Call ya house girl kwa mume wangu

Call ya house girl kwa mume wangu

Asante mkuu lakini issue pia kwanini alificha ile simu wakati yeye alipigiwa? si angesema tu ni dada wa kazi? sasa hii ya kuficha ndio ambayo imenipa maswali zaidi
Mambo ya kujifanya wa Dar, mjanja mjanja kwenye Ndoa hayapo. Mheshimu mumeo. Kupeleleza hayo mambo utapoteza vyote. Tamaa ya Mwanaume inaingiaga kwa sekunde moja na kumjaa .
Yawezekana iliingia kweli, lakini punde bado anajipinga ku-harmonize hisia zake wewe unakurupuka.
Mpe heshima yake kwenye hisia za maumbile yake ata cool down, wewe ndio chaguo lake. Ukirudi nyuma uangalie alivyo kupata wewe, utashangaa, ilikuwa less than a second akakupenda hadi kukuoa.
Ni mtu mzima Mpe nafasi ya kusettle hisia zake.
 
Katika makosa unayoweza kufanya ni kujiumiza ili kumlinda mwenza wako. Wewe umeshampa dada job description yake, usimfukuze isipokuwa pale ambapo ameshindwa kutimiza wajibu wake. Hgal ni mfanyakazi Kama ww ulivyo ofisini kwako.

Hayo ya kuchunga mume utajichosha Bibie. Wewe tulia (kwanza umekosea Sana kumuweka kikao mumeo na dada. Umewapa sababu ya kuwa na common problem ya kuhisiwa. Usirudie kamwe, huwezi kumuweka boss wako na subordinate wako kikao, unaongea na kila mmoja separately). Wewe tulia, Fanya majukumu yako. Siku watakapojisahau ukawabamba red handed tutaanzia hapo kuwajadili.
Nakuambia sio mwanamke mpenzi tuuuuu,hakufundwa huyooo aibu kama nini,jamaa hapo ndio atakula mzigo
 
Mambo ya kujifanya wa Dar, mjanja mjanja kwenye Ndoa hayapo. Mheshimu mumeo. Kupeleleza hayo mambo utapoteza vyote. Tamaa ya Mwanaume inaingiaga kwa sekunde moja na kumjaa .
Yawezekana iliingia kweli, lakini punde bado anajipinga ku-harmonize hisia zake wewe unakurupuka.
Mpe heshima yake kwenye hisia za maumbile yake ata cool down, wewe ndio chaguo lake. Ukirudi nyuma uangalie alivyo kupata wewe, utashangaa, ilikuwa less than a second akakupenda hadi kukuoa.
Ni mtu mzima Mpe nafasi ya kusettle hisia zake.
Well said,dada anakuwa roho juu kama jamaa ndio wakwanza kutembea nae,mpaka anakuoa alikupa heshima kubwa sana wapo aliotoka nao mbali mpaka alipokukuta wewe nakukutongoza kwa muda mfupi na kukuoa, anakupenda sana hayo mengine potezea, ngoja niuuhulize wewe hao wanaume wanaokutongoza njiani,maofisini mume wako unamwambia au yeye anashika simu yako..
 
Nakereka sana na Wanawake wa dizaini yako aiseee, nimeshampiga stop mke wangu kushika simu yangu. Haimhusu, ukiona una mke wa dizaini yako ujue una hasara, kumbuka uaminifu haujengwi kwenye simu, haya sasa umenyimwa simu kule nako kwa yule binti umekosa uhakika, Binti anataka kuondoka huoni kwamba umejidhalilisha mwenyewe? yaani umemsaidia HG kujua kuwa hamuaminiani ndani ya nyumba moja na kitanda kimoja?? Sijawahi kupokea simu ya mke wangu na hua hapokei simu yangu.

Kwahio tukio hilo limethibitisha kuwa Simu si chochote wala lolote... Muombe MUNGU akutunzie ndoa yako na sio kuacha simu ikutunzie Ndoa yako
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani
Wewe ndiyo unaharibu, yanini kuchunguzana kiasi hicho...? Kwani kila simu lazima ujue imetoka wapi...? Mpende mumeo na muamini vinginevyo unayeumia zaidi ni wewe.....
 
Dada i can assure u hata mdogo wako wa kike akija anaweza kuwa bize na mumeo kuliko wewe, since mwanaume na mwanamke they know to handle each other friendly, ni kweli mumeo na hyo dada inawezekana wanachart muda tu since ndio yeye aliyeenda kumpokea stand,

cha msingi ufurahi umeweza kukomesha mazoea mapema lakin pia ongera kupata msichana anayefanya kazi maana sikuiz wafanyakazi ni hatari, tatizo lenu wanawake hamjui kujaliana mwenzio alivyoombwa vocha akaenda kufata dukani course anamthamini hyo dada wa kazi anayekaa na watoto wake,

kingine wala usimfukuze maana kama wanataka kuwa pamoja ndio utawapa uhuru zaid. Kingine usijaribu tena kumuweka kiti moto mumeo na house girl hasa kama huna ushaid kwamba wanatoka kimapenzi.
 
Wew mwanamke sijakuelewa mtu kumpigia simu mfanyakazi wa ndani ni kosa...
 
Umeleta mke mdogo nyumbani, amin usiamin... bahati mbaya ulikuwa na papara ila ungetulia, ungegundua mengi, hapo jamaa atakula hata kama alikuwa hataki, ili kukukomoa... mhim kama unataka kuwa self suluhisho ni dada kuondoka,

ila zingatia, kama ukiendelea kununa ndani ndo unaongeza tatzo badala ya kuliondoa...
 
kwa baadhi ya tabia ya KIUME!!! lazima atahakikisha anamla, si umemhisi now ataflatten kabisa.... halafu hii tabia ya kuchunguzana simu hii,,, iacheni jamani,,, kabisa masikio yamedinda unasikiliza mwenzio anaongea nini na nani.......GUBU litakupeperushia ndege wako....miaka sita ni michache sana....
 
Yaani Evelyn si unajua kupata binti ilivo shida sasahivi, sijui naanzia wapi kwakweli najisikia kuumia mno, binti ni mchapakazi, anaamka mapema, anafanya kazi zake vizuri na anaelewa alafu unakuja kumuharibu, wanaume tuhurumieni jamani

dada huna sababu ya kutafuta mwengine , bora umejua haya mawasiliano mapema itawapa wasiwasi kama kweli walikua na nia ya kumegana.

uzuri umekili kabisa una miaka sita na mmeo na hujawahi kumkuta au kumhisi na makandokando mengine.
muite tu mmeo mwambie hujapendezwa na mawasiliano ya siri na mfanyakazi wenu wa ndani.

kosa jengine ulilofanya na usirudie tena kulifanya ni kumuonya mmeo pamoja na housegarl pamoja
ulimdhalilisha mmeo kiaina muombe radhi kwa hilo.

pia si dhambi mmeo kua na no ya mfanyakazi wenu maana huwezi lolote laweza tokea nyumban wewe haupatikani akamua kupiga kwa Mr wako.
 
Binti wa kazi tu kakuchanganya,je ukisikia ana nyumba ndogo si utaandika kila mtandao kuomba ushauri,sasa wewe baada ya kujua ni binti wa kazi ndio kapiga wasiwasi wako ulikuwa ni nini?! Wakati ulisikia kila kitu,.Mume wako hakutaka kutengeneza tatizo ndio maana hakutaka kukupa simu,maana mmlishajijengea kuwa beki tatu ni mke mdogo,relax endelea kumuani mume wako
 
Muamini mume wako. Tena iliwezekana mpende zaidi coz hata kama ukijua kweli amekula house girl huta badili kitu chochote zaidi ya kujipa stress. Kaeni muongee kwa upendo muya maliza. Pia kama inawezekana epuka sana kuchunguza kila kitu coz uta jiumiza sana tena sana.
 
Hujachoka ni wivu tu kitu ambacho ni normal cuz unampenda mmeo. Inawezekana alishindwa kutokana na kuhofia zogo kwa mda ule. Mpe mda na kama ndio mara ya kwanza hilo limetokea there's an explanation.
 
kweli kupata dada wa kazi ni shida awe mchapakazi ama si mchapakazi awe anavutia ama la! cha msingi kukitokea umeudhiwa na mme wako anahusika kwanza tulia na umwombe mungu masiku ama week ama mwezi jinsi ya kuliongelea hilo tatizo na kulitatua, pili tafuta siku ya amani na furaha ambayo mme wako hakutegemea kwamba mtaongelea swala flani muulize na ukufafanulie kilichotokea! na sio katika kuhukumiana na kutukanana! baada ya hapo kitachoamuliwa kitunze na kifatilie na kiweke kwenye maombi. vivyo hivyo kwa dada wa kazi ongea nae! kama ana mimba atakwambia! kama wote wanakudanganya ipo siku mungu atakiweka wazi! iwe ndani ama nje ya nyumba na wasichana wengine! Usikurupuke ukataka solution ya siku moja na ujue vyote na uamue vyote wewe siku hiyo, vitu vingine vinahitaji muda na upole kuvitatua!
 
Hahaha ukiona manyoya...
Jiandae kwa lolote
Just saying though
 
Back
Top Bottom