ACCOUNT FULL
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 1,995
- 389
mkuu Masuke, karbia kila post yko unaongea uhalisia mtupu.Nadir Haroub na Kelvin Yondani wanatakiwa wafanye kazi kubwa sana ya kumlinda Deogratius Munishi, Domayo afanye kazi kubwa sana ya kuziba penetration passes zote, kungekuwa nauwezekano akapata japo nusu ya uwezo wa Gilberto Silva wakati yuko Arsenal itakuwa nzuri sana, kama wataruhusu mashambulizi ya mara kwa mara mabeki wa Yanga huwa wanashindwa kuelewana hasa wale wa kati. Sina wasi wasi sana na mabeki wa pembeni ingawa pia hata mashambulizi ya Ah Ahly mara nyingi huwa wanapenda kutokea pembeni na kumimina krosi kwa hiyo Msuva na Okwi nao inabidi wawe wanafanya jitihada za kurudi kusaidia wakati timu inashambuliwa. Kiiza na Kavumbagu hawatakiwi kufanya makosa ya kosa kosa, nafasi moja goal moja, nafasi ya pili goal la pili.
ni kuomba MUNGU vijana wetu wafanye kweli ili tuweze kuwatoa hao waarabu.
Last edited by a moderator: