Butiku na wenzake ni 'wahaini'

VYAMA vya The Tanzania Democratic Alliance (Tadea) na United Peoples Democratic (UPDP), vimeeleza kushangazwa kwa kutochukuliwa hatua kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Butiku, kwa madai wametenda kosa la jinai na uhaini kwa kumtusi Rais Jakaya Kikwete.

Wakitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Tadea, John Chipaka na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, walisema kuwa viongozi hao wa taasisi hiyo wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri wengine waliohudhuria kongamano la kujadili mustakabali wa nchi katika kumbukumbu ya miaka 10 baada ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere ,waliligeuza kongamano hilo kuwa la kutukana watu, uchochezi na kujitangaza kugombea na kung’ang’ania madaraka.

“…iweje leo viongozi hao wakutane na kuchochea chuki ya waziwazi hadharani ili wananchi waichukie na kuikasirikia serikali pamoja na kiongozi wa nchi, eti hawezi kuongoza kwa vile dhaifu isipokuwa wao tu wanaweza, ni aibu, huu ulikuwa uhaini kamili.

“Viongozi na wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere isipokuwa Butiku, wote ni mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri, wamekosea kuonyesha misimamo yao katika warsha hiyo na kumchafua kwa matusi Rais Kikwete, jambo ambalo si sahihi, tunashangaa kwa nini hawakukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya jinai na uhaini, kesi ambazo huvuta adhabu kali na kubwa,” walisema bila kutaja majina ya viongozi hao.

Wakimchambua Butiku, walidai kiongozi huyo hana uwezo kikazi na alishindwa kutekeleza kazi alizopewa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

Alipokuwa Katibu Myeka wa Mwalimu Nyerere alitingisha Ikulu na alikuwa na mamlaka ya kutoa vibali kwenda vijijini na mitaani akiamuru anachotaka.

Butiku anadaiwa baada ya Mwalimu Nyerere kung’atuka kwenye madaraka, yeye hakuwa tayari kuondoka Ikulu na tamko hilo kuongeza,

“sina hakika kama aliachia nyumba ya serikali na aliendelea kuishi bila kulipa pango na hata alisahau kustaafu kwenye Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)…Maoni ya Butiku ni ya mashaka kwani haamini kama kuna wananchi wengine wanaweza kuwa na uwezo kuliko yeye ndiyo maana analilia madaraka”.

Viongozi hao walisema kuwa Rais Kikwete ni kiongozi bora na muwazi ambaye kwa hulka na tabia yake, hawezi kuharibu sifa yake kwa kuwafuata viongozi hao wanaotaka awarithi tabia zao za ukandamizaji. Rais Kikwete ametajwa kutekeleza ilani ya CCM na kuimarisha uhuru na ujenzi wa demokrasia endelevu.

Walisema wakati wa utawala wa Rais Kikwete wananchi wamepewa uhuru wa kutoa maoni yao na kujinafasi huku mwenyewe akifuatilia maendeleo kwa makini na hakuna vitisho kama ilivyo siku za nyuma.

Bila kutaja majina, walisema kutokana na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuutangazia umma kuwa CCM imepoteza dira ni vema wakaondoka kwenye chama hicho na kujiunga kwenye vyama vingine au kuunda chama chao ambapo wasisitiza :

“Inaonekana viongozi na wadhamini wa taasisi hiyo hawana maono na hawataki kukubali kila zama ina kitabu chake na nchi haiwezi kung’ang’anizwa zama za ujamaa wakati nchi nyingine zinaendeshwa kwa uchumi huria”.

Walisema nia ya kuwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere haikuwa kuunda taasisi ya kugombea na kung’ang’ania madaraka au taasisi korokoroni wa siasa za CCM kama chama cha siasa mbadala, bali iliundwa kufanya utafiti wa mambo mbalimbali kama ya siasa na kuwa kiongozi wa maadili mema ya kisiasa.

Wakati wa kongamano hilo baadhi ya viongozi wastaafu, wakiwemo mawaziri na wakuu wa mikoa na wanasiasa walimnyooshea vidole Rais Kikwete kuwa uongozi wake dhaifu na aachie madaraka.

Hata hivyo Rais Kikwete ambaye wakati tuhuma dhidi yake zinatolewa hakuwepo nchini, aliporejea alisema hashangai kukosolewa na viongozi hao wastaafu, bali angeshangaa kusifiwa nao.

Kauli za viongozi hao dhidi ya Rais Kikwete pia zilipingwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliyesema viongozi hao wakati wa uchaguzi walikuwa katika kundi la mgombea aliyekuwa akichuana na Rais Kikwete na hawajafurahishwa mgombea wao kushindwa hivyo kuendeleza chuki.

