Bwana Freeman Mbowe, tumia lugha ya staha unapoishauri Serikali ya Rais Magufuli dhidi ya COVID19

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Salaam Wana JF,

Kupitia ukurasa wa twitter Bwana Freeman Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo" CHADEMA" ametumia haki yake ya Kikatiba kushambulia serikali hasa kiongozi wa nchi juu ya hatua zinazochukuliwa dhidi ya Covid19, Ukweli ni kwamba Bwana Mbowe ameshindwa kuonyesha nia ya kushauri na badala yake "ametuhumu na kushambuli rais wa nchi na taasisi zake" huu ni udhaifu kwa Bwana Mbowe, Binafsi namheshimu sana Bwana Mbowe kwa sababu natambua mchango wake wa siasa za upinzani katika kuchochea maendeleo ya nchi na watu wake, Kwa nafasi yake anayo fursa ya kuongea na Rais wa nchi endapo anaona kuna jambo aliendi sawa kwa maslahi ya umma badala ya kutumia mitandao ya kijamii kuwasilisha mambo mazito yanayohusu maisha ya watu.

Aidha Bwana Mbowe, unaposema "Watu wasio na hatia wanakufa, na huu ni uharamia" una maana gani? Kwamba Serikali imeshindwa kuwajali watu wake dhidi ya janga hili la Covid 19, au ni uzembe wa nani huu? Kwa nafasi yako kama kiongozi wa kisiasa ulipaswa kutoa ushauri kwa viongozi waandamizi wa serikali juu ya hatua gani zichukuliwe dhidi ya tatizo hili la Corona ambalo kwa sasa ni Janga la dunia endapo tu umebaini uwepo wa tatizo hili nchini, hata hivyo Tanzania ni taifa linaloingiliana na mataifa mengine inawezekana kwa njia moja au nyingine kuna tatizo, Kwahiyo kutumia lugha za kejeli na vijembe kwa serikali na Rais kamwe si suluhisho la kupambana na Covid19, toeni ushauri utakao saidia kuleta mabadiliko chanya katika jamii yetu na si lawama hasi zenye mchango hasi kwa Watanzania.

Ukweli ni kwamba jambo hili linakuzwa na kuwa agenda pana mitandaoni pasipo na umuhimu mkubwa wa kufanya hivyo, kwa ufupi kuna" upotoshaji uliopitiliza" Rai yangu kwa Bwana Freeman Mbowe ni kujiepusha na mtego wa kuingia kwenye makundi ya wale watu wanaoshinda mtandaoni kuibua na kuzusha mambo mabaya yenye nia ovu dhidi ya serikali na watu wake kwa sababu wewe ni kiongozi mwenye dhamana kubwa katika taifa hili, Bwana Mbowe tunza heshima yako na angalia usije ukaangukia kwenye makundi haya "maovu"

Hata hivyo Kinga ni bora kuliko tiba, Kwa sababu Tanzania sio Kisiwa na tunaambiwa nchi majirani zetu bado Covid 19 inawasumbua sana, ni rai kwa Watanzania wenzangu kuchukua hatua za kutumia miti shamba kama sehemu ya maandalizi ya kinga, hoja ya kusubiri kiongozi mkuu wa nchi atoe kauli ya kutumia dawa dhidi ya corona ndo tuanze kutumia huo ni utumwa wa kifikra ndani ya maisha yetu.

Niwatakieni Jumapili njema.

Deogratias Mutungi
 
Kuua sio lazima kutumia bunduki au sumu. Hata kuacha watu kufa kwa maradhi ambukizi bila kuwapa tahadhari nako ni mauaji. Hayana tofauti na mauaji ya Kimbari.. Mbowe yuko sahihi na lugha aliyo tumia kwa maana viongozi wana fanya mauaji kwa kukusudia
 
tunafundishana na jinsi ya kushauri ?, punde si punde tutashauriana nini tushauri....
Mimi nadhani mngeacha kupiga hizi kelele ili watu wafe na UTAWALA WA magufuli UFELI.
kwani watu wakifa upinzani mnaumia nini?
We jilinde na familia yako
Familia yake io watu? au kifo kinachagua ? Duh mababu zetu waliopigania umoja wangesikia hizi fikra kwamba kuna watu, utawala na wapinzani ambao wapo kwenye mashindano basi huo muda wa kutuunganisha wangeutumia kucheza bao
 
Mbona kama tunakimbilia CHATO !!!??? ... Kabisa ilikua hivyo hapo mwanzo inaonekana hivyo hata sasa ... na itakua hivyo hapo baadae

Amakweli watanzania wasasa sio wajinga tena ... kama na dhambi nizipate ila nafsi yangu inaomba waanze kupukutika huko juu ...

Watakapoanza kuputika wao ndio watachukua hatua zitakazo pelekea na sisi wachini tunusurike otherwise wataendelea kutuhadaa kwa faida zao za kisiasa hali yakuwa sisi wachini ndio tunaumia na familia zetu

Haya twendeni tuombe kwa pamoja ...

... Ewe Mungu Baba tunakuomba uanze kuwapukutisha mmoja baada ya mwingine kuanzia barazani chamwino mpaka pale sebuleni mjengoni ili hatua za makusudi zichukuliwe na sisi wachini tunusurike AMEN!!!
 
Sasa watu wakif si ndo vizuri
Ili UTAWALA wa magufuli UFELI.
2025 tupate points
tunafundishana na jinsi ya kushauri ?, punde si punde tutashauriana nini tushauri....

familia yake io watu? au kifo kinachagua ? Duh mababu zetu waliopigania umoja wangesikia hizi fikra kwamba kuna watu, utawala na wapinzani ambao wapo kwenye mashindano basi huo muda wa kutuunganisha wangeutumia kucheza bao
 
Deo, unataka kutuaminisha kuwa serikali haijafunga milango kuhusu uwepo wa Korona Tanzania! Hakuna mjadala unaoruhusiwa kuhusu Korona, vyanzo vya mjadala vinatakiwa vitoke ngazi ya juu kabisa nchini, rejea kilichotokea Shule ya Kimataifa Moshi. Mhe. Mbowe ameongea baada ya kuona ukweli ambao hauruhusiwi uliotokea kwenye shule hiyo ambayo ilitakiwa ikanushe!
 
Deogratias sijui hata Kama unamfahamu maana ya jina lako.

1. Ugonjwa upo wazi dunia mzima unajua hatua za kuchukua. Sisi tumehimizwa tusizifuate

2. Taarifa sahihi ya usambaaji ikiwa no pamoja na hot spots wananchi wanapaswa kufahamishwa hakifanyiki.

3. Upimaji kwakuwa ni janga ulipaswa kugarimikiwa na serikali isipokuwa wasafiri tu. Badala yake gharama za vipimo ni kubwa watu wengi hawamudu (Tsh 232,000 au Dola 100).

4. Tumekataa kushirikisha na mataifa mengine kwa kutangaza hatuna.

Katika mazingira hayo ukitaka mtu akuambie kwa lugha gani?

Mimi ni Mkristu, pepo huwa halikemewi kipemba lazima utumie lugha ngumu na kukaza sauti kuonyesha authority.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom