CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

CAG sio Muongo kwa vigezo hivi

Bwana Mayalla acha kutetea huu utumbo utajivunjia heshima.Hata kutetea tumbo nako kuna mipaka. CAG hawezi kuzunguka kwenye maGodown yote ya serikali kujiridhisha km mzigo uliingia au haukuingia anatumia documents. Wote tumemshuhudia kangi Lugoda akimuita CAG muongo!
Huwa sielewi ni vipi huwa mnashindwa kuelewa anachoandika Pasco.
 
Mimi naomba niendelee kumtia CAG wetu Profesa Assadi moyo.
Kanyaga twende Baba, Usicheke na kima.

Sisi wamasai hua tunaamini Dawa inayoponyesha ni ile chungu.
Hahahaha
 
Watanzania tunaumia kuona CAG anavyoshambuliwa bila sababu,CAG ndiye mkaguzi wa kodi zetu , watanzania tuna wajibu wa kusimama nae ili kuwe na usimamizi imara wa fedha zetu (effective finance management).

Haijawai kutokea duniani CAG kuitwa muongo isipokuwa Tanzania mbele ya umma na Bunge,tena kuitwa na waziri wa serikali inayopambana na rushwa na matumizi mabaya ya fedha.

Mchakato wa ukaguzi yaani "Audit process" ni mpana sana, kufahamu mchakato huu ndio unaweza jua uongo wa CAG au Ukweli wa CAG . Tutagusa gusa sehemu kadhaa .
Case study iwe *sare za Jeshi la polisi*

Ukisoma Ripoti ya CAG ya 2018 , kurasa 309 hadi 312 . Anasema ukaguzi juu ya sare za jeshi la polisi ni kufuatia ombi la Takukuru ,yaani Takukuru walipata taarifa wakampa CAG achunguze ,suala hili la sare ni la tangu 2015 Novemba hivyo kwa CAG huu ulikuwa ukaguzi maalumu, sheria ya ukaguzi wa umma Na 11 ya 2008 kifungu cha 29 na 36 kinampa nguvu hata kama ripoti yake hii ni ya 2018.

CAG anasema mkataba ulisainiwa tar 2/Nov/2015 Kati ya katibu mkuu wizara ya mambo ya ndani na mzabuni "Daissy General Traders" kununua sare za polisi china mhasibu alipaswa awe ameingiza mzigo Kipindi kisichozidi siku 180 ,ila mzigo ulifika kwa siku mbili tangu call of order.

CAG anasema alitaka kujiridhisha kama kweli mzigo huo upo na umeingizwa kweli, CAG aliomba nyaraka kutoka kwa mzabuni (Daissy General Traders) kama mzigo uliingia kweli ,Hati ya kupokelea shehena,hati ya madai,orodha ya mali zilizo ktk meli,cheti cha ukaguzi.

CAG hakuishia hapo akaenda kuuliza Bohari kuu ya jeshi la polisi ambapo mzigo huo ulipaswa kufikia huko ,majibu yakawa hakuna mzigo wowote uliopokelewa.

CAG hakuishia hapo akaenda Bandarini katika Mfumo wa forodha TANCIS wa TRA yaani Tanzania Customer intergrated system) kupitia TANCIS katika mfumo(web-based) unaweza kuona mzigo wowote uliotoka au kushushwa na taarifa zake hubaki (discharged cargo and it's report). Soma "TANSCIS Bronchure of Jun 2016.Tancis makes cargo clear easy" bado CAG hakuona mzigo wowote.

CAG huwa haishii hapo ,huangalia pia mambo ya internal control system ya Ofisi inayokaguliwa, financial system, ledger na mambo ya sheria kwa utaalamu na taratibu itakuwa CAG alifanya hivyo pia.

CAG haishi hapo bado Kuna majadiliano mafupi huyafanya na wakaguzi wa ndani (internal auditors) au kamati ya ukaguzi (Audit committee) huitwa Exit meeting au Exit conference , wakaguzi wa ndani wananafasi ya kutoa utetezi wao juu ya findings za CAG.

CAG haishi hapo,ana andikia barua Ofisi iliyokaguliwa inaitwa "Audit management letter" akielezea kuhusu alichokigundua kama ni madudu ,rushwa ,ufisadi (Deficiencies in internal control) atajikita kushauri ,kutoa maoni na mapendekezo kwao waboreshe mifumo yao na utendaji (internal Control system ) Kama sheria inavyomtaka afanye hivyo kifungu cha 12 ,sheria ya ukaguzi wa Umma 2008.

CAG haishii hapo tuu ,kabla ya kutoa Ripoti yake ya ukaguzi (CAG Report) kwa Mh.Rais, na baadaye Bungeni .Ofisi zilizokaguliwa huwa zina nafasi ya kujibu kwa zinazopenda ,barua yao huitwa "Management representation letter au Management response" huwa wanaweza kukiri na kukubali kujirekebisha au wakaendelea kujitetea au pia waka kaa kimya ingawa kimya huonesha dharau.

Pia wengine huwa wanajibu kwa kuendelea kujitetea,
Ingawa kujitetea kwa hatua hii inahitaji facts zaidi ya alizonazo CAG ,na barua hii ya kujibu CAG pia huichukulia Kama ushahidi wa ukaguzi (Audit Evidence).

Sasa mchakato wote huu CAG anaitwa "MUONGO" ?

1.Mh.waziri anasema mzigo upo kwenye Kontena alienda kuona ,Mzigo uliagizwa 2015 leo 2019 huo mzigo upo kwenye makontena badala ya kuwa Bohari kuu ya jeshi la polisi au hata kuwa tayari kugawiwa kwa polisi , katika Kontena sare zinafanya nini ?

2.Je, anajua kilichojadiliwa katika Exit meeting ya CAG na wakaguzi wa ndani wa wizara?

3.Barua ya management response kwa CAG ,waliokaguliwa walikuwa na nafasi ya kuendelea kujitetea ,je walifanya hivyo ili waweke utetezi wa Mh.wazir ?

4.Fedha za umma zinapotumika kununua vitu ,lazima ziwe recorded katika ledger (Purchase ledger au costomer deposit) ,je CAG alipewa ledger ili aone transactions ya malipo kwa mzabuni?

5.Hizo sare katika Kontena zilifika lini ? ,Kama ni muda mrefu kwanini CAG aliangalia katika mfumo wa forodha (TANCIS-TRA) hakuona mzigo ulioingia ? ,kwanini alinyimwa nyaraka na mzabuni Daissy General Traders? ,Kwanini watu wa Bohari kuu walikataa hakuna mzigo ? ,Kama kulikuwa na taarifa yeyote kuhusu uwepo wa mzigo kwanini hakuambiwa kabla ya report yake kupelekwa kwa Rais ?

Tufahamu kuwa CAG hajitungii stori kuhusu ukaguzi,wala hafanyi yeye tuu bila kuhoji ,hitimisho la CAG linaundwa pia na majibu aliyojibiwa na wakaguliwa.Hivyo kauli ya kusema CAG ni muongo inapaswa ipingwe sababu itajenga Precedents kwa viongozi kadhaa wakitenda mskosa rushwa kwa kujua kabisa ,watabishia ukaguzi na kumuita CAG muongo,hii itakuwa ni hatari kwa ulinzi wa fedha zetu.

Hivyo tuhitimishe kwa kukubaliana pamoja kwa kusema CAG sio MUONGO,CAG anafanya kazi kwa nyaraka, utata ni pale nyaraka zinapokosekana.

Shukrani sana.

Abdul Nondo

abdulnondo10@gmail.com
Duh!
Sare za polisi pia mpaka ziagizwe kutoka nje ya nchi?
 
Pascally unaibagaza tu taaluma yako ya uandishi kwa kusema kila akisemacho Rais ni kweli tupu, nae ni mwanadamu pia kama wewe anaweza asiseme kweli wakati fulani for a political circumstances,

Hata albashir wa Sudan alikuwa Rais na upo uwezekano wakati fulani aliwaaminisha wananchi wake kwamba yeye ni muadilifu na sio mwizi wa mali za umma, lakini wanasudan walivyokinukisha tuliona maburungutu ya madolari na mapaundi aliyoyaficha nyumbani kwake.

So sio kisa ni Rais tumuamini kwa kila kitu yeye sio mungu. Jikite kwenye ufisadi wa jeshi la polisi, huku kwa Rais unaibagaza taaluma yako tu.
Ukimuelewa Pascal wala hupati tabu. Hebu msome vizuri, hanaga shida huyo mshkaji na huwa habadiriki sema kwasasa inatakiwa umuelewe maudhui yake tu basi.