Alisema Rais Kikwete anapendwa zaidi na wananchi kuliko hata CCM yenyewe hivyo atasimamishwa tena kugombea urais mwakani.

Butiku alipotafutwa kujibu madai ya viongozi hao wa UPDP na Tadea alijibu kwa njia ya simu, “nikukatishe kauli mwandishi, mimi sitaki kuzungumza kitu maneno yangu yaliisha kwenye kongamano, mengine sitaki,” alisema na kukata simu.

Chanzo: HabariLeo

Duh mpaka uchaguzi mkuu utakapofika mwaka 2010 tutaona mengi,nashindwa kuelewa hawa jamaa nani kawatuma.

Ikifika mahali kujadili mapungufu ya serekali iliyoko madarakani unaitwa mhaini basi inabidi tusifie hata udhaifu uliowazi.

Mkuu kuichambua si kosa ila kuweka matusi ni tatizo hapo.kwa uchambuzi wa Tadea na wengine binafsi nauukubali,kwani kufanya hivyo ni kuatarisha amani ya nchi.kwa viongozi wakuu wastaafu kuikosoa serikali kwa njia kama ile ni hatari sana.wao naamini wananjia nzuri tu ya kupeleka mawazo kwa serikali iliyopo madarakani.

wamekiuka miiko na viapo walivyokula wakati wanahika nyadhifa zao.

Bravo TADEA NA WENZIO
 
Dang,

I can't even tell who is CCM and who is opposition, especially after these CCM stalwarts attacking Kikwete and these fake opposition leaders singing Kikwete's song, reversal of roles.

That wouldn't be much if it didn't carry some undertones of totalitarianism of an Orwellian par. I mean even Kikwete himself has been benevolently (or is it cowardly?) observing freedom of speech.

Unless these are stage puppets running on a string from Kikwete it doesn't even make sense.These are the ghost kind of opposition "leaders" who can't even get 1% out of presidential elections and no parliament seat.Why should we listen to them?
 
VYAMA vya The Tanzania Democratic Alliance (Tadea) na United Peoples Democratic (UPDP), vimeeleza kushangazwa kwa kutochukuliwa hatua kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Butiku, kwa madai wametenda kosa la jinai na uhaini kwa kumtusi Rais Jakaya Kikwete.

Vyama vya TADEA na UPDP ni miongoni mwa vyama vilivyoanzishwa kuganga njaa za waanzishaji. Kwa hiyi haishangazi kwa viongozi wa vyama hivyo vya 'upinzani' kutoa maneno ya uchochezi. Hakuna yeyote katika Kongamano ambaye alimtusi Rais Kikwete popote pale. Aliyewatusi wenziwe ni Makamba aliyediriki kuwaita viongozi na wana CCM wenziwe wehu!

Wakitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Tadea, John Chipaka na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, walisema kuwa viongozi hao wa taasisi hiyo wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri wengine waliohudhuria kongamano la kujadili mustakabali wa nchi katika kumbukumbu ya miaka 10 baada ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere ,waliligeuza kongamano hilo kuwa la kutukana watu, uchochezi na kujitangaza kugombea na kung’ang’ania madaraka.

Huu ni uzushi wa dhahiri. Hakuna mahali popote viongozi walioshiriki kwenye kongamano lile walitoa kauli za aina yoyote iliyoashiria wao kujitangaza kugombea ama kung'ang'ania madaraka! The statement is totally farce utawaitaje viongozi wastaafu na wakati huo huo kudai kwamba wanang'ang'ania madaraka?! Yepi?

“…iweje leo viongozi hao wakutane na kuchochea chuki ya waziwazi hadharani ili wananchi waichukie na kuikasirikia serikali pamoja na kiongozi wa nchi, eti hawezi kuongoza kwa vile dhaifu isipokuwa wao tu wanaweza, ni aibu, huu ulikuwa uhaini kamili.

Chipaka anaishi mitaani na anapanda daladala, anasikia maneno yanayozungumzwa na wananchi juu ya Serikali yao. Malalamiko ya wananchi ya kila siku dhidi ya Serikali hayakutokana na kongamano wala maneno yaliyozungumzwa. Kongamano lilitoa fursa kwa wananchi wa aina mbali mbali kutoa mawazo yao juu ya mustakabali wa nchi yao ambayo wanahaki nayo.

“Viongozi na wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere isipokuwa Butiku, wote ni mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri, wamekosea kuonyesha misimamo yao katika warsha hiyo na kumchafua kwa matusi Rais Kikwete, jambo ambalo si sahihi, tunashangaa kwa nini hawakukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya jinai na uhaini, kesi ambazo huvuta adhabu kali na kubwa,” walisema bila kutaja majina ya viongozi hao.

