CAG: Magufuli na Mwakyembe wawajibishwe

CAG: Magufuli na Mwakyembe wawajibishwe

Kila kunapokucha Taifa letu linaendelea kuingia katika giza tororo hasa kutokana na baadhi wa wale walioaminiwa na Raisi kuhakikisha kuwa wanaendelea kuziacha Wizara zikiwa hoi kutokana na Ufisaidi wa kutisha.

Kabla hata swala la Escrow halija futika katika mioyo na fikra za Watanzania jambo ambalo limepelekea baadhi ya Mawaziri kuwajibishwa sasa limeibuka lingine kubwa na la aibu.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali amependekeza hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya Dkt. John Pombe Magufuli (Waziri wa Ujenzi) na Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyekuwa Naibu Waziri) kutokana na Ufisaidi unaofikia kiasi cha Shilingi Bilioni 256.

Hoja hii ilishawahi kuibuliwa Bungeni ila kama kawaida yake Magufuli aliizima kiujanja ujanja jambo ambalo sasa limeibuka upya na CAG kujiridhisha kuwa majibu waliyoyatoa Waziri hayakiwa na usahihi wowote hivyo alilidanganya Bunge na fedha hizo hazijulikani zilikopelekwa kwa kuwa hakukuwa na barabara mpya zilizojengwa na kama haitoshi madeni ambayo Magufuli alisema yamelipwa hayaendani ama kulingana na kiasi hicho cha zaidi ya Bilioni 256.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Zuberi Kabwe amesema huwa ana mashaka sana na majibu ya Magufuli manake kujiamini kwake hupelekea watu wengi kumwani hivyo hata anapofanya mambo ya hovyo watu hucheka na kumpigia magofi.... Hivyo yale majibu aliyoyatoa Bungeni kipindi kile hakuyaamini na kuamua kuendelea kulifuatilia jambo ambalo sasa limeibua ukweli kwamba Magufuli alilidanganya Bunge na hili halivumiliki hata kidogo lazma hawa mabwana sasa wakatujibu Bungeni na wajiandae kuwafuata wenzao kwa kuwajibika.

Itakumbukwa kuwa Magufuli amekuwa akitunukiwa jina la "The Chosen" kwamba ndiye anayetakiwa kumrithi JK baadhi ya watu wakisema kwamba huyu bwana ni msafi kumbe ndo yale yale waliwahi kuyasema wahenga Usilolijua ni kama usiku wa kiza........

Kama ilivyokuwa kwa Escrow sasa hili nalo Watanzania wanalisubiri kwa hamu kubwa.

Chanzo: Mwananchi


Huyu magufuri anafedha nyingi sana za kifisadi na ili kujua hilo angalia barabara za rami hasa za dar zote zisha bonyea bonyea na viraka sababu ya 10%,ukuweka na huo ufisadi uliogundulika na cag basi awajibike kama wenzake kina tibaijuka hana uzalendo wowote
 
Zitto naye ni mtu wa kujificha kwa wenzie, Ngelejakamtingisha kidogo tu juzi ameibukia kwa Maghufuli? Maghufuli tunaye na tutasonga naye mbele.

Magufuri mwisho wake ndio umefika na tutakuona wewe kama ndiye magufuri umeingia kwa fake id,inakuwaje unatetea wizi wa mali za watanzania?
 
Hivi kazi ya CAG ni kupendekeza hatua za kumchukulia mtumishi anaethibitika au kudhaniwa kuwa kafuja mali ya umma au anaishia kuonyesha ubadhirifu alioufanya na hatua za kuchukuliwa ni jukumu la mwajiri! Tunatia chumvi hata pasipotakiwa chumvi. Wakati mwingine tunatia sukari panapotakiwa chumvi. Kiukweli ndani ya CCM hakuna aliyemsafi. Hii ni kutokana na mfumo wlionao kwani unaheshimu sana wanaopora na kujinufaisha na mali za umma. Bila shaka Magufuli na Mwakyembe bado watabakia kuwa ni walio na nafuu kama tukiwaweka kwenye kipimo cha uchafu.
 
Maghufuli hata kama kweli angwkuwa ameiba tofauti wanavyomsongizia bado kura za watanzania atazizoa endapo ataamua kugombea

Huyu magufuri hawezi hata kufika ktk nafasi ya kugombea urais lazima atawajishwa ktk bunge linalo kuja.Hatutaki viongozi majizi hata kama ni ukoo wa panya
 
Semeni yote ila kwa Maghufuli wananchi watawapigeni mawe. MAGHUFULI ni lulu. Hayo anayozushiwa ni saw kwa binadamu yeyote kama ilivyo kwa ZITTO na Leka Dutigite.

Huna lolote wewe na unaonekana itikadi ndio zinaku endesha zaidi kuliko uhalisia kwa taarifa zako magufuri ana ng'olewa bunge lijalo penda husipende ana ng'oka.
 
Kweli kabisa mkuu. Hata kura yangu ataipata

Magufuri atapata kura yako wewe tu kwani atakuwa asha ng'olewa toka uwaziri na kwa kashfa hii hataweza kugombea cheo chochote ndani ya nchi hii.
 
hatujachelew kumuwajbsha ni muda sahihi kwa mtu sahihi km huyu magufuli unayesem uongo kwakujiamn
 
Nashangaa mijitu mingine inashabikia wizi.nadhani hakuna mkamilifu msimchukulie magufuli kama malaika asiyetenda kosa.Eti asubir data!labda za wizi atazitoa na barabara za kiwango cha chini would be valid.
 
Maghufuli hachafuliki kirahisi hivi, wewe mleta mada , Gazeti la Mwananchi na huyo fisadi kupitia Leka Dutigite jipangeni upya

Hahaaa, mmechelewa sana

Zitto naye ni mtu wa kujificha kwa wenzie, Ngelejakamtingisha kidogo tu juzi ameibukia kwa Maghufuli? Maghufuli tunaye na tutasonga naye mbele.

Wamechokoa mzee wa takwimu watakiona cha moto.

Badala ya kutaka ukweli wa jambo kwanza wewe unatiririka kama Isuzu tipper iliyokosa break mlimani. Huwezi kuja na mautetezi mfululizo kwa jambo ambalo CAG wa serikali hii hii ndio chanzo cha habari yenyewe.
Hata huyo Magufuli akisoma hapa atakuona kuwa wewe ni bogus hata kama unamtetea yeye. Unadhani hata mhalifu anapenda kupata wakili anayebwabwaja tuu bila points? Zisome facts kwanza kisha njoo na data. Kumshambulia Zitto nao ni ujinga maana yeye ni msemaji wa kamati ya Bunge wala hayo sio mawazo yake pekee, na ile kamati tulisha ambiwa inawajumbe 25 na ni 6 tuu ndio hawatoki CCM.
 
Maghufuli hata kama kweli angwkuwa ameiba tofauti wanavyomsongizia bado kura za watanzania atazizoa endapo ataamua kugombea

Sema kura yako wewe na mamburumundu wenzio lakini si zetu tunaojitambua. Looser!!!
 
Nionavyo, Magufuli anafaa kuwa Waziri Mkuu. Uraisi siafiki.
 
Magufuli na lowasa wote wanafanana wakati wanaonekana ni wachapa kazi ni wezi wakubwa katika kundi hilo pia yuko mwakyembe tunahitaji watu waadilifu na wachapakazi hatuhitaji watu wa kutengenezwa na magazeti
 
Back
Top Bottom