Kuna siku aliposti kitu humu, nilifura balaa...nikamsubiri barabarani apite na pikipiki yake nimtandike manati, wakati namsubiri...nikawa napitia tena maandiko yake ili kuongeza hasira, nilichokiona...nikaishia kugonga like na kurudi home.
 
Huwa sielewi ni vipi huwa mnashindwa kuelewa anachoandika Pasco.
Hauna clip yeyote ya mfano tuiweke hapa labda itasaidia?? Maana wakati fulani ufundishaji unakua mwepesi kwa kutumia nyenzo

Hebu tafuta clip moja hasa ya Mr Bean ndio itakua rahisi kuielewa
 
Duh!
Sare za polisi pia mpaka ziagizwe kutoka nje ya nchi?
Hilo sasa ni jambo jingine zito, CAG angeweka na hilo nafikiri waziri sasa angeingia bungeni na boksa kabisa akitishia kuivua ampe laana CAG
 
Mkuu, huwa naamini sana katika busara zako ila hapa nadhani umepotoka au unataka kupotosha japo sidhani Kama una maslahi yoyote katika kufanya hivyo.

Unasema report ya CAG sio msahafu, hii ni kweli maana report inaweza kuwa na mapungufu kadha wa kadha. Ila ambacho sikubaliani na wewe ni hapo unapobariki manunuzi yasiyofuata kanuni, taratibu na sheria za fedha eti kwa kigezo kwamba manunuzi hayo yalifanyika kwa manufaa ya umma na umetolea mfano manunuzi ya ndege. Hii sio sawa mkuu.

Kama tuliweka taratibu/kanuni/sheria za manunuzi basi ni lazima zifuatwe na mtu akiacha kuzifuata anapaswa kuwajibishwa kwa maana kutofuata sheria halali zilizowekwa ni kosa kisheria na huwa tunasema no one is above the law, hata rais mwenyewe hayupo juu ya sheria.

Najua kuna ideology mbili katika kufanya maamuzi ambazo ni rule based na result based, wewe umebase kwenye result based, kwamba japo sheria hazikufuatwa ila results zimekuwa nzuri Sasa swali ni je vipi ingetokea result mbaya, mfano tungekuwa tumepigwa, ungekuwa na msimamo huo huo?

Halafu Kama unaongozwa na good will kwanini usifuate taratibu katika manunuzi? Watu wasio safi ndio mara nyingi huwa hawafuatwi sheria. Nahitimisha kwa kusema japo report ya CAG sio msahafu ila kwa kuwa nyaraka za manunuzi hazipo na taratibu zilisiginwa basi ni lazima watu wawajibishwe no matter results walizo deliver. Na hizo ndege naamini tumepigwa na ipo siku ukweli utaelezwa na inshaalah wote waliohusika watawekwa behind bars.
Mkuu dawa yenu
Paskali anapoandika,yakupasa usome mara mbili ili kwenda nae.
Nakushauri rudia tena pole pole andiko lake. Naamini utamwelewa.
 
Hao wakina Lugola ndio wale waliokimbia hesabu leo nikimjibu majibu yanayohusu hesabu hatuwezi kuelewana na ndio maana hamuelewi CAG...
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P

Sawa kabisa P....lakini pia kuwepo kwa nguo store ni jambo moja..mkataba wa manunuzi wa nguo hizo ni jambo jingine. Nani anaweza kutudhibitishia kwamba wakati tunaingia mkataba wa kununua nguo stoo ilikuwa nyeupe? Au nani anaweza kutudhibitishia nguo hizi sio za magendo? L****i is still a legend.msicheze na malegend buanaaaa
 
HUKO KOOTE MNAZUNGUSHANA TU,

Kifupi NI hivi SARE ZA POLIS HAZIKUWA ZIMENUNULIWA KIPINDI CHA UKAGUZI WA CAG.

ZIMENUNULIWA wiki moja baada ya ukaguzi,

Hivi hujiulizi tangu CAG atoe Ripoti Yake Kwanini hakukanusha siku hiyo hiyo na awaoneshe waandishi wa habari Hilo kontena la nguo? Jibu hazikuwepi Hivyo ametumia wiki nzima kuzinunua na kuzipaki kwenye kontena!!!

Pili, Pesa za sare hizo zilitoka tangu 2015, Hadi Leo Zipo kwenye Makontena zikifanya Nini badala ya kugawiwa kwa wahusika?

Kama hapakuwa na uhitaji wa hizo sare Kwanini waliidhinisha manunuzi ya hizo sare ? Kukaa kwenye kontena na kuzidi kuchujuka hii siyo Hasara kweli?

Mwambieni siyo wote tunaakili kama zake.

Bangi wavute kwa kiasi,Hawakuambiwa wazidishe kipimo
LUGOLA HAFAI HATA KUONGOZA KUKU WA KISASA.
 
Ndugu dawa yenu

Pascal Mayalla ni verified user na sio kama mimi na wewe. Kwahiyo msome vizuri.

Pascal ni yuleyule na hajabadirika na alichokiandika kisome vizuri, utagundua hoja zake ndio haswa ni kile ulichokisema wewe. Huna haja ya kupingana nae, msome vizuri kwenye mistari yake huku ukizingatia "inayo trend kwa sasa" nina amini utamuelewa

Usisahau aliwahi kutuhumiwa na kuitwa mzobe mzobe kwa kosa dogo tu la mtu kutoizingatia alama ya kiulizo matokeo yake maoni yake huru yenye maneno zaidi ya mia mbili yote yakaharibika kwa kukosewa tu kuiona alama ya kiulizo. Watu zaidi ya 300 walioaminiwa na watanzania kutusimamia mambo yetu wote walipata upofu hawakuiona hiyo alama ilhali iliendelea kuwepo.

Kamati yenye wataalam wakatumia muda wao hadhim wa kufanya mambo muhimu kwa kujikita kuhukumu jambo kwa kushindwa tu kuiona alama ya kiulizo.
Sawa mkuu, ngoja nimsome tena huenda nikakiona hicho ulichokiona wewe katika comment ya Pascal Mayalla
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Matumizi mazuri kwa sheria za kiuhasibu na ukaguzi lazima zifuate taratibu mlizojiwekea kinyume na hapo ni wizi. Waziri anatakiwa aguate audit recommendation alizowekewa kwenye management letter kujibu hoja na sio kutishia watu kuwa atavua uwaziri sijui nguo. Sare kuwa kwenye makontena sio hoja hoja ni kuwa kwa nini pia mpaka Leo ziko kwenye makontena
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza asante kwa nondo hii, sidhani kama mtu mzima mwenye akili timamu kichwani kwake anaweza kumuita CAG ni muongo, ujue tuna vichaa wengi kuliko tunavyojijua.

Kwa vile humu sio members wote wanaweza kusoma kila kitu, ni vema pia ungeweka ref ya aliyemuita CAG muongo kama hivi

Ila kwenye ripoti ya CAG, sio kila upotevu wa fedha za umma au matumizi makubwa ya fedha kwenye manunuzi bila kufuata taratibu ni matumizi mabaya ya fedha za umma au ni ufisadi.

CAG anakagua kufuatwa kwa sheria taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma. Hivyo kuna maeneo ni kweli sheria taratibu na kanuni zilikiukwa lakini fedha zikatumika vizuri kwa ajili ya manufaa ya taifa mfano mzuri ni fedha za kununua zile ndege mpya, hazikufuata mchakato wa manunuzi wala taratibu za matumizi ya fedha za umma, ikiwemo kupangiwa bajet, kuidhinishwa na Bunge, CAG kusaini etc, kwa vile tumefanya manunuzi kwa utaratibu mpya wa Rais Magufuli unaoitwa kupiga tanchi, hatimaye ndege zimekuja na tumezishuhudia.

Hata matumizi makubwa kwenye Vote 20, japo hayakuidhinishwa na Bunge, lakini ni matumizi mazuri tuu, sote tunashuhudia rais wetu katika ziara zake, anatembea na mabulungutu ya hard cash na kugawa kwa wananchi.

Pia kuna maeneo ya matumizi makubwa, sheria taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini huko ndiko tunapigwa.

Ukaguzi huanza kwa Entrance Meeting na kumalizika kwa Exit Meeting, hivyo inawezekana hadi CAG anafanya exit meeting, hizi sare za Polisi zilikuwa hazijaingia, lakini baadae ziliingia na ni kweli ziko ndani ya makontena.

Japo Ripoti ya CAG sio Masahafu au Bible, ila kiukweli kabisa aliyemuita CAG muongo, sikuzote ni kama kituko fulani.
P
Kaka yangu, you are smart!
 
Back
Top Bottom