Butiku na wenzake ni 'wahaini'

Mpaka hapo tutakapoondoa woga na kuwa tayari kwa lolote, hakuna jema litakalotokea. Tusitarajie CCM na vibaraka wake wajiondoe na kukaa pembeni bila kulazimishwa kuondoka. Tusitarajie kuwa tutaitoa CCM kwa kutumia 'chaguzi' endapo mfumo uliopo unaipa fursa ya kushinda bila kushindana. Vyama vya upinzani vimejaa ubinafsi na havishughulikii mambo ya msingi zaidi ya kupigania ruzuku. Kuna haja ya kusema imetosha, liwalo na liwe...tuweke uzalendo mbele, masilahi binafsi nyuma...longolongo haitatufikisha popote...kuna haja ya kupambana na ndiyo njia pekee ya kubadili utawala uliopo. Vinginevyo tutulie tuli na waendelee kutunyoa kwa kutumia kipande cha chupa!

Watanzania wengi hawana uti wa mgongo (not assertive) na ndiyo maana mtu akikosoa kidogo kunakuwa na 'reaction' kubwa. Mimi naamini wanaokosoa wana hoja na wanaomtetea Jakaya Kikwete/Serikali wanadhani kukosoa ni kumumaliza/kuimaliza Serikali. Hii inapelekea watu wengi kuwa wanafiki, wakidhani 'flattery' ndiyo njia ya ku'survive'.

Mawazo yangu ni haya: kama kundi moja la watu linakosoa basi kundi jingine lisije na kuwapinga waliokosoa. Kama wanataka waanze kuelezea mema ambayo kundi la kwanza halikuona. Lakini kurudiarudia tu maneno na kuanza kuaanika maovu ya wakosoaji kunaonyesha tu jinsi tunavyo'abuse' uwezo wetu wa kufikiri. Tuwaache watu waseme kero zao - wenye kusifia acha wasifie na wenye kukosoa acha wakosoe! Hii ndiyo njia sahihi!
 
Back
Top Bottom