CAG na Peter Madeleka wanapotosha umma, serikali ilikosa ushahidi kesi ya VISA- KIA na kuamua kuifuta; watuhumiwa walikaa Gerezani zaidi ya mwaka.

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Jamii forum Facebook account pamoja na Habari leo ni baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hoja ya visa bandia zilizokamatwa zikitokea afrika kusini; Kwa urahisi wa rejea wanajamvi tunaweza kupitia google kuuliza habari hizi na tutapata taarifa za ndani. Tukio hili linaonekana kuripotiwa Kwa mara ya kwanza tarehe 06/08/2019

Siku chache baadaye alikamatwa wakili Peter Madeleka Kwa issue ya vibali feki akiwa na mke wake ambaye alikuwa ameacha kazi Uhamiaji nakuamua kujihusisha na shughuli za uwakili kupitia kampuni ya familia iliyopo hapa Arusha. Naamini kukamatwa kwake pia kuliripotiwa kwenye vyombo vya habari na taarifa zipo mitandaoni

Lakini pia nakumbuka nikiwa Moja wa Mawakili tuliofanya kazi Arusha that time ilifunguliwa kesi Kuhusu wizi wa mapato ya visa katika kituo cha KIA na baadhi ya watuhumiwa wakiwa ni maafisa Uhamiaji walikwenda mahabusu Kwa kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi hii ilifunguliwa baada ya JPM kuelekeza Takukuru Kufanya uchunguzi na baadaye wale waliokamatwa walifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na vyombo vya habari viliripoti taarifa hii kwenye frontpage zao ikiwemo taarifa ya habari. Waliripoti na majina ya watuhumiwa wote waliorodheshwa. Niombe turudi kwenye technology tuulize google ni rafiki yetu atatusaidia facts za kujadili na kuvikumbusha vyombo vya habari Kuhusu walichowahi kueleza umma.

Mimi nikiwa moja ya Mawakili waliokuwa wanasaidia jopo la utetezi kuandaa baadhi ya hoja nakumbuka watuhumiwa walipohojiwa walikataa tuhuma na walieleza wazi kwamba " Mwaka huo 2019 Uhamiaji ilianza kutoa visa online na hivyo visa nyingi zilitolewa nje ya nchi na siyo mipakani kama ilivyokuwa imezoeleka, lakini mifumo mipya haikuwa na uwezo wakutunza kumbukumbuku za visa zilizotolewa ubalozi" udhaifu wa mifumo ukapelekea wageni waonekane wameingia nchini bila visa. Nakumbuka Moja ya watuhumiwa aliwataka Takukuru kwenda kuhakiki visa hizo kwenye mfumo wa malipo ya Serikali hazina kabla yakuwatuhumu na kuwachafulia CV zao. Baada ya Mtuhumiwa Mmoja kuibua technicality hii ililazimu ukusanyaji ushahidi ufanywe upya na hivyo kupelekea watuhumiwa wale kuwekwa ndani kwa zaidi ya mwaka kila siku DPP akawa anadai upelelezi unaendelea. Upelelezi haikupata ushahidi wowote wa wizi na Hii iliwekwa wazi na Mawakili wa jamhurii ila dana Dana zikawa nyingi. I was expecting peter to narrow down this story to remind law enforcement about misconduct, lakini nayeye kajifanya hii kesi hana taarifa nayo wakati he knows each and everything na Hawa walikuwa wahanga wenzake.

Naomba niwajulishe nini kilitokea; baada ya watuhumiwa wale kukaa ndani kwa zaidi ya mwaka Kwa tuhuma za uhujumu uchumi DPP alifuta kesi Ile baada ya awamu ya Sita kuja madarakani Kwa kukosekana ushahidi na watuhumiwa wote kuelekezwa warejeshwe kazini japo Sina uhakika kama walirejeshwa au Wapo wanasugua benchi.

Taarifa za kukamatwa maafisa waliotuhumiwa huko Kilimanjaro ziliripotiwa Sana kwenye vyombo vya habari na zipo uzuri Ruge alitifundisha texhnologia haidanganyi. Wakili mwenzetu Peter Madeleka alikuwa gereza Moja na wahanga wenzake na walipigania HAKI pamoja japo yeye alikubali kusarender akaenda kwenye prebagaining na wenzake walioteswa bila hatia wakakomaa Hadi mwisho wakigoma kukiri makosa Kwa sababu waliamini kwamba Wapo innocent.

Leo mtu yule yule anayeelewa undani wa kesi nzima iliyowakuta wenzake Kwa uonevu hataki kuweka wazi upande wa pili wa namna vyombo vya dola vilivyotumika kuwaweka watu wasio na hatia zaidi ya mwaka ndani anajadili hii kama hoja mpya na anapotosha umma akitaka umma uhamini kulikuwa na wizi wakati mwendesha mashtaka alisema wazi hakukuwa na ushahidi wa tuhuma hizi.

Lakini anapotosha akiamini wazi kwamba Watanzania awapendi kutafuta taarifa,anapotosha akitambua wazi kwamba waandishi wa habari w Tanzania awana muda wa kufanya kazi za kichunguzi. Endapo yupo kiumbe anapingana na hoja hii aende aulize status ya kesi iliishaje? Kama mahakama iliwaacha hawana hatia Leo tunataka kuibeba hii hoja Kwa uchunguzi na ushahidi Gani? Je, Madeleka anatetea haki au anajitetea mitandaoni? Nimechukizwa Kwa sababu Mimi ni mmoja wa watu walioangaika kwenye kesi hizi leo hii tunaposhindwa kusimamia kupiga vita uonevu tunakosea taaluma zetu.

Nilitegemea Madeleka amwone CAG kama ofisi yenye mapungufu kwa sababu kesi hii imefutwa akiwa uraiani na watuhumiwa baadhi ni watu wa karibu na mke wake na alikuwa nao jela. Au anataka kusema DPP alikosea kuifuta kesi hii? Anataka kutiaminisha CAG Hana taarifa hizi ambazo ziliripotiwa na vyombo vya habari? Je mahakama ilikosea? Mbona hakuna rufaa ya maamuzi haya?

Nilitegemea waandishi wa habari ambao waliiweka front page hii taarifa miaka ya nyuma waje watueleze stori nzima Kwa sababu walikuwa wanaripoti live kutoka mahakamani Moshi na mitandaoni utapata habari zao. Leo hii vyombo vya habari hata kufukua taarifa za nyuma kwao imekuwa kikwazo.

Hakuna sehemu CAG anatuambia Takukuru waliwakamata maafisa Uhamiaji na DPP akawafungulia mashtaka, hakuna sehemu CAG anaeleza kwamba vyombo vya uchunguzi na DPP walifuta kesi baada ya kukosekana ushahidi; hakuna sehemu CAG anaeleza kwamba hakukuwa na wizi Bali kulikuwa na Changamoto ya mifumo ambayo ukiingia hata kwenye google ukauliza lini immigration walianza kutoa visa online you will get it.

Hapa ndipo ninapokubaliana na mtoa hoja Mmoja humu JF kwamba ripoti ya CAG Ina mapungufu. Inataka kuwaaminisha watu Kuna wizi lakini wizi hauonekani, irregularities au kufail kucomply na Sheria kwake yeye tayari ni wizi which is not true.

Mwisho; nalaani kitendo Cha kushikiliwa mwenzetu Peter na niombe endapo wanaomshilia Wana hoja au ana hatia Sheria zifuatwe. Tulimtesa for more than a year Leo lazima tukubali awezi kuwa normal ana machungu; nakubali mapungufu lakini siyo kigezo Cha kumweka ndani ana Uhuru wa kusema. Serikali ilichopaswa kufanya nikutoa tu ufafanuzi wa hoja siyo kutumia nguvu.

Niwaombe moderators mtutaftie magazeti na video zinazohusu sakata la visa KIA mweke hapa mtasaidia Sana kuwafundisha kazi waandishi ambao wameshindwa kugoogle hata walichorupoti Jana. Endapo tutarudi kwenye JF ya zamani ya kuvunja hoja Kwa hoja tutalifanya jukwaa letu kuwa imara na vyombo vya habari vitalazimika kuanza kuifanya kazi Yao.

Tumuulize CAG endapo serikali ilishindwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha hata shs mia kwamba iliwekwa mfukoni; yeye huo ushahidi wake kwamba serikali ilipata hasara ameutoa wapi na kwanini vyombo vya uchunguzi havikubaini huo wizi kama yeye anavyosema? Nina hasira Kwa sababu hii ni Moja kesi ambayo unaona wazi Watumishi wa Umma wanavyoweza kubambikiana kesi kijinga huku wenyewe wakikiri kwamba hakuna kesi eti ni maelekezo kutoka angani.

Nimeshare taarifa hizi Kwa sababu tu zipo public lakini hakuna aliyeikumbusha public kureview na kuelewa ukweli. Wanaponda kutafuta ukweli watautafuta.
 
Nadhani analalamika mchakato wa kubambikwa kesi asiyohusika nae, kwa mujibu wa maelezo yake. Mkweli nani sasa.
 
Kwa mujibu wa maelezo yake analalamika juu ya kuhusishwa kwa kosa asilotenda. Nini ukweli wa hili.
 
Mleta mada ni kwanini peter atuhumiwe kuwa ni mtu mbaya anamuandama sana mkuu wake wa zamani wa kazi na kwa madai yake mwenyewe walipanga kumdhuru.

Hivi mbowe au dr slaa wamelaumiwa mangapi mbona wako kimya wanaendelea na maisha yao. Kwanini peter akilaumu twitter basi atafutwe apotezwe.

Ningewashauri hao uhamiaji wangemuacha peter akapiga kelele mwisho wake angechoka akanyamaza huu ndio unaitwa uhuru wa maoni na ndio unaopelekea wananchi wadai katiba mpya. Maana lazima tujifunze kusikiliza maoni tofauti na tunayopenda. Tanesco kila mtu anawaona magumashi lakini mbona wanaacha watu waseme.
 
Jamii forum Facebook account pamoja na Habari leo ni baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti hoja ya visa bandia zilizokamatwa zikitokea afrika kusini; Kwa urahisi wa rejea wanajamvi tunaweza kupitia google kuuliza habari hizi na tutapata taarifa za ndani. Tukio hili linaonekana kuripotiwa Kwa mara ya kwanza tarehe 06/08/2019

Siku chache baadaye alikamatwa wakili Peter Madeleka Kwa issue ya vibali feki akiwa na mke wake ambaye alikuwa ameacha kazi Uhamiaji nakuamua kujihusisha na shughuli za uwakili kupitia kampuni ya familia iliyopo hapa Arusha. Naamini kukamatwa kwake pia kuliripotiwa kwenye vyombo vya habari na taarifa zipo mitandaoni

Lakini pia nakumbuka nikiwa Moja wa Mawakili tuliofanya kazi Arusha that time ilifunguliwa kesi Kuhusu wizi wa mapato ya visa katika kituo cha KIA na baadhi ya watuhumiwa wakiwa ni maafisa Uhamiaji walikwenda mahabusu Kwa kesi ya uhujumu uchumi.

Kesi hii ilifunguliwa baada ya JPM kuelekeza Takukuru Kufanya uchunguzi na baadaye wale waliokamatwa walifunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na vyombo vya habari viliripoti taarifa hii kwenye frontpage zao ikiwemo taarifa ya habari. Waliripoti na majina ya watuhumiwa wote waliorodheshwa. Niombe turudi kwenye technology tuulize google ni rafiki yetu atatusaidia facts za kujadili na kuvikumbusha vyombo vya habari Kuhusu walichowahi kueleza umma.

Mimi nikiwa moja ya Mawakili waliokuwa wanasaidia jopo la utetezi kuandaa baadhi ya hoja nakumbuka watuhumiwa walipohojiwa walikataa tuhuma na walieleza wazi kwamba " Mwaka huo 2019 Uhamiaji ilianza kutoa visa online na hivyo visa nyingi zilitolewa nje ya nchi na siyo mipakani kama ilivyokuwa imezoeleka, lakini mifumo mipya haikuwa na uwezo wakutunza kumbukumbuku za visa zilizotolewa ubalozi" udhaifu wa mifumo ukapelekea wageni waonekane wameingia nchini bila visa. Nakumbuka Moja ya watuhumiwa aliwataka Takukuru kwenda kuhakiki visa hizo kwenye mfumo wa malipo ya Serikali hazina kabla yakuwatuhumu na kuwachafulia CV zao. Baada ya Mtuhumiwa Mmoja kuibua technicality hii ililazimu ukusanyaji ushahidi ufanywe upya na hivyo kupelekea watuhumiwa wale kuwekwa ndani kwa zaidi ya mwaka kila siku DPP akawa anadai upelelezi unaendelea. Upelelezi haikupata ushahidi wowote wa wizi na Hii iliwekwa wazi na Mawakili wa jamhurii ila dana Dana zikawa nyingi. I was expecting peter to narrow down this story to remind law enforcement about misconduct, lakini nayeye kajifanya hii kesi hana taarifa nayo wakati he knows each and everything na Hawa walikuwa wahanga wenzake.

Naomba niwajulishe nini kilitokea; baada ya watuhumiwa wale kukaa ndani kwa zaidi ya mwaka Kwa tuhuma za uhujumu uchumi DPP alifuta kesi Ile baada ya awamu ya Sita kuja madarakani Kwa kukosekana ushahidi na watuhumiwa wote kuelekezwa warejeshwe kazini japo Sina uhakika kama walirejeshwa au Wapo wanasugua benchi.

Taarifa za kukamatwa maafisa waliotuhumiwa huko Kilimanjaro ziliripotiwa Sana kwenye vyombo vya habari na zipo uzuri Ruge alitifundisha texhnologia haidanganyi. Wakili mwenzetu Peter Madeleka alikuwa gereza Moja na wahanga wenzake na walipigania HAKI pamoja japo yeye alikubali kusarender akaenda kwenye prebagaining na wenzake walioteswa bila hatia wakakomaa Hadi mwisho wakigoma kukiri makosa Kwa sababu waliamini kwamba Wapo innocent.

Leo mtu yule yule anayeelewa undani wa kesi nzima iliyowakuta wenzake Kwa uonevu hataki kuweka wazi upande wa pili wa namna vyombo vya dola vilivyotumika kuwaweka watu wasio na hatia zaidi ya mwaka ndani anajadili hii kama hoja mpya na anapotosha umma akitaka umma uhamini kulikuwa na wizi wakati mwendesha mashtaka alisema wazi hakukuwa na ushahidi wa tuhuma hizi.

Lakini anapotosha akiamini wazi kwamba Watanzania awapendi kutafuta taarifa,anapotosha akitambua wazi kwamba waandishi wa habari w Tanzania awana muda wa kufanya kazi za kichunguzi. Endapo yupo kiumbe anapingana na hoja hii aende aulize status ya kesi iliishaje? Kama mahakama iliwaacha hawana hatia Leo tunataka kuibeba hii hoja Kwa uchunguzi na ushahidi Gani? Je, Madeleka anatetea haki au anajitetea mitandaoni? Nimechukizwa Kwa sababu Mimi ni mmoja wa watu walioangaika kwenye kesi hizi leo hii tunaposhindwa kusimamia kupiga vita uonevu tunakosea taaluma zetu.