Wakimchambua Butiku, walidai kiongozi huyo hana uwezo kikazi na alishindwa kutekeleza kazi alizopewa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

Alipokuwa Katibu Myeka wa Mwalimu Nyerere alitingisha Ikulu na alikuwa na mamlaka ya kutoa vibali kwenda vijijini na mitaani akiamuru anachotaka.

Butiku anadaiwa baada ya Mwalimu Nyerere kung’atuka kwenye madaraka, yeye hakuwa tayari kuondoka Ikulu na tamko hilo kuongeza,

“sina hakika kama aliachia nyumba ya serikali na aliendelea kuishi bila kulipa pango na hata alisahau kustaafu kwenye Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)…Maoni ya Butiku ni ya mashaka kwani haamini kama kuna wananchi wengine wanaweza kuwa na uwezo kuliko yeye ndiyo maana analilia madaraka”.

Nikitumia lugha ya Mzee Makamba naweza kusema "ya kale hayanuki!" Vilevile maneno haya ni uzushi usiokuwa na msingi na kumpaka mtu matope kwa shutuma ambazo hazina tija. Maneno ya aina hii hutolewa na watu wanaoitwa wambeya wa mitaani ambao hawana kazi ya maana ya kufanya na kwa zama hizi yanatolewa na wale wanaojidhalilisha kwa kulipwa vijisenti ili wayaseme.

Viongozi hao walisema kuwa Rais Kikwete ni kiongozi bora na muwazi ambaye kwa hulka na tabia yake, hawezi kuharibu sifa yake kwa kuwafuata viongozi hao wanaotaka awarithi tabia zao za ukandamizaji. Rais Kikwete ametajwa kutekeleza ilani ya CCM na kuimarisha uhuru na ujenzi wa demokrasia endelevu.

Walisema wakati wa utawala wa Rais Kikwete wananchi wamepewa uhuru wa kutoa maoni yao na kujinafasi huku mwenyewe akifuatilia maendeleo kwa makini na hakuna vitisho kama ilivyo siku za nyuma.

Mimi nadhani inabidi msajili wa vyama vya siasa afanye kazi ya kuchambua na kuhakiki uhalali wa kuwepo vyama kama TADEA na UPDP kwa sababu havionekani kuwa na faida yoyote katika medani ya siasa. Vyama hivyo ni bora vijiunge na CCM tujue moja kuliko kujidai ni vyama vya upinzani ambavyo vinaipigia debe la wazi Serikali iliyo madarakani bila kujali wananchi/wanachama wao wanasema nini juu ya Serikali yenyewe!

Bila kutaja majina, walisema kutokana na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuutangazia umma kuwa CCM imepoteza dira ni vema wakaondoka kwenye chama hicho na kujiunga kwenye vyama vingine au kuunda chama chao ambapo wasisitiza :

Haya ndiyo maneno pekee yenye maana katika kubwabwaja kote kwa Chipaka na wenziwe. Umefika wakati wa viongozi wa Taasisi na viongozi wengine pamoja na wanachama wa CCM ambao wanaona wazi kwamba Chama chao kimevurugwa na hakiwezi tena kurudia hali yake ya kuwa Chama madhubuti chenye kuheshimika, wajitoe na kuunda Chama kingine kitakachoheshimika. Naamini watakuwepo wananchi watakaojitokeza kukiunga mkono kwa dhati chama hicho.

“Inaonekana viongozi na wadhamini wa taasisi hiyo hawana maono na hawataki kukubali kila zama ina kitabu chake na nchi haiwezi kung’ang’anizwa zama za ujamaa wakati nchi nyingine zinaendeshwa kwa uchumi huria”.

Hivi kweli 'maono' ya Chipaka yanaweza yakashindana na 'maono' ya Salim, Warioba, Sumaye na wasomi wale wote waliochangia mawazo yao kwenye Kongamano hilo?

Walisema nia ya kuwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere haikuwa kuunda taasisi ya kugombea na kung’ang’ania madaraka au taasisi korokoroni wa siasa za CCM kama chama cha siasa mbadala, bali iliundwa kufanya utafiti wa mambo mbalimbali kama ya siasa na kuwa kiongozi wa maadili mema ya kisiasa.

Kama Taasisi iliundwa kufanya utafiti wa mambo mbalimbali kama ya siasa, Kongamano lile la mustakabali wa nchi kisiasa lilikuwa haswa likitekeleza wajibu wake, likimuenzi Mwalimu Nyerere na kazi zake za kisiasa alizozifanya nchini mwetu kwa manufaa vizazi vilivyopita na vijavyo.

