Butiku na wenzake ni 'wahaini' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Butiku na wenzake ni 'wahaini'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Dec 17, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  VYAMA vya The Tanzania Democratic Alliance (Tadea) na United Peoples Democratic (UPDP), vimeeleza kushangazwa kwa kutochukuliwa hatua kwa viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wake, Joseph Butiku, kwa madai wametenda kosa la jinai na uhaini kwa kumtusi Rais Jakaya Kikwete.

  Wakitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa Tadea, John Chipaka na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, walisema kuwa viongozi hao wa taasisi hiyo wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri wengine waliohudhuria kongamano la kujadili mustakabali wa nchi katika kumbukumbu ya miaka 10 baada ya kifo cha Mwalimu Julius Nyerere ,waliligeuza kongamano hilo kuwa la kutukana watu, uchochezi na kujitangaza kugombea na kung’ang’ania madaraka.

  “…iweje leo viongozi hao wakutane na kuchochea chuki ya waziwazi hadharani ili wananchi waichukie na kuikasirikia serikali pamoja na kiongozi wa nchi, eti hawezi kuongoza kwa vile dhaifu isipokuwa wao tu wanaweza, ni aibu, huu ulikuwa uhaini kamili.

  “Viongozi na wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere isipokuwa Butiku, wote ni mawaziri wakuu wastaafu na mawaziri, wamekosea kuonyesha misimamo yao katika warsha hiyo na kumchafua kwa matusi Rais Kikwete, jambo ambalo si sahihi, tunashangaa kwa nini hawakukamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya jinai na uhaini, kesi ambazo huvuta adhabu kali na kubwa,” walisema bila kutaja majina ya viongozi hao.

  Wakimchambua Butiku, walidai kiongozi huyo hana uwezo kikazi na alishindwa kutekeleza kazi alizopewa wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

  Alipokuwa Katibu Myeka wa Mwalimu Nyerere alitingisha Ikulu na alikuwa na mamlaka ya kutoa vibali kwenda vijijini na mitaani akiamuru anachotaka.

  Butiku anadaiwa baada ya Mwalimu Nyerere kung’atuka kwenye madaraka, yeye hakuwa tayari kuondoka Ikulu na tamko hilo kuongeza,

  “sina hakika kama aliachia nyumba ya serikali na aliendelea kuishi bila kulipa pango na hata alisahau kustaafu kwenye Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)…Maoni ya Butiku ni ya mashaka kwani haamini kama kuna wananchi wengine wanaweza kuwa na uwezo kuliko yeye ndiyo maana analilia madaraka”.

  Viongozi hao walisema kuwa Rais Kikwete ni kiongozi bora na muwazi ambaye kwa hulka na tabia yake, hawezi kuharibu sifa yake kwa kuwafuata viongozi hao wanaotaka awarithi tabia zao za ukandamizaji. Rais Kikwete ametajwa kutekeleza ilani ya CCM na kuimarisha uhuru na ujenzi wa demokrasia endelevu.

  Walisema wakati wa utawala wa Rais Kikwete wananchi wamepewa uhuru wa kutoa maoni yao na kujinafasi huku mwenyewe akifuatilia maendeleo kwa makini na hakuna vitisho kama ilivyo siku za nyuma.

  Bila kutaja majina, walisema kutokana na viongozi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere kuutangazia umma kuwa CCM imepoteza dira ni vema wakaondoka kwenye chama hicho na kujiunga kwenye vyama vingine au kuunda chama chao ambapo wasisitiza :

  “Inaonekana viongozi na wadhamini wa taasisi hiyo hawana maono na hawataki kukubali kila zama ina kitabu chake na nchi haiwezi kung’ang’anizwa zama za ujamaa wakati nchi nyingine zinaendeshwa kwa uchumi huria”.

  Walisema nia ya kuwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere haikuwa kuunda taasisi ya kugombea na kung’ang’ania madaraka au taasisi korokoroni wa siasa za CCM kama chama cha siasa mbadala, bali iliundwa kufanya utafiti wa mambo mbalimbali kama ya siasa na kuwa kiongozi wa maadili mema ya kisiasa.

  Wakati wa kongamano hilo baadhi ya viongozi wastaafu, wakiwemo mawaziri na wakuu wa mikoa na wanasiasa walimnyooshea vidole Rais Kikwete kuwa uongozi wake dhaifu na aachie madaraka.

  Hata hivyo Rais Kikwete ambaye wakati tuhuma dhidi yake zinatolewa hakuwepo nchini, aliporejea alisema hashangai kukosolewa na viongozi hao wastaafu, bali angeshangaa kusifiwa nao.

  Kauli za viongozi hao dhidi ya Rais Kikwete pia zilipingwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliyesema viongozi hao wakati wa uchaguzi walikuwa katika kundi la mgombea aliyekuwa akichuana na Rais Kikwete na hawajafurahishwa mgombea wao kushindwa hivyo kuendeleza chuki.

  Alisema Rais Kikwete anapendwa zaidi na wananchi kuliko hata CCM yenyewe hivyo atasimamishwa tena kugombea urais mwakani.

  Butiku alipotafutwa kujibu madai ya viongozi hao wa UPDP na Tadea alijibu kwa njia ya simu, “nikukatishe kauli mwandishi, mimi sitaki kuzungumza kitu maneno yangu yaliisha kwenye kongamano, mengine sitaki,” alisema na kukata simu.


  Chanzo:
  HabariLeo

  Duh mpaka uchaguzi mkuu utakapofika mwaka 2010 tutaona mengi,nashindwa kuelewa hawa jamaa nani kawatuma.

  Ikifika mahali kujadili mapungufu ya serekali iliyoko madarakani unaitwa mhaini basi inabidi tusifie hata udhaifu uliowazi.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Watoto wengine wana tabia mbaya. Akiona hakuna mtu anayemsikiliza, anajiangusha chini na kupasua kilio cha nguvu. Kazi ipo kadri tunavyokaribia 2010!!
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna mtu anaweza kunisaidia kupata defition ya uhaini? Mimi ninachoelewa uhaini ni kitendo cha kutaka kuiondoa serikali halali, madarakani kwa nguvu au njia ambazo hazifuati misingi ya demokrasia. Au naelewa vibaya?
   
 4. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chipaka 'anajibu mapigo' ama 'analipiza kisasi' kwa sababu enzi za Mwalimu aliwahi kuwekwa ndani kwa uhaini.
   
 5. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hiyo ndiyo maana hasa ya uhaini. Hawa wanasiasa wa opposition wamekurupuka tu, na bila shaka wametumwa kwani nasikia kuna mtandao ulioandaliwa kumsafisha JK baada ya kumwagiwa tuhuma nzito kwenye kongamano la Mwalimu Nyerere.
   
 6. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Kwa hivyo hivyo navyo ni vyama vya upinzani? na vinajua nini maana ya uhuru wa kutoa maoni, ni vinajua nini maana ya tusi na vinajua madhumuni ya makongamano ya kisiasa. Kazi ipo.

  Eti kusema CCM imekosa dira ni uhaini (na hawa ni wapinzani!), kusema Kikwete ni dhaifu asipewe kipindi kingine cha Urais ni uhaini :( :( :confused:
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Mzee Punch,

  Ni kweli hata mimi nimesikia kuna mpango kabambe wa kumsafisha Muungwana kabla ya uchaguzi mkuu mwakani tutasikia vimbwanga na vibweka kibao yetu macho.

  Ukichunguza sana utagundua kitu kimoja watu au taasisi zinazojichomoza kumtetea Muungwana mara nyingi hawapendi kujibu hoja bali wanakimbilia kujadili watu na masula binafsi.Hoja zote zilizojadiliwa katika kongamano la Mwl Nyerere ni za kweli kuzijibu ni vigumu ndio maana Muungwana mpaka leo hajasema kitu anajaribu kuwatumia wanasiasa na taasisi za hovyo kuwaondoa watanzania katika masuala ya msingi.
   
 8. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #8
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Niliweka bandiko langu asubuhi hapa kutaka kupata maoni ya wanajf kuhusu hili sakata la akina Butiku na Qaresi.Sijui modes waliona linaziba nafasi au vipi wakaamua kuliondoa baada ya muda mfupi, lakini nilisema kuwa hata ndani ya nyumba ya mtu binafsi na famila yake, kama maisha yako unayaendesha upendavyo wewe bila hata kutaka mkeo, watoto au ndugu kukuuuliza na kukushauri hutafika mbali. Butiku na wenzake walichokifanya kwa maoni yangu ni sahihi kabisa. Tatizo watanzania tuna tabia ya unafiki huku tunagugumia kwa maumivu. Suala liko wazi mambo yanakwenda ndivyo sivyo watu wakisema eti washitakiwe kwa uhaini, hivi tutaendelea kuwa mazoba mpaka lini? Nchi inatafunwa tu watz tunaangalia. Kwa kweli huyo atakayejaribu kufunua mashtaka ya uhaini hao akina Butiku nitakuwa na mashaka na bongo yake.