Nilitegemea Madeleka amwone CAG kama ofisi yenye mapungufu kwa sababu kesi hii imefutwa akiwa uraiani na watuhumiwa baadhi ni watu wa karibu na mke wake na alikuwa nao jela. Au anataka kusema DPP alikosea kuifuta kesi hii? Anataka kutiaminisha CAG Hana taarifa hizi ambazo ziliripotiwa na vyombo vya habari? Je mahakama ilikosea? Mbona hakuna rufaa ya maamuzi haya?

Nilitegemea waandishi wa habari ambao waliiweka front page hii taarifa miaka ya nyuma waje watueleze stori nzima Kwa sababu walikuwa wanaripoti live kutoka mahakamani Moshi na mitandaoni utapata habari zao. Leo hii vyombo vya habari hata kufukua taarifa za nyuma kwao imekuwa kikwazo.

Hakuna sehemu CAG anatuambia Takukuru waliwakamata maafisa Uhamiaji na DPP akawafungulia mashtaka, hakuna sehemu CAG anaeleza kwamba vyombo vya uchunguzi na DPP walifuta kesi baada ya kukosekana ushahidi; hakuna sehemu CAG anaeleza kwamba hakukuwa na wizi Bali kulikuwa na Changamoto ya mifumo ambayo ukiingia hata kwenye google ukauliza lini immigration walianza kutoa visa online you will get it.

Hapa ndipo ninapokubaliana na mtoa hoja Mmoja humu JF kwamba ripoti ya CAG Ina mapungufu. Inataka kuwaaminisha watu Kuna wizi lakini wizi hauonekani, irregularities au kufail kucomply na Sheria kwake yeye tayari ni wizi which is not true.

Mwisho; nalaani kitendo Cha kushikiliwa mwenzetu Peter na niombe endapo wanaomshilia Wana hoja au ana hatia Sheria zifuatwe. Tulimtesa for more than a year Leo lazima tukubali awezi kuwa normal ana machungu; nakubali mapungufu lakini siyo kigezo Cha kumweka ndani ana Uhuru wa kusema. Serikali ilichopaswa kufanya nikutoa tu ufafanuzi wa hoja siyo kutumia nguvu.

Niwaombe moderators mtutaftie magazeti na video zinazohusu sakata la visa KIA mweke hapa mtasaidia Sana kuwafundisha kazi waandishi ambao wameshindwa kugoogle hata walichorupoti Jana. Endapo tutarudi kwenye JF ya zamani ya kuvunja hoja Kwa hoja tutalifanya jukwaa letu kuwa imara na vyombo vya habari vitalazimika kuanza kuifanya kazi Yao.

Tumuulize CAG endapo serikali ilishindwa kutoa ushahidi wa kuthibitisha hata shs mia kwamba iliwekwa mfukoni; yeye huo ushahidi wake kwamba serikali ilipata hasara ameutoa wapi na kwanini vyombo vya uchunguzi havikubaini huo wizi kama yeye anavyosema? Nina hasira Kwa sababu hii ni Moja kesi ambayo unaona wazi Watumishi wa Umma wanavyoweza kubambikiana kesi kijinga huku wenyewe wakikiri kwamba hakuna kesi eti ni maelekezo kutoka angani.

Nimeshare taarifa hizi Kwa sababu tu zipo public lakini hakuna aliyeikumbusha public kureview na kuelewa ukweli. Wanaponda kutafuta ukweli watautafuta.

Huwezi andika yote haya bila interest
 
Katika mawakili ya hovyo, huyu anaongoza, hajawahi kushinda kesi hata moja mahakamani, na wateja wake wengi wanamkimbia wanasema ni kichaa, wakati mwingine huwa anatembea anaongea peke yake.

Wakati mwingine anatembea kifua wazi na bukta mabarabarani
 
Inawezekana anavuta bangi
 
Back
Top Bottom