PreGE2025 POTOSHI BUTIAMA: Mzee Butiku asema tangu awali hakukubaliana na Uhuni na Uendawazimu wa Humphrey Polepole

PreGE2025 POTOSHI BUTIAMA: Mzee Butiku asema tangu awali hakukubaliana na Uhuni na Uendawazimu wa Humphrey Polepole

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1753444363533.png


Mzee Butiku asema, Ngoja nimwite Kwa lugha ya Mtaani Muhuni au Mwendawazimu na pengine si mwenzetu,
 
Tunachokijua
Mzee Joseph Butiku ni Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Mwalimu Nyerere ambaye pia alikuwa msaidizi binafsi wa utafiti wa Hayati mwalimu Nyerere alipokuwa Rais, pamoja na kuwa Mkuu wa Wafanyakazi na Mjumbe Binafsi kabla ya kushika nafasi yake ya sasa. Pia alihudhuria Chuo cha Kijeshi cha Monduli na kuhitimu kama Luteni, na baadaye kupandishwa hadi cheo cha Meja.

Baadaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Rais na Mkuu wa Wafanyakazi chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi, Katibu wa Chama wa CCM wa Mkoa wa Mara, na baadaye kuwa Mkuu wa Mkoa.

Mnamo mwezi Julai 23, 2025 Mzee Butiku alifanya mahojiano kupitia kipindi cha 'Dakika 45' cha ITV ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia uoga wa watanzania kutoa mawazo tofauti akisisitiza kuwa hiyo ni kasoro katika demokrasia.

"Tunako katabia kidogo Watanzania, nadhani kitaifa, 'uwoga' wa kutoa mawazo tofauti, na nadhani nayo ni kasoro, katika demokrasia kila mtu lazima asikilizwe hata kama hukubaliani naye, na umuheshimu atoe mawazo yake mpaka yakamilike na umjibu kwa hoja usimtusi wala kumkashifu, jibu kwa hoja"


Kipande cha video kinachomhusisha Mzee Joseph Butiku


Kipo kipande cha video kilichochapishwa mtandaoni kikimuonesha Mzee Butiku akitajwa kumrejelea Balozi Humphrey Polepole kwa kusema "Ngoja nimwite Kwa lugha ya Mtaani Muhuni au Mwendawazimu na pengine si mwenzetu"


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search pamoja na marejeo ya video, umejiridhisha kuwa kipande hicho cha video kimepotoshwa kutoka kwenye video ya kipindi cha 'Dakika 45' iliyochapishwa kwenye ukurasa wa ITV mtandao wa Youtube.

Kipande hicho kimepotoshwa kwa kukata sehemu ya kipindi ndogo ya kipindi hicho na kutengeneza ujumbe usiokamilika hivyo kupotosha uhalisia. Lakini pia Sauti ya video hairandani na matamshi yanayoonekana kwa Mzee Butiku jambo linalothibitisha kuhaririwa kwa video hiyo.

Aidha kipande hicho cha video kinahusisha majibu ya Mzee Butiku alipoulizwa ni nini kauli yake dhidi ukosaji uliofanywa na Balozi Humphrey Polepole dhidi ya utawala Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambapo sehemu ya majibu yake mzee huyo alisema,

"Kijana nilipomuona alisema kama, huyo naye mzee hakuridhika, ni kweli hatukukubaliana, nashauri kama watu wazima, amefanya kitu gani, nitumie lugha nayoona ya mtaani, wengine wanasema Muhuni, wengine wanasema mwendawazimu, wengine wanasema si mwenzetu.

Huyu kwa hadithi ile niliyoisikia, unakumbuka ile hadithi ya mfalme kila mtu anatoa sifa akatokea mtoto huyu, mmoja. Mimi sisemi tuwe na vijana wanaodharau katiba, wanaodharau viongozi wao, ambao hawaheshimu .

Lakini vijana wetu lazima wawe jasiri kwa sababu ujasiri utakaolinda misingi ya taifa letu na taratibu tulizoweka kulinda misingi na kusaidia kwenda tunakokwenda kwa kuzingatia misingi na pale ambapo tunabidi tubadili misingi hiyo wajue namna ya kubadili baba wa taifa letu ndivyo alivyotufundisha"


View: https://www.youtube.com/live/CTwcso_0pVg?si=xA6zzVa57NG6bSI4&t=2615
Dah mzee vp tena.h polepole hakusema kweli hata km n mhuni?embu hukumu kauli yake
 
Acha uongo.



Mzee Butiku: Wengine wanasema muhuni, wengine wanasema, mwendawazimu!

Ushauri wangu......
 
Back
Top Bottom