C.W.T BUKOMBE ,uchaguzi sio maagizo toka Juu ni mchakato huru,wazi na wa haki.

C.W.T BUKOMBE ,uchaguzi sio maagizo toka Juu ni mchakato huru,wazi na wa haki.

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
175
Reaction score
61
Salaam kwenu wana wa nchi.

Nimepita hapa jimbo la Bukombe na nimekutana na mambo ya ajabu sana.
Moja ya mambo haya ni Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania.

Katika mchakato wa kuwapata viongozi mbalimbali wa chama hiki cha wasomi wa Tanzania na walezi wa watoto wa Watanzania nimeambiwa na kuona mengi.

Baadhi ya mambo hayo ni :

1) Kuna kauli za wagombea kutumwa na viongozi wa juu wa serikali na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa.
Hapa kuna hoja ya huyu ni mteule wa wakubwa,nimepita runzewe na ushirombo na nimeisikia hii kauli.

2) Kuna kauli kuwa viongozi wa kila sekta katika jimbo hili wanawekwa na mtu mmoja tu,ukiwa nje ya mawazo ya huyu mtu basi hakuna utakachokipata hata Kama una mawazo mazuri kiasi gani.
3) Tayari wajumbe/wapiga kura wanapewa kauli juu ya nguvu ya mgombea aliyeagizwa kutoka juu.

4) Walimu ambao ndo stakeholder wa C.W.T wamesema endapo atapita mgombea toka juu ,tutegemee anguko la C.W.T BUKOMBE.

MAONI YANGU.
Ninatambua nguvu ya wanasiasa na vyama vyao,lakini yafaa sana waiache C.W.T ifanye uchaguzi wao bila kuingiliwa na mtu yeyote.

Wenye mahela na madaraka makubwa nawataka mtumie madaraka na pesa zenu vizuri kwa kujenga miundo mbinu kwa ajili ya matumizi ya wananchi wote.
Mfano pelekeni pesa zenu mkaezeke madarasa ,mkajenge nyumba za walimu na kusaidia ujenzi wa vyoo mashuleni.

Walimu wema wa Bukombe,msikubali kuchaguliwa viongozi na mtu mmoja,chagueni viongozi watakao simamia maslahi ya walimu na chama chenu sio atakayehakikisha kura zinapatikana katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Msilete vibaraka wa mtu au wa chama chochote cha siasa,mtapoteza uhalali wa C.W.T.
Walimu mnategemewa na Taifa na mkumbuke ninyi ndio mama wa taaluma zote Duniani.
Haitakiwi kuishi kwa kauli na mawazo ya mtu mmoja.
La mwisho ,Wajumbe toka Runzewe na ushirombo kwa ujumla ,tunahitaji kiongozi wa C.W.T sio kibaraka wa mtu.
Tufanye uchaguzi wa haki,huru na wazi.Pesa tutakula,kura tutapiga kwa mgombea sahihi.
Tunakula runzewe,tunalala Ushirombo.
C.W.T sio tawi la chama chochote cha siasa wala sio chama cha mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom