Bwana harusi aingia Mitini, Ndoa yabuma

Bwana harusi aingia Mitini, Ndoa yabuma

Huo ni unyanyasaji dhidi ya watoto! Kwa nini amdanganye mtoto kuwa anamwoa halafu asitokee? Inatakiwa huyo jamaa atafutwe, akamatwe na afunguliwe mashtaka kwa makosa ya:
1. Kumdanganya mtoto
2. Kumsababishia maumivu ya kisaikolojia mtoto mdogo
3.Kumsababishia maumivu ya kisaikolojia mtoto mdogo kwa kumdanganya kuwa atamwoa
4.Kumsababishia maumivu ya kisaikolojia mtoto mdogo kwa kumdanganya kuwa atamwoa na akashindwa kufanya hivyo
5.Kumsababishia maumivu ya kisaikolojia mtoto mdogo kwa kumdanganya kuwa atamwoa na akashindwa kufanya hivyo huku akijua kuwa anatenda kosa
6. Kuitelekeza ndoa yake tarajiwa!
7.............................................................................................................................

(jamani natania, ila huwa nasikia na kuona makosa yakiunganishwa namna hiyo hiyo hadi yanafika 15 wakati ungedhani ni mawili tu!)
 
Suala la kuolewa na miaka 16 sio la Kiislamu, ni suala la kisheria. Sheria ya ndoa inaruhusu binti wa hadi miaka 14, kwa ruhusa ya Mahakama.

Kama hao wazazi hawakupata kibalo cha mahakama kuruhusu hiyo ndoa, basi bwana harusi amefanya la maana sana. Kaepusha ubawa wake.

Vv
Haya sawa sawa. Yetu ni macho tu hapa. Dada wa watu kaachwa mataa
 
Mtalaamu umeona eeehh

Hakuna kitu kama hicho sheria ya ndoa ya mwaka 71 inaruhusu bint wa miaka 15 kuolewa kwa ruhusa ya wazaz,istoshe miaka 16,hamna kesi hapo,labda kama wazazi hawakuridhia!
 
Huyo bibi hapo pembeni hata haya hana kutaka kumwoza mtoto?????

Na husna kisa cha kukimbilia dushelele ni nini?

Na rahim bahati yako miaka 30 ingekuhusu

Ni Tanzania hii hii ilikuwa na sheria inayoruhusu binti kuolewa akiwa under 16 sijui kama sheria imebadilishwa

Nadhani kosa ingekuwa ni kuoa mwanafunzi lakini kwa age hiyo huo mtego kama ulikuwepo utanasa kitu kingine
 
Jamaa lengo lake la kula mzigo huyo binti limesha timia kaamua kuchapa mwendo.
 
Kwa wataalam wa sheria hebu mtujuze sheria ya ndoa! Binti wa miaka 16 si anaruhusiwa kuolewa kama kwa utashi wake mwenyewe atakubali kufunga ndoa?

Labda kama ni mwanafunzi hapo kuna kuwa na kesi nyingine, ila kama si mwanafunzi nadhani sheria ya ndoa iliyopo sasa inaruhusu kwa huyo binti kuolewa!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1977, hata angekuwa na miaka 14 na ameridhia pamoja na wazazi wake haina shida. Lakini kama kweli ni mwanafunzi kuna sheria nyingine inamzuia kabisa kuolewa.
 
Bwanaharusi aliyetambulika kwa jina moja la RAHIM (miaka 30) ameshindwa kutokea ktk tukio linalomuhusu la kufunga kati yake na BI HUSNA (miaka 16)

Bwanaharusi huyo aliamua kuingia mitini baada ya kuhisi kwamba huenda aliandaliwa mtego wa kukatwa na kufunguliwa kesi ya ubakaji kwa kumuoa binti wa miaka 16 ambapo kwa mujibu wa sheria za Tanzania binti wa miaka 16 anahesabiw kuwa bado ni mtoto asiyeweza kufanya maamuzi makubwa kama hayo.

Hongereni sana watu wa kutetea haki za kinamama na watoto kwa kuandaa mtego huo.


Hebu kafanye utafiti kidogo kuhusu umri halali wa kuolewa hapa tanzania.

Usiandike tu kwa hisia au kwa maoni wanayotoa wanaharakati wanaopigania mabadiliko ya sheria kandamizi.

Kwa taarifa yako, huo umri ni halali kabisa lakini isiwe binti kakatishwa masomo au wazazi hawana taarifa!
 
Mbona anaonekana ana umri sawa na yule miss tz wetu!
 
Sheria ya ndoa haimzui mtoto wa kike mwenye miaka 16 kuolewa waandishi wa habari wa tanzania ni mbumbu na sio wafatiaji,hiyo ni general rule kwamba ili mtoto wa kike aolewa inabidi awe katimiza miaka 18 ambayo ndiyo age of the majority,exptions za hiyo rule ni kua chini ya hyo miaka mtoto anaweza kufunga ndoa kwa makubaliano maalum ya wazazi wa pande zote na mtoto mwenyewe
 
Bado wanaweza kumfungulia kesi ya ubakaji iwapo binti atafanyiwa vipimo na daktari na kukuta ameingiliwa kingono, Rahim anaweza kuwa na kesi ya kujibu.
 
10408810_1517792231794151_2873940184065646692_n.jpg


Mtoto HUSNA (miaka 16) akiwa analia baada ya kidume ,,RAHIM, (miaka 30) kuto onekana siku ya tukio. mama yake akiwa anamfariji.

Vipi wazazi wa huyo binti wamekamatwa?
 
Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 1977, hata angekuwa na miaka 14 na ameridhia pamoja na wazazi wake haina shida. Lakini kama kweli ni mwanafunzi kuna sheria nyingine inamzuia kabisa kuolewa.

Mwanafunzi wa shule ya msingi (pupil) ni haramu kbsa ukibainika unanyeshewa mvua tena ya mawe, kwa mwanafunzi wa sekondari (student) sheria haijamtaja ila naye ni sumu. hapo sasa!!
 
ni uelewa tu, ila sheria ya ndoa inaruhusu kwa binti wa umri huo kuolewa kwa ridhaa na uangalizi wa mlezi au mzazi, pole binti na familia..
 
Kwa nini msisomi hiyo rasimu ya katiba mpya inasemaje suala la ndoo hata leo mnamtia aibu na hasa huku uswahilini kuna vimbea na wa chochezi si wanamzidisha hiyo homa ya penzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom