CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

tatizo ni malezi,kama umelelewa katika misingi mibovu,hayo ndo madhara yake,ubinafsi,uchoyo,uroho,ulafi,wizi,etc
 
Mimi niliwahi kushauri viongozi wetu wapimwe afya ya akili from time to time, wanaweza kuingia wakiwa timamu, halafu ukichaa ukawapata, namna rahisi ya kutambua mushkeli wa afya ya akili zao ni kwa maneno yao na matendo yao.
P

Ukiwapima ukakuta wamevuta bangi kali ya Iringa kwa ruhusa ya rais ili wawe wakali utafanyaje?
 
Kwahiyo RAIS aliteua CAG MUONGO ILI AWE ANAMUONGOPEA?

HAKUFANYA VETINGI WAKATI WA UTEUZI WAKE?
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Shukrani mkuu Mayalla

Nimefurahi umekua ukisisitiza vuongozi kupimwa afya ya akili mara kwa mara. Hili naliina ni jambo la msingi sababu mtu anaweza kupotezea uwezo wa kufikiria as time goes. Ni wazo muhimu lisilotiliwa mkazo na watanzania kwa sasa but muda unavyosonga umuhimu wa hili suala na endelea kuuona

Pili sijakubaliana na point kuwa kuna baadhi ya maeneo taratibu hazikufuatwa ila fedha zilitumika vizuri. Hiyo sio sahihi sababu kwanini usifuate taratibu kama una Nia njema?

CAG hufanya auditing ambayo iko based on accounting principles and standards accepted by international board of accounting and auditing. So any exceptional of CAG kuandika reports ambayo iko opposite na standard auditing ni kwenda kinyume na professionalism yake naye ni prof

Kwenye mfano yako , CAG anakua guided na two principles
1. Objectivity principle, all transactions and information should be free from bias and capable of independent verification. Maana kama mtu kanunua kitu cha Uma kupitia fedha za Uma Uma unatakiwa uwe na uwezo wa kujiridhisha hayo mnunuzi kama yako sahihi. Unaweza kusema naenda kununua tv na ukanunua kwa mil 1 halafu ukasema nimenunua kwa mil 3. Ikiwa huna evidence tutaamini ipi

2. Principal of disclosure, means all relevant information should be desclosed in the financial statements of respective year. Hapo Nondo kasema ununulizi ulifanyika mwaka 2015 Nov, leo ndio unasema mzigo upo, je hizo pesa zilikua wapi toka mwaka 2o15 , nani alikua incharge

Niishie hapo ila tujifunze kuweka pembeni u professional wa watu muhimu kama CAG sio kuongea maneno ya kejeli bila facts.
 
Mkuu, huwa naamini sana katika busara zako ila hapa nadhani umepotoka au unataka kupotosha japo sidhani Kama una maslahi yoyote katika kufanya hivyo.

Unasema report ya CAG sio msahafu, hii ni kweli maana report inaweza kuwa na mapungufu kadha wa kadha. Ila ambacho sikubaliani na wewe ni hapo unapobariki manunuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria za fedha eti kwa kigezo kwamba manunuzi hayo yalifanyika kwa manufaa ya umma na umetolea mfano manunuzi ya ndege. Hii sio sawa mkuu.

Kama tuliweka taratibu/kanuni/sheria za manunuzi basi ni lazima zifuatwe na mtu akiacha kuzifuata anapaswa kuwajibishwa kwa maana kutofuata sheria halali zilizowekwa ni kosa kisheria na huwa tunasema no one is above the law, hata rais mwenyewe hayupo juu ya sheria.

Najua kuna ideology mbili katika kufanya maamuzi ambazo ni rule based na result based, wewe umebase kwenye result based, kwamba japo sheria hazikufuatwa ila results zimekuwa nzuri Sasa swali ni je vipi ingetokea result mbaya, mfano tungekuwa tumepigwa, ungekuwa na msimamo huo huo?

Halafu Kama unaongozwa na good will kwanini usifuate taratibu katika manunuzi? Watu wasio safi ndio mara nyingi huwa hawafuatwi sheria. Nahitimisha kwa kusema japo report ya CAG sio msahafu ila kwa kuwa nyaraka za manunuzi hazipo na taratibu zilisiginwa basi ni lazima watu wawajibishwe no matter results walizo deliver. Na hizo ndege naamini tumepigwa na ipo siku ukweli utaelezwa na inshaalah wote waliohusika watawekwa behind bars.
naunga mkoni hoja
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ? Wakati mzigo unaingizwa alikuwa na kesi ya rushwa halafu Leo anakuja kuongea upupu. Lugola ni msanii mzee mwenye matukio utafikiri mgonjwa wa akili maybe anaugonjwa wa akili. Unakumbuka kuna kipindi alikuwa anaingia bungeni mara kavaa kofia za kininja mara red cross mgongoni. Inaweza ukawa mikakati kutoka juu kwa kushirikiana na spika na baadhi ya wabunge wa ccm kuendelea kumsema ili aonekane hafai lkn kwa CAG Wameshika pabaya. Magufuli hawezi kumwondoa labda amtume Bashite ampige risasi. Lkn anavyolindwa na mungu co rahisi risasi kutoka. Wanashindwa wao
 
Mh awamu hiui tutaona mengi, Waziri ni serikali na tamko lake ni tamko la Serikali . sasa amkaguzi mkuu wa hesabu za serikali leo hii anaitwa ni Muongo na kwamba hatakiwi kuaminiwa imekaaje hiyo wadau?
 
Pale njaa inapotoka tumboni na kuhamia kichwani, haya ndo matokeo yake, na ni matatizo makubwa, huyu jamaa anayumba sanaaaa. Asante Abdul Nondo umetufanya tuujue mchakato wa Auditing japo in Brief.
 
Mkuu Dyuteromaikota, you are right, sasa ni mwendo wa trust tuu, mambo ya transparency na uwajibikaji waachie wengine, ndio maana Tanzania tumejitoa kwenye ule mkakati wa open government Initiatives.
P
Rais Magufuli awe makini, kwasababu sasa taratibu baadhi ya wabunge na mawaziri wa CCM wanaikataa serikali yao wenyewe. Where is this leading to? Na kwavile hata yeye mwenyewe huwa anasema baadhi ya watendaji wake ni... ..asishangae siku wakimwita na yeye ni mwongo!
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
Unahitimisha kukubaliana na nani? Wewe umetoka chuo juzi utayajua yanayotendeka maofisini? Hata hao wakaguzi wa CAG wengine ni wababaishaji ile mbaya wako kirushwa zaidi wakipewa kitu kidogo hata hawakaguwi kabisa! Wasipopewa kitu kidogo wanaandika ripoti kukukomoa na ndiyo maana audit queries zao nyingi zinaishia kwenye Kamati za Bunge za PAC na LAPF hiyo inazihirisha audit queries zao nyingi hazina mashiko. Ingekuwa audit queries zao ni conclusive kuwa ni wizi zisingepelekwa Bungeni for reviews. Hivyo tuache kupotosha kuwa RIPOTI YA CAG ndiyo conclusive kuwa ni wizi.
 
HUKO KOOTE MNAZUNGUSHANA TU,

Kifupi NI hivi SARE ZA POLIS HAZIKUWA ZIMENUNULIWA KIPINDI CHA UKAGUZI WA CAG.

ZIMENUNULIWA wiki moja baada ya ukaguzi,

Hivi hujiulizi tangu CAG atoe Ripoti Yake Kwanini hakukanusha siku hiyo hiyo na awaoneshe waandishi wa habari Hilo kontena la nguo? Jibu hazikuwepi Hivyo ametumia wiki nzima kuzinunua na kuzipaki kwenye kontena!!!

Pili, Pesa za sare hizo zilitoka tangu 2015, Hadi Leo Zipo kwenye Makontena zikifanya Nini badala ya kugawiwa kwa wahusika?

Kama hapakuwa na uhitaji wa hizo sare Kwanini waliidhinisha manunuzi ya hizo sare ? Kukaa kwenye kontena na kuzidi kuchujuka hii siyo Hasara kweli?

Mwambieni siyo wote tunaakili kama zake.

Bangi wavute kwa kiasi,Hawakuambiwa wazidishe kipimo
Issue ya Lugumi ameshindwa kuimaliza na anarukia ya CAG, wakati anapewa uwaziri alimpiga mkwara Lugumi ila baada ya Kumtembelewa ofisini kwake naona mdomo ukashonwa, ila kwenye ripoti hii ya CAG zimwi la Lugumi bado linamuandama na ndo maana anatumia nguvu kujaribu kuonyesha ripoti ya CAG si kitu. Ukweli ni kwamba tuna wapiga dili kibao wanaojifanya mikono yao ipo safi.
 
kwahiyo ni sawa hela za umma zitumike bila bunge kuhidhinisha hata kama tutaona matokeo ya kutumika fedha hizo?

wanaweza kusema ndege wamenunua kwa elfu moja kumbe wamenunua kwa mia tano...au walichukua elfu mbili wakatumia elfu moja,

hii serikali bado ina uongo uongo mwingi sana, sasa repoti ya CAG inawaumbua wanapaniki.
CAG ameshabugi kwa kuungana na akina Zitto hajua kuwa wakina Zitto ni wanasiasa uchwara!
 
Mimi niliwahi kushauri viongozi wetu wapimwe afya ya akili from time to time, wanaweza kuingia wakiwa timamu, halafu ukichaa ukawapata, namna rahisi ya kutambua mushkeli wa afya ya akili zao ni kwa maneno yao na matendo yao.
P
Nafikiri wewe ndiyo ungepimwa kwanza. Kwa sababu hujulikani kama ni ndege au mnyama! Ni sawa na popo!
 
Kumuita CAG kwamba ni muongo, ni kuwatukana walipa kodi wa nchi hii. Kiongozi mzuri ni yule anayekubali kukosolewa na kurekebisha mambo kwa manufaa ya Taifa. I stand with CAG.
 
Mkuuu, zingatia mkuu @paschalmayallajuu ya jiwe hawezi ona lolote ovu bali wasaidizi wa jiwe ndio hua pasikali anawatupia kamba.
Mkuu, huwa naamini sana katika busara zako ila hapa nadhani umepotoka au unataka kupotosha japo sidhani Kama una maslahi yoyote katika kufanya hivyo.

Unasema report ya CAG sio msahafu, hii ni kweli maana report inaweza kuwa na mapungufu kadha wa kadha. Ila ambacho sikubaliani na wewe ni hapo unapobariki manunuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria za fedha eti kwa kigezo kwamba manunuzi hayo yalifanyika kwa manufaa ya umma na umetolea mfano manunuzi ya ndege. Hii sio sawa mkuu.

Kama tuliweka taratibu/kanuni/sheria za manunuzi basi ni lazima zifuatwe na mtu akiacha kuzifuata anapaswa kuwajibishwa kwa maana kutofuata sheria halali zilizowekwa ni kosa kisheria na huwa tunasema no one is above the law, hata rais mwenyewe hayupo juu ya sheria.

Najua kuna ideology mbili katika kufanya maamuzi ambazo ni rule based na result based, wewe umebase kwenye result based, kwamba japo sheria hazikufuatwa ila results zimekuwa nzuri Sasa swali ni je vipi ingetokea result mbaya, mfano tungekuwa tumepigwa, ungekuwa na msimamo huo huo?

Halafu Kama unaongozwa na good will kwanini usifuate taratibu katika manunuzi? Watu wasio safi ndio mara nyingi huwa hawafuatwi sheria. Nahitimisha kwa kusema japo report ya CAG sio msahafu ila kwa kuwa nyaraka za manunuzi hazipo na taratibu zilisiginwa basi ni lazima watu wawajibishwe no matter results walizo deliver. Na hizo ndege naamini tumepigwa na ipo siku ukweli utaelezwa na inshaalah wote waliohusika watawekwa behind bars.
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Ukimuangalia Kangi kwa muonekano tu unaweza ukajua ni comedian yule brother K au ndugu? Vivyo hivyo anapeleka na anaongea mara nyingi like comedian
 
Back
Top Bottom