Butiama wananyang'anywa sufuria, jembe kisa michango ya elimu. Shinyanga wanagawiwa ID za ujasiriamali kwa mtutu na askari. Tutafika?

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
1,971
2,000
Habari mwana JF..

Je tumekosa dira au tumeamua kwa makusudi kuwaumiza watu wetu?!

Hivyo ndivyo navyoweza kuuliza kwa hali tuliyofikia sasa.

Sasa hivi tunavyozungumza huko Butiama ktk baadhi ya vijiji kama Buturu, michango ya ujenzi wa sekondari inalazimishwa hata kwa asiye na uwezo. Buturu wanachangishwa sh. 40,000/= (awamu ya 1). Juzi wenyekiti wa vijiji wameanza oparesheni kukamata kuku, jembe, sufuria n.k kwa yeyote ambaye mpaka sasa hajachanga.

Ikumbukwe sasa hivi kaya nyingi ndio zipo ktk kilimo, ni msimu wa kupanda ila kwa umaskini wa kaya zile hata mbegu ya kilimo ni shida. Mbolea ndio hawanunui kabisaa..! Ni maskini wa kutupwa. Hizo 40,000/= watatoa wapi?!

Hiyo mnayosema ni serikali sikivu, ni ipi?! Hii inayo engineer unyonyaji mkubwa hivi?!

Sasa huku Shinyanga ndio nimeshangaa.
Waponda mawe ya mgodini, kina mama wauza mchicha n.k wamelazimishwa kuuziwa vitambulisho vya ujasiriamali.

Ktk taarifa ya habari ya ITV usiku wa saa 2, tarehe 15 march 2019, ameonekana mkuu wa wilaya ya shinyanga akitimka mbio na askari wake kuwakimbia waganga njaa wa mgodini ambao waliandamana kwenda kulalamika kulazimishwa chini ya ulinzi mkali na bunduki kununua vitambulisho hivyo.

Wamehoji kuwa wao sio wajasiriamali! Mama mmoja akahoji yeye anauza mchicha na mtaji wake ni sh. Elfu 3. Anatoa wapi 20,000/-???!

Ni wapi tunafeli. Inakuwaje project za JPM zinageuka mateso kwa mwananchi?

Au ukitembelea VX unisahau uhalisia wa maisha ya wananchi wako?!

Cc: barafu , technically , magongwa mtambuka, UCD . Wakudadavuwa
 
Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,034
2,000
Sasa hivi tunavyozungumza huko Butiama ktk baadhi ya vijiji kama Buturu, michango ya ujenzi wa sekondari inalazimishwa hata kwa asiye na uwezo. Buturu wanachangishwa sh. 40,000/= (awamu ya 1). Juzi wenyekiti wa vijiji wameanza oparesheni kukamata kuku, jembe, sufuria n.k kwa yeyote ambaye mpaka sasa hajachanga.
Ikumbukwe saivi kaya nyingi ndio zipo ktk kilimo , ni msimu wa kupanda ila kwa umaskini wa kaya zile hata mbegu ya kilimo ni shida. Mbolea ndio hawanunui kabisaa..! Ni maskini wa kutupwa. Hizo 40,000/= watatoa wapi?!
Hiyo mnayosema ni serikali sikivu, ni ipi?! Hii inayo engineer unyonyaji mkubwa hivi?!
.
Kuhusu michango shuleni, kuna jambo ungefanya ili kuboresha hoja yako.

Pitia shule tano huko Butiama.

Tafuta watoto watano kutoka familia tofauti.

Tambua wazazi wao.

Watafute wazazi hao huko nyumbani kwao.

Kila mzazi mwulize maswali mawili.

1. Kwa mwezi unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya gharama za karo ya mtoto wako? (Rekodi jibu la kwanza kama X)

2. Kwa mwaka unatumia shilingi ngapo kwa ajili ya gharama zilizo nje ya karo ya mtoto wako? (Rekodi jibu la pili kama Y).

