CAG: Magufuli na Mwakyembe wawajibishwe

CAG: Magufuli na Mwakyembe wawajibishwe

Nina wasiwasi mkubwa sana kama masomaga au hata kuelewa kinachoendelea... magufuli hujibu maswali kishabiki na nyie mashabiki mnayapokea... bila kujiuliza kama ninkweli ssa mnaambiwa kuwa ofc ya CAG imejiridhisha bado mnatetea..??? Kweli???

Hiki kixungumkuti kinahamasishwa na mtindo wa kupenda kusikia taarifa mbaya kwa viongozi.hata zikisahihishwa tunashikilia taarifa hasi
 
Makandarasi wa barabara wanaidai Tanroads zaidi ya 1.2 trillion. Wakati bajeti tarajiwa ya tanroads ni 0.7 trillion. Watanzania walivyo watadanganywa na waziri kuwa barabara zote zitaisha kabla ya JK kutoka madarakani. Jk na waziri wa ujenzi wametengeneza mazingira magumu sana kwa Rais ajae kutekeleza majukumu haswa ya miradi ya maendeleo.
 
WeY97J07RoQ
[video=youtube_share;WeY97J07Ro Q]http://youtu.be/WeY97J07RoQ[/video]
[video=youtube_share;9SOTVAOSyIE]http://youtu.be/9SOTVAOSyIE[/video]​
 
Makandarasi wa barabara wanaidai Tanroads zaidi ya 1.2 trillion. Wakati bajeti tarajiwa ya tanroads ni 0.7 trillion. Watanzania walivyo watadanganywa na waziri kuwa barabara zote zitaisha kabla ya JK kutoka madarakani. Jk na waziri wa ujenzi wametengeneza mazingira magumu sana kwa Rais ajae kutekeleza majukumu haswa ya miradi ya maendeleo.
Kama watu huwa wanamsikiliza magufuli kwa makini utagundua kuwa ni mbabaisha mkubwa! Magufuli kwa kipindi hiki cha Jk hakuna anachofanya zaidi ya kupiga siasa tu kwenye kila jambo. Wabunge wakimbana safari hii amwpatikana sina mashaka na huu wizi maana kwa taarifa za watu waliowahi kufanya kazi chini ya magufuli wanajua rangi halisi ya magufuli. Watanzania kwa kuwa ni malimbukeni hutishwa na mbwembwe tu na kudhani kuwa jamaa ni bonge la mtendaji! Kwa wasiomjua huyu jamaa yeye kila kitu ni siasa na kutaka sifa!

Ngonja tuone mwisho wake, kuna watu walisema mhongo hataachia ngazi lakini kikaango kilipocheka alitepeta ingawa siku ya kujibu hoja alionekana anahoja!
 
Mambo ya Dini yatofautishwe na Serikali.Hawa ndio uzao unaohitaji Mahakama ya Kadhi ianzishwe na Serikali wakati hawaitambui BAKWATA iliyoanzishwa na Serikali.

Chuki tu.. Hapa linazungumzwa suala lingine we unaleta suala lingine! Kama vipi anzisha uzi basi!
 
Nakumbuka mvutanano huu bungeni kati ya Zitto na magufuli. Siku zote naamini ZItto ni mwanasiasa bora zaidi anaesimamia ukweli.
 
kila kunapokucha taifa letu linaendelea kuingia katika giza tororo hasa kutokana na baadhi wa wale walioaminiwa na raisi kuhakikisha kuwa wanaendelea kuziacha wizara zikiwa hoi kutokana na ufisaidi wa kutisha.

Kabla hata swala la escrow halija futika katika mioyo na fikra za watanzania jambo ambalo limepelekea baadhi ya mawaziri kuwajibishwa sasa limeibuka lingine kubwa na la aibu.

Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali amependekeza hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya dkt. John pombe magufuli (waziri wa ujenzi) na dkt. Harrison mwakyembe (aliyekuwa naibu waziri) kutokana na ufisaidi unaofikia kiasi cha shilingi bilioni 256.

Hoja hii ilishawahi kuibuliwa bungeni ila kama kawaida yake magufuli aliizima kiujanja ujanja jambo ambalo sasa limeibuka upya na cag kujiridhisha kuwa majibu waliyoyatoa waziri hayakiwa na usahihi wowote hivyo alilidanganya bunge na fedha hizo hazijulikani zilikopelekwa kwa kuwa hakukuwa na barabara mpya zilizojengwa na kama haitoshi madeni ambayo magufuli alisema yamelipwa hayaendani ama kulingana na kiasi hicho cha zaidi ya bilioni 256.

Akizungumza na gazeti la mwananchi mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya pac mhe. Zitto zuberi kabwe amesema huwa ana mashaka sana na majibu ya magufuli manake kujiamini kwake hupelekea watu wengi kumwani hivyo hata anapofanya mambo ya hovyo watu hucheka na kumpigia magofi.... Hivyo yale majibu aliyoyatoa bungeni kipindi kile hakuyaamini na kuamua kuendelea kulifuatilia jambo ambalo sasa limeibua ukweli kwamba magufuli alilidanganya bunge na hili halivumiliki hata kidogo lazma hawa mabwana sasa wakatujibu bungeni na wajiandae kuwafuata wenzao kwa kuwajibika.

Itakumbukwa kuwa magufuli amekuwa akitunukiwa jina la "the chosen" kwamba ndiye anayetakiwa kumrithi jk baadhi ya watu wakisema kwamba huyu bwana ni msafi kumbe ndo yale yale waliwahi kuyasema wahenga usilolijua ni kama usiku wa kiza........

Kama ilivyokuwa kwa escrow sasa hili nalo watanzania wanalisubiri kwa hamu kubwa.

chanzo: mwananchi

sijawahi kusikia cag mshenzi kama asaadi
cag anatakiwa kuchukua hatua za ukaguzi ndipo aongee na media
cag anatakiwa kucomment baada ya kuchukua hatua na si kuongea na media kama mwanasiasa
code zinapingana.
Jaji anayesimamia kesi fulani hawezi ku pre-just kabla hata hajahukumu
asaad amewekwa ili kulinda mambo fulani

kama mangufuli ni mwizi alipaswa kuwa ameshapeleka timu hapo
bi sawa na polisi kulalamika majambazi badala ya kuwakamata
 
nchi hii ya ajabu sana cag kamtia mtu hatiani nyie mnatetea,mnajua kama ofisi ya cag duniani kote ndio mwokozi wa upotevu wa fedha za umma?afu kumbukeni hapa tunaongelea kodi na mikopo sio pesa zake lazima tuhoji.
Mwaka juzi waziri aliyefanya mapinduzi ya reli nchini china alishtakiwa na kuhukumiwa kunyongwa kwa ufisadi na katika china ndo waziri bora wa uchukuzi kuwahi tokea.acheni upuuzi hawa sio malaika
kwa nini cag hakukagua ripoti ya richmondi na downs ??
 
magufuli kala pesa za fidia za ardhi ya wananzega akawalipa sh. 150 kwa mita skwea moja ya ardhi badala ya sh. 5000!! nilimwandikia barua nikaituma kwa njia ya ems amini usiamini hadi leo hajajibu barua yangu mwaka mmoja sasa.
 
Kama watu huwa wanamsikiliza magufuli kwa makini utagundua kuwa ni mbabaisha mkubwa! Magufuli kwa kipindi hiki cha Jk hakuna anachofanya zaidi ya kupiga siasa tu kwenye kila jambo. Wabunge wakimbana safari hii amwpatikana sina mashaka na huu wizi maana kwa taarifa za watu waliowahi kufanya kazi chini ya magufuli wanajua rangi halisi ya magufuli. Watanzania kwa kuwa ni malimbukeni hutishwa na mbwembwe tu na kudhani kuwa jamaa ni bonge la mtendaji! Kwa wasiomjua huyu jamaa yeye kila kitu ni siasa na kutaka sifa!

Ngonja tuone mwisho wake, kuna watu walisema mhongo hataachia ngazi lakini kikaango kilipocheka alitepeta ingawa siku ya kujibu hoja alionekana anahoja!

