CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
CAG mstaafu mh Uttoh amesema hakuna shirika la ndege lolote duniani lililowahi kupata faida katika miaka ya mwanzo ya operations zake.

Kuhusu gawio mh Uttoh amesema dividend hutolewa baada ya biashara kupata faida na huamuliwa na bodi kiasi gani cha faida kigawiwe kama dividends.

Uttoh amesema kwa uelewa wake ATCL haijawahi kulipa dividend kwa serikali, na kama kuna fedha ziligawiwa kwa serikali na ATCL hicho ni kitu kingine siyo dividend

CPA Uttoh amesema kimsingi mashirika ya umma hayapaswi kulipa dividend kwa sababu hayafanyi biashara na ametoa mfano UDSM wanalipa dividend serikalini kwa biashara gani wanayofanya?

Chanzo: ITV kipindi cha Kipima Joto
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
 
KAKURUPUKA huyo Mkuu. Hakuwahi kuendesha shirika la ndege popote pale duniani hiyo conclusion yake ni UCHWARA halafu kaminya kuhusu faida itapatikana baada ya muda gani.
Uttoh amesema mashirika ya ndege huwa yanapata faida baada ya miaka mingapi?

Hizo pesa wanazogawiwa serikalini sio dividend zitafutiwe jina lingine, hata Tume ya uchaguzi ilitoa hizo pesa kwa serikali wakati walikuwa wakidaiwa posho na wasimamizi wa uchaguzi.
 
Mzee Uttoh yuko sahihi kabisa, mashirika yote ya ndege huwa hayaleti faida ya moja kwa moja kwa taifa. Biashara ya usafirishaji wa ndege kama yenyewe huwa haiingizi faida, ila faida zake huja kutokana na shughuli mbalimbali za kiuchumi ambazo safari hizo za ndege hufanikisha ndani ya nchi husika.

Mfano mzuri shirika kubwa kama la Fly-Emirates au Air-China hayapati faida za moja kwa moja, lakini shughuli za kiuchumi ambazo haya mashirika yamezifanyikisha ndizo huingiza faida. Fly-Emirates linafanikisha shughuli za kiutalii na biashara ya kimataifa ndani ya ile falme ya Kiarabu.

Faida ambazo zinapatikana kutoka kwenye utalii na biashara ya kimataifa ndiyo hutumika kufidia (Compensate) gharama ya uendeshaji wa shirika la Fly-Emirates. Biashara ya ndege ina gharama kubwa sana kuendesha, na mashirika yanayoingiza faida kama Ethiopian Airlines hayaingizi kutokana na safari za anga pekee, bali kazi nyingine (Kufundisha marubani na wahudumu, pamoja na kufanya marekebisho ya ndege) ambazo shirika hufanya.

Ambacho sisi hatukukubaliana na Raisi Magufuli ni ile tabia ya kusema unanunua ndege kwa pesa taslimu kuinua UTALII nchini, ilhali umeweka sera mbovu ambazo zinawakimbiza watalii: Hata mpango-mkakati wa biashara (Business Plan) hajatupa wananchi. Kila jambo linafanyikia gizani tu....

Lingine ni hili la kununua ndege kwa pesa taslimu bila kuweka wazi mikataba yake linatia ukakasi sana. Halafu shirika bado liko kwenye majaribio ya kufufuliwa na halijasimama vizuri: Tungejaribu kwanza kuchukua ndege chache chini ya Lease (Dry or Wet Leases ) huku tukipima upepo unaendaje.....
 
Dah.....yaani Sh60bn kwa mwaka! Hivi shule moja ya msingi nzuri kabisa inaweza kugharimu kiasi gani kujenga? Hizi 60bn zinaweza kujenga shule ngapi?

Au:
Hizi 60bn zinaweza kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wangapi....kuanza mpaka kumaliza (say kozi za miaka 3)?

JPM bana......mwanzo alianza na gia za kubana matumizi....

Kuna jamaa juzi tunapiga soga akaniuliza: "hivi SMU katika hizi shughuli za mazishi ya JPM mbona walikuwa hawaoneshi nyumba ya JPM?" Sikumjibu.
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
BAK unaniangusha, yaani unaendekeza mambo ya from hands to mouth?

Mishahara itapanda kama tutazalisha kiwango cha juu na hakiji tu bila kutoka jasho...Imagine miradi yote ya kimkakati iishe mishahara si ita triple?

So far hayati alijitahidi sana kwanza kupunguza inflation na deflation kwenye riba, kisha social service kama elimu na afya aliiongezea budget even three times mlitakaje? Aliigawa cake ya taifa kwa wemgi zaidi...Wafanyakazi Tanzania hawafiki hata 11% kisha wanachukua 60% ya budget...Aliilipa mishahara bila kuchelewesha hata sekunde na in a very sustainable way

Tuongeze tija ndiyo mishahara kuongezeka iwe justified, otherwise tunafanya unyonyaji kwenye population ya ambao hawajaajiriwa...Ubinafsi wa hali ya juu!
 
ATCL pengine ilitoa contributions and not dividend to the Govt. Fatilieni msichanganye mambo.
Wewe unaandika "pengine" halafu unawataka watu wengine wafuatilie?

Mbona hata wewe huna uhakika na ulichoandika mpaka umetumia neno "pengine", na kama kufuatilia ni muhimu, ulitakiwa kufuatilia wewe kujua kwa uhakika kilichotolewa kilikuwa ni nini usije hapa kuandika "pengine".
 
BAK unaniangusha, yaani unaendekeza mambo ya from hands to mouth?

Mishahara itapanda kama tutazalisha kiwango cha juu na hakiji tu bila kutoka jasho...Imagine miradi yote ya kimkakati iishe mishahara si ita triple?..
Umeeleweka mkuu ila hawataelewa andiko lako!!
 
Huyo uttoh hapo amesema out of context, amekwepa hoja.

Kuweka kumbukumbu sawa.
-ATCL ilianzishwa mwaka 1977 (Hivyo imekuwa akifanya biashara kwa zaidi ya miaka 40 sasa).

-Ndani ya miaka mitano iliyopita serikali imewekeza zaidi ya Trilioni 2 (zaidi ya bilioni 2000) kwa kununua ndege mpya kwa cash ili kuiwezesha ATCL kutengeneza faida kubwa.

-Mwaka 2018 ATCL ilitangaza kupata faida ya zaidi ya bilioni 28.

-Kila mwaka, tangu mwaka 2018 mpaka 2020 ATCL imekuwa miongoni mwa mashirika ya serikali yaliyotangazwa na waziri wa fedha kuwa yanaipa serikali gawio.

-Mwaka huu CAG imesema kwa mwaka 2019/20 pekee ATCL imepata hasara ya zaidi ya bilioni 60, na kwa miaka mitano mfululizo ATCL imekuwa ikivuna hasara tupu, na hakuna mwelekeo wowote wa ATCL kuja kupata faida ikiwa mwenendo wake wa kisasa kiuendeshaji hautabadilishwa.

Tulitaka Uttoh ajikite kujadili hizo 'facts' kwanza kabla ya kudandia vioja vya kuokoteza kwa mataga.
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
Tatizo la ATCL ni jinsi fedha za wananchi zilivyotumika bila weledi katika uwekezaji wa jinsi ndege zilivyonunuliwa na sequencing ya ununuzi wa ndege hizo!!! Kulikuwa na uharaka gani wa kununua dreamliner wakati safari za local na regional zilikuwa bado kutoshelezwa? Matokeo yake ndege kuota jua kiwanjani na kutengeneza hasara!!!
 
Back
Top Bottom