Wakati wa kongamano hilo baadhi ya viongozi wastaafu, wakiwemo mawaziri na wakuu wa mikoa na wanasiasa walimnyooshea vidole Rais Kikwete kuwa uongozi wake dhaifu na aachie madaraka.

Kama Chipaka alikuwepo kwenye kongamano awe mkweli kwa sababu walichokifanya viongozi wale wastaafu ni kumlinda na kumsaidia Rais dhidi ya wale wanaomzunguka ambao ndio wanaomhujumu na kuliangamiza taifa letu.

Hata hivyo Rais Kikwete ambaye wakati tuhuma dhidi yake zinatolewa hakuwepo nchini, aliporejea alisema hashangai kukosolewa na viongozi hao wastaafu, bali angeshangaa kusifiwa nao.

Napenda kuamini kwamba Rais alitoa kauli hii haraka haraka (sweeping statement) bila kuwa na taarifa sahihi za yaliyosemwa kwenye kikao hicho.

Kauli za viongozi hao dhidi ya Rais Kikwete pia zilipingwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliyesema viongozi hao wakati wa uchaguzi walikuwa katika kundi la mgombea aliyekuwa akichuana na Rais Kikwete na hawajafurahishwa mgombea wao kushindwa hivyo kuendeleza chuki.

Alisema Rais Kikwete anapendwa zaidi na wananchi kuliko hata CCM yenyewe hivyo atasimamishwa tena kugombea urais mwakani.

Tutegemee nini kutoka kwa Makamba?!

Chanzo: HabariLeo -

Inasikitisha sana kuona gazeti la serikali linavyoweza kutoa Taarifa za upotoshaji wa hali ya juu! Kweli nchi imebadilika.

Duh mpaka uchaguzi mkuu utakapofika mwaka 2010 tutaona mengi,nashindwa kuelewa hawa jamaa nani kawatuma.

Ikifika mahali kujadili mapungufu ya serekali iliyoko madarakani unaitwa mhaini basi inabidi tusifie hata udhaifu uliowazi
.

Njaa zinawasumbua!
 
Hizi njaa zimewafanya baadhi yetu kuvamia siasa bila kuwa na utaratibu.Tunaishia kuwa vituko tu.JK hahitaji watu wa aina hii wamsafishe.Si aende CCM ambako wote hawa wanaosemwa yeye ndio mwenyekiti wa chama chao? Imagine, eti nao ni vyama vya upinzani!!
 
Nafikiri hawa viongozi wa vyama pinzani vya kufikirika wanashindwa kuelewa tofauti kati ya kukosoana kwa minajili ya kuleta maendeleo. Maana kama kuna udhaifu wa kiuongozi kama ilivyo sasa na watu waendelee na wimbo wa kumpamba na kumtukuza mkuu wa nchi itabidi ichunguzwe dhamiri inayowasukuma kufanya hayo. Hawa ni viongozi wa vyama ambavyo kimsingi vishajifia havipo lakini ingelikuwa vizuri na tungewaunga mkono kama wangezijadili hoja zilizotolewa na jukwaa la taasisi ya jkn kwa hoja. Pia kuna hao walioandalia maandamano ya j/mosi kujinadi kama viongozi wa dini. Hawa nao wanafahamika vizuri. Ni waalimu wa ile mihadhara ya usiku inayoanza saa 1 usiku hadi saa sita. Watakuwa hawana jipya ila kujadili watu. Sidhani kama hapa tutapata mjadala wa hoja kupanguliwa kwa hoja.
 
Makuwadi wa siasa kipindi cha mavuno kimeshafika,bado tutasikia wengi watakuja na staili tofauti tofauti.

waliowatuma wakati huu watakuwa wanajilaumu sana,unajua wamekuja na staili ya kitoto kiasi kwamba inakera na kutia kinyaa.
 
Hivi huyu ndiye amerithi chama kilichoanzishwa na Kambona?
Alianzisha yeye hicho chama pamoja na Kambona. Alifungwa miaka mingi na Nyerere kwa uhaini pamoja na akina Otini Kambona na Bibi Titi. Hawa ndio old time wapinzani ambao walipambana na Nyerere toka 60s. Kachoka mzee kwa sasa. Kachoka sana Chipaka. Tumpuuze tu katika haya aliyoyasema maana ni dhahiri ya kutumwa
 
VYAMA vya The Tanzania Democratic Alliance (Tadea) na United Peoples Democratic (UPDP)
Bila kutaja majina, walisema kutokana na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuutangazia umma kuwa CCM imepoteza dira ni vema wakaondoka kwenye chama hicho na kujiunga kwenye vyama vingine au kuunda chama chao ambapo wasisitiza

Kwa hili, sioni kilichobaki kwa hawa viongozi kuvunja vyama vyao na kujiunga na ccm, kwani upande walikosimama sio sahihi. Kwani kina Bujiku hawawezi kutoka ccm na kuingia kwenye vyama vyao kwani wao tayari ni copy ya ccm!
 
Mkuu kuichambua si kosa ila kuweka matusi ni tatizo hapo.kwa uchambuzi wa Tadea na wengine binafsi nauukubali,kwani kufanya hivyo ni kuatarisha amani ya nchi.kwa viongozi wakuu wastaafu kuikosoa serikali kwa njia kama ile ni hatari sana.wao naamini wananjia nzuri tu ya kupeleka mawazo kwa serikali iliyopo madarakani.

wamekiuka miiko na viapo walivyokula wakati wanahika nyadhifa zao.

Bravo TADEA NA WENZIO
Mkuu, viapo vyao vili-expire baada ya kuacha madaraka waliyokuwa nayo. Hivyo wana haki ya kutoa maoni yao kama mtu mwingine yeyote.

Kwa kweli sioni tatizo la mtu kusema mapungufu ya serikali na viongozi wake (kama yapo na anayaona). Haiwezekani kusubiri kusemewa wakati mambo yanaharibika. Vile vile, sidhani kama kilichosemwa na viongozi hao hakijawahi kusemwa na watu wengine katika mijadala ya kawaida. Ni mambo ambayo yamesemwa na wengi sana kabla ya kufika kwenye kongamano hilo. Tofauti iliyopo katika kauli hizo, ni nani aliyesema tu.

Nadhani ni vyema kusubiri kusikia hao wanaoandamana wanataka kutoa ujumbe gani.
 
Mpaka hapo tutakapoondoa woga na kuwa tayari kwa lolote, hakuna jema litakalotokea. Tusitarajie CCM na vibaraka wake wajiondoe na kukaa pembeni bila kulazimishwa kuondoka. Tusitarajie kuwa tutaitoa CCM kwa kutumia 'chaguzi' endapo mfumo uliopo unaipa fursa ya kushinda bila kushindana. Vyama vya upinzani vimejaa ubinafsi na havishughulikii mambo ya msingi zaidi ya kupigania ruzuku. Kuna haja ya kusema imetosha, liwalo na liwe...tuweke uzalendo mbele, masilahi binafsi nyuma...longolongo haitatufikisha popote...kuna haja ya kupambana na ndiyo njia pekee ya kubadili utawala uliopo. Vinginevyo tutulie tuli na waendelee kutunyoa kwa kutumia kipande cha chupa!
 
Du kazi kweli nchi hii ina mijitu ya hovyo hovyo kuliko wanaadamu wote kwenye sayari hii.
 
VYAMA vya The Tanzania Democratic Alliance (Tadea) na United Peoples Democratic (UPDP), vimeeleza kushangazwa kwa kutochukuliwa hatua kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Butiku, kwa madai wametenda kosa la jinai na uhaini kwa kumtusi Rais Jakaya Kikwete.

Wakitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Tadea, John Chipaka na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa,
.

- Well, hoja zijibiwe kwa hoja sio viroja kama hawa wakuu, eti mnawaita ni opposition hawa? No wonder CCM itaendelea kushinda daima, I mean hawa kweli ni wenyeviti wa kuchaguliwa? Yaani na wao kama Kikwete, wameshindwa kujibu hoja za Butiku na Quaresi, badala yake wanajibu yale yale ya chuki na wivu kama Bibi Sophia!

- Unajua kwa mara ya kwanza nimeielewa case ya Chadema kukataa kujiunga na vyama vingine, hivi unawezaje kujiunga na vyama mufilisi namna hii? Hawa nao ni mafisadi hawa, hivi wamewahi kugombea nini katika taifa hili mbona hatujwahi kuwasikia? garademiti!

- Ujumbe wangu kwa Rais na washauri wako, acha kutumia hawa wachovu, nilijua huwezi kujibu kama ulivyoahidi sasa umeamua kutumia zile njia zako kama za kamati ya madini, it won't work, sasa do all of us wananchi a big favor, stand up as man kubali mapungufu yako kiuongozi, and then do something about it, au kama huwezi jiuzulu, waachie wengine, wapo wengi sana wanaoweza na usipoangalia very soon wananchi tutaamua bora shetani Lowassa! Kutumia wachovu katika jamii kujaribu kujisafisha kisiasa ina gharama zake kwa taifa, na moja ambayo ni mbaya kuliko zote ni kuigawa jamii katika makundi yanayopingana bila sababu, umeigawa CCM sasa unataka kuligawa taifa, please onea huruma watoto na wajukuu wetu, maana ukiendelea hivi hakitabaki kitu kwa taifa!

- Wakuu sio siri kwamba sasa huu ndio ule Mtandao, tayari umeanza kazi wanayoijua best ya kuchafua yoyote aliyeko kwenye njia yao, sasa ni vyema wananchi tukawa careful na kutokuangukia kwenye mitego yao, tujitahidi kuwa one step ahead huku tukiwaambia ukweli kwamba kama wameshindwa uongozi waondoke lakini hatuwezi kudanganywa kirahisi hivi, shame on you Kikwete na hizi very cheap politics!

Respect.

FMEs!
 
Na hii hapa je ?
Luku ya Makamba imedondoka
Na Ndimara Tegambwage - Mwanahalisi.

YUSUF Makamba, Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amepoteza "luku." Hajui lini ilidondoka na ilipodondokea. Tunaambiwa anahaha kuitafuta. Potelea mbali!
Sasa kuna wanaosema Yusufu angekuwa na luku yake, ambayo haizibi kauli bali inachuja maudhui kulingana na mtu alipo na wale anaoongea nao, asingesema wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama chake ni “wehu.”
Lakini yamemwagika. Hayazoleki. Ni wale walioongea kwenye Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere ambao Yusufu ameita wehu. Atakayeokota luku ya Yusufu ampelekee haraka.
Kongamano hilo la siku tatu liliandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere inayoongozwa na Mwenyekiti Salim Ahmed Salim na Katibu Mkuu Joseph Butiku katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Ni kwenye kongamano hilo, lililohudhuriwa na watu mashuhuri nchini, baadhi yao walibwaga mitima yao hadharani; bila woga wala aibu. Palipohitaji uchambuzi, lawama, shutuma, malalamiko na hata kejeli, paliguswa vilivyo.
Kongamano lilikuwa shamba la fikra huru na lilitoa mwanya kwa maoni na uchambuzi wa mazingira ya sasa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hakuna aliyenyimwa nafasi kwa misingi yoyote ile. Kama kulikuwa na adui wa mtu, basi alikuwa mmoja: Muda.
Wasomi walichambua. Viongozi wa vyama vya siasa walichangia. Mawaziri walitetea serikali. Wananchi wa kada mbalimbali walisema kilichoko rohoni. Viongozi wa sasa na wa zamani katika CCM na serikali walitoa mawazo na wengine walikandia walichoita “mwenendo” mbaya katika utawala.
Yusufu Makamba hakuwepo. Hakuingia katika darasa la umma. Ameshiba au alikimbia elimu? Ni yeye anayejua sababu iliyomzuia; lakini lazima alikuwa anasikilizia mbali au kupitia vyombo vya habari au “vijana wake” wanusaji.
Ni kutoka huko Yusufu amechomoka na kusema waliomkandia Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakisema hafanyi maamuzi makubwa na kwamba anastahili kuwekwa kando katika uchaguzi ujao, ni wehu.
Kongamano halikuwa la wehu. Halikujadili wehu. Lilisisitiza kuwa taifa linatoswa katika lindi la ufisadi na utovu wa maadili kwa upande wa viongozi. Lilijadili. Lilichambua. Lilikosoa. Lilipendekeza. Lilikanya. Lilijenga muono mpya na mwelekeo. Lilileta mwamko.
Hakukuwa na mwehu aliyealikwa rasmi wala aliyeingia kwa makosa. Kwa Yusufu kuona wehu ndani ya ukumbi wa Karimjee, na waandaaji wasione mwehu na kumsaidia au kumchukulia hatua, bila shaka kunalenga kudhalilisha kazi iliyofanywa.
Wakati wengi wamebaki wakiuliza lini wataitwa tena kwenye mavuno mengine katika shamba la Mwalimu Nyerere Foundation, Yusufu anaona wehu. Anataka kuwaziba midomo. Anataka pia wanaounga mkono yale ambayo walisema, nao waitwe wehu. Wakiogopa kuitwa wehu, basi wanyamaze.
Miongoni mwa wehu au waliokaa na “wehu” katika Karimjee ni Dk. Salim Ahmed Salim, mwana-diplomasia wa kuigwa na Waziri Mkuu wa zamani. Atakayeokota luku ya Yusufu ampelekee haraka.
Wengine ni mawaziri wakuu wa zamani Joseph Warioba na Frederick Sumaye. Tanua orodha. Kulikuwa na Askofu mstaafu Elinezar Sendoro, Profesa Issa Shivji, Profesa Mwesiga Baregu, Balozi Daudi Mwakawago na Askofu Methode Kilaini.
Kulikuwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM; wale waajiri wa Yusufu; wale ambao Yusufu ni karani wao: Harisson Mwakyembe, Kate Kamba, Nape Nnauye na wengine.
Ama wote hawa walikuwa wehu au walifurahia wehu wa wehu ukumbini. Kumbuka jina mojamoja la maaskari hawa: Brigedia Mwita, Brigedia Mbena, Hashim Mbita na Meja Jenerali Rashid Makame. Aliyeokota luku ya Yusufu ampelekee haraka.
Kulikuwa na walimu wa vyuo vikuu na wakuu wa asasi mbalimbali za kijamii, ambao kwa siku tatu, walishiriki kugeuza ukumbi kuwa shamba la fikra na uchambuzi maridhawa. Nisisahau Ibrahim Kaduma alyewahi kuwa makamu mkuu wa vyuo vikuu Dar es Salaam na Mzumbe.
Siyo kweli kwamba Yusufu aliona wehu wawili au watatu. Hapana. Alitaka kudhalilisha kazi ya waliohudhuria wakiwa ni pamoja na viongozi wa vyama vya siasa – James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, John Cheyo wa UDP, wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kiongozi wa UPDP.
Katika ukumbi kulikuwa na katibu mkuu wa zamani wa CCM, Phillip Mangula, wakili na mbunge Stella Manyanya, wakili mashuhuri Tundu Lissu, mabalozi wa Ujerumani, Burundi na Kenya, waziri Stephen Wassira na waziri Hawa Ghasia. Atakayeokota luku ya Yusufu ampelekee haraka.
Katika ukumbi wa Karimjee kulikuwa na wanawake na wanaume. Achana na viongozi. Watu waliojisikia kwenda pale, kusikiliza kwa makini na hatimaye kuchangia kwenye mijadala. Kulikuwa na waandishi wa habari.
Nilivutiwa sana na kuwepo kwa Gulus Abeid. Huyu aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Ngorongoro. Alipomaliza kuongea nilisimama, peke yangu kwa heshima yake. Niliona baadhi ya waalikwa wakinishangaa.
Abeid alisema anaifahamu wilaya ya Ngorongoro na vitongoji vyake. Alisema anaifahamu Loliondo, hasa eneo ambako wafugaji walifukuzwa kwa njia ya kuwachomea makazi yao na kuswaga mifugo yao maporini.
Abeid alisema amesikia majina ya vijiji – Arash, Soitsambu, Ororosokwani na vingine vya Loliondo. Akasema vyote ni vya asili. Vimekuwa na wakazi kwa miaka nendarudi. Akahitimisha kwa kusema anashangaa kusikia serikali inadai kuwa watu anaowahahamu kwa miaka mingi ni wahamiaji kutoka Kenya.
Kilichonifurahisha ni kukuta Abeid ni shahidi wangu. Alisema kile nilichoandika nilipokwenda Loliondo na serikali ikakana. Na Abeid siyo mwehu. Atakayeokota luku ya Yusufu ampelekee haraka.
Kwenye lango la ukumbi kulikuwa na wauza vitabu. Vingi vilikuwa juu ya Nyerere – hotuba zake na maandishi yake mwenyewe; uchambuzi wa Nyerere mtu na Nyerere kiongozi. Wote hawa walinufaika na shamba la Mwalimu Nyerere Foundation. Hawakuwa wehu.
Tunaleta ushahidi. Soma maazimio ya Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ukurasa 7. Lakini atakayeokota luku ya Yusufu ampelekee mara moja.
Kwamba Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation liligeuzwa jukwaa la wehu na wahaini - duh, kaazi kweli kweli !
 
