsa,dada mwenye mume muandae mume wako kuwa bora kwako nasio ushauri Wa haba na haba hapa
 
uache kutengeneza mahusiano yasiyofaa na wanawake wewe. jiheshimu.

sifanyi utani wa hivyo mimi.
 
Kwa maelezo yako sijaona udhibitisho usio na shaka kwamba ulichohisi kimetokea ndicho. Inaonekana unaamini hata kwa hisia tu. Nilidhani ulipohisi ungetulia kwanza uweke mtego na bila shaka ungewafuma tu maana hiyo kitu haijifichi muda mrefu. Kwa vile umewahi watatafuta mbinu nyingine kama kweli walishaanza uhusiano.
 
Husiejielewa wewe, maana umeperuzi tu hujasoma, rudi kasome tena utaelewa na utajua uzungumze nini? eti kamshusha mumewe njiani, umesoma uko juu?? ata ulichoandika hakieleweki sio kila mada lazima ucomment ikikupita kushota nawe pita kushoto

Mkebora, kua kama jina lako usiwe na hasira za haraka haraka. Imagine mkiwa barabarani ulitofautiana kidogo na baba watoto mume wako kipenzi kwa sababu anazozijua yeye na mungu wake akafungua mlango wa gari akashuka, na wewe ukaona isiwe tabu ukawasha gari ukaondoka zako ukamuacha njiani. Really is this what he deserve? You are a GOOD wife, please show to your husband how good you are. Mme wako alikosea ndio lakini kwa ushauri wangu punguza pia kuchunguza chunguza simu ya Mr wako. Usinielewe vibaya dadaangu.
 
Halafu dada mbona kauliza kwa confidence sana "uko wapi sasa hivi", inaonekana huwa wanawasiliana na wana mazoea,hata kama mfanyakazi angekua na siku moja huwezi kumuuliza boss wako such a qn
Kosa ulilofanya ni kuwauliza mapema kuhusu kupigiana simu, hayo mambo unatakiwa uwe mafia, chunguza kwanza, kusanya ushahidi wa kutosha halafu ndio uweke kikao.

Ukisema umfukize huyo dada sahivi utapata wapi mwengine?,na wadada shida sikuhizi ukipata mmoja shukuru,pia tunaweza kukushauri umwache yakawa majanga zaidi ya jana,kama watoto bado wadogo mwache ila endelea na uchunguzi kimyakimya huku unatafuta mfanyakazi mwengine.

Mwisho nakuomba tu achana na habari za kushika simu ya mume,utapata vidonda vya tumbo kabla ya siku zako ohhhhh!

[emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435][emoji1435]

Si ameuliza yuko wapi ili ajue kama ataweza mnunulia vocha au vipi. Sasa angeulizaje?
 
baki nae huyo binti.. kila binti wa kazi ana flaws zake.. mwingine ukute atakuletea wanaume ndani kwako pindi haupo.. tena kwene chumba chako..
au mkitoka..na yy ndo huyo anachomoka. mida ya kuosha vyombo vya usiku ataosha saa 11 akichek mnakaribia kurudi..
cha kifanya vunga tu.. kama ni kwel ulihs kitu na kama ni cha ukweli..basi utawadaka mbeleni.
mwisho kabisa.. jifunze kumwamin mmeo. hata kama humwamini dont **** show it to his face. imagine kama hajawah kufikiria hata uhusiano na huyo binti, ni jinsi gani utakuwa umemvunja moyo..na kumuumiza. mwombe msamaha aisee
 
Approach uliyotumia ndo inakugarimu mpaka sasa unatamani mgawane mijengo ya serikali na hubby Wako.
Ulikosea Sana kumuuliza hubby suala hilo mbele ya dada.
Ungemuulizia chumbani mparuane vya kutosha, hata mgombane Sana ili ajue ni kwa kiasi gani umekwazika but si kupeana maonyo mbele ya House girl.
Wanaume hawapendi kukemewa au kufokewa hata Kama wamekosea
pia ulipaswa kumuuliza dada kwa upendo, usingetanguliza hasira mummy, Hawa wadada ni kuwa handle kwa tahadhari kwa sababu mwisho wa siku wewe ndiye utaumia kwa kazi nyingi

Mwisho nakushauri ujifunze kufikiri rizuri (positively) hutoumia mummy. Mfano hubby alivyokuambia kuwa ameongea na waliombebea mizigo yake ungeridhika hata Kama unajua kuwa siyo Kweli. kwenye ndoa Mambo mengine unafunika kombe mwanaharamu apite.

Pole sana ndio kukua huko.
 
Back
Top Bottom