KERO Buti ni kama tiketi ya kuingia Soko la Mabibo kipindi cha Mvua, ahadi ya ukarabati wa Manispaa ya Ubungo umeota mbawa?

KERO Buti ni kama tiketi ya kuingia Soko la Mabibo kipindi cha Mvua, ahadi ya ukarabati wa Manispaa ya Ubungo umeota mbawa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
photo_2026-03-13_10-52-02.jpg

photo_2026-03-13_10-52-01.jpg
Soko la Mahakama ya Ndizi lililopo Mabibo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo limeendelea kuwa katika hali mbaya licha ya kuahidiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo yangeweza kutatua kero zilizokuwa zikilalamikiwa kwa muda mrefu.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilitoa taarifa ya kulichukua soko hilo na kuanza kulisimamia rasmi, ambapo ilieleza wazi kuwa baada ya kulichukua marekebisho yangefanyika. Baada ya kuanza kulisimamia, tuliona baadhi ya marekebisho yakianza kufanyika, ikiwemo kujenga mitaro na kurekebisha baadhi ya maboma ya wafanyabiashara waliopo ndani ya soko hilo. Hatua hiyo ilileta matumaini, na tuliamini kuwa baada ya muda hali ya soko ingekuwa nzuri.

Pia soma ~ Manispaa ya Ubungo ilituahidi baada kuanza kulisimamia Soko la Mabibo miundombinu itakuwa shwari, lakini bado hali ni tete

Hata hivyo, hadi sasa ukarabati huo uliishia katikati. Eneo kubwa la soko limejaa matope, hali ambayo inawalazimisha wateja pamoja na wafanyabiashara kuvaa buti maalumu ili kukabiliana na matope yaliyopo.
photo_2026-03-13_10-51-57.jpg

photo_2026-03-13_10-51-50.jpg
Wateja wengi kipindi cha mvua hushindwa kufika sokoni kutokana na hali ya soko kutopitika. Hali hiyo inatuletea changamoto kwenye mauzo kwa kuwa idadi ya wateja inapungua. Aidha, baadhi ya wateja hulazimika kukodi buti au kuwalipa vijana ili wawasaidie kupita kwenye matope. Vilevile mvua zikinyesha, magari ya mizigo hupata shida kushusha mizigo kutokana na hali mbaya ya eneo la soko.

Hali ya soko si rafiki kabisa. Hata mitaro iliyojengwa haisafishwi kwa wakati, na katika maeneo mengi kumejaa taka ambazo zinaweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu, hasa ikizingatiwa kuwa uchafu mwingi unatokana na mabaki ya matunda.

Niungane na wenzangu Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ichukue hatua za uwajibikaji. Pia mamlaka za juu, hususan TAMISEMI, ziangalie kwa karibu kubaini nini kinachokwamisha kuendelea kwa ukarabati wa soko hilo, ilhali wafanyabiashara na wananchi wanaendelea kutozwa ushuru.

Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ilitoa taarifa takribani miaka miwili iliyopita kuwa ilikusanya zaidi ya shilingi bilioni 1.2 kwa mwaka kutoka katika soko hilo kupitia mapato mbalimbali, ikiwemo ushuru ikiwa ni baada ya kuanza kulisimamia.
photo_2026-03-13_10-51-55.jpg

photo_2026-03-13_10-51-52.jpg
 
Kwani wao wanakuja kununuaga mahitaji yao hapo. Kama sio city mall au mlimani city.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom