Call ya house girl kwa mume wangu

Call ya house girl kwa mume wangu

Kuna baadhi ya issue wanaume wanashindwa kujitetea hapo kwa hapo kwa maswali ya kushtukizwa. Kuna uwezekano kabisa kwamba hakuwa na nia mbaya na huyo binti bali alikuwa anataka kumsaidia kwa nia njema kisha amweleze kwamba anachofanya hakubaliani nacho na kumuonya aache tabia hiyo asirudie tena.
Aliogopa akikwambia inaweza kujenga ufa kati ya dada wa kazi na wewe na kama mkitofautiana na dada wa kazi anaweza kuondoka ikawa ni shughuli nyingine kupata dada wa kazi mwingine.

Mimi naamini swali lilikuwa la kushtukiza.
Huyu mama nae hata haangalii,huo ni wivu uliopitiliza coz h'girl ndo kwanza ana siku tatu ndo mumewe aanze mapema yote hiyo kuanza kumtongoza?haingii akilini hata kama bwana ni malaya vipi hawezi kukurupuka hivyo.
 
HA HA HA HA WEWE JAMAA ACHA KUMTETEA SANA, Sema ukikamatwa na jambo la ukweli unakosa nguvu, au ukifumaniwa hata kama bounsa unanyweaaaa...jamaa atakuwa ana jambo , Kwanini asingesema tu ni mdada wa kazi? na akatoa simu kwa mkewe? usikute hawajafanya chochote ila pengine dada ndo anataka kumuanza shemeji na mume alishaliona hilo kama ulivyoongea kwenye line yako kwamba alihofia kusema ingeleta taharuki kwa mke, mana hawa wadada wa mjini nao mmmh.

Kutokana na maelezo yake inaonyesha tu jamaa alitaka kumsaidia msichana wa kazi kiroho safi. sema tu swala la kupigiwa simu kwa mara ya pili kuulizwa uko wapi huku akiwa na mkewe lilikuwa la kushtukiza.

Mimi naamini kama alikuwa na nia ovu ya kumtaka msichana wa kazi angekuwa amejiandaa kisaikolojia kujitetea.

Kosa kubwa ambalo analifanya mleta uzi hapa ni kutengeneza mazingira magumu kimawasiliano na mumewem badala ya kumalizana na mumewe na kusonga mbele na maisha kwani mume anamuhitaji na msichana wa kazi anamuhitaji pia. Kujenga ufa kwa hisia ni mbaya sana na hapo ndipo anapopitisha Greda kumchongea mumewe barabara ya kuelekea kwa msichana wa kazi kiulaini.

Ukweli mchungu kwa wanawake ni kwamba nyie ndiyo mnaoshikilia ndoa na ndiyo mnaoamua kwamba ndoa iwepo au ivunjike.

Hizo sarakasi za kutunishiana msuli na mwanaume ndani ya nyumba kwa sababu ya hisia tu mwisho wa siku mwanamke ndiye atakayepoteza.

Naomba mkumbuke kanuni ya nguvu ya mvuto ambayo hata kwenye vitabu vya dini ipo isemayo ALIWAZALO MJINGA NDILO HUMFIKA.

Yaani kile mtu anachowaza ndicho huwa sasa kama unajaza nguvu hasi mawazoni mwako kuhusu mumeo ndiyo unachokiomba na ndicho kitakachokutokea. Kwa nini usiwe na Amani tu na kumuamini mumeo na kumjengea kujiamini na kuomba mambo mema yakutokee kwenye ndoa yako kuliko kujaza fikra hasi kuhusu msichana wa kazi.

Kwani huko barabarani wako wasichana wangapi wanaowinda wanaume wanaopewa stress na wake zao. Wapo wengi tu tena wa kiasi cha kutosha.

Acha fikra hasi, jenga ndoa yako mwanamke.......

Huo ndiyo ushauri wangu.
 
Kweli Mke bora , Mr alikosea kuficha simu yake baada ya kuongea na HG.
Na ulichofanya cha kuwaita au kukaa nao pamoja na kuongea nao umefanya vizuri sana maana umewadhihirishia kuwa hujapenda kitendo kule walichokifanya , na ukamwelewesha huyo HG utaratibu anaotakiwa kuufuata pale anaokuwa anashida na kitu chochote.

Sasa kilichobaki kuanzia mwisho wa kikao chako pamoja na wao ni kuanza upya na Mr. wako kwa kumpenda zaidi na kuongea naye kwa upendo huku muda wako mwingi ukimpa yeye, yaani kwa kumpigia mara kwa mara na kuchat naye mara kwa mara, kwa kufanya hivyo penzi lenu litakuwa jipya kila nukta mpya inayoingia Kati yenu.

Unajua mambo mengine au vishawishi vingine vinatokea kwa sababu labda wewe unakuwa busy sana kiasi unaruhusu pepo la zinaa kutoka kuchukua nafasi kuharibu ndoa yenu nzuri. Kumbuka kujishusha ni kitu cha muhimu sana kwa wote wawili wewe na Mr. na kwa kujishusha ndiyo kuliboresha agano lako na mumeo, Mithali 14:1 imeandikwa, kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake, bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Lakini ukifanya maamuzi ya hasira bila kujua nini nilikuwa chanzo utaharibu tena sana na hapo utaanza kusema wanaume wote ni wabaya , bila kujua hasira zako ndiyo zimekufikishakabisa, Maana imeandikwa, Mhubiri 7:9
Usifanye haraka kukasirika roho ni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwaka mpumbavu.

Sasa nimalizie kwa kushauri hivi, msamehe kabisa na wewe is hike vizuri nafasi yako sawa na Yeremia 31:22-imeandikwa, hata lini utatangatanga, we binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanamume.

Nakutakia kila la heri Mkebora.
 
Tunza ndoa yako mkebora hayo na majaribu na mitihani wapaswa kuishinda usichukulie hasira!
 
Ushauri wangu anza kutafuta dada mwengine kimya kimya ikiwezekana tafuta mama mtu mzima kidogo kwani nyumba yako ina kazi nyingi kiasi gani mpaka bibi ashindwe kufanya kazi? hutaishi kwa Amani kabsaa, na nyumbani ndio sehemu ya kupunguzia stress ila wewe itakuwa inakupa stress hasa ukimuona dada anaongea na shemeji yake. muondoe uishi kwa Amani.
Hii safi.....
 
Huyu mama nae hata haangalii,huo ni wivu uliopitiliza coz h'girl ndo kwanza ana siku tatu ndo mumewe aanze mapema yote hiyo kuanza kumtongoza?haingii akilini hata kama bwana ni malaya vipi hawezi kukurupuka hivyo.

kaka usichelewe kuwaza, we are born in a one day, we die in one day, we can change in one day and we can fall in love in one day anthing can happen in just one day, dalili ya mvua mawingu, na usisubiri paharibike kabisa ndio uanze nilihisi, usizipa ufa utajenga ukuta ndugu
 
Pole sana, naomba nikulize umesema mfanya kazi tangu aje hana mda mrefu na wewe na mr mnayo tabia yakupekura simu zenu au niseme its okay kwa wewe kuchukua cm yake na yeye pia kuchukua cm yako sasa hapo ni jambo gani lililo kukera sana lakukufanya usiwe na maelewano mazuri na MR wako lakini dada wa kazi mnaongea vizuri?

Je huko nyuma alikua na tabia yakuwataka wafanya waliopita au ulishawahi kumkuta ana cheat?

Usihisi namtete labda mr wako lakini usimpe mfanyakazi nafasi ya kukuona kua hujiamini,

Na ulikua nanafasi nzuri sana yakujua mapema kinachoendelea ila ulikua na haraka, ungejifanya hukusikia hata wanaongea nini na ulivyo fika nyumbani ungefanya utafiti wako kwa makini na kwa ushahidi, ila tuu isinune na mumeo muongeleshe kama vile hakuna kitu na kama kuna chochote baina yao utajua la sivyo unahisi atakuharibia nyumba yako mruhusu aende,ni bora ukatabika kwa mda mwengine wa week au mwezi kuliko kua kazini au sehemu na huna amani nyumbani baina ya mr na Dada

Sorry kama ntakua nimekuudhi ..........
 
Kweli Mke bora , Mr alikosea kuficha simu yake baada ya kuongea na HG.
Na ulichofanya cha kuwaita au kukaa nao pamoja na kuongea nao umefanya vizuri sana maana umewadhihirishia kuwa hujapenda kitendo kule walichokifanya , na ukamwelewesha huyo HG utaratibu anaotakiwa kuufuata pale anaokuwa anashida na kitu chochote.
Sasa kilichobaki kuanzia mwisho wa kikao chako pamoja na wao ni kuanza upya na Mr. wako kwa kumpenda zaidi na kuongea naye kwa upendo huku muda wako mwingi ukimpa yeye, yaani kwa kumpigia mara kwa mara na kuchat naye mara kwa mara, kwa kufanya hivyo penzi lenu litakuwa jipya kila nukta mpya inayoingia Kati yenu.
Unajua mambo mengine au vishawishi vingine vinatokea kwa sababu labda wewe unakuwa busy sana kiasi unaruhusu pepo la zinaa kutoka kuchukua nafasi kuharibu ndoa yenu nzuri. Kumbuka kujishusha ni kitu cha muhimu sana kwa wote wawili wewe na Mr. na kwa kujishusha ndiyo kuliboresha agano lako na mumeo, Mithali 14:1 imeandikwa, kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake, bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Lakini ukifanya maamuzi ya hasira bila kujua nini nilikuwa chanzo utaharibu tena sana na hapo utaanza kusema wanaume wote ni wabaya , bila kujua hasira zako ndiyo zimekufikishakabisa, Maana imeandikwa, Mhubiri 7:9
Usifanye haraka kukasirika roho ni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwaka mpumbavu.
Sasa nimalizie kwa kushauri hivi, msamehe kabisa na wewe is hike vizuri nafasi yako sawa na Yeremia 31:22-imeandikwa, hata lini utatangatanga, we binti mwenye kuasi? Kwa maana BWANA ameumba jambo jipya duniani, mwanamke atamlinda mwanamume.
Nakutakia kila la heri Mkebora.

Asante kwa mchango wako mtishbieliya, nimekuelewa sana
 
Huyo dada mrudishe, wanaanza hivyo hivyo mwisho anageuka mke mwenzio. Kwanini mumeo afiche simu kama hakuna lolote! Nini ujinyime amani ya roho na nyumba yako mwenyewe. Na mumeo ongea nae vizuri mkiwa chumbani sio kwa hasira, mwambie tu asitengeneze mazingira ya kukupa wasiwasi.
 
Habari zenu wana, Ijumaa nikiwa ofisini dada angu wa kazi alinitumia msg akiniomba nimtumie vocha anataka kuwasiliana na kwao, nikamjibu mazingira ya ofisini hapa hakuna duka hivo nitakununulia nikiwa narudi home na nitakuletea jioni. Tukiwa njiani tunarudi home niko na mr simu yake iliita akaipokea sasa ilikuwa na sauti ya kusikika as if kaweka loud, sauti ya house girl wangu iliuliza uko wapi sshivi? mr akajibu nipo njiani narudi nyumbani, yule dada akamwambia simu yangu haina pesa nashindwa kuwasiliana na nyumbani, mr akajibu sawa na simu ikaishia hapo, alipokata tu nikamuuliza mr. ukiongea na nani? akaniambia na watu ambao walinibebea mizigo leo kutoka bandarini, nikamwambia ok, naomba simu niangalie akagoma kutoa simu, nilikuwa naendesha mimi so nikapark maana tulikuwa mtaani tu uko ambako uko free kupark popote, nikamuomba tena naomba simu niangalie, akafungua mlango wa gari na kushuka, kwa kawaida ikitokeaga issue kama hivo anatoaga simu fasta bila shida akijua hakuna shida, same kwangu mimi nikiongea na mtu akitaka kujua ni nani uwa nampa simu aangalie, sasa hii ya juzi imenishangaza, Niliamua kuondoka na nikafika nyumbani tu nikamuita dada, nikamwambia dada naomba simu nikuunge na kifurushi, dada akanipa simu, nikakagua simu yake hakukuwa na mawasiliano, japo namba zingine alizopiga zilikuwepo, ikumbukwe kwamba sio dada mshamba, ni dada wa kujielewa tu alieishi mjini na kijijini ana 20 yrs (hapa mr aliposhuka nilimuona anapiga simu wakati naondoka bila shaka akimwambia futa hizo calls) huyu dada mpk hiyo friday alikuwa na siku 3 tu maana alikuja j5, niliona nisiishie hapo. usiku watoto walipoenda kulala nikawaita wote dada na mr. nikamuuliza dada una ukaribu upi na baba hapa ndani mpaka unampigia simu na kumuuliza yuko wapi na kuomba vocha wakati mimi ulishaniomba? dada akasema mi sijampigia baba, nilimpigia siku nakuja tu kwa vile ndie alikuja kunipokea, nikamwambia dada umempigia baba nina uhakika sipendi hii tabia ukiwa na tatizo wakuniambia ni mimi, nikamwambia na mr kuwa hii tabia siipendi, naomba uniheshimu kama ninavokuheshimu tukamaliza hapo. Siku ya pili dada akaniita anashida anataka tuongee, nikamsikiliza akaniambia yeye imemuumiza sana kilichotokea hivo anaona bora aondoke maana asije akaleta shida zaidi baadae, hajisikii amani, nikamuuliza na vp ukiondoka utajisikia amani? akasema hapana ila tu nakuhofia wewe maana utakuwa na wasiwasi na mimi, nikampigia kaka ake ambae alinipa huyo dada, nilipompigia na yule dada alikuwa ameshamtumia msg yule kaka ya kumwambia kilichotokea, hivo yule kaka akaniuliza mimi kuwa sasa naamua vp? nikamwambia dada amekataa kuwa yeye hajafanya hivo na sio mfanyaji wa hayo kama anakiri maneno yake mi sina maneno ila pia kama anataka kuondoka pia sina maneno, yule kaka akamwambia dada yake kwa vile hapo haujafukuzwa mi naomba ukae, ila kaa kwa heshima, usije kunitia aibu mimi nilokuleta uko, kama haujafanya na una hakika hautafanya hayo basi kaa, kama unaona linaweza kutokea hili jambo basi unaweza kuondoka, dada akasema basi nitakaa kaka. Mdada yupo home namuongelesha vizuri tu, ila nina hasira mno na huyu mr. tumekaa bila msichana 3 weeks hapo nyuma nimehangaika sana kuhudumia familia unarudi umechoka, unapika, unafua uniform za watoto, unanyoosha, unaosha vyombo unapanda kitandani saa 6 kasoro na saa kumi na moja umeshaamka, tunapata dada mchapakazi yeye analeta upuuzi, huyu mwanaume hajasema lolote mpaka sasa kuhusiana na hili na hapa tunapishana tu ndani, hivo ubabe huu anaojitika ni wanini? niko nae huyu mtu 6 yrs now mambo haya sijawai yaona ndio kwanza kwa house girl huyu ila in short ukisikia wadogo zake kwao wana kesi na wake zao basi ni za kutoka na mahouse girl wao hivo ni pepo au wapuuzi? naombeni ushauri wenu maana nimechoka moyo wangu unavonituma naona naweza kufanya jambo baya nipeni mwongozo
Nikuulize haya...
Kilichokukera ni nini?
1. Hoise girl kumpigia simu mumeo..?
2. Mumeo kukatazia simi yake..?
3. House girl kumuomba vocha mumeo..??
4. House girl kuongea na mumeo..?
 
Pole sana, naomba nikulize umesema mfanya kazi tangu aje hana mda mrefu na wewe na mr mnayo tabia yakupekura simu zenu au niseme its okay kwa wewe kuchukua cm yake na yeye pia kuchukua cm yako sasa hapo ni jambo gani lililo kukera sana lakukufanya usiwe na maelewano mazuri na MR wako lakini dada wa kazi mnaongea vizuri?
je huko nyuma alikua na tabia yakuwataka wafanya waliopita au ulishawahi kumkuta ana cheat?
usihisi namtete labda mr wako lakini usimpe mfanyakazi nafasi ya kukuona kua hujiamini,
na ulikua nanafasi nzuri sana yakujua mapema kinachoendelea ila ulikua naharaka,
ungejifanya hukusikia hata wanaongea nini na ulivyo fika nyumbani ungefanya utafiti wako kwa makani
na kwa ushahidi,ila tuu isinune na mumeo muongeleshe kama vile hakuna kitu na kama kuna chochote
baina yao utajua la sivyo unahisi atakuharibia nyumba yako mruhusu aende,ni bora ukatabika kwa mda
mwengine wa week au mwezi kuliko kua kazini au sehemu na huna amani nyumbani baina ya mr na Dada
sorry kama ntakua nimekuudhi ..........

NImpende nani, hapana na nimesema pale juu kuwa tabia hii sijawai iona kwake, na ndio maana nilitaka nisiipe muda, kuna mambo mengine hayafai kuyachelewesha yanapotokea maana pindi unapoyachelewesha ndio yanakomaa zaidi, ni nini kilichomshinda mr. kutoa simu wakati namuomba ili nihakiki? kama simu alipiga alombebea mizigo kutoka bandarini kwanini hakunipa na alipata hofu ya kuendelea na safari mpaka akaamua kushuka njiani? nimekuelewa na asante kwa ushauri wako
 
Toka lini housegirl anamuuliza baba uko wapi??? SHAMELESS. hata kama baba ndo alimtafuta. kuna visichana visivyojielewa mnaweza kukuta haijulikani mother house ni nani..

Tatizo akiondoka atakayepata shida ni wewe. Jitahidi kutafuta mwingine kabla hujamtoa. Ushampa warning lazima ana wasiwasi kidogo.

wanaume wa kibongo wasivyo na adabu, kuongelea michepuko utafkiri kitu cha kawaiiida. Ovyo. Hopefully you know where your man stands. Anaweza kuwa kati ya wanaojiheshimu.

(Ingawa inashangaza, simu afiche, na kanuna juu! mh)
 
Tena wakati mie mama hajawai ata kunipigia simu, ata hio kuniomba vocha aliomba kwa msg tu, ni ukaribu upi unaopelekea kumuuliza mr uko wapi? maana angempigia tu nakumuomba vocha ingekuwa pia tofauti na kuanza kumuuliza uko wapi? hivo wakaka upo na mkeo shamba boy anampigia simu anamuuliza uko wapi? naomba uninunulie vocha mtanyamazia tuu? na bado wife unamuuliza kakupigia nani hakuambii ukweli, utakuwa na hisia ipi?
 
Back
Top Bottom