Habari mwana JF..
Je tumekosa dira au tumeamua kwa makusudi kuwaumiza watu wetu?!
Hivyo ndivyo navyoweza kuuliza kwa hali tuliyofikia sasa.
Sasa hivi tunavyozungumza huko Butiama ktk baadhi ya vijiji kama Buturu, michango ya ujenzi wa sekondari inalazimishwa hata kwa asiye na uwezo. Buturu wanachangishwa sh. 40,000/= (awamu ya 1). Juzi wenyekiti wa vijiji wameanza oparesheni kukamata kuku, jembe, sufuria n.k kwa yeyote ambaye mpaka sasa hajachanga.
Ikumbukwe sasa hivi kaya nyingi ndio zipo ktk kilimo, ni msimu wa kupanda ila kwa umaskini wa kaya zile hata mbegu ya kilimo ni shida. Mbolea ndio hawanunui kabisaa..! Ni maskini wa kutupwa. Hizo 40,000/= watatoa wapi?!
Hiyo mnayosema ni serikali sikivu, ni ipi?! Hii inayo engineer unyonyaji mkubwa hivi?!
Sasa huku Shinyanga ndio nimeshangaa.
Waponda mawe ya mgodini, kina mama wauza mchicha n.k wamelazimishwa kuuziwa vitambulisho vya ujasiriamali.
Ktk taarifa ya habari ya ITV usiku wa saa 2, tarehe 15 march 2019, ameonekana mkuu wa wilaya ya shinyanga akitimka mbio na askari wake kuwakimbia waganga njaa wa mgodini ambao waliandamana kwenda kulalamika kulazimishwa chini ya ulinzi mkali na bunduki kununua vitambulisho hivyo.
Wamehoji kuwa wao sio wajasiriamali! Mama mmoja akahoji yeye anauza mchicha na mtaji wake ni sh. Elfu 3. Anatoa wapi 20,000/-???!
Ni wapi tunafeli. Inakuwaje project za JPM zinageuka mateso kwa mwananchi?
Au ukitembelea VX unisahau uhalisia wa maisha ya wananchi wako?!
Cc: barafu , technically , magongwa mtambuka, UCD . Wakudadavuwa