Butiama wananyang'anywa sufuria, jembe kisa michango ya elimu. Shinyanga wanagawiwa ID za ujasiriamali kwa mtutu na askari. Tutafika?

.
Ndiyo wanasema sehemu nyingi.

Lakini, mimi ninayo mawazo chanya na dhana husika.

Hata hivyo, kuna shida mbili ningependa zitatuliwe.

Moja ni ukosefu wa mwongozo wa kima cha chini cha mtaji.

Na pili ni suala la kisheria--Makusanyo hayo yanaongozwa na sheria gani?

Kuna shida hapo.
sawa kabisa pia nadhani ile siku rais anaelezea kima hicho kuna watu hasa watendaji wake hawakumuelewa, mpaka sasa tafrisri ya machinga ni yupi haina kikomo, yaani badala wapewe wamachinga, wanapewa mpaka wauza mchicha na nyanya, kuhusu kisheria sina utalamu nalo ila nadhani haitatungwa, kwanza ni nani atamshauri jiwe afanye hivyo? hii kitu atakua ameachiwa mkurugenzi na baadae tutaambiwa inapelekwa hazina, hawa watu we waskie tu! sina hamu nao!
 
Whaaaaacha waisome namba akili ziwakae sawa tuliposema lazma awe na final say asiwe yeye final say waliona sie vilaza kwa sasa akili itawakaaa sawa tuu wanunue vitambulisho pesa zikafanye uchaguzi nyaaaaaaambaaaaaf
 
Walimu na watumishi wa serikali wamebaki hopeless,maslahi Yao kwisha habariii, Mishahara inazidi katwaa.Na bado.Kuna Ka ujumbe nilikatumia sn humu moods wakanipiga ban, watumishi pambaneni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha ule ujumbe wako kwa watumishi wa serikali kumbe ulisababisha ukala ban mkuu!! Pole sana, ujumbe ule ulikuwaga mzuri sana
 
Uongozwe na mwanakijiji mrowa samaki harafu utegemee matokeo chanya maajabuu ya bata kutngisha body la nyuma
 
.
Kuhusu hizo kadi zilizotolewa na Mhe. Rais Magufuli nadhani kuna maagiza ambayo yanapaswa kuongezeka kutoka kwake.

Nilimsikia akisema kuwa vitambulisho hivyo ni kwa watu wenye mtaji usiozidi milioni nne.

Sijasikia akitoa maelekezo kuhusu kima cha chini cha mtaji.

Tangu yule mbunge Sugu alipopata msukosuko, Maafisa wetu kutoka secret service walipaswa kuwa wameona tatizo lililoibuliwa na kushauri ipasavyo.

Wamefanya hivyo?

Kama tayari, Mhe. Rais anapaswa kuchukua hatua sasa.

Kama bado hawajafanya hivyo, waharakishe kuweka sawa jambo hili.

Usalama wa nchi ni pamoja na usalama wa kiuchumi katika kaya hizi za watu maskini.

Nimesikia huko Kaskazini wanasema hii ni sawa na kodi ya kichwa.

Kuna jambo halijakaa sawa.
Kwa taarifa za ndani nilizonazo ni kwamba jambo ambalo huwa mh Rais ameamua, kila mtu anaogopa kugusa. Hata hao usalama unaowaita hapa wanafunga mdomo kabisa. Yani ni hatari..
 
.
Ndiyo wanasema sehemu nyingi.

Lakini, mimi ninayo mawazo chanya na dhana husika.

Hata hivyo, kuna shida mbili ningependa zitatuliwe.

Moja ni ukosefu wa mwongozo wa kima cha chini cha mtaji.

Na pili ni suala la kisheria--Makusanyo hayo yanaongozwa na sheria gani?

Kuna shida hapo.
Haya maswali ya msingi sana. Ila hawawezi kujibu hilo swali la hivi vitambulisho vinatolewa kwa sheria ipi na mapato yapo ktk sheria ipi..
Hawana majibu ya hili swali
 
Hii iko poa, tuendelee hivi hivi. Maendeleo hayana chama.
Ni matumaini yangu hao wanaoteseka ni wanachama wa Chadema.
2020, hao hao wanaolia hali mbaya wakipewa kofia, kitenge na elfu kumi, wnasahau kuwa watakuwa na miaka mitano ya kuteseka tena. Safi sana, magu kaza buti.
 
.
Kuhusu michango shuleni, kuna jambo ungefanya ili kuboresha hoja yako.

Pitia shule tano huko Butiama.

Tafuta watoto watano kutoka familia tofauti.

Tambua wazazi wao.

Watafute wazazi hao huko nyumbani kwao.

Kila mzazi mwulize maswali mawili.

1. Kwa mwezi unatumia shilingi ngapi kwa ajili ya gharama za karo ya mtoto wako? (Rekodi jibu la kwanza kama X)

2. Kwa mwaka unatumia shilingi ngapo kwa ajili ya gharama zilizo nje ya karo ya mtoto wako? (Rekodi jibu la pili kama Y).

Gawanya X kwa Y. (Rekodi jibu kama Z)

Zidisha Z mara 100. Rekodi jibu kama R

Tafuta R kwa kila kaya.

Mwisho tafuta wastani wa R.

Halafu utwambie majibu hapa.

Kwa vile Profesa Ndalichako ni msomi atakuwa amepata ujumbe kisayansi.
Nimekaa sana Butiama, pia mimi ni mwana hisabati niliyefuzu. Hicho unachokijenga nakuelewa ila tambua watu wale ni maskini sana.
Nyumba za tembe na wanajitahidi kula tu. Wengine kipato chao kula tu hakitoboi mwaka, wanachangiwa "udaga" na majirani wenye nafuu.
Sasa kama hujui udaga ni nini Njoo tena uulize logic zako...
 
Back
Top Bottom