Na hii hapa je ?
Kwamba Kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere Foundation liligeuzwa jukwaa la wehu na wahaini - duh, kaazi kweli kweli !

Hii ni satire.. sijui umeelewa hilo ? Ukisoma vyema utaona wamemtukana sana Makamba na mtandao wa Kikwete wanaodai eti ukosoaji ni uhaini! Na wajue 2010.. bado mapema... watasikia mengi... watanzania si mabwege tena.....
 
Nilielewa sana ila na mimi nilikuwa nazidi kupigilia msumari wa mwisho kwani Makamba ni karani mkuu na mpishi mkuu wa JK na CCM. Swali ni je, chakula anachowapikia Makamba wanakifurahia ? Vinjonjo wanavyoongezea akina Chipaka wa Tadea na Dovutwa wa UPDP wanavi enjoy ? Na vibwagizo vinavyotolewa na akina Chifu Msopa, Shehe Mwaipopo, Mch. Bulegi na kubarikiwa na Kamanda Kenyela wa jeshi la polisi vinamezeka ? Surely the country has gone to the dogs and they are fighting for the pieces of her poor torn body. Only a revolution can save us now - nothing less, nothing more.
 
Huyu mwandishi nae unaweza sema chizi mwingine tu. Anasema kikwete anataka ku promote demokrsia; alafu hapo hapo anasema wanaotoa maoni yao ni wahaini wanao staili kusfunguliwa mashtaka.

Where does freedom of speech falls into au demokrasia kwetu ina maana nyingine; maana ana sound as if hawa jamaa wame commit high treason ukati Kikwete and co ndio wanaweza hukumiwa kwa kesi hii.

Kama jamaa ni weak ni weak tu its obvious; wanasema litakua gwaride bovu iwapo kiongozi anakosea routine zake. Iwapo gwaride huushuudiwa na mamia anachosema mhudhuria mmoja ujue kimeshudiwa na wengi anawakilisha tu/

If he has to be taken serious he has to be serious mfano kwanini Tz maskini sijui; ukati leo hii tunasoma BoT inatoa mikopo kwa wakazi wake ili wajenge nyumba aihitaji muelevu kuelewa asilimia kubwa ya hawa watu wananyumba tayari. What does he do the next day anawaalika Mamiss sijui nini IKULU

Huu ujinga kiasi MKANDARA asuse
 
Inaonekana na ni wazi kwamba mtoa mada ya uhaini ni kati ya wale Asilimia 70 wanaofuata upepo maana ukisoma kwa makini hata uhaini waliofanya akina Butiku hauelezeki au hajaelezwa...

Ni kweli kwamba asilimia 30 ya misaada yote hutafunwa na wajanja mkulu amesema hayo na akiambiwa achukue maazmuzi magumu anasuasua... sasa uhaini uko wapi...

Ukweli siku zote unauma full stop
 
- Well, hoja zijibiwe kwa hoja sio viroja kama hawa wakuu, eti mnawaita ni opposition hawa? No wonder CCM itaendelea kushinda daima, I mean hawa kweli ni wenyeviti wa kuchaguliwa? Yaani na wao kama Kikwete, wameshindwa kujibu hoja za Butiku na Quaresi, badala yake wanajibu yale yale ya chuki na wivu kama Bibi Sophia!

- Unajua kwa mara ya kwanza nimeielewa case ya Chadema kukataa kujiunga na vyama vingine, hivi unawezaje kujiunga na vyama mufilisi namna hii? Hawa nao ni mafisadi hawa, hivi wamewahi kugombea nini katika taifa hili mbona hatujwahi kuwasikia? garademiti!

- Ujumbe wangu kwa Rais na washauri wako, acha kutumia hawa wachovu, nilijua huwezi kujibu kama ulivyoahidi sasa umeamua kutumia zile njia zako kama za kamati ya madini, it won't work, sasa do all of us wananchi a big favor, stand up as man kubali mapungufu yako kiuongozi, and then do something about it, au kama huwezi jiuzulu, waachie wengine, wapo wengi sana wanaoweza na usipoangalia very soon wananchi tutaamua bora shetani Lowassa! Kutumia wachovu katika jamii kujaribu kujisafisha kisiasa ina gharama zake kwa taifa, na moja ambayo ni mbaya kuliko zote ni kuigawa jamii katika makundi yanayopingana bila sababu, umeigawa CCM sasa unataka kuligawa taifa, please onea huruma watoto na wajukuu wetu, maana ukiendelea hivi hakitabaki kitu kwa taifa!

- Wakuu sio siri kwamba sasa huu ndio ule Mtandao, tayari umeanza kazi wanayoijua best ya kuchafua yoyote aliyeko kwenye njia yao, sasa ni vyema wananchi tukawa careful na kutokuangukia kwenye mitego yao, tujitahidi kuwa one step ahead huku tukiwaambia ukweli kwamba kama wameshindwa uongozi waondoke lakini hatuwezi kudanganywa kirahisi hivi, shame on you Kikwete na hizi very cheap politics!

Respect.

FMEs!

Heshima kwako FMEsm

Nimependa andiko lako kwa kweli Muungwana kashikwa pabaya mbaya zaidi bado anafikiria Watanzanda ni mabwege.Kwa mara ya kwanza nadhani Muungwana anamuhitaji Ngoyai amsaidie kuweka mambo sawa,Ngoyai angekuwepo asingekubali hizi cheap propaganda kuwatumia kina Chipaka na maandamano ya waislam jumamosi ni makosa ya kuwa na timu ya watu wa hovyo
 
Back
Top Bottom