CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

Wakuu mnaumiza kichwa badala ya kuangalia ni type gani ya watu wanaomjibu pumba CAG,.

Angejibiwa na mtu makini kama, MAJALIWA, JAFFO, BASHE, au MWINYI kwakweli ningeanza kutetemeka.

Kuna upuuzi na kuna wapuuzi.
Linapokuja swala la ccm hao wote uliowataja wana compromise
 
Serikali hii imejaa wahuni, wezi, waongo, mafisadi na wendawazimu waliokusudia kumchafua na kumdhalilisha CAG Assad hadharani.

Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Kweli umesema. Lakini huwa nashangaa jambo moja kubwa. Sielewi limekaaje. Rais anapiga vita ufisadi wa kila aina na kutofuata taratibu za kiserikali. Lakini imekuwa nongwa pale ufisadi unapoibuliwa. Imekuwa kosa kubwa taasisi nje ya serikali inapoinyooshea serikali kuwa hapa au pale kuna tatizo la ufisadi au kutofuatwa taratibu. Wapinzani wakisema wanaandamwa, magazeti yakisema shida, taasisi za kiraia ndio kabisaa. Sasa wameanza kumwandama CAG sijui watafikishana wapi.
 
Mimi niliwahi kushauri viongozi wetu wapimwe afya ya akili from time to time

Wetty shit Gone stone.
Spika alianzisha naona asaivi wafuasi wameanza kufuata mkumbo, hapa nafikiri lengo ni kufanya report ya CAG ikose nguvu kwa umma ili sasa kuwe hakuna tena kitu watu watakiamini na wao waendelee kupiga pesa zetu bila kwa amani.

Miluzi imeanza kuwa mingi lakini Mbwa hawezi kupotea.
 
Tuhitimishe kwa kusema, tuna safari ndefu sana kupiga hatua kisiasa na kiuchumi.

Ni vigumu kumtambua mzalendo kama utasikiliza maneno yake tu. Matendo ya viongozi wetu hayaendani na wanayozungumza majukwaani, tunasafari ndefu sana kuandaa kizazi cha wazalendo.

Huenda hyo mipesa ilitumiwa na chama fulani ktk kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, aibu yao.
 
Mkuu, huwa naamini sana katika busara zako ila hapa nadhani umepotoka au unataka kupotosha japo sidhani Kama una maslahi yoyote katika kufanya hivyo.
Unasema report ya CAG sio msahafu, hii ni kweli maana report inaweza kuwa na mapungufu kadha wa kadha. Ila ambacho sikubaliani na wewe ni hapo unapobariki manunuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria za fedha eti kwa kigezo kwamba manunuzi hayo yalifanyika kwa manufaa ya umma na umetolea mfano manunuzi ya ndege. Hii sio sawa mkuu.
Kama tuliweka taratibu/kanuni/sheria za manunuzi basi ni lazima zifuatwe na mtu akiacha kuzifuata anapaswa kuwajibishwa kwa maana kutofuata sheria halali zilizowekwa ni kosa kisheria na huwa tunasema no one is above the law, hata rais mwenyewe hayupo juu ya sheria.
Najua kuna ideology mbili katika kufanya maamuzi ambazo ni rule based na result based, wewe umebase kwenye result based, kwamba japo sheria hazikufuatwa ila results zimekuwa nzuri Sasa swali ni je vipi ingetokea result mbaya, mfano tungekuwa tumepigwa, ungekuwa na msimamo huo huo?
Halafu Kama unaongozwa na good will kwanini usifuate taratibu katika manunuzi? Watu wasio safi ndio mara nyingi huwa hawafuatwi sheria. Nahitimisha kwa kusema japo report ya CAG sio msahafu ila kwa kuwa nyaraka za manunuzi hazipo na taratibu zilisiginwa basi ni lazima watu wawajibishwe no matter results walizo deliver. Na hizo ndege naamini tumepigwa na ipo siku ukweli utaelezwa na inshaalah wote waliohusika watawekwa behind bars.

Ahsante kwa majibu mazuri mkuu. Kama unania njema, kwann usifuate sheria na utaratibu?.

Kwann baadhi ya mambo uyafanye sirini hata kama ni ya heri?.
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
query ya cag siyo kuona uniforms hata kama zipo auditors wao wanataka procedure zilifuatwa kuzipata hizo uniforms? Invoice zipo vizuri?
 
NCHI WAMEPEWA WASHAMBA KAZI TUNAYO MSIMU HUU..
Washsmba ndio hujenga miji yote mikubwa na waswahili yaani wale wa mjini huishia kukaa kwenye kahawa kuendeleza stori za "hutwambii kitu wewe,umekuja humu tukikuona"
Sasa endeleeni ujanja wenu wa mjini!
 
.
 
Lakini pia mkuu Pascal Mh Rais anazo taarifa za upigaji huo na aliwaambia maafisa wa polisi ikulu tena live juu ya suala hilo sasa ukisema CAG ni mwongo kwa suala ambalo Mh Rais alikwisha lisema unamaanisha Mh Rais nae mwongo? Achunge kauli
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
 
Mihemko imemfikisha hapo, katka harakat ya kutetea ugali wake anajikuta anajidhalilisha

Hana fact hana documents
 
Kumuita CAG muongo ni kwamba ile ripoti 'ameipika'.Na kwa ripoti hii maridhawa ya CAG,itatusaidia kujua akili za baadhi ya waheshimiwa wetu wengi.
 
Back
Top Bottom