Gawanya X kwa Y. (Rekodi jibu kama Z)

Zidisha Z mara 100. Rekodi jibu kama R

Tafuta R kwa kila kaya.

Mwisho tafuta wastani wa R.

Halafu utwambie majibu hapa.

Kwa vile Profesa Ndalichako ni msomi atakuwa amepata ujumbe kisayansi.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,430
2,000
Wakati wanamchi maskini wanapolazimishwa kuchangia aina hiyo ya michango, ghafla unaambiwa kuna mbunge/diwani wa kutoka upande fulani amejiuzulu ili aunge mkono juhudi hivyo inabidi kufanya uchaguzi mdogo na mtu huyo huyo eti anagombea tena kupitia chama kingine na kushinda kwa kishindo au kupita bila kupingwa!

Hayo mabilioni wanayochezea kurudia uchaguzi kwa mgongo wa demokrasia si yangeweza kutumika kujengea hayo majengo na wananchi wakaachwa wapambane na hali zao pasipo kuwanyanyasa?
 
Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,034
2,000
Sasa huku Shinyanga ndio nimeshangaa.
Waponda mawe ya mgodini, kina mama wauza mchicha n.k wamelazimishwa kuuziwa vitambulisho vya ujasiriamali.
Ktk taarifa ya habari ya ITV usiku wa saa 2, tarehe 15 march 2019, ameonekana mkuu wa wilaya ya shinyanga akitimka mbio na askari wake kuwakimbia waganga njaa wa mgodini ambao waliandamana kwenda kulalamika kulazimishwa chini ya ulinzi mkali na bunduki kununua vitambulisho hivyo.
Wamehoji kuwa wao sio wajasiriamali!!..
Mama mmoja akahoji yeye anauza mchicha na mtaji wake ni sh. Elfu 3. Anatoa wapi 20,000/-???!
Ni wapi tunafeli. Inakuwaje project za JPM zinageuka mateso kwa mwananchi?

Au ukitembelea VX unisahau uhalisia wa maisha ya wananchi wako?!
.
Kuhusu hizo kadi zilizotolewa na Mhe. Rais Magufuli nadhani kuna maagiza ambayo yanapaswa kuongezeka kutoka kwake.

Nilimsikia akisema kuwa vitambulisho hivyo ni kwa watu wenye mtaji usiozidi milioni nne.

Sijasikia akitoa maelekezo kuhusu kima cha chini cha mtaji.

Tangu yule mbunge Sugu alipopata msukosuko, Maafisa wetu kutoka secret service walipaswa kuwa wameona tatizo lililoibuliwa na kushauri ipasavyo.

Wamefanya hivyo?

Kama tayari, Mhe. Rais anapaswa kuchukua hatua sasa.

Kama bado hawajafanya hivyo, waharakishe kuweka sawa jambo hili.

Usalama wa nchi ni pamoja na usalama wa kiuchumi katika kaya hizi za watu maskini.

Nimesikia huko Kaskazini wanasema hii ni sawa na kodi ya kichwa.

Kuna jambo halijakaa sawa.
 
mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,961
2,000
Habari mwana JF..

Je tumekosa dira au tumeamua kwa makusudi kuwaumiza watu wetu?!
Hivyo ndivyo navyoweza kuuliza kwa hali tuliyofikia sasa.

Sasa hivi tunavyozungumza huko Butiama ktk baadhi ya vijiji kama Buturu, michango ya ujenzi wa sekondari inalazimishwa hata kwa asiye na uwezo. Buturu wanachangishwa sh. 40,000/= (awamu ya 1). Juzi wenyekiti wa vijiji wameanza oparesheni kukamata kuku, jembe, sufuria n.k kwa yeyote ambaye mpaka sasa hajachanga.
Ikumbukwe saivi kaya nyingi ndio zipo ktk kilimo , ni msimu wa kupanda ila kwa umaskini wa kaya zile hata mbegu ya kilimo ni shida. Mbolea ndio hawanunui kabisaa..! Ni maskini wa kutupwa. Hizo 40,000/= watatoa wapi?!
Hiyo mnayosema ni serikali sikivu, ni ipi?! Hii inayo engineer unyonyaji mkubwa hivi?!

Sasa huku Shinyanga ndio nimeshangaa.
Waponda mawe ya mgodini, kina mama wauza mchicha n.k wamelazimishwa kuuziwa vitambulisho vya ujasiriamali.
Ktk taarifa ya habari ya ITV usiku wa saa 2, tarehe 15 march 2019, ameonekana mkuu wa wilaya ya shinyanga akitimka mbio na askari wake kuwakimbia waganga njaa wa mgodini ambao waliandamana kwenda kulalamika kulazimishwa chini ya ulinzi mkali na bunduki kununua vitambulisho hivyo.
Wamehoji kuwa wao sio wajasiriamali!!..
Mama mmoja akahoji yeye anauza mchicha na mtaji wake ni sh. Elfu 3. Anatoa wapi 20,000/-???!
Ni wapi tunafeli. Inakuwaje project za JPM zinageuka mateso kwa mwananchi?

Au ukitembelea VX unisahau uhalisia wa maisha ya wananchi wako?!

Cc: barafu , technically , magongwa mtambuka, UCD . Wakudadavuwa
Vibweka vya jiwe huwezi kuvikuta kwenye hii thread
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
14,508
2,000
Wabunifu sera wa serikali ya magu na ccm wamefika mwisho wao wa kufikiri. Hawana jipya la kufanya zaidi ya kuzidisha mateso kwa wale wanaowaita wanyonge. Hadi siku mnyonge atakapotambua kuwa ananyongwa ndipo tutapata ukombozi wa kweli.
Walimu na watumishi wa serikali wamebaki hopeless,maslahi Yao kwisha habariii, Mishahara inazidi katwaa.Na bado.Kuna Ka ujumbe nilikatumia sn humu moods wakanipiga ban, watumishi pambaneni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,698
2,000
.
Kuhusu hizo kadi zilizotolewa na Mhe. Rais Magufuli nadhani kuna maagiza ambayo yanapaswa kuongezeka kutoka kwake.

Nilimsikia akisema kuwa vitambulisho hivyo ni kwa watu wenye mtaji usiozidi milioni nne.

Sijasikia akitoa maelekezo kuhusu kima cha chini cha mtaji.

Tangu yule mbunge Sugu alipopata msukosuko, Maafisa wetu kutoka secret service walipaswa kuwa wameona tatizo lililoibuliwa na kushauri ipasavyo.

Wamefanya hivyo?

Kama tayari, Mhe. Rais anapaswa kuchukua hatua sasa.

Kama bado hawajafanya hivyo, waharakishe kuweka sawa jambo hili.

Usalama wa nchi ni pamoja na usalama wa kiuchumi katika kaya hizi za watu maskini.

Nimesikia huko Kaskazini wanasema hii ni sawa na kodi ya kichwa.

Kuna jambo halijakaa sawa.
mkuu hata hapa wanasema hivyo, kua ni kodi ya kichwa imerudishwa kwa staili tofauti!
 
Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,034
2,000
mkuu hata huku wanasema hivyo, kua ni kodi ya kichwa imerudishwa kwa staili tofauti!
.
Ndiyo wanasema sehemu nyingi.

Lakini, mimi ninayo mawazo chanya na dhana husika.

Hata hivyo, kuna shida mbili ningependa zitatuliwe.

Moja ni ukosefu wa mwongozo wa kima cha chini cha mtaji.

Na pili ni suala la kisheria--Makusanyo hayo yanaongozwa na sheria gani?

Kuna shida hapo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom