CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

Hakupaswa kumuita CAG muongo... kama anavielezo vyote kwamba mzigo upo kwenye mokenta angevileta front kama ushahidi na kuondoa sintofahamu...

Hizi ni dharau sababu tu CAG alikwisha kua na maelewano mabaya na Bunge sababu ya kutumia neno dhaifu ndiyo kila kiongozi amtende kama mtoto vile anayvojisikia...

Pascal Mayalla umesema... "Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena"

na...

Abdul Nondo ameelezea kwamba... "Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?"

Ukaguzi na taratibu zote zimefanyika kwa nini hizo sare zisionekane, zije kusemwa zimeonekana baada ya ukaguzi kupita? kama kweli zipo...

Cc: mahondaw
 
Mkuu Dyuteromaikota, you are right, sasa ni mwendo wa trust tuu, mambo ya transparency na uwajibikaji waachie wengine, ndio maana Tanzania tumejitoa kwenye ule mkakati wa open government Initiatives.
P
Nakuelewa sana mkuu katika mabandiko yako huwa unamtakasa sana raisi kuwa ni mtu safi asiye na doa lakini kiukweli huwa humaanishi hivyo
Ni aina ya ukosoaji usio wa direct
Unampa sifa mtaka sifa za kijinga na wenye akili huwa wanaelewa unachomaanisha
 
Hivi Kweli Mayala nduguyangu, hujui Madhara ya kutofuata utaratibu? Hujui Sababu za Utaratibu kuwekwa? Kweli unatuambia kutokufuata utaratibu kunaweza kuwa Sahihi? Sahihi kwa Nani? Sahihi kwa Mda gani? Nashindwa kuelewa umepatwa nanini ndugu yetu.😥😥😥😥🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️🤦‍♂️

Wasalaam Nondo, kazi ya kuelimisha hawa nduguzetu nikubwa sanaa.
 
HUKO KOOTE MNAZUNGUSHANA TU,

Kifupi NI hivi SARE ZA POLIS HAZIKUWA ZIMENUNULIWA KIPINDI CHA UKAGUZI WA CAG.

ZIMENUNULIWA wiki moja baada ya ukaguzi,

Hivi hujiulizi tangu CAG atoe Ripoti Yake Kwanini hakukanusha siku hiyo hiyo na awaoneshe waandishi wa habari Hilo kontena la nguo? Jibu hazikuwepi Hivyo ametumia wiki nzima kuzinunua na kuzipaki kwenye kontena!!!

Pili, Pesa za sare hizo zilitoka tangu 2015, Hadi Leo Zipo kwenye Makontena zikifanya Nini badala ya kugawiwa kwa wahusika?

Kama hapakuwa na uhitaji wa hizo sare Kwanini waliidhinisha manunuzi ya hizo sare ? Kukaa kwenye kontena na kuzidi kuchujuka hii siyo Hasara kweli?

Mwambieni siyo wote tunaakili kama zake.

Bangi wavute kwa kiasi,Hawakuambiwa wazidishe kipimo
😁😁😁😁😃😃😃😃😂😂
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
Nondo umenifundisha kitu,ahsante!
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Uandishi wako mtu anaweza jua unamsifia halafu katika akaona kama unambeza mwishoni akabaki njia panda!!!Kazi nzuri sana ya fasihi kaka!
 
Mkuu Dawa Yenu, kwanza asante kwa hili, nimependa objectivity yako kwenye hoja ya kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni, za matumizi ya fedha za umma, lakini kama ulimsikia rais Magufuli akizungumzia mtindo wa manunuzi kwa kupiga tanchi, utakubaliana na mimi Magufuli did the right thing kununua ndege kwa cash kwa kupiga tanchi.

Kinachotakiwa ni uwepo tuu wa nia njema na ya dhati na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa, kuhalalisha kukiukwa Sheria taratibu na kanuni.
P
Pascal tukiendekeza hii tabia ipo siku tutaumizwa!Maana itazoeleka kwamba Manunuzi yanaweza kufanyika bila kufuata utaratibu kwa maslahi yetu,lakini ni nani ambaye anaweza kuthibitisha kuwa yaliyofanyika ni kwa maslahi?Si vema kushabikia uvunjifu wa sheria kwa kigezo cha maslahi,kama sheria hazifai tuzibadili twende kwa utaratibu huo!
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Naendelezea hapahapa~~chochote chenye public interest kina mawazo na maamuzi yanayotoka kwa watu kwa ajili ya watu,mwenyekiti wa ccm ndiye anejigeuza kuwa mwenyekiti wa Tanzania,yeye ndiye anayeamua nini kiwe for public interest na kipi kisiwe,alipomtimua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali baada ya mkaguzi huyo kusimamia public interest wewe Pascal Mayalla hukumgombeza magufuli au kumkumbusha kuwa pesa iliyopotea ni ya umma,na mkaguzi ndiye jicho la umma,unamshangilia mwizi halafu unaongea habari za public interest,fool
Mkuu Capt Tamar ,
Asante,
Ubarikiwe
Japo sina uhakika, kwavile siwezi kusoma mabandiko ya watu wote humu, lakini humu JF, mimi ni miongoni mwa tuliomuongelea sana CAG, Ofisi ya CAG na Ripoti za CAG!.
Nakutakia Jumapili Njema
P
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Wapo wengi ndani ya bunge kwanini mtu mmoja afanye hivyo kwa yeye malaika?

Mbona sheria mbovu zinakuja kupiteshwa bungeni, kwanini yeye asipitishe mwenyewe?

Kwenye ujinga lazima usemwe na tusitetea ujinga au unasubiri afanye kama Mkapa kwenye kitabu chake?

Hela za umma mnazifanya kama mawe acha siasa kwenye ukweli.
 
Back
Top Bottom