Tatizo ya hayo majibu ni kuwa TANROADS walizitumiaje hizo fedha mbali ya kuwa hiyo siyo taarifa ya CAG ila PAC.
Last edited by a moderator:
Tatizo ya hayo majibu ni kuwa TANROADS walizitumiaje hizo fedha mbali ya kuwa hiyo siyo taarifa ya CAG ila PAC.
Huyu C.A.G toka aonyeshe nia ya Kujenga Msikiti Ofisini,nimemdharau sana.
sidhani kama una taarifa sahihi. amekaa pale udsm miaka mingapi? mbona hajajenga msikiti kwenye ofisi yake? tatizo la huyo jamaa kwenu nyinyi ni kuswali kwake tu. hayo mengine mnayatengeneza ili kumpa jina baya.Narudia tena.Mambo ya Dini yasichanganywe na ya Serikali.Kitendo cha kutaka kujenga Msikiti kwenye Eneo la Ofisi ya Serikali ni Udini uliokubuhu.Nimemdharau sana huyu Jamaa.Kama wote wenye mamlaka wakifanya kama yeye mbona hata Parking zitakosekana.Nashukuru Mungu baada ya kutikisa Kibiriti,amekikuta kimejaa akarudi nyuma.
Magufuli na Mwakyembe serious? Nasubiri ushahidi wanasiasa siwaamini hata kidogo huenda kuna maslahi binafsi kwenye hizo tuhuma.
Mkuu Mbona CAG Utoh alishamaliza siku nyingi:
[video]http://m.youtube.com/watch?v=9SOTVAOSyIE&feature=youtu.be[/video]
Mkuu nmemuelewa vizuri sana Mh Utoh kaeleza vizuri na kamaliza na pongezi kwa wizara.. siasa uchwara zinarudisha nyuma hii nchi .. Asante kwa chanzo
Published on Aug 26, 2013
Zitto alipomtuhumu Waziri wa Ujenzi Dr.Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni
Zitto Kabwe alimtuhumu Waziri wa Ujenzi Dr. Magufuli kwa upotevu wa Tsh 252 Bilioni. Baada ya Zito kutaka kutoa hoja ya kutoa shilingi ya mshahara wa Magufuli, Naibu Spika Ndugai akutoa ufafanuzi kuwa Zito ni Mwenyekit wa PAC, swala hili litaongelewa kati mikutano hiyo ya PAC.
Ufafanuzi wa Wizara ya Ujenzi: JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Yah: USAHIHI WA MATUMIZI YA KASMA MAALUM YAUJENZI WA MIRADI YA BARABARA NCHINI SHS. 252,975,000,000.00 Tarehe 22/08/2013, Wizara ya Ujenzi ilikutana na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kwa ajili ya kujadili Hesabu zilizokaguliwa za Fungu 98 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kikao hicho kilifanyikia katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Mhe. Gaudence Cassian Kayombo Mbunge wa Mbinga Mashariki, ambaye alitoa maamuzi na maelekezo rasmi ya Kamati. Katika kikao hicho hoja kadhaa zilijadiliwa ikiwamo hoja kuhusu Matumizi ya Kasma Maalun ya Ujenzi wa Miradi ya Barabara nchini ambayo ilitengewa kiasi cha Shs. 252,975,000,000.00. Katibu Mkuu (Afisa Masuhuli) wa Wizara ya Ujenzi alikiarifu kikao hicho kuwa fedha za Mradi huo Maalum zilitumika kwa ajili ya kulipia madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri kwa miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mipango na bajeti ya Serikali. Katika ujenzi wa barabara; jukumu la msingi kwa Wizara ni kulipa madai ya Makandarasi na Wahandisi Washauri. Aidha, alifafanua kwamba Mradi huu umekuwa na matokeo mazuri kwani ulifanikisha shughuli za ujenzi wa barabara nchini. Afisa masuhuli aliendelea kufafanua kwamba mradi huu wa barabara haukuwa mradi kivuli bali ulikuwa ni mradi maalum kwa lengo la kufanikisha programu ya barabara na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Tarehe 22/08/2013 na tarehe 23/08/2013 zimetolewa taarifa za upotoshaji na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu ukweli wa suala hili ambapo baadhi ya vyombo hivyo vilinukuliwa kusema kuwa kumekuwepo na ufisadi, matumizi tata na ubadhirifu katika mradi huu. Wizara inapenda kuudhibitishia umma kwamba katika utekelezaji wa mradi huu hapakuwepo na ufisadi, ubadhilifu, au matumizi tata. Ukweli huu umethibitishwa kwa maandishi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwamba hoja ya ukaguzi huu haikuhusu ubadhirifu au matumizi mabaya yoyote ya fedha bali ni suala la uandishi wa vitabu vya fedha uliohitaji kuboreshwa. Wizara ya Ujenzi inapenda kutoa ufafanuzi huu na kuudhibitishia tena umma kwamba hakuna upotevu wowote wa fedha kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimetaka ieleweke. Taarifa hii imetolewa na; Balozi Herbert E. Mrango KATIBU MKUU (AFISA MASUHULI) WIZARA YA UJENZI
MY TAKE:
wakuu nilivyoelewa mimi ni kuwa kwa wakati ule CAG akuthibitisha kuwa ulikuwa ni UFISADI moja kwa moja, ila alitoa angalizo kuwa kunauwezekano kuna ufisadi na wizara inatakiwa kuweka mahesabu sawa sawa.
sasa basi kilichoandikwa leo na mwananchi kuna uwezekano mkubwa kuwa baada ya karibu mwaka na miezi kadha akupita bado wizara imeshindwa kuthibitisha/kuweka mahesabu sawa sawa na hapo ndipo tunapopata conclusion kuwa huu ni UFISADI.
Wamechokoa mzee wa takwimu watakiona cha moto.