  Hivi watu hawaoni nini kinchotokea humu nchini. Hizi story za ufisadi kila kukicha wanadhani ni nyimbo za kufurahisha tu? Hata kama wao akina Butiku na mawaziri wastaafu walikosea katika nyakati zao, ina maana wakiona mambo yanaharibika sasa wasiseme? Kwa huu uozo ulipo sasa nadhani umekithiri kuliko nyakati nyingine zozote!!

  Mzee mwanakijiji ana bandiko lake kuwa " we are screwed" kwa hali hii tutaendelea tu kuwa screwed mpaka siku tutakayotia akili.
   
 9. b

  bigilankana Senior Member

  #9
  Dec 17, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hawa kina chipaka wapuuzwe tu maana ni dhahiri wametumwa. nchi haina uhuru wa watu kutoa maoni yao, tena watu wenyewe wametumikia taifa kwa uda mrefu. Kichekesho kweli eti Butiku na wenzake mahaini. wajinga hawa na vyama vyao vya mifukoni
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Na tusikie hoja kinzani kwa maendeleo yetu


  BARAZA ka Habari la Kiislamu Tanzania (BAHAKITA) kwa kushirikiana na baadhi ya wachungaji wa madhehebu ya kikristo wameandaa Jumamosi ya wiki hii maandamano ya amani kulaani "wanaobeza utendaji wa Rais Jakaya Kikwete."

  Mbali ya kuwalaani wale wanaoamini kwamba wanabeza utendaji kazi wa Rais Kikwete, maandamano hayo yatakayoanzia kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja na kuishia viwanja vya Kidongo Chekundu, Dar es Salaam, imeelezwa yanalenga pia kumuunga mkono Rais Kikwete na Serikali yake kwa juhudi za kuliletea Taifa maendeleo na kupambana na ufisadi nchini.

  Tumefurahi kwamba Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeruhusu maandamano hayo kufanyika. Tunalipongeza Jeshi la Polisi kwa hilo kwani walioandaa maandamano hayo wana haki ya kufanya hivyo.

  Hiyo ndiyo demokrasia tunayoitaka ya watu kuwa huru kutoa mafundo ya kooni hasa baada waandalizi wa maandamano hayo kusema wazi kwamba wamelazimika kuandaa maandamano hayo baada ya ‘baadhi ya viongozi wastaafu serikalini kumshambulia Rais Kikwete na Serikali yake' kupitia kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 2 mwaka huu.

  Wakati nasi tunaungana na Polisi Dar es Salaam kuwapa fursa ya kuandamana, tungependa kutoa angalizo letu kwa waandamanaji hao kwamba wana haki ya kutafsiri namna wanavyojua yaliyojadiliwa katika kongamano hilo lakini katika maandamano yao ni vyema wakajikita kwenye hoja na si kuwajadili watu. Hivyo ndivyo ilivyokuwa katika kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

  Kama walivyo wao, washiriki wa Kongamano la Mwalimu Nyerere walikuwa na haki ya kuzungumza na kila mmoja alisema lililokuwa likimkereketa na kubwa lililojitokeza katika kongamano hilo ni ukweli ambao haupingiki kwamba mambo hayako sawa katika uongozi wa Taifa letu.

  Nani anayepinga kwamba Taifa limepungukiwa kwa kiasi kikubwa na maadili upande wa uongozi? Na kama walivyobaini katika kongamano hilo, mmononyoko huo wa maadili unadhihirishwa na ongezeko kubwa la rushwa, ufisadi, uvunjaji wa haki za binadamu, tabia na hulka za viongozi kushindana kwa kujilimbikizia mali kutumia mgongo wa umma, kutoheshimiana na kujengeka kwa mitandao mbalimbali isiyo rasmi yenye sura ya vyama vya siasa.

  Je, si kweli pia kwamba upungufu huo unatishia amani, utulivu, maendeleo na ustawi wa muda mrefu wa Taifa letu? Ni kutokana na kasoro hizo ndiyo maana Kongamano la Taasisi ya Mwalimu Nyerere lilipendekeza kuchukuliwa kwa maamuzi magumu na hatua za haraka zichukuliwe kwa ujasiri kwa lengo la kurejesha maadili aliyotuachia Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

  Kongamano halikuzungumzia matatizo ya uongozi tu, bali hata ustawi wa Taifa letu kwa ujumla kwamba kunahitajika kufanyika marekebisho kadhaa katika sekta ya madini na ardhi kwa faida ya vizazi vijavyo.

  Kongamano liliitahadharisha Serikali kwamba si busara kuchimba madini yote kwa wakati huu bila kuzingatia mahitaji ya vizazi vijavyo kwani wananchi na Serikali watambue kizazi hiki cha sasa ni wadhamini tu wa rasilimali na ardhi.

  Tunawatakia maandamano ya amani na ya heri Jumamosi tukisubiri kusikia hoja mpya kinzani ambazo wao wanadhani zitasaidia kusukuma mbele maendeleo ya taifa letu na wananchi wake kwa ujumla, si majina ya watu. Kwani hawa wapo leo, tunaweza kuamka kesho tusiwakute, lakini hoja kama ni hoja ni za kudumu.  Source: Raiamwema.


  MzeePunch bila shaka ule mtandao wa kumsafisha Muungwana umeshaanza kufanyakazi.Nitapenda kusikia tamko rasmi la hayo maandamano ya amani.Mlioko Dar mtuwakilishe.
   
 11. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  ntoke vipi tu hizo za kuelekea 2010,ila wameaza na mguu mbaya
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ngongo...Mi nakwambia ndugu yangu watu wetu sijui wana ugonjwa gani? eni wei, ngoja tuone hayo maandamano yao, lakini nadhani hawajui walifanyalo katika ardhi hii ya Tz inayomeng'enyuliwa na mafisadi kila kukicha...Eh Mungu tusaidie ubadirishe bongo za watu wetu tupate fikra mpya za kuondokana na hili jinamizi la watu kufata mkumbo hata kwenye mambo yasiyo na maslahi si kwao tu bali na taifa zaima. Amen!
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Dec 17, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kuna vyama viliwahi kuitwa CCM B, sishangai sana.
   
 14. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #14
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,836
  Likes Received: 1,090
  Trophy Points: 280
  Kuna haja na sisi wa upande mwingine kuanzisha maandamano ya kutoridhishwa na utendaji wa JK. Wanapaswa waanze kuona joto la jiwe hawa. Tatizo ni nani wa kutuongoza, wenzetu Zimbabwe wanae Morgan Tsvangirai, Kenya Odinga, SA walikuwa nao akina Steve Biko, Mzee Mbeki na Mandela. Sisi masikini hatuna mtu.
   
 15. e

  echonza Senior Member

  #15
  Dec 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na Laligeni kabisa kuhusiana na tabia yetu watanzania, tuko wanafiki sana. Hebu tujaribu kupiga hatua hata tatu tu mbele kujaribu kuuvua unafiki wetu katika maisha yetu. Halafu tutaona matokeo mazuri yatakavyokuja, na tena tutajiuliza maswali sana, kwamba mbona tulichelewa kuuvua unafiki?
   
 16. O

  Omumura JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watakaoandamana wote siku hiyo wasife kabla ya kuonja maumivu ya ufisadi wa nchi hii!
   
 17. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #17
  Dec 17, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,637
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 160
  JK haitaji kusafishwa na mtu/watu /asasi au chama chochote, kwani yu msafi tokea asubuhi...
   
 18. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #18
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  ama kweli watu wanajua kujipendekeza, tangu wamesikia Juma Duni Haji na mwenzake wamezawadiwa Uwakilishi basi na wao wanakuja na mpya eti Uhaini kukosoa Serikali, wanatamani kukumbukwa kwa vyeo, jamani amakweli hadi uchaguzi mkuu 2010 tutaona mambo mengi, ila huu ni mkakati wakusafishana kwa ahadi za kijingakijinga.
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,886
  Trophy Points: 280
  Yu msafi tokea asubuhi? Kama kachafuka mchana asisafishwe jioni? mkuu Kibunango waulize hao wanaochemka kumsafisha watamuweza kweli?
   
 20. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Tabia ya baadhi ya Watanzania kujikombakomba kwa viongozi imeota mizizi sana. Wanaotumia lugha kama hiyo wanataka waonekane wao ndio tu wenye haki ya kutoa maoni. Kwa nini hata hoja ya jumla ikitolewa hao wanaojikomba wanasema 'wakosoaji wamemtukana Rais Kikwete?'

  Nadhani hata Kikwete mwenyewe anawapuuza wanapojikomba kwake na wakiona hasemi kitu wanadhani anapendezwa na kujikomba kwao. What a shame!

  Wakosoaji wanaeleza matatizo yaliyopo Tanzania na ni haki yao kufanya hivyo. Wao (hao wanaojikomba) kama wangependa wangeleta mazuri ambayo Serikali inawafanyia Watanzania ili wasomaji waone pande zote mbili - hasi na chanya.

  Sasa badala ya kufanya hivyo, wanaropokaropoka tu na lugha kama: 'Taasisi ya Mwalimu Nyerere washitakiwe kwa uhaini' na wengine 'Genge la wanataasisi ya Mwalimu Nyerere' etc. Kweli mtu aliyesoma na akaelimika anaweza kufanya kama wanavyofanya hao wenye kujikomba kwa Kikwete? Hivi hawaoni aibu kujikomba?
   
Loading...