Call ya house girl kwa mume wangu

Call ya house girl kwa mume wangu

Ni hivi, una gubu sana na unafokafoka bila sababu na kuzira baadhi ya mambo including kumpa unyumba mumeo, sasa mumeo kakuchoka na ni suala la muda tu atakusaliti vibaya, muombe radhi vinginevyo jiandae kuwa dada
 
Nenda Ka print call history. Fanya hivi for your own peace of mind! Otherwise itakupa shida na kuharibu mahusiano na mumeo. Utakuwa unahisi unaibiwa muda wote.
Kama alikuwa amwamini Mr wake ikawaje Mr kwenda kumpokea
 
chanzo ni wewe kutomtumia vocha huyo dada wa kazi. nahisi ungetuma vocha huo mgogoro ungekuwa haupo maana hangempigia mumeo kuomba vocha. Uzuri ni kwamba wewe mwenyewe unasema ulisikia sauti ya huyo dada akiomba vocha kwa mumeo ili apige simu nyumbani kwao. Sion tatizo kwa mumeo zaidi ya wewe kujaribu kulikuza jambo dogo kuwa kubwa.

Pia unaonekana kuhamisha tabia za shemej zako (wadogo zake mumeo) na kuzihamishia kwa mumeo huku ukikiri kwamba mumeo hajawahi kuwa na tabia kama hizo. acha kubomoa ndoa yako kwa mikono yako.
Hao mashemeji amejua kama wanatabia hizo kama sio mambo yaumbea unafiki,ulishawai kumwambia mume wako Habari za wadogo wake,yaani na wamekwisha kutambua wamesema wanakusubiri sana sana tuuu
 
Nawashauri tu dada zangu mnapoleta house girl majumbani mzigatie kuwapeleka kupima magojwa ya kuambukiza kama UKIMWI na mengineyo. Nakumbuka kuna familia imepukutika yote baada ya kuleta mfanyakazi wa ndani aliyekuwa tayari yuko positive. Kwa wanaotokea Sehemu za Geita Nyamikonze mtaifahamu familia ya Bugeni. Baba mji alimgeuza kuwa mke mdogo na familia yake hadi ninavyoandika hivi ni historia tu. Kwa kifupi house girl ni mke mweza wako japo wanaume wengi hapa mtapinga. Mie nishakataa kuajiri house girl kwani najifahamu madhaifu yangu.
 
Kuna baadhi ya issue wanaume wanashindwa kujitetea hapo kwa hapo kwa maswali ya kushtukizwa. Kuna uwezekano kabisa kwamba hakuwa na nia mbaya na huyo binti bali alikuwa anataka kumsaidia kwa nia njema kisha amweleze kwamba anachofanya hakubaliani nacho na kumuonya aache tabia hiyo asirudie tena.
Aliogopa akikwambia inaweza kujenga ufa kati ya dada wa kazi na wewe na kama mkitofautiana na dada wa kazi anaweza kuondoka ikawa ni shughuli nyingine kupata dada wa kazi mwingine.

Mimi naamini swali lilikuwa la kushtukiza.
Umeona na hii kukosa busara alafu atamsingizia shetani kaivuluga ndoa yake au anatengeneza mazingira ya Mumewe kuwa na mahusiano na msadizi wao wa nyumbani

Ningesaidia zaidi kumsahuri lkn hii inshu unajiona umekosa alafu unaomba msaada wa kukuelekeza ulipo ni mgumu sana,,
 
Mimi nimewaza tofauti...

Inawezekana unamuhukumu housegirl pasipo hatia,ukampa all blames kumbe inawezekana kabisa MR alikuwa anaongea na mchepuko wa nje na huenda amekuwa akichepuka kisiri.... Sema sasa umeunganisha doti doti na ishu ya housegirl kwa kuwa housegirl alikuomba hela ya vocha huku pia maongezi ya MR na mtu wa pili kwenye simu yalikuwa ni ya kuomba pesa inawezekana kabisa mchepuko ndiyo ulikuwa unaomba pesa kwa MR... Na baada ya wewe kuwa mkali MR alivyoshuka tu kwenye gari aliupigia simu mchepuko usimpigie tena simu yupo na wewe ila wewe ukaunganisha hadithi.na ndiyo maana housegirl wako ametamani hadi kuondoka, usikurupuke nenda taratibu

Huna haja ya kumfukuza housegirl usije muhukumu bure and simply you need to prove ur suspicious beyond reasonable doubt... Weka mitego pasipo mr wako kujuwa
 
Haya hutokea kwa wanawake wengi kuwa na wasiwasi na house girl ila dada tulia jenga nyumba yako mwanamke mjinga huibomoa nyumba yake mwenyewe usiwe kama hao omba mungu Huyo shetani anayetaka kubomoa nyumba yako atoke
 
Hii ya kutomiliki namba nilijifunza kwa jamaa yangu mmoja, ila jamaa alitahamaki tu, angesema ukweli fasta isingekuwa issue kubwa hivyo, ambacho kingetokea ni wewe kumkanya dada na mchezo ukaishia hapo.

Pia anaweza kuwa aliamua kutosema ukweli kwa sababu anakufahamu utakavyoreact juu ya hilo, so kuzima soo ilikuwa ni kukwambia hivyo alivyofanya.
Wanaume wengi tuna tabia hiyo, kuwa kama ni jambo ambalo anaona litazua mjadala au kushindwa kueleweka kwako hawezi kukwambia ni afadhali uelewe utakavyoelewa wewe
 
Kha...
Tafuta fasta hg mwengine , huyo anatafuta mji.!
Na mpaķa mr kuhaha na kuficha ficha!
Gg anaomba vocha, anamuuliza baba eti uko wapi!
Hao washa elewana.
Ukiona manyoya ujue kishaliwa....
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
Huwajui? 90% ndio zao, pole sana, ila tafuta bint mwingine ukipata huyo aondoke tena haraka
 
Habari zenu wanaJF,

Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni.

Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sasa hivi? Mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. uliongea na nani? Akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu.

Nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hiyo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie.

Sasa hii ya juzi imenishangaza, niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpaka hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo.

Usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. Nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? Dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wa kuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavyokuheshimu tukamaliza hapo.

Siku ya pili dada akaniita ana shida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivyo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vipi ukiondoka utajisikia amani? Akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka yake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka yake kumwambia kilichotokea, hivyo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vipi?

Nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivyo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka.

Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani.

Hivyo ubabe huu anaojitika ni wa nini? Niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao, hivi ni pepo au wapuuzi?

Naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo.
Umechoka siku moja tu, huna moyo wa kupotezea, mnona mme mwenyewe katulia zake hana maneno, ushauri tuliza moyo acha visasi utavunja familia yako..
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
Hilo ni jaribu dogo tu, lishinde, familia yako sio paradiso majaribu yapo, usiwe na jazba sana, tena una mme mpole mno..
 
Sasa unajiumiza nini wakati huna ushahidi... na kwa nini muishi maisha ya kupekuana simu..m daah poleni sana...
Kaka hapo hauko sahii nikmaana mtu na mwenziwe kuachiana simu ndio kupekuana! Mke wako akiwa anakuomba simu kumpgia mtu mwingine ushindwe kumpa kisa atakupekua so far likewise..
 
Kaa na mume wako mueleze na muulize tatzo lko... mwanamke mjinga huivunja ndoa yake kwa mikono yake si unajua?
Ishi kma hakuna mitandao ya jamii wakt mwngne ndoa ni busara na pia uelewa.
 
Back
Top Bottom