Kwa kawaida kodi za wananchi na ada mbalimbali ndizo michango yao ya "lazima" kwa serilali iliyoko kisheria. Hivi ndivyo vyanzo vikuu vya mapato ya serikali ambayo yanayowezesha uendeshaji wake: kugharamia matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) na kuwaletea maendeleo (development expenditure).Wabunifu sera wa serikali ya magu na ccm wamefika mwisho wao wa kufikiri. Hawana jipya la kufanya zaidi ya kuzidisha mateso kwa wale wanaowaita wanyonge. Hadi siku mnyonge atakapotambua kuwa ananyongwa ndipo tutapata ukombozi wa kweli.
Mamlaka zenye dhamana ya kukusanya mapato ya serikali katika kutekeleza majukumu yao zinapaswa kuzingatia hali halisi za uchumi wa wananchi.
Ipo wizara ya mipango na fedha, na taasisi ya takwimu (Tanzania Bureau of Statistics). Wizara na Takwimu kama wanafanya kazi zao barabara ikiwemo maoteo (projections), habari ya " watoto wengi zaidi ya ilivyotarajiwa wameandikishwa mashuleni kwa sababu ya elimu ya bure" haipaswi kuwepo.
Aidha, utekelezaji wa kibajeti uni hauzingatiwi! Serikali haina vipaumbele katika miradi ya maendeleo kwa maana ya kuwa mirandi ya maendeleo inayotekelezwa kwa wakati mmoja imekuwa mingi mno na inazidia mapato yetu ikitiliwa maanani kuwa wafadhili/washirika wetu wa maendeleo wamepunguza ufadhili wao kwa sababu mbalimbali. Ndiyo sababu za kubuniwa na kunaibuliwa vitambulisho vya wajasiriamali na michango ya ujenzi wa shule za sekondari.
Fikiria viuzwe jumla ya vitambulisho mil. 5, tu @ 20,000/-. Tsh mil. 100 zinaweza kupatikana. Na wastani wa Tsh elfu 30 @ kaya, kwa kaya milioni 20, wananchi watakamuliwa bila huruma bil 600 nje ya bajeti ya serikali. Si haba. Mtanzania wa kaeaida anapatwa wasiwasi na uendeshwaji na hali ya uchumi wa nchi. Kampuni na mtu binafsi hufilisika kwa kukosa ukwasi na kushindwa kugharamia na kulipa madeni.