[video]http://m.youtube.com/watch?v=9SOTVAOSyIE&feature=youtu.be [/video]​
 
Kama watu huwa wanamsikiliza magufuli kwa makini utagundua kuwa ni mbabaisha mkubwa! Magufuli kwa kipindi hiki cha Jk hakuna anachofanya zaidi ya kupiga siasa tu kwenye kila jambo. Wabunge wakimbana safari hii amwpatikana sina mashaka na huu wizi maana kwa taarifa za watu waliowahi kufanya kazi chini ya magufuli wanajua rangi halisi ya magufuli. Watanzania kwa kuwa ni malimbukeni hutishwa na mbwembwe tu na kudhani kuwa jamaa ni bonge la mtendaji! Kwa wasiomjua huyu jamaa yeye kila kitu ni siasa na kutaka sifa!

Ngonja tuone mwisho wake, kuna watu walisema mhongo hataachia ngazi lakini kikaango kilipocheka alitepeta ingawa siku ya kujibu hoja alionekana anahoja!

[video]http://m.youtube.com/watch?v=9SOTVAOSyIE&feature=youtu.be [/video]​
 
Semeni yote ila kwa Maghufuli wananchi watawapigeni mawe. MAGHUFULI ni lulu. Hayo anayozushiwa ni saw kwa binadamu yeyote kama ilivyo kwa ZITTO na Leka Dutigite.

Huyu nae ni msakatonge tu anakauli kama za chenge mara wananchi wapige mbizi mara malori wayachemshe anatumia nguvu kuliko akili
 
Tatizo la watanzania wengi wanaishi kwa ushabiki na kudanganywa na mbwembwe za kipuuzi... kama atagombea urais ataishia kuambulia kura za vichwa maji, sija wahi kumuelewa huyu jamaa, na kujiona anajua kila kitu kumbe ni kama kima wengine

Huyu mzee ziro tuu anajua kucheza na akili za watanzania vilaza eti akileta zile hesabu za samaki trilion blah blah blah vilaza wana,uona anaakilii
Kumbe bure huyu si aliwaambia wananchi wa kigamboni wapige mbizi
Kisha wenye malori wayachemshe
Hana tofauti ma chenge
Kauli za kijingajinga kwa wananchi wanaolipa kodi na hazikubbaliki mxxxx
 
Nashangaa mijitu mingine inashabikia wizi.nadhani hakuna mkamilifu msimchukulie magufuli kama malaika asiyetenda kosa.Eti asubir data!labda za wizi atazitoa na barabara za kiwango cha chini would be valid.

Buku 7 ndo kaz haswaaaaa wanayofanya
 
Magufuli na lowasa wote wanafanana wakati wanaonekana ni wachapa kazi ni wezi wakubwa katika kundi hilo pia yuko mwakyembe tunahitaji watu waadilifu na wachapakazi hatuhitaji watu wa kutengenezwa na magazeti

Hahahaha jana huyu olesosopai alisema anakerwa na ifisadi khaaaaaaa mamvi akili imechakaa kwakweli mpaka oct ifike patachimbika
 
Huu nao ulevi.. We uliyeandika hii habari nenda katairiwe kwanza.
 
[h=1]Ufisadi wa kutisha waibuliwa[/h]
magufuli_clip.jpg
Waziri wa Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli akikagua ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (BRT) Morocco jijini Dar es Salaam siku za hivi karibuni. Picha na Maktaba
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi



Kwa ufupi
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.


SHARE THIS STORY

0
inShare​




Dar es Salaam. Machungu ya Watanzania yakiwa hayajapoa kutokana na kashfa ya Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya wizara ya ujenzi.
Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya CAG katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.

Kutokana na ufisadi huo, habari zilizolifikia Mwananchi zinasema CAG amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa wizara ya ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi katika bajeti kwa jamii na wahisani.

“Wizara (ya ujenzi) ililidanganya Bunge kuwa kuna ujenzi wa barabara hizo wakati wakijua kwamba walikusudia kulipa madeni ya wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara...mpango mkakati wa wakala wa barabara wa mwaka wa fedha 2011/12 pamoja na manunuzi ulioidhinishwa havikuonyesha utekelezaji wa mradi huo,” chanzo cha habari kilikariri ripoti ya CAG.

Matumizi hayo yasiyo sahihi yaliibuliwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Novemba 22, 2013 baada ya kutilia shaka kiasi hicho cha fedha na ofisi ya CAG kuagizwa kufanya ukaguzi.



Katika kikao hicho ambacho wizara ya ujenzi iliwakilishwa na Katibu Mkuu wake wa wakati huo, Balozi Herbert Mrango alihojiwa na Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe kuhusu hati ya mashaka waliyoipata kutoka kwa CAG mwaka 2011/12.

Kamati hiyo ilieleza kuwa kwenye Bajeti ya mwaka huo Sh348.1 bilioni zilizokuwa zimetengwa chini ya fungu lililokuwa limetajwa kuwa ni la mradi maalumu hazikutumiwa kwa malengo yaliyoelezwa bungeni.

“Ni vizuri leo (ilikuwa Novemba 22 mwaka 2013) uiambie kamati fedha hizi ziliombwa kwa kitu gani na zilitumika kwa jambo gani. Tunajua kwamba fedha hizi zilipunguzwa Sh95 bilioni na kupelekwa Wizara ya Uchukuzi, zilibakia Sh252.975 bilioni katika kifungu hicho lakini kuna bilioni 100 zimetumika visivyo,” alisema Zitto.

Alisema katika majumuisho ya bajeti wizara hiyo, Dk Magufuli na Dk Harrison Makyembe aliyekuwa Naibu waziri wa wakati huo aliyekuwa Waziri wa Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi walitoa maelezo yasiyo ya kweli bungeni kuhusu fedha hizo.

Zitto alikariri maneno yaliyorekodiwa kwenye Hansard ya Bunge yaliyosemwa na viongozi hao watatu.

“Tunaomba fedha Sh252 bilioni kwa ajili ya kuanzia kazi za ujenzi wa barabara.”

“Fedha hizi zitachangia miradi ya wafadhili,” haya yalikuwa maneno ya Dk Makyembe ambaye sasa ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifafanua majumuisho.


“Hizi ni fedha kwa ajili ya Counterpart fund,” alimkariri Lukuvi ambaye sasa ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati akichangia hotuba ya wizara hiyo.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa ripoti ya CAG imeeleza kuwa, “Katika kikao cha kuanza ukaguzi huo Aprili 3, mwaka jana uongozi wa wizara ulithibitisha kwamba hakukuwa na barabara mpya bali walifanya hivyo baada ya kuona madeni yamekuwa makubwa kiasi cha Sh420 bilioni kama yalivyokuwa kwenye hesabu za wakala wa barabara za mwaka wa fedha 2010/11.”

Katika ukaguzi huo imebainishwa kuwa Sh3 bilioni hazikujulikana matumizi yake.

Taarifa zaidi zinasema baada ya wizara kupeleka fedha kwa wakala wa barabara, fedha hizo zilifanyiwa mchakato wa kuzigawa upya lakini nyaraka halisi zilizotumika kugawa fedha hizo hazikuwasilishwa kwa ukaguzi.

“Hata hivyo, kati ya Sh175.3 bilioni zilizopitia kwenye akaunti ya maendeleo ya wakala wa barabara, kiasi cha Sh3,048,365,229 hakikuweza kupatiwa maelezo jinsi kilivyotumika.

“Pia, kati ya malipo ya Sh77.7 bilioni yaliyofanyika kwa wakandarasi au washauri wa barabara moja kwa moja kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Novemba 30, mwaka 2011 kupitia barua ya kumbukumbu namba GA.65/263/01/VOL.XI Gavana Mkuu wa BoT, alikanusha kulipa asilimia 30 ya fedha hizo Sh30.6 bilioni.

“Gavana wa BoT amekanusha kulipa Sh30.6 bilioni kwa kampuni ya M/S Strabag Internationl Gmbn na M/S China-Engineering Corporation Co, kati ya Sh77.7 ambacho kilipelekwa BoT kwa ajili ya malipo kwa wakandarasi au washauri mbalimbali,” alifafanua zaidi mtoa habari hizi na kuongeza:

“Ukaguzi maalumu umeshindwa kuthibitisha malipo yenye jumla ya Sh47.1 bilioni sawa na asilimia 61 kama yalilipwa kwa walengwa waliokusudiwa kwa sababu Gavana wa BoT amesema kuwa kisheria hatakiwi kutoa taarifa za wateja.”

Pia, habari za ndani kutoka ofisi ya CAG zinadai kuwa, Sh13.4 bilioni za ujenzi wa barabara za mikoa zilitumika kulipia barabara binafsi na za halmashauri za wilaya ambazo hutengewa fedha kupitia mfuko wa barabara kinyume na makusudio yaliyopitishwa na Bunge.

“Pia, nimebaini kwamba baadhi ya miradi haikuwamo kwenye kasma zilizopitishwa na Bunge kwenye makisio ya mwaka wa fedha 2010/11 na miradi mingine ilitengewa fedha kidogo lakini wakala wa barabara alitumia fedha nyingi kulipia miradi hiyo bila kuonyesha jinsi alivyozipata,” chanzo cha habari kimekariri ripoti ya CAG.

Katika ukaguzi huo, ufisadi mwingine wa Sh36.6 bilioni ambazo ni malipo ambayo hayakutolewa taarifa kwenye ripoti za washauri au wakandarasi, jambo linaweza kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa wakandarasi kuidai Serikali zaidi ya mara moja na kuitia Serikali hasara.

Mtoa habari wetu alisema kuwa Sh6.2 bilioni zilitumika kuwalipa wakandarasi ambao hawakuonyeshwa katika orodha ya madeni yaliyowasilishwa bungeni pamoja na malipo ya Sh6.6 bilioni yaliyokwishalipwa yaliombewa tena.


“Madeni hayo yalikuwa yamelipwa na wakala wa barabara katika mikoa husika. Hali hii inaashiria kwamba kwa hati ya madai moja kuna uwezekano wa mkandarasi kulipwa mara mbili au zaidi.

Katika mapendekezo ya jumla, chanzo chetu kimesema ofisi ya CAG imeishauri Serikali kusimamisha kuingia mikataba mipya ya ujenzi wa barabara na ilipe madeni ya wakandarasi yaliyopo kwa sasa ili kuepuka ukuaji wa deni hilo kwa siku za baadaye na kuwa mzigo kwa Taifa na wananchi.

“Serikali ihakikishe inaheshimu mikataba iliyowekwa kati yake na wakandarasi ili kuepuka malipo yenye riba na kushtakiwa na wakandarasi kutokana na kuvunja masharti yaliyowekwa kwenye mikataba,” kilifafanua chanzo chetu na kuongeza:

“Zabuni za ujenzi wa barabara mpya ziendane na fedha zilizotengwa katika mwaka wa fedha husika kama itakavyokuwa imeainishwa katika mpango wa manunuzi wa mwaka huo.”

Ukaguzi huo maalumu uliohusisha miradi 46 ya ujenzi wa barabara kuu na barabara za mikoa ambazo wakandarasi na washauri wa ujenzi wa barabara walitoa huduma kwa wakala wa barabara.

“Mbali na miradi hii 46, miradi yote ya wakala wa barabara ilikuwa imezalisha madeni ya jumla ya Sh420 bilioni kama yalivyo kwenye hesabu za wizara kufikia mwaka wa fedha 2010/11,” kilieleza chanzo chetu.

Sakata hili limeibuka wakati lile la uchotwaji wa fedha za Akautni ya Tegeta Escrow halijapoa na hadi sasa limesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la mawaziri kufuatia kumfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka huku Profesa Sospeter Muhongo alitangaza kuachia wadhifa wa Waziri wa Nishati na Madini.

Mbali na hao, pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alitangaza kujiuzuru huku Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi kupisha uchunguzi wa sakata hilo.

Katika mlolongo wa hatua za kinidhamu kuchukuliwa, baadhi ya watumishi wa umma wamefikishwa mahakamani na wengine mbele ya Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 
Back
Top Bottom